Uchaguzi 2020 CHADEMA kutikisa Dar kwa siku tatu, Uchaguzi Mgombea Urais Tanzania na Zanzibar

Je lissu atamuunga mkono Membe?
Je Membe atamuunga mkono Lissu?
Kama hawataungana si watagawana kura?
Je itakuwa live?
Membe hana madhala yeyote,hata akigombea Membe hawezi kupata hata kura elfu hamsini,sisi huku mitaani hatumjui labda kama zitapigwa za mitandaoni.
 
Ninajua hapa tunazubaishwa tu, ila wenye Kufuatilia mambo Kiundani tumeshajua kuwa Tundu Antipasi Lissu ndiyo atakuwa CHADEMA Flag Bearer.
 
Kama tittle inavyosemeka ndugu wadau, naanza kwa kutangaza interests kwanza kwamba mimi si shabiki wa chama chochote cha siasa sijawai na natarajia kuwa sitakuwa shabiki in shaa Allaah.


Turudi katika mada yetu, kesho 02/08/2020 mchakato wa kumpata mgombea kupitia chedema utaanza huku makada watatu wakiwania nafasi hiyo.

1.Tundu Antipas Mghwai Lissu

2.Lazaro samwel Nyalandu

3.Rosemary Majinge


Katika wagombea hao watatu nampaka nafasi ya Moja kwa moja Rosemary majinge kuwa mgombea mwenza yaani makamu wa Rais kwa sababu zifuatazo.

i.Rosemary aliwekwa kimkakati juu ya gender balance hivyo hafikiriwi kupata nafasi ya moja kwa moja ya kugombea urais wa JMT.

ii.Wajumbe wa chadema hawamjui Rosemary kwa sababu si mtu wa majukwaani na siyo mwanamke wa prukushani na vuruamai.

ktk nafasi ya urais yoyote anaweza kupita utategemea wajumbe wameamkaje siku ya jumanne.
 
Hapa ndipo tunaukumbuka umuhimu wa Makonda kuwa RC wa Dar, wajumbe wote hawa wangepitishiwa bahasha za khaki wampitishe yeyote bali Tundu Lissu kwa maslahi mapana ya Chama cha Kijani.
 
Naimani Kamati Kuu italeta mgombea mwenye sifa, mwenye uwezo wa kusimamia mambo, anayeelewa mahitaji halisi ya wananchi. asiyekubali kuyumbishwa, anayefahamika kwa wapiga kura, aliye na historia ambayo wengi watatamani kuisikia.
 
Kila LA heri chadema, ushauri. Uwazi ukatawale, haki ikatendeke.wagombea wakahesabu kura wenyewe.pia waombe vyombo vya habari virushe live...
 
Naona vipofu mmeshikana mikono alafu mnashaurana anza kuruka wewe
 
Mbona kama umeshaweka wazi Tundu ndie umtakaye?
 
Kwa mjibu wa katiba ya nchi, kama mgombea urais atatoka Tanzania bara lazima mgombea mwenza atoke Tanzania visiwani and vice versa. Hivyo Rosemary hana sifa hiyo ya kuwa mgombea mwenza.

Hayo majina matatu yapange kulingana na mapendekezo ya kura za wajumbe ambazo Lazaro Nyarandu aliwaacha kwa mbali hao wengine. La sivyo tutakuelewa vingine. Kura za wajumbe lazima ziheshimiwe kama zilivyoheshimiwa zile za CCM kwa kuwang'oa vigogo kama Makonda, Mwakyembe, Mwamri, Lugora, Wasira, Nyerere watatu nk. Wajumbe wa chadema nao walishang'oa vigogo kama Tundu Lissu nk. Hiyo ndiyo demokrasia. Mkienda nje ya hapo chadema itapasuka vipande viwili, kitu ambacho ccm inakisubiri kwa hamu.
 
Wewe akili huna,mgombea akitoka bara mgombea mwenza lazima atoke Zanzibar,kati ya hao watatu hakuna mzanzibar,huo ugombea mwenza huyo Catherine ataupataje?
 
Fomu ya urais ilichapishwa moja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…