Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Watashitakiwa kwa Majina yao binafsi kama wanavyoshitakiwa vibaka wengine, hii ni baada ya kuamuru na kushiriki wizi wa nyaraka za Chadema waziwazi bila kificho chochote.
OCD wa Dodoma ameonekana wazi akishiriki kuvunja ofisi ya Kanda ya kati na kuiba nyaraka kadhaa pamoja na pesa Taslimu, huku OCD wa Kigoma akituhumiwa kuvunja kijiwe cha Chadema na kuiba mlingoti wa bendera na bendera yenyewe ambavyo vyote ni Mali ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Tayari Mawakili wa Chadema wameelekezwa kufungua mashitaka hayo ifikapo Jumatatu saa 2 asubuhi.
Taarifa hii Muhimu imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Mh Benson alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za Chama hicho Kinondoni , pamoja na hayo pia Mh Kigaila amehoji IGP anakotoa mamlaka ya kukamata Wafuasi wa Chadema wanaohudhuria Kesi ya Mbowe Mahakamani, ambapo amemtaka IGP Sirro kuonyesha Kifungu chochote cha Katiba ya Nchi kinachokataza wananchi kuhudhuria kesi Mahakamani kabla hajafunguliwa Mashitaka ya kusababisha fujo isiyo na tija yoyote, kwake binafsi , kwa familia yake wala kwa nchi Jumatatu asubuhi.