CHADEMA kuweni makini na mapokezi ya Lissu wakati huu wa msiba, mnafanya kosa la kiufundi, mtawapa watu mtaji wa kiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu

CHADEMA kuweni makini na mapokezi ya Lissu wakati huu wa msiba, mnafanya kosa la kiufundi, mtawapa watu mtaji wa kiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Salaam wakuu,

Maneno yangu ni machache sana kwa chama kikuu cha upinzani CHADEMA kuwa waachane haraka na mpango wao wa maandamano ya amani/ sherehe ya mapokezi ya mh Tundu A. Lissu siku ya jumatatu ya 27 jul 2020.

Ndugu zangu huu ni mtego ambao umejitokeza kwa bahati mbaya kwenye njia ya CHADEMA wanapaswa kuukwepa haraka iwezekanavyo, nchi ipo kwenye msiba wa kitaifa wa Rais mstaafu, tupo kwenye siku saba za maombolezo, nchi jirani mfano kwenye bendera zinapepea nusu mlingoti, viongozi wa mataifa mbalimbali watakuja hapa kuomboleza pamoja nasi n.k

Sasa kwa hali hii si sahihi kwa CHADEMA kufanya hayo mapokezi; mtakuwa mmefanya Jambo la kijinga na wengi watawadharau kabisa na mtapoteza Imani kwa watu wengi.

Kwenye sakata la kuondoka bungeni kujiweka karantini wakati wa kitisho cha COVID-19 tuliwashauri muachane na mpango ule hamkusikia na hatimae mkajitia aibu kubwa na kudharaulika kwa kiasi kikubwa sana, safari hii pia tunawashauri tena achaneni na huu mpango sio salama kwa ustawi wenu kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu mtapoteza wapiga kura wengi sana kwa sababu hili tukio.

Licha ya hayo mtasababisha mgawanyiko ndani ya Chama kwa wale ambao hawata kubaliana nanyi kuto kuhudhuria msibani badala yake kwenda kwenye mapokezi, ikiwa ubabe utatumika kwenye hili basi hakika Kuna watu watenda kuunga juhudi.

Shitukeni CHADEMA, achaneni na huu mpango mtawapa watu mtaji wa kisiasa bure. Tafakarini upya mkiwa kama CHAMA makini.

Natanguliza hongera zangu kwenu kama mtakuwa wasikivu.
Sisi wanaccm tuna amini Chadema imeshakufa.
 
Katika yote uliyo yasema naomba nikusahihishe kidogo tu kwamba nchi yetu bado haijawa na mgawanyiko wa namna hiyo kama unavyosema hapo, ila utofauti wa kiitikadi lazima uwepo kwenye taifa lolote lile duniani kwasababu watu hawawezi wakawa na mawazo yanayofafana.
Hapo sikuandika mgawanyiko unaohusiana na 'itikadi'.
Mgawanyiko juu ya 'itikadi' hauleti uhasama ndani ya jamii.
 
Waache wawape watu chakusema, yani we bendera zinapepea nusu mlingoti hadi nchi jirani, watu wanaacha shughuli zao za kitaifa kwenye nchi zao huko wanakuja hapa nchini alafu eti wewe mtanzania unaenda kufanya maandamano ya mapokezi.

Sasa wewe "hao nchi jirani" wameacha shughuli zao?.....

Bendera kupepea nusu mlingoni hakuzuii shughuli za watu kuendelea.....

Ndiyo maana shule zinaendelea, sherehe za harusi zinaendelea hazizuiliwi na "bendera nusu mlingoni"...

Mnazungumza kana kwamba mmemuua Mzee wa watu makusudi ili tu kuzuia shughuli ya CHADEMA, right?...
 
Msimba kwani huyo akiyekufa ninani hapa Tz labda kama angekuwa amekufa Mbowe ndo ningekuelewa
Ndio shida ya kujadili na wanaolala na kinyesi kwenye chupi, bado hamjitambui Yaani wewe hujui umuhimu wa Hayati Mkapa kweli mpaka umfananishe na Mbowe kweli?? Mtu wako hajawahi hata kuwa katibu wa wizara leo umfananishe na Mhe Marehemu Mkapa!!
 
Mkuu ukitulia utaona msingi wa hoja yangu ni nini.

Ndugu, wengi tunakusoma. Wengi tuna akili na maarifa kukuzidi wewe. Hoja yako haina msingi wowote. Tumekusoma na kuona kusudi lako...

Hata hujiulizi ni wangapi wamekufa leo, Jana na wengine watazikwa kesho?

Obviously ni wengi lakini kazi za watu mtaani ndani ya kijijini ulipo msiba haziwezi kusimama. Watu wataomboleza huku wengine wanafanya kazi zao....

Kwa hiyo, hapa huna hoja mkubwa. Hicho unachoita "hoja", basically ni "hofu" yako binafsi iliyo na elements zote za ki - propaganda za CCM na watawala....
 
Kwani Vyombo vya usalama havina mawasiliano na Chadema kujulisha hali ya mambo itakavyokua ikiwa kuna uwezekano ama lah?
 
Mama yako
Chizi kweli wewe.chunguza mitaani hakuna mtu ana time na kifo cha mkapa.sikia ipo hivi ukitendea watu mabaya utaliliwa na wanafiki tu tena wanalia uku moyoni wanasema afadhali ameenda
 
Back
Top Bottom