GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mbona Chadema wata shiriki uchaguzi? Tunacho taka ni Reforms ili tuingie na tuna kwenda kuingia kwenye uchaguzi kwa Reforms za uhakika. Hebu angalia wao wenyewe wana nyimana form??
survival of the fittest
 
Kwa taarifa yako kwenye soka kuna technology ya VAR, sio kwamba mshindi alikuwa hapatikani, bali technology hiyo ililetwa ili kuondoa malalamiko yasiyokwisha kuhusu baadhi ya ushindi uliokuwa unapatikana. Umewahi kusikia kuna team au nchi inagomea VAR kisa washindi tafauti walikuwa wanapatikana?

Hakuna maridhiano, bali ule ulikuwa utapeli kama utapeli mwingine. Na maridhiano yale yalikuwa binafsi kwa Mbowe na genge lake. Lisu tunamuona wa maana kwakuwa hana muda wa kulamba asali, na kuingizwa mjini kwenye maridhiano fake.
 
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
angebaki ubelgiji kama yalikua haya maaana! na pia lissu sio mpigania haki kama unavodhan
 
Siyo kweli!

Kwanza chadema haijasusia uchaguzi, bali itauzuia uchaguzi.

Hakutakuwa na uchaguzi kama mabadiliko hautafanyika. CCM bado wana mwenzi mmoja wa kutafakari upya jambo hili. Vinginevyo uchaguzi hautafanyika.
100%✓✍️
 
angebaki ubelgiji kama yalikua haya maaana! na pia lissu sio mpigania haki kama unavodhan
Siwajibiki kwenye hisia zako. Najua ni mpigania haki, na ushahidi wa hayo upo.
 
KAKA ASANTE KWA KUWASHAURI. LAKINI TATIZO NI KUWA MBONA WAKIJA HAMTAKAGI KUWAPA FOMU?
Wapinzani walikuwa wanafanyiwa figisu kwa mtindo wa mutatis mutandis, Japo Mama sio mtu wa figisu ila wahafidhina wa chama chake!, tumemshauri Mama aachane na hizi mambo za figisu, Pre GE2025 - LGE2024 - Ombi Maalum, Kwa Mtu Maalum Achana na Hizi Mutatis Mutandis Kwenye Chaguzi za SM2024 & U/Mkuu2025, Tumia Ceteris Peribus, Utabarikiwa, Tutabarikiwa!

Na hata kale ka simba ka Kizimkazi, tumeshauri akaachie!.
P
 
Haki ipi anapigania? Najua mm ni opportunist tu.
Hakuna mwenye tatizo na mtazamo wako juu yake, sisi wengine tunamtazama kwa ukweli wake, sio zaidi ya hapo.
 
Kwanza jifunze kutofautisha mazingira. Pili kujaribu kitu kile kile na ukawa unapata matokeo yale yale tena kwa maumivu na mateso makali kutoka kwa watu wale wale waliopo kwenye mifumo ile ile ni kujiondosha ufahamu!
Tatu, wananchi walishasusa chaguzi kabla hata ya CDM! ccm wanatambua hilo ndo maana wanakwambia Oktoba Wanatiki!
Kuna Dola liko mbioni kuimarishwa! Lisije tu likawa la kimalkia au kidikteta!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…