Uchaguzi 2020 CHADEMA kutikisa Dar kwa siku tatu, Uchaguzi Mgombea Urais Tanzania na Zanzibar

Sasa ni Rasmi.

Chama kikuu Cha upinzani nchini Chadema kitaanza vikao vyake kwa siku 3 mfululizo kuanzia Jumapili tarehe 2 mpaka Jumanne tarehe 4 katika ukumbi maarufu nchini wa Mlimani City.

Kikao Cha Kamati Kuu kitafanyika kesho Jumapili huku Baraza Kuu likiwa siku ya Jumatatu na Mkutano Mkuu utakuwa siku ya Jumanne.

Agenda Kuu ya vikao hivi ni kuchambua na hatimaye kupiga kura kumpitisha Rasmi mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema.

Tayari wajumbe wa vikao hivi wameshaanza kuwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na shauku kubwa ya kutimiza takwa la kikatiba.

Mchuano mkali kwenye nafasi ya Urais ni Kati ya mafahali wawili Lazaro Nyalandu Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu akipambana na Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na mwanasiasa mashuhuri zaidi kwa Afrika.

Ikumbukwe Chadema ilitikisa nchi siku ya Jumanne wiki hii wakati maelfu kwa maelfu ya watu walipojaa majiani kumlaki Tundu Lissu aliyerejea matibabuni huku kukiwa na maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kumsindikiza mwanasiasa huyo makao makuu ya Chama huku umati huu ukiimba 'Rais' Rais' Rais' kote alikopita ambapo Barabara ilifungwa kwa masaa manne kumsindikiza shujaa huyo.

Sisi wa Molemo Media Kama Sikuzote Tunatarajia kuwaletea matangazo ya moja kwa moja wasomaji wetu wa Jamii Forums ili Dunia kuweza kujua kinachoendelea ndani ya vikao hivyo muhimu.Tuna Imani hatukuwahi kuwaangusha wafuatiliaji wetu.

Wagombea wa CHADEMA ni;

Wakili Simba Neo

Lazaro Nyalandu

Tundu Lissu

Dk.Maryrose Majinge

Wakili Gaspar Mwanalyela

Isaya Mwita

Mchungaji Leonard Manyama
Hapa ndipo ninapoona tofauti kati ya CCM na CHADEMA wakati ccm wakitumia ukumbi wao chadema wanaenda kukodi ukumbi
 
Wanatikisa nani? Au wanajitikisa wenyewe unamaanisha.
 
Hadithi za sungura na fisi et rais wala siyo RAIS
 
Ningekua mpiga kura
kura yangu ningempa Lazaro Nyalandu Anafaa wakati huu KULIKO wakati mwingine wowote ila kwa Zanzibar sidhani Kama CDM wanachao kule unamsimamisha mtu hapati hata kura elfu 50 haina haja
 
Lisu ateuliwe nje ya hapo, kura mtapiga wenyewe
Huo ndio ukweli
Nina uhakika akisimama Lissu hata ACT Watamuunga mkono, sio Nyalandu. Sasa hapa Mbowe alete siasa zake za 2015 kulazimisha Lowassa agombee aone CHADEMA itakavyokuwa kama TLP
 
Mchuano mkali kwenye nafasi ya Urais ni Kati ya mafahali wawili Lazaro Nyalandu Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu akipambana na Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na mwanasiasa mashuhuri zaidi kwa Afrika.
ishajulikana nani atapita, sema wacha watu wafanye mchakato kutimiza matakwa ya demokrasia.
 
IMG_20200801_153107.jpg
 
Je lissu atamuunga mkono Membe?
Je Membe atamuunga mkono Lissu?
Kama hawataungana si watagawana kura?
Je itakuwa live?
 
bangi za jioni:

  1. chadema wakimteua tundu lissu itamlazimu zitto na chama chake waunge mkono juhudi (coalition).
  2. chadema wakimteua nyalandu au mgombea mwengine ni furaha kwa zitto na chama chake.
 
Back
Top Bottom