Sasa ni Rasmi.
Chama kikuu Cha upinzani nchini Chadema kitaanza vikao vyake kwa siku 3 mfululizo kuanzia Jumapili tarehe 2 mpaka Jumanne tarehe 4 katika ukumbi maarufu nchini wa Mlimani City.
Kikao Cha Kamati Kuu kitafanyika kesho Jumapili huku Baraza Kuu likiwa siku ya Jumatatu na Mkutano Mkuu utakuwa siku ya Jumanne.
Agenda Kuu ya vikao hivi ni kuchambua na hatimaye kupiga kura kumpitisha Rasmi mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema.
Tayari wajumbe wa vikao hivi wameshaanza kuwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na shauku kubwa ya kutimiza takwa la kikatiba.
Mchuano mkali kwenye nafasi ya Urais ni Kati ya mafahali wawili Lazaro Nyalandu Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu akipambana na Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na mwanasiasa mashuhuri zaidi kwa Afrika.
Ikumbukwe Chadema ilitikisa nchi siku ya Jumanne wiki hii wakati maelfu kwa maelfu ya watu walipojaa majiani kumlaki Tundu Lissu aliyerejea matibabuni huku kukiwa na maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kumsindikiza mwanasiasa huyo makao makuu ya Chama huku umati huu ukiimba 'Rais' Rais' Rais' kote alikopita ambapo Barabara ilifungwa kwa masaa manne kumsindikiza shujaa huyo.
Sisi wa Molemo Media Kama Sikuzote Tunatarajia kuwaletea matangazo ya moja kwa moja wasomaji wetu wa Jamii Forums ili Dunia kuweza kujua kinachoendelea ndani ya vikao hivyo muhimu.Tuna Imani hatukuwahi kuwaangusha wafuatiliaji wetu.
Wagombea wa CHADEMA ni;
Wakili Simba Neo
Lazaro Nyalandu
Tundu Lissu
Dk.Maryrose Majinge
Wakili Gaspar Mwanalyela
Isaya Mwita
Mchungaji Leonard Manyama