CHADEMA Kutumia Sakata la DP World Kueneza "Hate Speech" Haikubaliki na Ni Kinyume na Maadili ya Nchi na Umoja wa Mataifa

Kumbe na wewe ni mpumbavu kiasi hiki
 
Wewe nae kwa akili kama hizi lazima mtukanwe tu. Imagine mtu anatetea rasilimali za nchi yake ila panatokea wapumbavu flani hivi wasiokuwa na akili badala waungane kutetea, wao wanawatukana wale wanaotetea vya kwao. Tumeshawaambia kuwa hili la bandari mmeyakanyaga. Hakuna Mtz mwenye akili atakaewaelewa! Time will tell. Rejeeni mikataba ya migodi yetu. Raia walipiga kelele ila hawakuskizwa!
 
Ungewakemea kwaza walioapa, huku wameshikilia misahafu, kuwa watalinda maslahi ya nchi, halafu wakageuka kuwa madalali wa kuuza rasilimali za Tanganyika. Waliapa watatenda haki na kutotoa upendeleo wowote, lakini wakazilinda bandari za Zanzibar na kuziuza zaTanganyika. Waliapa kuilinda katiba, katiba inayotamka wazi kuwa mamlaka ya juu kabisa ni umma wa Watanzania, lakini wamejimejifanya miunguwatu, na kutamka wazi kuwa wamefunga masikio, hawana habari kuhusu wenye nchi wanataka nini.

Kwa upande mwingine, nawapongeza viongozi wa CHADEMA kwa kuwa wakweli. Mbaguzi mkuu ni Rais. Aliwezaje kusaini document inayoruhusu uporaji wa bandari za Tanganyika akaziacha za kwao Zanzibar? Ina maana jambo hili halikufanyika kwa bahati mbaya. Mbaguzi ni Rais, kwa nini awaweke wazanzibari kwenye wizara isiyo ya Muungano? Ina maana alikosa mtu kutoka kwa wenye wizara yao, hadi kulazimika kuwachukua watu toka Zanzibar?

Kama kjna wabaguzi nchi hii, basi wa kwanza atakuwa ni Rais.
 
Wapi umewaona wanatumia hate speech?
 
Huyu anaeongea upumbavu hapa ndio Rais si ndio?
 
Hapa mods hawawezi kufuta Kwa sababu ni mwanachama wao katoa lugha ya kudhalilisha kinyume na Maadili Yao
Nionyeshe ulipokemea speech ya Chawa wenu Manara aliposema Bandari ya Dar haiwahusu watu wa mikoani maana ilianzishwa na Waarabu na wamerudishiwa Waarabu!
 
Sijawah kuona mpango mkakati wa CHADEMA zaidi ya kurukia mambo,Mara DP world wakati wao ndiyo waliojinadi na sera za ubinafsishaji wa uwanja wa ndege n.k inakuwaje CCM wanataka kubinafsisha bandari wao wabweke hovyo. Suala la uwekezaji lazima liwe la faida kwa upande wa muekezaji serikali ni watcher ,regulator na collecter msituchanganye. Kwani enclousere system sindo ilimfanya BRITISH kuwa super power!! Na open door policy/marshall plan kwa U.S.A na vyote vilipigiwa kelele.
 
Safi sana Serikali msicheke na nyani
 
Tanzania ya 1985-95 ni tofauti sana na hii ya leo.

Hao wanapiga kelele na wanapata wasikilizaji wenye upeo mpana wa nini kinaendelea usitegemee wao kuwa na uhalali wa kudumu wa kuongea huo ujinga.

CCM wanagusa maisha ya mtu mmoja mmoja hivyo kina Lissu wanadumu na ushujaa wao wa midomoni na humu majukwaani walipo wasomi wachache.
 
Punguza kuweka LINKS.

Hizo videos za Twitter ungedownload ukaupload humu.

Pili punguza lundo la maandishi.

Unaandikaga pumba sana, hala zinakuwa pumba square kwa kujaza maandishi 3000 kusififia watu
 
 
Nyie madalali rudisheni pesa ya muarabu ,hamuwezi kuuza nchi halafu watu wawaangalie tu ,kama mlileta mkataba bungeni ni wazi wananchi lazima waudiscuss kama mlikuwa hamtaki mngeuza kimya kimya tu bandari.
 
Nyie madalali rudisheni pesa ya muarabu ,hamuwezi kuuza nchi halafu watu wawaangalie tu ,kama mlileta mkataba bungeni ni wazi wananchi lazima waudiscuss kama mlikuwa hamtaki mngeuza kimya kimya tu bandari.
Mbona wewe unaangalia tuu huendi kuandamana?
 
Ila ccm kupora chaguzi za nchi hii inakubalika na sheria za umoja wa mataifa.
 
Matusi na kueneza Chuki sio ushujaa unless wewe ni punguani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…