CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
ajiuzulu ali awanufaishe hao mahusuda au kukunufaisha chama?
 
holalaaa!!!hata mimi nathani kuna chitu haiwezekani leo mtu hajafa mnakuwa negative nae then akifa positive ,it means leo mnapigana na mafisadi theni mkikamata usukani nanyi mtakuwa mafisadi?mh!! in dillema
 
Unajuaa nini kimsingi lazima tufahamu huyo anayetoa sijui niseme huja au wazo kwa jamaa ajiuzu lazima utuaambie
1) Kwanini unadhani ajiuzulu nini sababu
2) Anadhani wananchi nikimaanisha wanachadema wanataka kiongo wao ajiuzulu
manake chama (chadema) hakiwezi kufanya maamuzi makubwa kama hayo kwasababu upande fulani unataka kutokomeza upinzani
3) Akijiuzulu je? nini mwelekeo wa chama nani anachukua nafasi yake ?
4) Je anakubalika na wananchi
5)Nini mtazamowake ipi historia yake
6)Ipi mikakati yake kwa maslahi ya Taifa na chama
hayo ni baadhi tu masali mengi ambayo lazima tuhoji kabla yakufikia fira hizo
 
Mbowe kawa bwanyenye anatembelea Vogue, huku makamu wake akitumia mkweche gari masaa yote linakazwa nati utafikiri bedford za mkaa toka vigwaza. Matumizi ya fedha hayaeleweki mara ajichotee 175m at anajilipa deni bado anadai chenji imebaki, akha!

Matatizo ya watz ni umasikini, tunahitaji kuongozwa na mtaamu wafedha na uchumi, sio mtu mwenye uzoefu wa kuendesha Danguro (night clab). Ukweli zitto anastahili kuwa Mwenyekiti wa chama, kuliko Mbowe bora Mzee Mtei arudi kushika usukani.
 
Mbona anapokodi helkopta lwa ajili ya kam[eni za chama hatakiwi kujiuzulu?
 
There are no commonsensical points of view which can make Mboye to resign. Tanzanian we must be very careful for our prose otherwise we will provide an opportunity for the malevolence to continue grabbing our resources without any trepidation .Among the party in Tanzania which have proven to be responsible for the people is CHADEMA.Almost the corruption tittle-tattle were ascended by the opposition leaders. So if we won’t be careful the death of late Chacha Wangwe it could taken by the wickedness of CCM to devastate the opposition in Tanzania.P’se watch out.
 
Ningeelewa kama ungesema Mrema, Mbatia na Lipumba wajiuzulu. Hivi kweli tunaweza kusimama na kusema kuwa TLP ni tishio kwa serikali ya Tanzania? Jamani tuseme ukweli, kuna nguvu yoyote ndani ya NSSR Mageuzi leo? na kweli unaweza kusema kuwa CUF huku kwetu bara ina impact yoyote? Hawa walioshindwa kuvifanya vyama vyao kuwa vya maana ndio wanaotakiwa wajiuzulu ili ije damu mpya itakayoungana na akina Mbowe, Zitto, Slaa wa CHADEMA katika kuleta mapinduzi ya kweli hapa nchini.

Tuseme ukweli tu CHADEMA ndiyo tishio la CCM na kimekuwa hivyo chini ya uongozi wa MBowe sasa leo unasema Mbowe ajiuzulu, je unataka CHADEMA kiwe kama TLP au NSSR? Jemedari Mbowe na wenzako msikate tamaa uzi ni ule ule.
 
mmh! wakati zitto anakomaa na karamagi kuhusu buzwagi bwanyenye mbowe alikuwa anazurura London. Chadema imeshikiliwa na zitto na marehemu wangwe, leo zitto akihama itafanana tu na TLP, kwanza 2010 hawapati hata mbunge mmoja.
 
Hapa tusiwe na jasiba ndugu zangu, lengo letu ni kukifanya chama hiki chenye nguvu kwa sasa Tz bara kizidi kuwa na mwelekeo.
Na kwa kuwa jana muungano wa vyama vya upinzani (CUF, TLP NA NCCR) wamekanusha yale Zitto aliyokanusha kuwa Tarime hakukuwa na fujo badala yake wapinzani hao kwa pamoja wamesema kuwa kulikuwa na fujo, basi tunaweza kusema vyama hivi havina nia njema na CHADEMA, Na kwa kuwa mafisadi tayari wameshajipanga kufanya wanavyoweza kukipiga chini chama hiki, sasa basi naona ni vema Mbowe akatangaza kuwa amejiuzulu ili waendelee na uchunguzi wao

Halafu atakaye kuja mwingine, naye wamtafutie visa naye ajiuzulu, aje mwingine tena wamfanyie janja yao wajiuzulu.

HUJANICONVINCE-TUKO VITANI NO MATTER WHAT!!!!!!!!!!!!!!

WEWE NI CCM UKUBALI USIKUBALI MAWAZO YAKO SI YA KIPIGANAJI WALA MAPINDUZI, UMEKUWA KAMA WALE WAPELELEZI WALIOLETA TAARIFA MBAYA MUNGU AKAWAADHIBU HAPOHAPO!!!!

ALUTA CONTINUE..

Waberoya
 
Vita ya wazalendo dhidi ya mafisadi inahujumiwa na vita baina ya wanasiasa mufilisi dhidi ya CHADEMA. Mafisadi wanafurahia sana wanapoona vyama vya siasa vikiwashambulia CHADEMA na Mbowe/Zitto/Mnyika/Dr. Slaa nk. Wanawezesha huo mchezo kifedha. Wakati mkiendelea na hako kamjadala ka kipuuzi wao waleee wanaendelea kuchota madini yenu na kuwaibia kwa namna nyingi tu.

Haya endeleeni na haka kamchezo kenu ka hatari.
Fungukeni macho watanzania. hakuna fisadi anayechukia chama chenye nguvu. Wanachukia kuwekewa upinzani kwenye wizi wao. Hiki ndiyo chanzo cha mgogoro wao mkubwa dhidi ya CHADEMA na makamanda wake.

Hakika ni mambo ya kushangaza sana, kweli leo hawa akina Lipumba, Mrema na wengineo wanataka kupata umaarufu eti kwa kupitia kifo cha huyu wangwe, ina fikia mahali wanapeleka ushahidi kwa Mwema, kweli inasikitisha sana.
Ila naomba wajue kuwa CHADEMA kwa sasa ni chama cha kitaifa, ndicho chama mbadala ya CCM.
 
Ndugu zangu wanaJF sisi sote tunafahamu kuwa sasa jamaa wameamka, wamecharuka kwa njia yoyote wanataka kufanya lolote lile ili kutokomeza upinzani Tanzania, na kwa kuwa Mbowe sasa anatazamwa kwa jicho la husuda na wapinzani wenzake na pia *** sasa ushauri wa bure mbowe akae pembeni ili chama kipone

JF mnalitazamaje hili?

Huu ndio uhuru wa JF, na hapa mtoa mada amejijibu hata kabla hajajibiwa nadhani tusome kwa makini alichoandika.

wanataka kufanya lolote lile ili kutokomeza upinzani Tanzania,

Sasa kama wanataka kutokomeza upinzani, ndio Mbowe ajiuzulu (si Kujizuru) ili awape nafasi watokomeze upinzani? nadhani jibu ni HAPANA, umejijibu kabla.

na kwa kuwa Mbowe sasa anatazamwa kwa jicho la husuda na wapinzani wenzake na pia

Kwa kuwa wapinzani ndio wanaoshambulia mpinzani mwenzao, jibu tayari unalo kwamba wao ndio wamejipembua kutoka katika malengo yao ya msingi ya kuwa wapinzani, kwa hiyo jibu lako ni rahisi, wana uhuru wa kwenda huko kwa hao wanaowafanyia kazi. hakuna ajabu yuko Tambwe, yuko Salum Msabaha, yuko Juma Kilimbah, yuko Abass Mtemvu, yupo Festus Limbu, na wengineo ambao wamepata na nyadhifa wasijali waende tu.

*** sasa ushauri wa bure mbowe akae pembeni ili chama kipone

Kwa maelezo ya utangulizi, ushauri wako uende kwa kina Mbatia, Lipumba na Mrema ambao hata ubalozi wa Libya na polisi wamewaponda kiaina
 
Halafu atakaye kuja mwingine, naye wamtafutie visa naye ajiuzulu, aje mwingine tena wamfanyie janja yao wajiuzulu.

HUJANICONVINCE-TUKO VITANI NO MATTER WHAT!!!!!!!!!!!!!!

WEWE NI CCM UKUBALI USIKUBALI MAWAZO YAKO SI YA KIPIGANAJI WALA MAPINDUZI, UMEKUWA KAMA WALE WAPELELEZI WALIOLETA TAARIFA MBAYA MUNGU AKAWAADHIBU HAPOHAPO!!!!

ALUTA CONTINUE..

Waberoya

Hakika umenishangaza sana, unadhani kuwa mimi ni ccm, pole sana, CHADEMA ni chama cha kitaifa kwa sasa, chama chenye nguvu Tanzania bara, na hivyo mimi kutoa mawazo yangu kuwa Mbowe AJIUZULU NI Ili hao ccm wakose Mshiko, na si vinginevyo.

Usisahau wasomi wote wenye mlengo wa kushoto wote wanakiona CHADEMA kama mkombozi wao.

Ni kweli Mbowe amefanya makubwa sana hasa kukuza Demokrasia hapa nchini na kweli anakubalika sana ila kwa kuwa vijikashifa hivi vimeanza kumuandama ni bora sasa yeye akae pembeni akiache chama kisipate mtikisiko.
 
Ndugu Isayamwita
Salaam na heshima zako mkuu .Nimesoma bandiko lako tu sijasoma comments za wengine , nilkaona bora nikuombe sana uje na maelezo ya undani ya kwa nini awe Mbowe atoke na Chama kinusurike.Why Mbowe mkuu wangu
 
Mbowe kawa bwanyenye anatembelea Vogue, huku makamu wake akitumia mkweche gari masaa yote linakazwa nati utafikiri bedford za mkaa toka vigwaza. Matumizi ya fedha hayaeleweki mara ajichotee 175m at anajilipa deni bado anadai chenji imebaki, akha!

Matatizo ya watz ni umasikini, tunahitaji kuongozwa na mtaamu wafedha na uchumi, sio mtu mwenye uzoefu wa kuendesha Danguro (night clab). Ukweli zitto anastahili kuwa Mwenyekiti wa chama, kuliko Mbowe bora Mzee Mtei arudi kushika usukani.

Eddy
Wewe hautuumizi kichwa tunajua wewe ni CCM, na sasa tunajua mna furaha ya ajabu, eddy bila upinzani hapa Tanzania hatutafika, kitendo cha kumuita Mbowe kuwa ni bwenyenye hakika haumtendei haki hata kidogo, mbowe amejitolea kwa ari na mali kulikomboa Taifa ili kidemokrasia ,naomba tumpe heshima yake pale alipo fanya katika taifa letu hili la Tanzania.
 
Pole sana Eddy naona kweli una usongo na upinzani na beef na Mbowe .CCM ina matajiri wakubwa na tena wenye uzoefu wa kutuibia pesa zetu kila mara mbona Nchi inawashinda na Chama chao kina shida kubwa ?
 
Ndugu Isayamwita
Salaam na heshima zako mkuu .Nimesoma bandiko lako tu sijasoma comments za wengine , nilkaona bora nikuombe sana uje na maelezo ya undani ya kwa nini awe Mbowe atoke na Chama kinusurike.Why Mbowe mkuu wangu

Lunyungu,

Mkuu salaam zako nimezipata,
Mkuu kwa kuwa kuna thread moja iliwahi kupostiwa hapa kuwa ndani ya chama hiki kikubwa na cha kitaifa kuwa kina ukabila, na kwa kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kamvulugano ndani ya chama hiki,na kwa kuwa watanzania wengi kimbilio lao ni CHADEMA kwa sasa, ningepenga chama hiki tukijenge kwa sasa, hii ni pamoja na kuepuka yale yanayoweza kuibua maswali mengi kwa watanzania, ndiyo maana nikasema Mbowe ajiuzulu atafutwe mwingine aendeleze gurudumu hili la kupigania demokrasia ndani ya taifa letu hili
 
Huu ndio uhuru wa JF, na hapa mtoa mada amejijibu hata kabla hajajibiwa nadhani tusome kwa makini alichoandika.

Sasa kama wanataka kutokomeza upinzani, ndio Mbowe ajiuzulu (si Kujizuru) ili awape nafasi watokomeze upinzani? nadhani jibu ni HAPANA, umejijibu kabla.

Kwa kuwa wapinzani ndio wanaoshambulia mpinzani mwenzao, jibu tayari unalo kwamba wao ndio wamejipembua kutoka katika malengo yao ya msingi ya kuwa wapinzani, kwa hiyo jibu lako ni rahisi, wana uhuru wa kwenda huko kwa hao wanaowafanyia kazi. hakuna ajabu yuko Tambwe, yuko Salum Msabaha, yuko Juma Kilimbah, yuko Abass Mtemvu, yupo Festus Limbu, na wengineo ambao wamepata na nyadhifa wasijali waende tu.

Kwa maelezo ya utangulizi, ushauri wako uende kwa kina Mbatia, Lipumba na Mrema ambao hata ubalozi wa Libya na polisi wamewaponda kiaina

Halisi,
Kweli kwa mtizamo wako naona fikra zako bado hazijalitazama jambo hili kwa kina, unajua watanzania wamechoka na siasa mgando, 1995 walimshangilia Mrema huku wakidhani kama wangeleta mabadiliko ndani ya taifa lao, watanzania hawa wamekata tamaa,

Usisahau ni kipindi ambacho CHADEMA imeanza kukubalika kitaifa na watanzania wamekikubali chama hiki na hata CCM wanajua, sasa pale ccm wanapoanza propaganda zao ili kukiua chama hiki hakika tuwe macho, halisi usisahau hapa jamvini wamejaa kwelikweli,tuwe macho.

Na kama chama hiki cha CHADEMA kitapoteza mwelekeo tusitalajie upinzania ndani ya taifa letu, itatuchukua muda wa miaka mingi hadi kupata chama mbadala.

Na ndiyo maana nikasema Mbowe akae pembeni, tunao wasomi wengi wenye nia njema na taifa letu wanaweza kukiongoza na tukaendeleza mapambano haya na hawa mafisadi.
 
Lunyungu,

Mkuu salaam zako nimezipata,
Mkuu kwa kuwa kuna thread moja iliwahi kupostiwa hapa kuwa ndani ya chama hiki kikubwa na cha kitaifa kuwa kina ukabila, na kwa kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kamvulugano ndani ya chama hiki,na kwa kuwa watanzania wengi kimbilio lao ni CHADEMA kwa sasa, ningepenga chama hiki tukijenge kwa sasa, hii ni pamoja na kuepuka yale yanayoweza kuibua maswali mengi kwa watanzania, ndiyo maana nikasema Mbowe ajiuzulu atafutwe mwingine aendeleze gurudumu hili la kupigania demokrasia ndani ya taifa letu hili

Mkuu Isayamwita
Watu wa kumleta mtu mwingine ni wana Chadema ambao wanashiriki kwa uhakika kila jambo ndani ya Chadema na sisi wengine wa JF siamini kama tunaweza kusema tu Mbowe akae pembeni kwa light words like that ikakubalika . Ingia Chadema jenga hoja ndani ya Vikao na wapelekee mawazo haya haya usikie wanasemaje na labda uongezee mawazo zaidi ya haya .Huu ni ushauri tu .
 
Halisi,
Kweli kwa mtizamo wako naona fikra zako bado hazijalitazama jambo hili kwa kina, unajua watanzania wamechoka na siasa mgando, 1995 walimshangilia Mrema huku wakidhani kama wangeleta mabadiliko ndani ya taifa lao, watanzania hawa wamekata tamaa,

Usisahau ni kipindi ambacho CHADEMA imeanza kukubalika kitaifa na watanzania wamekikubali chama hiki na hata CCM wanajua, sasa pale ccm wanapoanza propaganda zao ili kukiua chama hiki hakika tuwe macho, halisi usisahau hapa jamvini wamejaa kwelikweli,tuwe macho.

Na kama chama hiki cha CHADEMA kitapoteza mwelekeo tusitalajie upinzania ndani ya taifa letu, itatuchukua muda wa miaka mingi hadi kupata chama mbadala.

Na ndiyo maana nikasema Mbowe akae pembeni, tunao wasomi wengi wenye nia njema na taifa letu wanaweza kukiongoza na tukaendeleza mapambano haya na hawa mafisadi.

Mawazo yako yana maana kubwa hasa kwa hali ya sasa ya Tarime. Kwa kweli Chadema ina kazi sana kushinda Tarime chini ya Mbowe baada ya CCM kuungana na CUF, TLP na NCCR Mageuzi kumpinga Mbowe.

Lakini, katika vita ni lazima kuwapo na maamuzi magumu na ya kudumu na si vyema sana kukubali kuzidiwa nguvu na upepo. Alipojiuzulu Lowassa, wafuasi na mashabiki wake na hata yeye binafsi (hadi sasa) waliamini kwamba kujiuzulu kwake kutamuibua SHUJAA ambaye atafanikiwa kuwamaliza maadui zake na yeye kurudi kwa kishindo katika siasa dakika za majeruhi na kuibuka kuwa RAIS..... Mawazo hayo SI SAHIHI maana tayari kujiuzulu kwake kumetoa picha halisi ya kuwa FISADI na hilo ni gumu kulifuta kama ambavyo sasa SUMAYE anapata shida kufuta tuhuma zilizopikwa na MTANDAO. Dhambi ya kuchafuana imewarudia kina EL kwa kasi na imekua sumu kwao. Tukirudi kwenye mada, kwa sasa Mbowe akijiuzulu itakuwa ni KUWAPA nguvu wapinzani wake na wenye malengo ya kusambaratisha upinzani wa kweli na itakua vigumu kuiepusha CHADEMA na kujiuzulu kwa Mbowe na hivyo Chadema itakufa, jambo ambalo ni hatari kwa demokrasia, maslahi na USALAMA wa TAIFA. Hakuna anayetaka hili litokee kwa sasa. Kwa sisi tusio na vyama tunadhani ni vyema Mbowe akajipanga na kufanya mambo kadhaa ya msingi yatakayomuwezesha kukabiliana na wimbi la kampeni chafu hasa kwa kuwa Watanzania walio wengi wana imani na Chadema na wamegundua kuna njama za kundi dogo la wana-CCM wanaotaka kuua upinzani wa kweli.

Ni vyema kwa sasa Mbowe akapambana kwa mbinu zote na si kujiuzulu ili kuwachanganya. Ni bora kupoteza hata jimbo la Tarime (japo iko kazi) ili kuimarisha upinzani kuelekea 2010 na si kwa maslahi ya wakati huu pekee au kwa kukubali kufuata upepo na kucheza ngoma inayopigwa na MAFISADI.

Mutakumbuka dua yangu ya wakati wa RICHMOND na leo naifufua tena.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI. MUNGU ULIYETUKUKA IVUNJE YAO DHAMIRA MAFISADI, WASIWEZE KUSIMAMA, WASIONE JAPO WANA MACHO, WASISIKIE JAPO WANA MASIKIO, WASITEMBEE JAPO WANA MIGUU, WAENDELEE KUSAMBARATIKA NA KUPUKUTIKA
 
Mkuu Isayamwita
Watu wa kumleta mtu mwingine ni wana Chadema ambao wanashiriki kwa uhakika kila jambo ndani ya Chadema na sisi wengine wa JF siamini kama tunaweza kusema tu Mbowe akae pembeni kwa light words like that ikakubalika . Ingia Chadema jenga hoja ndani ya Vikao na wapelekee mawazo haya haya usikie wanasemaje na labda uongezee mawazo zaidi ya haya .Huu ni ushauri tu .

Lunyungu,
Hakika labda haujanisoma kabisa, ama wewe haujaelewa, siasa ya nchi hii, kwa kuwa CCM wanatumia siasa chafu ndani ya chama hiki, na laiti ungejua nadhani ungenielewa, CCM kwa sasa wanajua kuwa watanzania wamewachoka hawawataki kabisa, watanzania wengi wameamua kikuunga chadema mkono, na sasa kwa kuwa ccm wameligundua hilo basi wameanza siasa zao chafu ili kukiharibu chama hiki, tuwe macho,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom