GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wananchi Hawa sio wajinga wa kiasi hicho. Nchi yao imejaa wakimbizi kutoka mataifa mengine yanayowazunguuka, wanaifahamu sababu ya wakimbizi hao kuja kwetu. Kwenye maendeleo wanajua tuko hatua gani na nchi nyingine zinazotuzunguuka ziko hatua gani. Mfano, ni nchi ngapi Afrika Zina SGR, DART, hospitali/zahanati nyingi, umeme Kila Kijiji, shule nyingi Kila kijiji, maji Kila Kijiji, kuzalisha chakula Chao wenyewe, chanjo kwa Kila mtoto, mifugo mingi, ligi yao inaonyeshwa mechi zote, Zina timu nne zinashiriki CAF, nk. Anaekwambia kuwa Tanzania hakujafanyika kitu si anakwambia upumbavu?

Kaka nikwambie kitu, hata Hawa akina Mnyika, Heche na wengine wanacheza ngoma wasiyoijua. Wenye shughuli hii ya no reforms no election ni Lissu, Lema na Maria. Ndio maana wenye akili wamejitoa na kukaa mbali nao. Vurugu nchini Zina faida kwa Lema, Lissu na Maria maana wanapata mafao ya kuwa wakimbizi huko ng'ambo. Vijana amkeni amkeni amkeni, mmesikia wapi chama fulani kimezuia uchaguzi wa nchi yao usifanyike bila kutokea majeruhi na vifo vingi? Hayo majeruhi na vifo vitakavyotokea kwenye no reforms no election ndiyo biadhaa yao hawa watu.
 
Wananchi ndo wenye shughuli ya No Reforms No Elections.
 
Wananchi akina nani hao?

Uchaguzi ukivurugika itajikoki yenyewe, wataendelea tu bila suluba.
Wananchi ni tofauti sana na wavaa njano njano!
Hadi leo...wananchi waliojiandikisha kushiriki mchakato wa dhuluma ni wachache sana... Wengi hawaoni tena umuhimu huo!
 
Wananchi ni tofauti sana na wavaa njano njano!
Hadi leo...wananchi waliojiandikisha kushiriki mchakato wa dhuluma ni wachache sana... Wengi hawaoni tena umuhimu huo!
Hiyo haikuanza leo. Tangu zamani watu huwa wanajiandisha ili kupata vitambulisho tu vya kupiga kura viwasaidie kwenye mambo yao mengine. Kupiga kura na kuacha ni haki ya kidemokrasia, lakini hakuna ukomo wa idadi ya watu wa kupiga kura ili uchaguzi uwe halali. Kama hutaki kupiga kura lala nyumbani usifanye vurugu ukaumizwa bila sababu, maana atakayevunjika miguu ni wewe sio chadema, atakaetupiwa bomu la machozi ni wewe sio chama.

Bro usifuate mkumbo maana wewe huna bima ya matibabu , Wala passport ya kuikimbia nchi Wala posho ya ukimbizi. Baada ya kupata michubuko ya hapa a pale itakuwa wewe na ndugu zako mtajua nini cha kufanya wakati wenzenu wako ubelgiji, Canada, Kenya na kwingineko. Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Mlisema wapinzani wanawachelewesha, mumebaki wenyewe leteni Sasa maendeleo.
Lakini naomba u some na kutafakari kauli hii:
"Nikuteuwe, nikulipe mshahara, nikupe gari na Nyumba, halafu Bado utangaze mpinzani ni Mshindi!!!"
 
Maono ndio yalizuia
 
Hujui mateso wanayopitia wapinzani wakati wa uchaguzi
 
Mlisema wapinzani wanawachelewesha, mumebaki wenyewe leteni Sasa maendeleo.
Lakini naomba u some na kutafakari kauli hii:
"Nikuteuwe, nikulipe mshahara, nikupe gari na Nyumba, halafu Bado utangaze mpinzani ni Mshindi!!!"
Mbona akina Lissu walikuwa wabunge kwa miaka 10, nani aliwatangaza kuwa wameshinda? Acheni sababu za kuoketeza. Mbona aliyesema maneno hayo hamkumchulia hatua kama huyu?

Sisi tunafahamu kuwa hii ya Sasa sababu yake kuu ni udini. Maneno yanakuwa mengi sana pale ambapo Rais sio mkatoliki. Tumeshuhudia Marais wakatoliki wakifanya mabaya sana lakini maneno hakuna. Mfano, tumeona Rais akihamisha watu na kuwatupa porini kusikokuwa na huduma yoyote akidai anajenga vijiji vya ujamaa, tumeona akina Kambona wakiwa wakimbizi, akina Jumbe wakisulibiwa, pesa zetu zikitumika kukombolea nchi nyingine, shule za waskristo zikitaifishwa kuwa za umma, mashirika ya umma yakiuzwa kwa bei chee, nyumba za serikali kuuzwa na kugawanwa na viongozi, nk. Tumeona Rais mkatoliki akiifuta Tanganyika na kutunga Katiba ya hii inayolalamikiwa na wakatoliki haohao ambao walikuwa kimya wakati Rais mkatoliki anajilimbikizia madaraka. Leo hii hawataki Rais wa dhehebu lingine asitumie katiba ileile iliyotumiwa na Nyerere, Mkapa na Magufuli kwa utulivu kabisa.
 
Mabadiliko yatakuja niwe hai ama nife!
 
Mleta mada tuna shaka na uwezo wako wa kufikiria. Nani Alikuambia CHADEMA wamesusia uchaguzi ni nani? Kauli mbiu yao iko wazi hawajasusia bali wametangaza kuwa kama hakuna marekebisho ya kanuni hakuna uchaguzi. Pia mtoa mada hana uchungu wowote watu kama mdude wanapopotezwa na kuuwawa. Anafurahia sana wapinzani wanaponyanyaswa kama kwamba wao sio Raia wa nchi hii.
 
Kwanini wewe hujatekwa? Ama ni wewe ni muoga, una adabu au unasaliti no reforms no erection. Ndio maana huoni maandamano ya watu wengi wanaoshinikiza kamanda wao aachiwe. Maana yake hoja yao haijafikia kuwa n hadhi ya kitaifa. Wewe hapo Sasa hivi uko mitaani unakunywa bia ili urudi nyumbani kwa watoto wako as if nothing has happened to commander.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…