CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Jamani CHADEMA mie naona Wangwe ana point naomba mfuate democrasia acheni propaganda..mnatukatisha tamaa watu tunaowafuatilia siasa zenu
 
Kwa maoni yako haya, inabidi Wangwe atafute mwanasheria mpya au sio?


Naona afanye hivyo maana kwanza wote wameshangaana ameanza Lisu akamwaga mboga na Chacha kamwaga Ugali.Hata hivyo huo ni mchezo kama soka mnapoingia uwanjani na rafiki yako ama ndugu yako mkawa timu pinzani mnakwatuana viatu ile mbaya na mkitoka uwanjani ushwahiba upo palepale.

Sasa mkikwatua mviatu uwanjani na mkatoka nje ya uwanja bado mkawa maadui jua viatu vile vilikua si viatu vya kimchezo bali WAZEE WA UHASAMA.
 
Jamani CHADEMA mie naona Wangwe ana point naomba mfuate democrasia acheni propaganda..mnatukatisha tamaa watu tunaowafuatilia siasa zenu

Mi naona ni bora vyama vya siasa Tanzania vifanye kama vyama vya USA. Wabunge na madiwani wasiwe viongozi wa vyama, kazi ya kuongoza vyama ifanywe na watu binafsi. Mfano Marekani, Howard Dean hana nafasi nyingine kisiasa zaidi ya uenyekiti wa Democrats.

Chacha awahudumie wananchi wa Tarime na aache kutumiwa na ccm kuharibu upinzani kama Marando alivyotumiwa na ccm kuvuruga NCCR.
 
... inabidi Wangwe atafute mwanasheria mpya au sio?

Ndio.

Siku Wangwe akipanda kizimbani kutoa ushahidi, mimi kama ni wakili wa yule anaeshindana na Wangwe nitaiambia mahakama jamani huyu mtu hana credibility.

Wakiniuliza kwa nini nitasema Wakili wake mwenyewe kasema client wake ni mwongo.

Halafu nitatoa vielelezo vya interview ya Tundu Lisu na Mwnjj wamsikie wakili anammaliza client wake, halafu mwisho anasema nitamtetea mahakamani kwa sababu tu tuna kiti cha ubunge tumekitolea jasho na damu.

Sio kwa sababu anamwamini Wangwe. Wakili hamwamini client!
 
Ndio.

Siku Wangwe akipanda kizimbani kutoa ushahidi, mimi kama ni wakili wa yule anaeshindana na Wangwe nitaiambia mahakama jamani huyu mtu hana credibility.

Wakiniuliza kwa nini nitasema Wakili wake mwenyewe kasema client wake ni mwongo.

Halafu nitatoa vielelezo vya interview ya Tundu Lisu na Mwnjj mahakama imsikie anammaliza client wake, halafu mwisho anasema nitamtetea mahakamani kwa sababu tu tuna kiti cha ubunge tumekitolea jasho na damu.

Sio kwa sababu anamwamini Wangwe. Wakili hamwamini client!

Na wao jasho lao na damu sio wanamtetea POOR CHACHA ila wanachotetea ni ile MILIONI 66 kwa mwezi ifike pale makao makuu.
kama sijakosea naomba mnirekebishe ni kua CHAMA kinapata ruzuku kutokana na wabunge iliyonao.Kama ni hivyo kumbe Wangwe akishindwa ubunge pale makao makuu watapunguze matanuz.

WEWe uliona mahelkopita kule KITETO ukafikiri wanampenda sana jamaa yule BIG NO jibu ni ili kale karuzuku kafike angalau M100 kwa mwezi.
 
Kulingana na maelezo ya Lisu, wabunge watano kati ya sita wana uhusiano wa karibu na mkoa wa Kilimanjaro. Watatu Wachaga, mmoja Mpare, mwingine kaolewa na Mchaga. Mmoja tu anatoka Kigoma.

Hapo kazi ipo kweli kweli, hivi CHADEMA mlikosa wanawake wengine wa kuchukua hizo nafasi?

Hapo mmejiingiza kwenye midomo ya simba kwa kujitakia kabisa. Unafikiri CCM watasema nini kwa mpangilio huo wa wabunge wa kuteuliwa.

Hata mimi ningelikuwa CHADEMA ningelalamikia upendeleo huo wa wazi.

Pili, Lisu kama mwanasheria wa Wangwe, hatakiwi kuongelea kabisa mambo ya yeye kumwakilisha Chacha kwenye radio. Hii ndio matatizo ya kuchanganya kazi binafsi za mtu na mambo ya siasa.
 
Zitto Kabwe bado hajaja hadi muda huu? Kitila yuko taabani anaomba Zitto aje kuthibitisha UNCCR NA UTLP wa Kitila.
 
Kulingana na maelezo ya Lisu, wabunge watano kati ya sita wana uhusiano wa karibu na mkoa wa Kilimanjaro. Watatu Wachaga, mmoja Mpare, mwingine kaolewa na Mchaga. Mmoja tu anatoka Kigoma.

Hapo kazi ipo kweli kweli, hivi CHADEMA mlikosa wanawake wengine wa kuchukua hizo nafasi?

Hapo mmejiingiza kwenye midomo ya simba kwa kujitakia kabisa. Unafikiri CCM watasema nini kwa mpangilio huo wa wabunge wa kuteuliwa.

Hata mimi ningelikuwa CHADEMA ningelalamikia upendeleo huo wa wazi.

Pili, Lisu kama mwanasheria wa Wangwe, hatakiwi kuongelea kabisa mambo ya yeye kumwakilisha Chacha kwenye radio. Hii ndio matatizo ya kuchanganya kazi binafsi za mtu na mambo ya siasa.

Maoni yangu
LISU alichojaribu kuoanisha ni ili kutuaminisha kua uamuzi uliotolewa ni sahihi na ya kwamba wangwe ndio mkorofi ya kwamba kajitolea kumsaidia ktk shida na ktk kupata ubunge lakini jamaa hana shukurani.

Hizo combinasheni za kuunga vipande vipande ili kutuaminisha ndio unamuona katoka nje ya maada na kumwita mtovu wa nidhamu kwa kuvunja kanuni za bunge ,mimi sielewi kama Lisu ni msemaji wa Bunge ama alitaka kutuaminisha nini?? Sasa sijui humo bungeni anavunja kanuni za CHADEMA tu ama vipi sielewi.

Ndio maana unaona kaenda mbali zaidi kutuambia ubia wao ulianza lini hii ni sehemu ya kuunga vipandevipande.

HIzi tuhuma ni za kupikwa.
 
Mwanakijiji,

Vipi namba zinakugonga? Laki moja kwa kila wilaya hata ukiwa na wilaya 300, bado ni milioni 30 tu kati ya milioni 66 kwa mwezi.

Mwanakijiji, asante sana kwa haya mahojiano maana kila mwenye masikio amesikia na unaweza kuona ukweli uko wapi.

Hivi vyama vyetu ndio maana wengine havitufai maana tutafukuzwa tu, ukiwa na independent minds huwezi kudumu kwa muda mrefu kwenye haya mavyama yetu kuanzia CCM mpaka hao CHADEMA.
 
Mwanakijiji,

Vipi namba zinakugonga? Laki moja kwa kila wilaya hata ukiwa na wilaya 300, bado ni milioni 30 tu kati ya milioni 66 kwa mwezi.


Labda mwakijiji alikua tayari nae kaingia na desa kwi kwi kwi kwi

Harafu CHADEMA wanafanya uhuni kabisa wa wazi hawawezi tuma laki moja tu tena ktk sehemu 27.

EURO 60 huu uhuni

Harafu pale wanamatumizi gani haswa kama hakuna uchaguzi maana Lisu amesema kuchapisha na kutengeneza Bendera DUUUUUUUUUUUUU.
 
Chacha Vs Lisu
kwa nilivyowasikiliza Chacha yuko sahihi kwa 99.9999999% harafu Lisu yupo sahihi kwa 0.0000001%.
Kwanini Hoja zote za Lisu hazina ushaihidi kwa namna nyingine 99.99999999% ni Uongo na upikaji wa habari.

Chacha
Amesema wabunge watano kati ya sita wanatoka mkoa mmoja kati ya mikoa 26. kitu ambacho ni 100% ukweli

Amesema nenda makao makuu ukaone wafanyakazi kitu ambacho ni 100% na akasema kama unabisha nenda mwenyewe ukajionee.

Amesema Chadema inafahamika japo hata haijajishughurisha kujienga matawi kitu ambacho ni 80% sahihi.

Amesema kama ni Yuda asigejishughurisha kujenga nyumba tokea msingi huko mara ili aje aibomoe kitu ambacho ni 90% ukweli.

Amesema kama wanapata milioni 66 kwa mwezi na wanakiona ni kidogo ambacho hakiwezi pelekwa matawini kwanini wanaendekeza Elkopita?? kitu ambacho ni 100% sahihi.

Na akasema mikoani walikua hawapeleki kabisa hata Tsh 0/= yani ilikua NULL mpaka alipoingia madarakani ndio wakaanza kupeleka baadhi ya maeneo,kitu ambacho Lisu alianza kujihami na muelewa utaelewa tu chacha anaongea ukweli 100%.

Kuhusu kabulu kuongea na chacha tena kumpa pole za msiba ndio wa campitalize kua anakihujumu chadema kwa kutoa siri za chama eti kwa vile ni CCM ,Chacha amezidi kuhoji kwanini wamuone kama mtoa siri kwa kuongea na mbunge wa ccm na kumtuhumu anahujumu siri za chama na kumuacha DR SLAA ambaye mkewe ni Kanda wa CCM na diwani wa CCM.?? hapo Chacha kaonyesha hoja hiyo ni feki .Na chacha akizidi kuonyesha ulewa mkubwa kwa kusema wao na CCM sio maadui Eti wa kutokua marafiki ama mawasiliano hoja zao ndio adui zinapogongana 100% .Ila kimaisha wao ni ma CDA yani wote watoto wa nyumbani.

Chacha kasema huo ukabila alikua hajauona nami naongeza wenda sio malengo yao CHADEMA kusheheni kabila moja Na akazidi kusema alisikia mtaani na kwa wanachama ikabidi aliangalie na akakuta kuna ukweli nami nasema huo uvumi nimeusikia siku nyingi sana hata kabla ya chacha kua mbunge.

CHADEMA acheni kukimbilia kusimamisha watu kwa sababu ya masilahi yenu binafsi angalieni hayo matatizo anayoyaongelea Chacha namyapatie ufumbuzi na sio kukimbilia kumtimua.
Hayo mambo ya siri ktk CHAMA mnayoyaita ndio ufisadi wenyewe huo kama chacha alivyosema.

Naomba maneno haya uyalete kule kwenye thread ya Chadema wamsimamisha Wangwe ambako nawaburuza sana wanakuja na majina mia, mkamap weka kule huu mchango ili niwamalize kabisa.
 
Naomba maneno haya uyalete kule kwenye thread ya Chadema wamsimamisha Wangwe ambako nawaburuza sana wanakuja na majina mia, mkamap weka kule huu mchango ili niwamalize kabisa.


Mkuu,'
Kumbe nia yako si kutafuta ukweli bali ni kuwamaliza CHADEMA? Kazi kweli kweli!
 
Ndio.

Siku Wangwe akipanda kizimbani kutoa ushahidi, mimi kama ni wakili wa yule anaeshindana na Wangwe nitaiambia mahakama jamani huyu mtu hana credibility.

Wakiniuliza kwa nini nitasema Wakili wake mwenyewe kasema client wake ni mwongo.

Halafu nitatoa vielelezo vya interview ya Tundu Lisu na Mwnjj wamsikie wakili anammaliza client wake, halafu mwisho anasema nitamtetea mahakamani kwa sababu tu tuna kiti cha ubunge tumekitolea jasho na damu.

Sio kwa sababu anamwamini Wangwe. Wakili hamwamini client!

wanasheria wengi Tanzania sio waamini na hawafuata kanuni za uwakili Lamwai alifungiwa kwa jambo hilo,na Tundu Lissu hafai kuwa wakili kwanza hatakiwi kuongea na mtu au chombo kisichojulikana kisheria(Klh news) na kutoa siri za mteja wake.

hivi akiulizwa Lissu mahojiano uliyoyatoa kwenye redio yalikuwa baina yako na mteja wako tupe jina la mtangazaji wa redio iliyochukua mahojiano yenu,atasema simjui au anaitwa Mwanakijiji, mahakama ikitaka kumuhoji mwanakijiji itampa wapi? huyu bwana alihudhuria kozi ya sheria lakini si Mwanasheria. Lawyer wengi hawakubali kujadili kesi kwenye simu labda iwe mwisho wa kesi imetoka hukumu hapo ndipo unaweza kusema mwenendo wa kesi ulikuwaje.
 
Mkuu,'
Kumbe nia yako si kutafuta ukweli bali ni kuwamaliza CHADEMA? Kazi kweli kweli!

Kumaliza ni kuwashinda kwa hoja katika thread ile ambayo nina uhakika na ninachochangia, wao wanamumunya maneno tu, na nimesema nawaburuza yaani nawapeleka mbio kwa hoja ya subject ya Wangwe sio Chadema as a whole. kiswahili somo gumu,usichoke kuuliza.
 
Mwafrika wa Kike,


Sikiliza maelezo ya Lissu alipohojiwa na Mwanakijiji...Kumbuka naelewa zivuri kuwa Kilimanjaro ni strong hold ya Chadema lakini swali naloweza kujiuliza hivi kweli wanahitaji wabunge watu kati ya sita wakati wananchi wengi wa Tanzania hutazama maswala haya kwa rangi zake!..
CUF walikuwa na kila sababu ya kuwa na waislaam wengi ktk chama chao (Zanzibar) lakini sio kulingana na maono ya Watanzania wengi hasa wasiokuwa waislaam. Je, mtu akiuliza swali hilo huoni kama ni muhimu jibu liwe ktk mtazamo mpana zaidi ya kile unachoona wewe..

Mkandara.

Maneno ya Mkamap yapitie,atakayeamua kubisha na kusema kuwa usawa Chadema ana lake jambo.
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=15050&page=3
 
Kumaliza ni kuwashinda kwa hoja katika thread ile ambayo nina uhakika na ninachochangia, wao wanamumunya maneno tu, na nimesema nawaburuza yaani nawapeleka mbio kwa hoja ya subject ya Wangwe sio Chadema as a whole. kiswahili somo gumu,usichoke kuuliza.

Unasubiriwa na MWK kutoa vizibiti kule kwenye ile thread.
 
Unasubiriwa na MWK kutoa vizibiti kule kwenye ile thread.

Shahidi namba moja-Zitto Kabwe
shahidi namba mbili-Augustine Mrema.
shahidi namba tatu-Sheikh Kassim Mtopea
shahidi namba nne -James Mbatia.
kuna Regista za Nccr na TLP vyote ni ushahidi.
 
Mimi wakuu naomba kutoa nyongeza tu hapa,

ukweli ni kwamba Chadema kama chama tunachokiaminia sana kwa siasa Bara, kwenye hili la Wangwe, wamechemsha sana, tena ni kwa sababu nyingi, ingawa kwangu ya muhimu kubwa ni moja tu, nayo ni wamekurupuka, tunasema wamekurupuka kwa sababu hatutaki kuamini kuwa this is the way they do their business, tena serious ones kama hii ya kumsimamisha makamu wa mwenyekiti wa chama, aliyechaguliwa only seven months ago,

Simtetei Wangwe, wala simjui vizuri kwa karibu, lakini ninazo tepu nyingi sana za video na majadiliano bungeni, anaoenakana kuwa kama mlevi mlevi hivi sometimes, kwa sababu hakuna wakati hata mmoja anweza kutoa hoja zake bila kukaripiwa na Spika, na huwa hana hoja nzito za marekebisho wala solutions zaidi ya maneno mengi ya kimtaani taani yasiyokuwa na ukweli, na kila akimabiwa na Spika kuondoa kauli huwa hana ubishi bali kuondoa, sasa hii inashusha heshima ya mbunge ndani ya bunge, na hasa wananchi anaowawakilisha,

However, tuliposikia kuwa amechaguliwa kuwa Veep wa Chadema, wengi tulishangaa sana kwamba how? Lakini sasa hii ishu ndio inatuambia kuwa hata kwenye kuchaguliwa kwakwe kulikuwa na walakini, lakini pia haina maana kuwa hana hoja ndani ya Chadema, ingawa ninasema tena kuwa ni kazi ya Chadema, kulitatua hili na wakiweza walimalize bila kelele, ingawa ukweli unabaki pale pale kuwa hii ni PR disaster ambayo itawachukua muda sana kuifuta,

Ni PR disaster, kwa sababu kwanza the timing haikuwa sawa katika kipindi cha bunge na hasa hoja za ufisadi, pili mwenyekiti wa Chadema amekosea sana kutolipa umuhimu mkubwa na kuli-handle kwa busara hili la tatizo, viongozi wote wa juu wa Chadema, pia hawakuwa makini kwenye kuamua na kulielezea hili tatiozo kwa taifa, mpaka sasa bado mnaendelea kujikanyaga kanyaga, jaribuni kuwa makini sana hasa in the future,

makamu aliyechaguliwa miezi saba wa chama kikubwa cha siasa, kama Chadema hasimamishwi mbio mbio namna hii wakuu, hivi majuzi timu ya mpira wa magogo ya Mets, imefanya kosa kama hili la Chadema, kwa kumfukuza kocha aliyekuwa hapendwi na washabikli wote wa timu hiyo, lakini kitendo cha kumfukuza saa kumi za usiku tena akiwa hotelini na timu yake safarini California, kimesababisha wale wote wasiompenda kulalamika kuwa ameonewa sasa Mets tena wanahangaika kujaribu kufanya damage control lakini aibu tayari,

Wangwe ninaamini kuwa anaweza kuwa na matatizo mengi tena makubwa, lakini the way Chadema, walivyoi-handle hii ishu sasa wanamfanya anakuwa shujaaa, naona wanajaribu kila njia hapa kuweka damage control, lakini wakuu mnapwaya sana, labda muiache tu hii ishu wananchi waseme kwanza msikilize tu, muende huko mkajadili na kuweka ufumbuzi, lakini msiruhusu hii ishu ikaja kwenye media tena, kama mnaweza,

Ni ushauri wangu wa bure tu!
 
Shahidi namba moja-Zitto Kabwe
shahidi namba mbili-Augustine Mrema.
shahidi namba tatu-Sheikh Kassim Mtopea
shahidi namba nne -James Mbatia.
kuna Regista za Nccr na TLP vyote ni ushahidi.


Chadema watume maeneo 40 yani kila mkoa angalau uwe na vituo viwili Harafu kila kituo watume milioni moja.wao makao makuu wabakie na milioni 26 kwa mwezi.
Jamaa wanakula bila kusaza .

Hilo fungu la hela za kutengeneza bendera na kuchapa makaratasi ni majukumu ya kila kituo hivyo kama fungu hilo lipo tuseme milion 20 wanagawa kwa vituo 40 kila kituo kinapata laki tano kwa ajili ya shughuri hiyo,hapo kwanza huduma inafika kwa wananchi na kwa urahisi zaidi.SWALI kwanini makao makuu wang'anganie shughuri zote wafanye wao??

Harafu huyu Mbowe mwenye sera ya Majimbo yani ku decentralize serikali mbona anashindwa kukadecentralize ka CHADEMA.
Hapo ndipo utagundua uhuni wa watafuta madaraka.
 
Mwanakijiji,
Nilichosema hapo nyuma ni mtazamo wangu ambao sio lazima Chadema waufuate, kisha kama ulivyohojiana na Lissu amesema mwenyewe kuwa wabunge walioteuliwa kutoka Mkoa wa kilimanjaro/Wachagga ni WATATU..hapo mkuu hujaweka hesabu ya wale walioshinda hivyo wapo watu watakao kerwa na sura hiyo.. Chacha Wangwe ni mmoja wapo na nina hakika ana watu nyuma yake ambao leo wanaitwa washabiki hali binafsi nalitazama swala hili kwa fikra huru na kuona kile ambacho Viongozi wa Chadema hawakukiona..
Pia ktk swala la CUF sio jinsi CUF na Uongozi wake wanavyojisikia isipokuwa ni mtazamo huru ambao unatoka pembe zote za Tanzania..Wananchi wengi ikiwa ni pamoja na hapa kijiweni wamesha sema mara kibao kuhusiana na CUF na kwa uhakika hakuna kilichowapa hisia hizo isipokuwa ni kutokana na nafasi zinazotolewa.. Mkusanyiko wa fikra hizo ndio hujaza hizi fikra duni za Ukabila, Udini, ama jinsia na mara nyingi sio swala la kuwepo mgao wa 50/50 isipokuwa ni kuwepo wawakilishi toka pande zao..
Mathlan, Tanzania ina mikoa mingi lakini kati ya mikoa hiyo kuna majimbo manne ama sita makubwa. Hivyo kumweka mwakilishi wa kila jimbo ingekuwa kipaumbele zaidi kwa sababu Tanzania hadi leo mwakilishi hutazamwa CV yake toka kabila, dini na makazi yake. Siku zote mkuu ni muhimu kumzawadia yule aliyekupenda nakwa kufanya hivyo kunampa mapenzi zaidi kwako. Ni mchezo wa kisiasa ambao hauna tofauti na Mapenzi ya kimwili. Huwezi kumnunulia binti vitu ati kwa sababu kakukataa, atakulamba na kukufanya chuma Ulete maisha yako yote, lakini kama unataka kumvuta binti huyo huyo basi mtunze vizuri yule aliyekutunuku, salaam zitafika kwa hao walioweka makufuli yao. Hivyo binafsi naamini kuwazawadia majimbo yaliyoshindwa kwa bahati ama kwa kuibiwa kura ndio ilikuwa njia nzuri zaidi kushinda kutazama nani mwenye uwezo wa kuzungumza bungeni ama ukaribu na viongozi. Ndio picha inayoonekana.

Na kuhusu CCM siku zote nimesema ni muhimu kwa vyama vya Upinzani kuepuka mabaya yanayotendwa na CCM na kuyafanya kuwa kigezo cha hoja. Kuwatolea wao mfano nadhani ni makosa makubwa kwa sababu siku zote humu ngoma yetu ni kuwachambua CCM hao na kusema makosa yao. Leo Chadema wafganye kama CCM tuanze kusema mbona CCM nao wanafanya hivyo hivyo hali asilimia 90 ya mada za humu ndani ni kuwashtumu CCM kwa utaratibu mbaya. Chadema wanatakiwa kuwa mfano bora na nadhani wana kila nafasi ya kujirekebisha kwa sababu wanasikiliza zaidi ya CCM ambo wameziba masikio yao kwa pamba ili wapte usingizi..Na ukweli ni kwamba CCM hawana haja ya kuweka 50/50 ya wabunge wao kwani wameshika mikoa yote tayari hivyo wanachoongezea ni kuchopeka watu hapa na pale kulingana na agenda zao. Na kilichompa sifa Kikwete ni kwamba alitazama unyonge uko wapi Kichama?.. akagundua kuwa bado ni swala la wanawake.. Mkuu, akawajaza ujinga (kile walichokitaka), leo husikii kelele za wanawake kuhusiana na wawakilishi wa kike...Hakuwa na ulazima wa kufanya hivyo hata kidogo.

Hadi sasa hivi ktk swala hili la Ukabila ndani ya Chadema ambalo ndilo madai yanayokera sio tu toka kwa Chacha Wangwe nimeyasikia muda mrefu tena hapahapa kijiweni na sijasikia jibu linaloweza kuwaridhisha wananchi. Pengine Chacha Wangwe kaliibua toka humu... who knows! Kwa hiyo binafsi pamoja na kwamba sipendi kuamini hivyo isipokuwa nashindwa kupinga hoja ya Wangwe kutokana na hali halisi... it's true kuna wachagga watatu, mwingine Mpare bado ni Kilimanjaro na mmoja toka zanzibar lakini mke wa mtu aliyetoka Kilimanjaro. Mimi naweza kusema sioni connection yoyote na malengo ya Ubunge kutokana na madai ya Wangwe lakini sii wote wanaolitazama swala hili kama mimi..
Sifahamu vizuri viongozi wa Chadema waliwachagua watu hao kwa kufuata vigezo gani lakini kusema kweli inaweza kujenga mawazo tofauti kabisa ktk vichwa vya Watanzania na pengine mgogoro mkubwa uliotokea ndani ya chama ni pale ChaCha Wangwe alipotaka wabunge wa toka sehemu nyingine wapewe nafasi ya kuteuliwa badala ya wale waliokuwepo jambo ambalo hata kama aliwaahidi watu wa Tarime, ambayo ni kazi yake kama mbunge.. kaiwakilisha kwa chama na hakukubaliwa. Hivyo ni muhimu vionmgozi wa chama kumpa jibu Chacha Wangwe la kuridhisha zaidi badala ya kumwita yeye majina mengi kama CCM wanavyomwona Dr. Slaa naZitto. Nina hakika kabisa kama dr. Slaa na Zitto wangekuwa CCM wangeisha fukuzwa maradakani wakionekana kama ni waharibifu wa chama..Hii haina maana hoja zao hazina msingi kwa wananchi...

Kwa kumalizia tu mkuu, CCM wajanja sana.. wanaelewa wazi kuwa Lowassa, Kiaramagi na wengine wote wame smell lakini hawawezi kuwaondoa ndani ya chama hata kidogo kwa sababu kufanya hivyo ni kupunguza nguvu ya chama. Kikwete anaweza kabisa kuwasimamisha wahalifu wote Uanachama na hata kuwapeleka Mahakamani lakini gharama yake itakuwa uchaguzi ujao.. Trust me, hoja ya kuwafukuza viongozi ndani ya chama itaondoa kabisa imani ya wananchi kwa chama isipokuwa Kikwete mwenyewe anaweza kushinda. Na CCM ikisha kufa ktk majimbo ndio imetoka!.. Kikwete hawezi ku risk kabisa tambala hilo ni upumbavu mkubwa kisiasa.
 
Back
Top Bottom