CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

nimekwambia mpigie Wangwe na umuulize kama sio kweli kuwa kila mwezi wilaya yake inapewa laki nne kwa mwezi.

Huyu si ndio utamwamini? mpigie atakupa majibu yeye ndipo uamini.

Hapana mimi namwamini mwanasheria Lisu
sina haja ya kumpigia mimi nabofya KLHnews napata WAngwe kasema laki moja na Lisu kasema laki moja .Labda uniconvice upya kua aliyeongea na KLHnews sio Lisu wala Wangwe,hapo ndipo nitakua na sababu ya kumpigia.

Mkuu mimi sifungamani na upande wowote ila naangalia tu maelezo na kutoa maoni yangu,Nakutokana na maelezo niyoyasikia yapande mbili naona kabisa Chacha ndiye mkweli maana maelezo yake yanaenda na VIVID examples na sio uvumi na hisia za LISU.
 
Nimekwambia Wilaya ya Tarme inapewa laki nne kwa mwezi.

Hii ni mkakati sasa usitake kila mmoja aseme nimeamua kusema kwa sababu ninajua na nina uhakika na hili jambo.

unataka nikueleze vipi unielewe?

tafuta kwa Mhe.Wangwe mwenyewe na muulize tangu July 2007 kabla hata hajawa makamu mwenyekiti Wilaya ya Tarime ilikuwa inapewa Laki Nne kila mwezi akanushe ama akubali.

Naamini kuwa unaweza kuchukua jitihada binafsi kuutafuta ukweli kama hukubaliani na huu wa kwangu.
 
% fulani Naamini unasema ukweli na pia na % naamini wewe ni Mr Mbowe Nakuomba usikilize KLHnews na vizuri upo mtandaoni.

Kama unayoongea ni ukweli basi mimi muono wangu ni kua MLIKUA MNAFANYA HUJUMA ktk hilo ,kwanini mbona wote wawili walilikwepa kuliongelea hilo na wote kwa pamoja na kwa mda tofauti na watu waliotofautiana wakasema mkoani kunapelekwa laki moja.something here hiden!!!!!!!!

Ila mimi nawaombeni nyie CHADEMA mfanyieni kazi malalamiko ya WANGWE hata kama yeye akiamua kukiacha chadema lakini malalamiko yake ktk chama chenu ni ya msingi mno.
 
Mara baada ya uchaguzi tulikaa kama chama kufanya kikao cha kuweka mpngo wa chama kuelekea mwaka 2010. Moja ya suala tulilokubaliana ni kusaidia chama ngazi ya chini kufanya kazi zao. Tuliamua kugawa rasilimali za chama kulingana na matokeo ya uchaguzi kwani hata hiyo ruzuku inapatikana kutokana na idadi ya kura. Wilaya zote ambazo CHADEMA inaongoza Halmashauri zinapewa sh 400,000 kila mwezi. Wilaya zenye madiwani kati ya 4 - 8, zinapewa shs 200,000 na wilaya nyingine zote shs 100,000. Hivyo mgawo wa ruzuku upo siku nyingi na chochote cha kusema pessa ya ruzuku haiendi wilayani sio kweli. Ruzuku inatumika tu kama silaha na propaganda lakini watu wa wilayani wenyewe wanajua suala hili.

Zitto
 
Mimi sio Mbowe, hakuna kilichofichwa ila jua kuwa vitani huwezi kuweka mbinu zako hadharani.

Ndio maana nikakutaka umuulize Wangwe kuwa wilaya yake inapewa laki nne kila mwezi.
 
Asante Zitto kwa maelezo mazuri.
Huyu Mkamap na uccm wake atakataa hata haya maelezo maana yeye anataka watu waache kujadili wizi BoT badala yake wajadili pumba zake.
 
% fulani Naamini unasema ukweli na pia na % naamini wewe ni Mr Mbowe Nakuomba usikilize KLHnews na vizuri upo mtandaoni.

Kama unayoongea ni ukweli basi mimi muono wangu ni kua MLIKUA MNAFANYA HUJUMA ktk hilo ,kwanini mbona wote wawili walilikwepa kuliongelea hilo na wote kwa pamoja na kwa mda tofauti na watu waliotofautiana wakasema mkoani kunapelekwa laki moja.something here hiden!!!!!!!!

Ila mimi nawaombeni nyie CHADEMA mfanyieni kazi malalamiko ya WANGWE hata kama yeye akiamua kukiacha chadema lakini malalamiko yake ktk chama chenu ni ya msingi mno.

Haya mambo ya kutaja ID za watu hapa JF ni kinyume na sheria za mtandao huu. Wewe Mkama unataka kufungiwa kisha uanze kupigapiga kelele. Mbona wewe mimi nafahamu (ninaamini kuwa ni nani) lakini sijakutaja?
 
Mara baada ya uchaguzi tulikaa kama chama kufanya kikao cha kuweka mpngo wa chama kuelekea mwaka 2010. Moja ya suala tulilokubaliana ni kusaidia chama ngazi ya chini kufanya kazi zao. Tuliamua kugawa rasilimali za chama kulingana na matokeo ya uchaguzi kwani hata hiyo ruzuku inapatikana kutokana na idadi ya kura. Wilaya zote ambazo CHADEMA inaongoza Halmashauri zinapewa sh 400,000 kila mwezi. Wilaya zenye madiwani kati ya 4 - 8, zinapewa shs 200,000 na wilaya nyingine zote shs 100,000. Hivyo mgawo wa ruzuku upo siku nyingi na chochote cha kusema pessa ya ruzuku haiendi wilayani sio kweli. Ruzuku inatumika tu kama silaha na propaganda lakini watu wa wilayani wenyewe wanajua suala hili.

Zitto

Zitto.. hii mifano ndiyo iliyokosekana katika tamko lenu. Nilivyomuelewa Wangwe baada ya kumbana kidogo ni kuwa yeye anataka ruzuku iende wilaya zote hata ambako hakuna wabunge/madiwani ili zitumike kuinua chama. Kwangu hiyo ni hoja tofauti kwani mara nyingi inapozungumzwa ilikuwa inaonekana kama fedha zote zinaishia "makao makuu".

Kama kuna fedha inapelekwa Tarime kila mwezi ina maana haiwezekani kuwa fedha zote zinaishia makao makuu. Lakini zaidi wilaya/halmashauri zinazopokea fedha toka Chadema wao ndio wangecounter madai ya Wangwe.
 
huu si mtindo mzuri, imani yako ya nani yuko nyuma ya jina hapa ishikiliwe wewe mwenyewe. Kama ungetaka kujua ni nani ungemuuliza chembe akuambie kama anataka kukuambia.
 
Haya mambo ya kutaja ID za watu hapa JF ni kinyume na sheria za mtandao huu. Wewe Mkama unataka kufungiwa kisha uanze kupigapiga kelele. Mbona wewe mimi nafahamu (ninaamini kuwa ni nani) lakini sijakutaja?

Mimi naitwa Peter Mkama =>kifupi mkamap
Kama kutaja ID nikosa basi mimi naomba nifungiwe wiki moja pia namuomba masamaha niliye mkwaza .
 
Zitto.. hii mifano ndiyo iliyokosekana katika tamko lenu. Nilivyomuelewa Wangwe baada ya kumbana kidogo ni kuwa yeye anataka ruzuku iende wilaya zote hata ambako hakuna wabunge/madiwani ili zitumike kuinua chama. Kwangu hiyo ni hoja tofauti kwani mara nyingi inapozungumzwa ilikuwa inaonekana kama fedha zote zinaishia "makao makuu".

Kama kuna fedha inapelekwa Tarime kila mwezi ina maana haiwezekani kuwa fedha zote zinaishia makao makuu. Lakini zaidi wilaya/halmashauri zinazopokea fedha toka Chadema wao ndio wangecounter madai ya Wangwe.

Hapo mwanakijiji nadhani watakuelewa vizuri maana wewe ni mwanahabari.Kimsingi na mimi hoja yangu ipo hapohapo
 
Una haki ya kutaja ID yako tu siyo ya mwingine.

Nimekuelewa mkuu lakini hizo ni ishara pia za kunguru
Hatuwezi kupigana vita kwa kujifichaficha mpiganaji anajitokeza wazi anapigana akiuwawa kifo kimemkuta vitani na si kitandani kwa kuficha ID.

Siri hua chanzo cha uovu mara nyingi ukisikia mtu anakwambia hii ni siri 90% ni uovu .Ok ila hayo ni mawazo yangu.

Mara nyingi mimi hua nachukulia mpiganaji wa siri ni YUDA anauma huku na kule.
 
mkamap... siyo wapiganaji wote wako mstari wa mbele, na wakati mwingine ni wale walio mstari wa nyuma ambao majina na nafasi zao hazijulikani ndio wana impact kubwa. Ukienda kwenye jengo la CIA utakuta kuna mahali ambapo wanawakumbuka maajenti waliokufa katika kazi zao. Maajenti ambao majina yao yanabakia sirini. Utaona wameweka nyota tu.

Hawa ambao ni "nameless" wanamchango mkubwa sana katika mapambano ya kuhakikisha nchi kama America inaendelea kuwa huru na yenye nguvu. Hawahitaji kujitaja majina yao, hawahitaji kujulikana bali kazi yao tu ndio inaonekana. Ndio maana hata Tanzania sheria inakataza kuwataja kwa majina maafisa wa Usalama wa Taifa (maajenti).

So, siyo kila siri ni ufisadi, bali kuna siri nyingine ni za lazima katika kushinda vita. Jifunze kutoka vita ya pili ya dunia ni jinsi gani kamandi za siri na maofisa wa siri walivyoweza kupenyeza habari za pande zinazopigana.
 
Mimi sio Mbowe, hakuna kilichofichwa ila jua kuwa vitani huwezi kuweka mbinu zako hadharani.

Ndio maana nikakutaka umuulize Wangwe kuwa wilaya yake inapewa laki nne kila mwezi.

Sawa Mkuu nimekuelewa sasa naamini Wangwe na Lisu hawako makini ktk masuala ya CHAMA.
Nawatakieni kila jema ktk kukijenga chama chenu .
 
Naam Ni Kweli Hicho Ni Chama Chako Na Si Chama Cha Wanachama Na Ndio Unafanya Utakavyo Asante Kwa Kutwambia Ukweli

mwenda wazimu usiyejua kiswahili kumbe siyo chama chake ni cha nani wakati yeye ni mwenyekiti, bila chadema huo ufisadi mngeujuaje wanafiki wakubwa nyie mliolaaniwa
 
Bw. Wangwe alisema kufukuzwa kwenye wadhifa huo ni mpango mahususi uliopangwa na agenda kubwa iliyo nyuma yake ni uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho unaofanyika mwaka huu.

" Mwenyekiti alitamka wazi (wakati wa kikao cha Kamati Kuu) kuwa siwezi wala sitaki kufanya kazi na makamu mimi, najiuzulu au yeye ajiuzulu" alisema Bw. wangwe na kueleza kuwa msimamo huo uliwashinikiza wajumbe wa Kamati Kuu kumng'oa madarakani.

Najua kweli JF haihusiki na ushabiki wa vyama vya siasa ila hii kweli jamani ndio utaratibu kwenye vyama vyetu? Siasa sasa inakwenda wapi jamani? Yaani Mhe. Mwenyekiti anasema tuu hawezi kufanya kazi na Msaidizi wake? Ha, ha, ha sasa naona usanii unaanza badala ya kujipanga tuendeleze kwasha moto upande wa pili tunaanza kutiana vidole vya mcho wenyewe, KULE UPANDE WA PILI KUMESHAKUBALI JAMAANI MIGONGANO YA NDANI YA NINI TENA?
 
Kwakweli watu wengine wanachekesha sana.
Hivi wewe kichwamaji unapouliza kuwa kwani lazima chacha wangwe awe makamu mwenyekiti? nami nakuuliza, kwani lazima mbowe awe mwenyekiti? Sio sahihi kutaja kuwa jimbo la tarime ccm wanalinyemelea na watalichukua 2010, kwa kuwa unajaribu kutushawishi tuamini kuwa chacha wangwe hafai kuwa kiongozi. Unatakiwa kufahamu kuwa siku zote ccm hawapati usingizi wanawaza na kuwazua kuwa ni namna gani wataweza kuyarejesha majimbo yote kwenye himaya yao.
inawezekana kweli chadema iko tarime tu, ingawa sikubaliani nawewe kwa hilo lakini tujiulize imekuwaje kigoma mjini?hii ilikuwa ngome imara ya chadema, sasa imerudi ccm.Hivi viugomvi na chuki za ndani kwa ndani huko chadema ndizo zinawarudisha nyuma.
Tukubali tusikubali, inaonekana dhahiri kuwa kuna tatizo hapo chadema na ubaguzi unatajwa sana katika hicho chama.Hata Paul Kyara wa SAU amewahi kuzungumzia suala hilo.Kuna watu wanodhani kuwa wao pekee ndio wanastahili kula matunda ya chadema hawataki kuona mtu mwingine akiwabugudhi.
chacha wangwe alikuwa amesha weka bayana kuwa anakusudia kugombea uenyekiti, hilo ndilo limemtisha mbowe!maana tunaambiwa kuwa ameamua kukatisha masomo kule hull uingereza ili kuinusuru nafasi yake ya kuruka na helikopta.
Chadema inatakiwa kuvumiliana sio lazima watu wote wawe na mawazo ya aina moja na mwenye mawazo mbadala asichukuliwe kama msaliti au mtoa siri.
Mbona inajulikana kuwa zitto kabwe ana mahusiano na mawasiliano ya karibu na warioba, JK, EL na wana ccm wengine lakini mbona yeye haambiwi msaliti?Kwanini wangwe awe msaliti kwa kuongea na walid kabouru?
hapa ndipo pana walakini.
 
Mara baada ya uchaguzi tulikaa kama chama kufanya kikao cha kuweka mpngo wa chama kuelekea mwaka 2010. Moja ya suala tulilokubaliana ni kusaidia chama ngazi ya chini kufanya kazi zao. Tuliamua kugawa rasilimali za chama kulingana na matokeo ya uchaguzi kwani hata hiyo ruzuku inapatikana kutokana na idadi ya kura. Wilaya zote ambazo CHADEMA inaongoza Halmashauri zinapewa sh 400,000 kila mwezi. Wilaya zenye madiwani kati ya 4 - 8, zinapewa shs 200,000 na wilaya nyingine zote shs 100,000. Hivyo mgawo wa ruzuku upo siku nyingi na chochote cha kusema pessa ya ruzuku haiendi wilayani sio kweli. Ruzuku inatumika tu kama silaha na propaganda lakini watu wa wilayani wenyewe wanajua suala hili.

Zitto

Mheshimiwa Zitto,

Sasa kama mambo yako wazi hivyo, hii habari si ndio mungeweka kwenye tamko lenu? Badala ya mambo mengi ambayo hayana maana kwenye lile tamko, mungeliweka facts kama hii uliyoandika hapo juu kama ni kweli.

Kama ulivyoandika, mlikubaliana mgawanyo wa pesa za ruzuku, lakini je hayo makubaliano yanatekelezwa? Kama yanatekelezwa basi hiyo ilikuwa ni fact nzuri kuitumia kukanusha madai ya Chacha.
 
Back
Top Bottom