GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mbona Chadema wata shiriki uchaguzi? Tunacho taka ni Reforms ili tuingie na tuna kwenda kuingia kwenye uchaguzi kwa Reforms za uhakika. Hebu angalia wao wenyewe wana nyimana form??
survival of the fittest
 
huezi kwepa hilo, chama cha siasa ni watu na kama rasilimali watu hamna hata mapato hamna na nyomi hamna
swala la kura mnalitumia kama mgongo wenu kila mara mnaposhindwa uchaguzi, ni serikaii hii hii na tume hii hii lisu aliotumia kushinda ubunge kwa miaka 10 pamoja na wenzake lema, mbowe.. sasa mda wa kushindwa ndo mnasema tume ni mbovu si ndio?

ni magari haya haya na posho hizi hizi mlikua mnapokea mlipokua bungeni leo hii hampo bungeni lawama znakua nyingi wengine wakipewa posho,

ni watu hawa hawa waliokua chadema mkasema tuwapigie kura wanafaa, leo hii hawakubaliani na agenda zenu za kususia uchaguzi wameenda sehem ingine mnawatukana, tunapowaambiaga icho ni kikundi mue waelewa!


lissu aliwakimbia akenda ubelgiji mwamba akabaki akafanya maridhiano waerudi salama leo hii aliewakimbia mnamuona wa maaana kama sio kulogwa ni nn
Kwa taarifa yako kwenye soka kuna technology ya VAR, sio kwamba mshindi alikuwa hapatikani, bali technology hiyo ililetwa ili kuondoa malalamiko yasiyokwisha kuhusu baadhi ya ushindi uliokuwa unapatikana. Umewahi kusikia kuna team au nchi inagomea VAR kisa washindi tafauti walikuwa wanapatikana?

Hakuna maridhiano, bali ule ulikuwa utapeli kama utapeli mwingine. Na maridhiano yale yalikuwa binafsi kwa Mbowe na genge lake. Lisu tunamuona wa maana kwakuwa hana muda wa kulamba asali, na kuingizwa mjini kwenye maridhiano fake.
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
Kwa taarifa yako kwenye soka kuna technology ya VAR, sio kwamba mshindi alikuwa hapatikani, bali technology hiyo ililetwa ili kuondoa malalamiko yasiyokwisha kuhusu baadhi ya ushindi uliokuwa unapatikana. Umewahi kusikia kuna team au nchi inagomea VAR kisa washindi tafauti walikuwa wanapatikana?

Hakuna maridhiano, bali ule ulikuwa utapeli kama utapeli mwingine. Na maridhiano yale yalikuwa binafsi kwa Mbowe na genge lake. Lisu tunamuona wa maana kwakuwa hana muda wa kulamba asali, na kuingizwa mjini kwenye maridhiano fake.
angebaki ubelgiji kama yalikua haya maaana! na pia lissu sio mpigania haki kama unavodhan
 
Siyo kweli!

Kwanza chadema haijasusia uchaguzi, bali itauzuia uchaguzi.

Hakutakuwa na uchaguzi kama mabadiliko hautafanyika. CCM bado wana mwenzi mmoja wa kutafakari upya jambo hili. Vinginevyo uchaguzi hautafanyika.
100%✓✍️
 
angebaki ubelgiji kama yalikua haya maaana! na pia lissu sio mpigania haki kama unavodhan
Siwajibiki kwenye hisia zako. Najua ni mpigania haki, na ushahidi wa hayo upo.
 
KAKA ASANTE KWA KUWASHAURI. LAKINI TATIZO NI KUWA MBONA WAKIJA HAMTAKAGI KUWAPA FOMU?
Wapinzani walikuwa wanafanyiwa figisu kwa mtindo wa mutatis mutandis, Japo Mama sio mtu wa figisu ila wahafidhina wa chama chake!, tumemshauri Mama aachane na hizi mambo za figisu, Pre GE2025 - LGE2024 - Ombi Maalum, Kwa Mtu Maalum Achana na Hizi Mutatis Mutandis Kwenye Chaguzi za SM2024 & U/Mkuu2025, Tumia Ceteris Peribus, Utabarikiwa, Tutabarikiwa!

Na hata kale ka simba ka Kizimkazi, tumeshauri akaachie!.
P
 
Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Kwanza jifunze kutofautisha mazingira. Pili kujaribu kitu kile kile na ukawa unapata matokeo yale yale tena kwa maumivu na mateso makali kutoka kwa watu wale wale waliopo kwenye mifumo ile ile ni kujiondosha ufahamu!
Tatu, wananchi walishasusa chaguzi kabla hata ya CDM! ccm wanatambua hilo ndo maana wanakwambia Oktoba Wanatiki!
Kuna Dola liko mbioni kuimarishwa! Lisije tu likawa la kimalkia au kidikteta!
Screenshot_20250630-232918.png
 
Back
Top Bottom