Hakuna mahakama huru linapokuja suala la kubambikiwa kesi na watawala. Toka umejiunga na NCCR hujawahi kuweka sera zao zaidi ya kuitaja cdm ili uzi wako uwe na post nyingi. Yaani uko Nccr, lakini kwa ajili ya nongwa dhidi ya cdm, umejikuta unaitaja zaidi cdm kuliko hiyo Nccr unayojifanya uko. Vuta post zako toka uliposema uko Nccr, kisha search nyuzi zako umeitaja mara ngapi cdm, na umeitaja mara ngapi Nccr. Kwa maneno marahisi ulidhani Nccr itapata mvuto, lakini umeona haina mvuto, na hiyo ccm haina mvuto bali imebaki kushurutisha kukubalika, wakati huohuo cdm ikibaki kuwa na mvuto. Jambo hili naona linakutesa kupita kiasi.
Ni hivi, cdm haitakaa iisifie ccm kwa lolote, na wala haitokaa iisujudie ccm wala mwenyekiti wake. Kuna vyama vinaweza kuisifia ccm na kumsujudia mwenyekiti wake, na vyama hivyo ni vile visivyokuwa na mvuto kama Nccr, Cuf, Tlp nk. Hivi ndiyo vinahitaji hisani ya ccm ili kupata uwakilishi.