CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?


Mpaka Kielewe.

Mbona maneno haya ni ya Mbowe kwenye statement yake iko Klh News yaani ume copy na kupaste. lete maneno yako.
 


Kamati Kuu Ya Chadema Inaundwa Na Wenyeviti Wa Mikoa Waliochaguliwa Mikoani Mwao.
Viongozi Sita Wa Kitaifa Yaani Mwenyekiti,makamu Bara Na Visiwani ,katibu Mkuu Na Manaibu Wake, Wajumbe 5 Waliochaguliwa Na Mkutano Mkuu, Wajumbe 5 Walioteuliwa Na M.kiti Na Kuidhinishwa Na Baraza Kuu, Kasome Katiba Acha Kupotosha.
 

Asante Mtanzania maneno yako msumari unatakiwa uwe jaji,kwanini usiwe Special Advisor wa Mbowe?
 
Madai ya Chacha ya ukabila ni kweli kabisa!haiwezekani katika nafasi saba kama sikosei za uwakilishi wa viti vya kuteuliwa wabunge wote ni kanda ya kaskazini kasoro wawili!je walishindwa kubalance hili?utleast kila kanda basi maana nafasi hazitoshelezi kila mkoa!
Mtu ukisema ukweli watu wanakuchukia!Ila afadhali maana hii inapunguza imani ya wanachama kwa chama chao!Hii itatoa mwanya kwa CCM kuendelea kudunda!Tatizo tunavihitaji sana vyama vya upinzani ili kuendeleza Taifa letu na kuufichua ufisadi!CHADEMA rekebisheni mambo yenu haraka iwezekanavya!
Asante!
Hollo
 
Kama Mrema na Marando vile au? ama kweli Mungu anaipenda CCM chama kilichokuwa na dalili ya kufika mbali wameanza kutimuana! MUngu ibariki CCM! Mungu tunaomba afukuzwe na mwingine Chadema! Lol
 

Mimi nakuambia hii ni ile picha ya Mrema na Marando inarudia hapa. Madai ya ukabila kama wakati ule. Inaoneka hii silaha ya ukabila ndiyo inawasambaratisha wapinzani.

Baada ya hapo itabidi wamtimue zitto na slaa ambao nao si wachagga.

Kidumu chama cha mapinduzi na udumu usalama wa taifa kwa kazi nzuri.
 

Nimekwambia kuwa Ngaiza na Baregu walichaguliwa na Mbowe naomba upinge hili? ni wewe uliyesema jana kuwa Ngaiza katumia diplomasia zake za UN kumuelewesha Wangwe hakuelewa,Baregu akatumia Conflict knowledge kumsomesha Wangwe bado Wangwe hakuelewa, Makani atatumia sheria lakini vyote havikusaidia,

ukitazama wajumbe hao ni matunda ya Mbowe, kisheria Wangwe ana haki ya kususia kikao kama hicho kwani hakutakuwa na fair hearing na zaidi itakuwa mambo ya BIASNESS ambayo kweli yamefanya kazi na yanaendelea kufanya kazi hapa JF.

Mtanzania
Naomba utusaidie kuliweka sawa hili ili MK aelewe vizuri.
 
Kama Mrema na Marando vile au? ama kweli Mungu anaipenda CCM chama kilichokuwa na dalili ya kufika mbali wameanza kutimuana! MUngu ibariki CCM! Mungu tunaomba afukuzwe na mwingine Chadema! Lol

We mwenyewe si unaona sasa hivi hakuna tena mambo ya EPA wala richmondu hapa JF.

hawa wapinzani wanacheza na chama kubwa la kijani.

Kidumu chama cha mapinduzi.
 

Kazi nzuri mgagagi, wape vidonge wapinzani hao. Wao walidhani ccm tumelala kumbe tulikuwa tunawatafutia nafasi tu. Hakikisha kuwa hii thread ndiyo inajadiliwa ili waumbuke. Mambo ya EPA ni story ya jana.
 
THE CHACHA CV.KUTOKA KWENYE MTANDAO WA BUNGE.

University of Dar es Salaam Certificate (Edu.) 1978 1979 CERTIFICATE
Kinondoni Muslim Secondary O-level Education 1973 1974 SECONDARY
Nyaroha Secondary School O-level Education 1969 1970 SECONDARY
Magoto Primary School Primary Education 1966 1968 PRIMARY
Rosana Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY

AJIRA.
Tarime Municipal Councilor (Tarime Town) 2001 2005
NCCR - Mageuzi Regional Secretary (Mara Region) 1998 2000
Africa Mashariki Gold Mines Field Supervisor 1994 1997
LACOP Interservices Co. Ltd Director 1983 1989
German Volunteer Service Language Tutor 1980 1982
National Bank of Commerce (NBC) Accounts Clerk 1977 1977

KIONGOZI WA MAHALI AMBAPO HAJASOMA.
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Chairman (Mara Region) 2002 2005
NCCR-Mageuzi Secretary General (Mara Region) 1998 2000
CHADEMA Chairman (Tarime District) 1994 1998
TANU Youth Chairman (Mkwawa High School) 1975 1976

KUNA MASWALI YA KUJIULIZA HUYU ALIENDA JE MKWAWA WAKATI HAKUSOMA .

SOURCE WWW.PARLIAMENT.GO.TZ
 
Weka na ya MBOWE!
 
Gembe ,kusema kuwa mimi ni mchagga its very wrong.

Usifanye ,usiwaze na wala usiandike kitu kwa hisia ,kuwa eti nami ni mchagga huu ni upotoswaji wa wazi kwani kwanza wewe hata hunijui wala sura yangu huijui.

Acha kupotosha .

Kwi kwi kwi!!!!

Mkuu, hata mimi nafikiri wewe ni Mchaga, kama sio kweli basi samahani.

Unajua inatosha kuwa na kumbukumbu nzuri na kuunganisha mambo ili kujenga profile ya mtu hapa JF. Hata mtu akibadili jina wengine tunajua tu maana maandishi yanasaliti.

Pia kujua mtu anatoka wapi sioni ubaya wowote. Mimi kwetu Kyela, Mbeya kwi kwi kwi!!
 
Mi naona Safari ya kusafisha chama kwaajili ya 2010 ndio imeanza..Tukaze buti lakini tusimwonee mtu.
 
si unaona hapo katika o level ni 1973 hadi 1974!je 1975 hadi 1977 alifanya nini?inawezekana ndo alikuwa Mkwawa high school!Maana UDSM kaingia 1978 refer to the CV!
BTW leo ndo mnahoji hilo si alikuwa makamu wa chama chenu?ulikuwa wapi kuquestion hicho kitu?!Kweli CCM NI BABA LAO!
 


Wanachofanya sasa ni political vendetta, yale yale ya akina Kingunge, inasikitisha sana.
 
Mi naona Safari ya kusafisha chama kwaajili ya 2010 ndio imeanza..Tukaze buti lakini tusimwonee mtu.


huku kweli kusafisha maana sasa mtakuwa weupe kiasi ambacho hamchaguliki. au hamuuziki



ndugu zetu siasa si lelemama, sasa nnategemea mtafahamu wananchi watanzania wako makini ktk kuchagua nani awakilishe taifa.


hivi ikiwa mmeshindwa kuvumiliana na kuekana sawa kwa haya madogo ingekuwaje mbowea angekuwa rais na wange waziri mkuu ?

nnaamini mzee wa wapuki na kikundi chake hawana sifa za uongozi ni watu wanaoongoza kwa kutumia hisia badala ya maaarifa, poleni sana

wazee wengi wa chama chenu walikihama tukazungumza hapa mkajidai ooh ccm imewanunua. tumehonga mapesa.

oo makamba kachaguliwa ili awanunuwe wapinzani, sasa semeni na huyu tumemnunua.

nyinyi wenzetu kwanza kubalini bado ni wadogo nakwa kukusaidieni 2010 tutakuwekeni benchi nyote na kisha mtajifunza siasa huko nje maana kupata hivyo vijiruzuku kidogo tu mshaanza kuvutana mashati na kutofautiana kiasi hicho


kufa kwa chadema ni faida kwa ustawi wa demokrasia​
 

Nimependa hayo maandishi kwenye blue, nccr na tlp vimekufa, chadema nayo itakufa karibuni, baadaye mambo yote yanahamia cuf zanzibar maana bara cuf imekufa. Baada ya muda si mrefu kutabaki vyama vya ajabu ajabu dhaifu kama chaustawi wa jamii... kwi kwi kwi

Kidumu chama cha mapinduzi na udumu usalama wa taifa kwa kazi nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…