Hapa tusiwe na jasiba ndugu zangu, lengo letu ni kukifanya chama hiki chenye nguvu kwa sasa Tz bara kizidi kuwa na mwelekeo.
Na kwa kuwa jana muungano wa vyama vya upinzani (CUF, TLP NA NCCR) wamekanusha yale Zitto aliyokanusha kuwa Tarime hakukuwa na fujo badala yake wapinzani hao kwa pamoja wamesema kuwa kulikuwa na fujo, basi tunaweza kusema vyama hivi havina nia njema na CHADEMA, Na kwa kuwa mafisadi tayari wameshajipanga kufanya wanavyoweza kukipiga chini chama hiki, sasa basi naona ni vema Mbowe akatangaza kuwa amejiuzulu ili waendelee na uchunguzi wao
Vita ya wazalendo dhidi ya mafisadi inahujumiwa na vita baina ya wanasiasa mufilisi dhidi ya CHADEMA. Mafisadi wanafurahia sana wanapoona vyama vya siasa vikiwashambulia CHADEMA na Mbowe/Zitto/Mnyika/Dr. Slaa nk. Wanawezesha huo mchezo kifedha. Wakati mkiendelea na hako kamjadala ka kipuuzi wao waleee wanaendelea kuchota madini yenu na kuwaibia kwa namna nyingi tu.
Haya endeleeni na haka kamchezo kenu ka hatari.
Fungukeni macho watanzania. hakuna fisadi anayechukia chama chenye nguvu. Wanachukia kuwekewa upinzani kwenye wizi wao. Hiki ndiyo chanzo cha mgogoro wao mkubwa dhidi ya CHADEMA na makamanda wake.
Ndugu zangu wanaJF sisi sote tunafahamu kuwa sasa jamaa wameamka, wamecharuka kwa njia yoyote wanataka kufanya lolote lile ili kutokomeza upinzani Tanzania, na kwa kuwa Mbowe sasa anatazamwa kwa jicho la husuda na wapinzani wenzake na pia *** sasa ushauri wa bure mbowe akae pembeni ili chama kipone
JF mnalitazamaje hili?
wanataka kufanya lolote lile ili kutokomeza upinzani Tanzania,
na kwa kuwa Mbowe sasa anatazamwa kwa jicho la husuda na wapinzani wenzake na pia
*** sasa ushauri wa bure mbowe akae pembeni ili chama kipone
Halafu atakaye kuja mwingine, naye wamtafutie visa naye ajiuzulu, aje mwingine tena wamfanyie janja yao wajiuzulu.
HUJANICONVINCE-TUKO VITANI NO MATTER WHAT!!!!!!!!!!!!!!
WEWE NI CCM UKUBALI USIKUBALI MAWAZO YAKO SI YA KIPIGANAJI WALA MAPINDUZI, UMEKUWA KAMA WALE WAPELELEZI WALIOLETA TAARIFA MBAYA MUNGU AKAWAADHIBU HAPOHAPO!!!!
ALUTA CONTINUE..
Waberoya
Mbowe kawa bwanyenye anatembelea Vogue, huku makamu wake akitumia mkweche gari masaa yote linakazwa nati utafikiri bedford za mkaa toka vigwaza. Matumizi ya fedha hayaeleweki mara ajichotee 175m at anajilipa deni bado anadai chenji imebaki, akha!
Matatizo ya watz ni umasikini, tunahitaji kuongozwa na mtaamu wafedha na uchumi, sio mtu mwenye uzoefu wa kuendesha Danguro (night clab). Ukweli zitto anastahili kuwa Mwenyekiti wa chama, kuliko Mbowe bora Mzee Mtei arudi kushika usukani.
Eddy
Wewe hautuumizi kichwa tunajua wewe ni CCM, na sasa tunajua mna furaha ya ajabu, eddy bila upinzani hapa Tanzania hatutafika, kitendo cha kumuita Mbowe kuwa ni bwenyenye hakika haumtendei haki hata kidogo, mbowe amejitolea kwa ari na mali kulikomboa Taifa ili kidemokrasia ,naomba tumpe heshima yake pale alipo fanya katika taifa letu hili la Tanzania.
Ndugu Isayamwita
Salaam na heshima zako mkuu .Nimesoma bandiko lako tu sijasoma comments za wengine , nilkaona bora nikuombe sana uje na maelezo ya undani ya kwa nini awe Mbowe atoke na Chama kinusurike.Why Mbowe mkuu wangu
Huu ndio uhuru wa JF, na hapa mtoa mada amejijibu hata kabla hajajibiwa nadhani tusome kwa makini alichoandika.
Sasa kama wanataka kutokomeza upinzani, ndio Mbowe ajiuzulu (si Kujizuru) ili awape nafasi watokomeze upinzani? nadhani jibu ni HAPANA, umejijibu kabla.
Kwa kuwa wapinzani ndio wanaoshambulia mpinzani mwenzao, jibu tayari unalo kwamba wao ndio wamejipembua kutoka katika malengo yao ya msingi ya kuwa wapinzani, kwa hiyo jibu lako ni rahisi, wana uhuru wa kwenda huko kwa hao wanaowafanyia kazi. hakuna ajabu yuko Tambwe, yuko Salum Msabaha, yuko Juma Kilimbah, yuko Abass Mtemvu, yupo Festus Limbu, na wengineo ambao wamepata na nyadhifa wasijali waende tu.
Kwa maelezo ya utangulizi, ushauri wako uende kwa kina Mbatia, Lipumba na Mrema ambao hata ubalozi wa Libya na polisi wamewaponda kiaina
Lunyungu,
Mkuu salaam zako nimezipata,
Mkuu kwa kuwa kuna thread moja iliwahi kupostiwa hapa kuwa ndani ya chama hiki kikubwa na cha kitaifa kuwa kina ukabila, na kwa kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kamvulugano ndani ya chama hiki,na kwa kuwa watanzania wengi kimbilio lao ni CHADEMA kwa sasa, ningepenga chama hiki tukijenge kwa sasa, hii ni pamoja na kuepuka yale yanayoweza kuibua maswali mengi kwa watanzania, ndiyo maana nikasema Mbowe ajiuzulu atafutwe mwingine aendeleze gurudumu hili la kupigania demokrasia ndani ya taifa letu hili
Halisi,
Kweli kwa mtizamo wako naona fikra zako bado hazijalitazama jambo hili kwa kina, unajua watanzania wamechoka na siasa mgando, 1995 walimshangilia Mrema huku wakidhani kama wangeleta mabadiliko ndani ya taifa lao, watanzania hawa wamekata tamaa,
Usisahau ni kipindi ambacho CHADEMA imeanza kukubalika kitaifa na watanzania wamekikubali chama hiki na hata CCM wanajua, sasa pale ccm wanapoanza propaganda zao ili kukiua chama hiki hakika tuwe macho, halisi usisahau hapa jamvini wamejaa kwelikweli,tuwe macho.
Na kama chama hiki cha CHADEMA kitapoteza mwelekeo tusitalajie upinzania ndani ya taifa letu, itatuchukua muda wa miaka mingi hadi kupata chama mbadala.
Na ndiyo maana nikasema Mbowe akae pembeni, tunao wasomi wengi wenye nia njema na taifa letu wanaweza kukiongoza na tukaendeleza mapambano haya na hawa mafisadi.
Mkuu Isayamwita
Watu wa kumleta mtu mwingine ni wana Chadema ambao wanashiriki kwa uhakika kila jambo ndani ya Chadema na sisi wengine wa JF siamini kama tunaweza kusema tu Mbowe akae pembeni kwa light words like that ikakubalika . Ingia Chadema jenga hoja ndani ya Vikao na wapelekee mawazo haya haya usikie wanasemaje na labda uongezee mawazo zaidi ya haya .Huu ni ushauri tu .