CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Mwanakijiji,

Vipi namba zinakugonga? Laki moja kwa kila wilaya hata ukiwa na wilaya 300, bado ni milioni 30 tu kati ya milioni 66 kwa mwezi.

nilidhani wamesema milioni moja kila wilaya, kwani laki moja kwa kila wilaya haikuingia akilini. Upande mwingine ni tatizo la umande.
 
``...Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni, na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. Tumekuwa yatima waliofiwa na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.

Tunakunywa maji yetu kwa fedha, kuni zetu twauziwa.


Watufuatao wako juu ya shingo zetu, tumechoka tusipate raha yoyote Baba zetu walitenda dhambi hata hawako, na sisi tumeyachukuwa maovu yao. Watumwa wanatutawala, hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.

``Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu, kwa sababu ya upanga wa nyikani. Ngozi zetu ni nyeusi kama tanuu, kwa sababu ya hali ya njaa ituteketezayo Wakuu hutungikwa kwa mikono yao, nyuso za wazee hazipewi heshima.

``... Wazee wameacha kwenda langoni, na vijana kwenda ngomani. Furaha ya mioyo yetu imekoma, michezo yetu imegeuka maombolezo.

``Mbona watusahau siku zote, na kutuacha muda huu mwingi. We Bwana, utugeuze kwako nasi tutageuka, zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. Isipokuwa wewe umetukataa kabisa, nawe una hasira nyingi sana juu yetu,`` hayo ni baadhi maneno ya Bibilia yanayopatikana kwenye kitabu cha Maombolezo sura ya 5:1-22.

Nimelazimika kunukuu sehemu hiyo ya Biblia kama kitabu kitakatifu, kuonyesha maonyo yaliyotolewa wakati wa zamani na dhuluma iliyopo sasa duniani, hasa katika nchi maskini na zile zinazoendelea, dhuluma zinazofanywa na baadhi ya watawala wake.

Katika kipindi cha takribani miaka miwili na miezi minne hivi, Watanzania na Walimwengu kwa ujumla, wameshuhudia viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya nne wanavyoachia nyadhifa zao.

Hatua hiyo ya viongozi kuachia nyadhifa zao haimaanishi wamehusika na tuhuma zinazoenezwa juu yao, bali ni ishara ya heshima na uwajibikaji.

Hatuwezi kuwahukumu viongozi hao kuwa `walivaa ngozi ya kondoo`, huku wakijijua ni `mbwa mwitu` bali walionyesha mfano mzuri wa kuwajibika ingawa wapo wengi wa aina hiyo wanaotakiwa kufuata nyayo zao.

Kuwajibika si dhambi, wala kuwajibika si aibu bali kama kiongozi, anazidi kujijengea heshima.

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, anatanabaisha kwamba baada ya Tanzania kupata Uhuru, uongozi wa wakati huo ulikuwa ukitegemea Rais zaidi.

Hata hivyo, alikiri kuwa viongozi wa wakati huo walikuwa na maadili makubwa ikilinganishwa na wa sasa.

Alisema mtu mbadhirifu au aliyepatikana na rushwa, alikuwa hana nafasi wala sifa ya kuendelea kuwa kiongozi, kwani Rais, wakati huo hayati Mwalimu Julius Nyerere, hakusita kumchukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kumfukuza kazi moja kwa moja.

``Wakati huo ilikuwa amri moja tu kwa kiongozi asiye na maadili. Zamani kiongozi akiitwa Ikulu anatetemeka, anajua akirudi hana kazi, ni kiama kwake, lakini sasa hivi mambo tofauti.`` alisema.

Alisema kipindi cha awamu ya kwanza, kulikuwa na matukio mengi ya viongozi kujiuzulu, kufukuzwa na kustaafishwa kazi.

Miongoni mwa tukio la kujiuzulu kwa kuwajibika ni la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kutokana na makosa yaliyotokea katika wizara yake.

Katika serikali ya sasa viongozi wengine walioachia ngazi zao kwa uwajibikaji mapema mwaka huu ni aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge.

Hata hivyo, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Daud Balali, alifukuzwa kazi ingawa ni baada ya kumuandikia Rais kuwa ameamua kujiuzulu.

Uwajibikaji ni sehemu ya uadilifu, nidhamu na kujijengea heshima ndani ya familia ya anayewajibika, lakini zaidi nje ya familia yake na nje ya mipaka ya nchi, kwani kiongozi anaonyesha kujutia kilichotokea akiwa kiongozi katika eneo lake, lakini kujiuzulu kwa shinikizo la umma, hilo halimletei heshima kiongozi.

Kwa mujibu wa Profesa Baregu, kumekuwa na matukio mengi ya ubadhirifu, hali ambayo imewaudhi wananchi hadi kufikia umma huo kuchukia kudanganywa huku mali zao wakishuhudia zikiporwa.

Profesa Baregu alisema shinikizo la nguvu ya umma limechangia kuibuka kwa mambo mengi maovu.

Pia alivipongeza vyama vya upinzani hasa ushirika wa vyama vinne vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

Alisema vyama hivyo kwa kushirikiana na umma wa Watanzania, waliweza kufanikiwa kuufikisha ujumbe, kilio chao cha kuporwa mali zao, na matokeo yalijidhihirisha na kwa upande mwingine serikali imeonyesha nia ya kushughulikia malalamiko hayo.

Hatua iliyofikiwa na serikali ya kuanika uozo uliojitokeza, ni hatua muhimu sana na ya kuungwa mkono na wananchi wengi, hicho ndicho kilichokuwa kikisubiriwa na umma wa Watanzania.

Aidha, hatua hiyo itairejesha heshima na imani ya Watanzania kwa uongozi wa Taifa na mihimili yote ya nchi.
Naye Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katholiki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methedius Kilaini, ameonyesha kukerwa na watu wanaohusika na ufisadi.

``Mimi simjui fisadi, lakini ninachukia sana hali hiyo. lakini nimeridhika jinsi suala hili lilivyoibuliwa, kwani haya mambo yalikuwepo tangu enzi za mababu, lakini, nani awe wa kwanza kumfunga paka kengele,`` alisema.

Aliwashauri Wabunge, kutokana na ujasiri wao kuliibua suala hili na kulizungumzia kwa kina, waendeleze jitihada hizo hadi mafisadi watakapojulikana na kufikishwa mahakamani, kwani huko wananchi watakapowajua na kupata haki yao.

Askofu Kilaini alikuwa akimaanisha, huwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni fisadi, kwani wengi wanaamini viongozi wote waliojiuzulu ni mafisadi, la hasha, hao walifanya hivyo kama sehemu ya uwajibikaji, kwani tuhuma hizo zimeibuka wakati wao wakiwa ni viongozi wa maeneo yanayotuhumiwa.

Kwa maana hiyo, uchunguzi unaofanywa na serikali katika maeneo hayo wananchi wanaamini utawaibua mafisadi, pengine ni wale waliojiuzulu kwa heshima au wengine.

Inawezekana kabisa, Rais Kikwete ana dhamira ya kweli ya kuwaondolea umaskini na kero zote zinazowakabili wananchi, lakini wapo wanaokwenda kinyume na dhamira hiyo.

Hata hivyo kuna dalili yawezekana Rais Kikwete ameonyesha kukerwa na ufisadi pamoja na rushwa, ndiyo maana alishindwa kulitolea maamuzi suala hilo na badala yake ameviachia vyombo vya dola kulishughulikia, na Watanzania wanasubiri kwa hamu sana matokeo ya uchunguzi huo.

Kumekuwa na maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi na viongozi wa dini, juu ya nini kifanyike kwa wale wote watakaobainika kuhusika na kupora mali za Watanzania.

Pia yapo maoni yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuchunguza tuhuma za Richmond.

Baadhi ya maoni ya wananchi na viongozi wa dini ni serikali kuwachukulia hatua haraka wale wote wanaodhani ni mafisadi ikiwa ni pamoja na kufilisi mali zao.

Maoni hayo ni ya haraka sana, tunaamini hakuna mtu anayemfahamu fisadi, cha msingi ni wananchi kuwa na subira, kusubiri uchunguzi unaoendelea wa vyombo vya dola.

Cha msingi ni vyombo hivyo kufanyakazi yake kwa umakini na ukweli na uwazi ili Watanzania waendelee kujenga heshima kwa serikali yao ya awamu ya nne na hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili suala hili lisiendelee kuwa mjadala, tena mjadala wa kutoaminiani, dhamana ya ukweli wa mambo yenyewe iko mikononi mwa vyombo vilivyoteuliwa na serikali katika kuchunguza masuala hayo.

Vyombo hivyo visipofanyakazi yake kwa makini na ukweli, viongozi waliojiuzulu nyadhifa zao hawatakwepa hasira za wananchi, na maisha yao yatakuwa juu ya mikono ya Watanzania.

Watanzania kama kawaida yao ni wapole, hivyo upole wao usichukuliwe kama ni mazuzu.

Tanzania ni yetu, hakuna mgeni atakayetutengenezea amani na utulivu, kwani suala hili likichukuliwa kwa jazba, urithi wa amani yetu utabakia kama historia, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
 
Mkandara.. swali langu ni swali la mantiki. Unapoamua kupima kitu na kusema hiki hakiko sawa unalinganisha na kitu gani? Wanaposema kuwa kuwa na idadi ya watu wa mahali fulani ni ukabila/umajimbo tunalinganisha na nini? Niulize swali la Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Dar.. ni wangapi wana asili ya Dar? Tukienda mwanza kwa mfano, ni wabunge wa kutoka Mwanza ambao ni wa kuteuliwa ambao hawana asili ya Mwanza? Ni lazima tuwe na kitu cha kulinganisha, hii ni kanuni ya kisomi tu.

Halafu tunapolinganisha tunauliza "why" tunajaribu kutafuta maelezo ya kisomi kwanini hali iko vile na kuangalia kama kuna ukweli. Swali ambalo Wangwe na mtu mwingine angetakiwa kuuliza ni mfumo gani Chadema inatumia kupata wabunge wake wa kuteuliwa, na kama mfumo huo ndio unasababisha hali hii kutokea. Kama mfumo ni wa haki, na ndio uliotumika sioni sababu ya kwanini tuone Ukabila. Kwa sababu matokeo yake kinachotakiwa kufanyika ni reverse discrimination, kwamba hata kama mtu anastahili kuwemo, kwa vile tu yeye ni Mchagga basi aachwe.

In principle, kama CUF kwa kufuata mfumo ulio wa haki na ulio wazi inajikuta inapata wabunge wengi wa kuteuliwa toka Pemba, well and good. Kama kuna mfumo mwingine ambao unaweza kutumika ni upi?

Hivyo mimi naamini swali letu la msingi ni la kutaka kujua ni mfumo gani ulitumika kupata wabunge hawa wa kuteuliwa kiasi cha kusababisha wabunge wa eneo moja kuwa wengi? Je mfumo huo ni kinyume na sheria/katiba, je ni mfumo ambao ukiwa applied in a large scale utaendelea kutoa wananchi wa eneo moja au utatawanya nafasi hizo?

Hata hivyo hadi hivi sasa hakuna mtu aliyejaribu kunieleweza kuhusu swali langu hapo nyuma, una nafasi 6 utazigawa vipi katika mikoa 27 na wilaya 137 na makabila 120 bila kusababisha manung'uniko kwa mtu yeyote? Tukipata jibu la swali hili nadhani tutakuwa tumetoa pendekezo la utatuzi wa tatizo tunalolidhania lipo.
 
Hivyo mimi naamini swali letu la msingi ni la kutaka kujua ni mfumo gani ulitumika kupata wabunge hawa wa kuteuliwa kiasi cha kusababisha wabunge wa eneo moja kuwa wengi? Je mfumo huo ni kinyume na sheria/katiba, je ni mfumo ambao ukiwa applied in a large scale utaendelea kutoa wananchi wa eneo moja au utatawanya nafasi hizo?

Sheria/Katiba ipi ya nchi au chama?

Kwa hiyo kama katiba inasema ni sawa kuchagua wabunge watano wachaga/wapare kati ya sita unaona ni sawa hiyo sheria?

Huwa unapenda kunukuu barua ya King kutoka jela. Alisema "unjust law is no law."

Halafu kuhusu kugawa nafasi sita kati katika mikoa 26 haiwezekani, kwa hiyo ndio uharibu ukasiba upeleke zote sehemu moja?
 
Sheria/Katiba ipi ya nchi au chama?

Kwa hiyo kama katiba inasema ni sawa kuchagua wabunge watano wachaga/wapare kati ya sita unaona ni sawa hiyo sheria?

I left that question open ili mtu achague kuangalia Katiba ipi. Na sidhani kama kuna Katiba itasema ni sawa "kuchagua wabunge watano wachaga/wapare". Na sijasema naona sawa, ninachoona ni kuwa sijaona msingi wa madai ya ukabila au umajimbo, kwa kuangalia idadi tu.


Huwa unapenda kunukuu barua ya King kutoka jela. Alisema "unjust law is no law."

very good, and that is my point. Kama ni mfumo ndani ya Chadema basi tuuangalie huo. Ndio maana nimeuliza ni utaratibu gani unatumika ndani ya Chadema ambao umesababisha kuwa na wabunge wengi kutoka eneo moja au kuhusiana na eneo moja.

Halafu kuhusu kugawa nafasi sita kati katika mikoa 26 haiwezekani, kwa hiyo ndio uharibu ukasiba upeleke zote sehemu moja?

You missed the point kwenye swali hilo. Ukiangalia kwa ukaribu unaweza kupata ni nini hasa ninakisema hasa kwa wale wenye kudai ukabila/ukanda.
 
Tangazo La Kuwavua Uongozi Viongozi Wa Chama Kwa Ngazi Ya Akina Wangwe Haikustahili Kuhubiriwa Ktk Mkutano Wa Hadhara Na Kibaya Zaidi Eti Tundu Lissu Ndiye Wa Kumuanika Makamu Wa Chama!!!!

Leadership Haionyeshi Ramani Ya Kujenga Hata Kidogo.

Ni Matukio Ya Kihuni Kama Haya Ndiyo Yanawafanya Wa Tz Kufadhaishwa Na Uwepo Wa Vyama Vya Siasa.

Twaweza Mlaumu Jk Kwa Kumtetea El Diamond Jubilee Na Huko Dom Lakini Ikumbukwe Muungwana Ameheshimu Mamlaka aliyekuwemo EL Aliyejeruhiwa na Richmond pia Mamlaka Yake yeye kama Rais na ndie aliyemteua Lakini Kama Maelezo ya JK Yangelitanguliwa Na Mwanasheria Wa Ccm ama mkuu wa proganda Msabaha/HIZA Au mwanasheria wa Serikali Hapo Angekuwa Amejivunjia Hadhi yeye kama Rais na M/kiti wa CCM, Hapo Mnaiona Tofauti Na Maono Ya Kwanini Jk Alifanya Utetezi Ule Yeye Mwenyewe Tena Kwa Kuchagua Aina Ya Majukwaa.

Mbowe Hapa Hajatupatia Fursa Ya Kumuamini Ki Uongozi.

Chadema Inashutumiwa Kwa Ukabila, Hoja Ziko Wazi Wakuu Tatizo Ni Ujasiri Wa Wana Chadema Kutouona Ukweli Kwa Makusudi! Unapoulizwa Kwanini Wabunge Wengi Wa Viti Maalum-akina Mama Ni Wa Kilimanjaro? Toa Majibu Yaliyo Wazi Ili Kumridhisha Hata Msomi Wa Memkwa Lakini Wapi Hamjibu!!!!

Kilimanjaro Mbunge -ndesamburo, Kigoma-zito, Rukwa -arfi, Mara-wangwe, Arusha -slaa Sasa Kwanini Uwakilishi Usifuate Ramani Hii Ya Ushindi Maana Ni Wazi Nyuma Ya Ushindi Wa Hawa Ndugu Kuna Akina Mama Wa Chadema Waaminifu Waliojitoa Muhanga Ili Hawa Waingie Bungeni, Iweje Suzy Lyimo,kiwelu,mdee,komu ??


Mbowe Ana Kazi Kubwa Kuturidhisha Kuwa Anao Wasifu Kimaadili Na Kiuongozi Kwa Ngazi Ya Taifa.
 
anataka msawhili arudi tena aje atuoneshe ukabila ndani ya CHA dema


nnaomba invisible ile thread uturejeshee tujikumbushe na wapya waone hili lishazungumzwa zamani barazani hapa
 
hawa hawawezi kuchukua nchi.... sisi ccm hatuna cha kutimuana wala nini.
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.

kidumu chama cha mapinduzi.

wewe ni mwendawazimu, na hujui ulimwengu unakoelekea , mbona lowasa karamagi msabaha balali wametimka na wako ndani ya serikali tusiseme kitu hiyo ndiyo maana ya demokrasia fisadi wewe. wao wameona wakisafishe chama mapema ili kisije waozea kama hiki kilichopo.dog
 
Hivi huko Chadema kinachosemwa kuwa ni tatizo ni nini hasa? Naomba kuelimishwa
 
Hivi huko Chadema kinachosemwa kuwa ni tatizo ni nini hasa? Naomba kuelimishwa

mimi kwa mtazamo wangu wa mbali ni siasa za kitanzania zinawasumbua.

Wanasiasa wengi wanapenda madaraka makubwa na jina kubwa.
Inapofikia ukweli kwamba jina ninafifia, basi huwa mwanasiasa anajikuta anahangaika kulinyanyua tu kwa vyovyote vile.

wengine wanatamani kupata pato kutokana na kazi kubwa wanayoifanya, na wanaona si haki mgao ulivyo kwa muda huo.

wengine wana inferirity complex, ya uchaga na ukyasaka.

labda katiba haiko wazi jinsi ya kushughulikia migogoro ya kawaida.

labda mazoea ya kufuata katiba hayapo, hivyo wanachama au viongozi hujikuta wakitaka kuipindisha katiba wenyewe ili iwanufaishe.

lakini chama kinakuwa zaidi baada ya kupita migogoro na kuimaliza kwa kufuata katiba yao.

yetu macho!!
 
Mbowe: Wanataka kuiua CHADEMA

2008-07-02 09:46:16
Na Simon Mhina


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amedai kwamba kinachotokea sasa hivi ndani ya CHADEMA ni mpango maalum wa kukiua chama hicho ili kisionekane katika uchaguzi mkuu 2010 na sio ruzuku inayotolewa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Akizungumza na Nipashe jijini jana, Mwenyekiti huyo alisema sio siri kwamba CHADEMA ni tishio kwa mafisadi, ambao wamejipanga vilivyo kutoa upinzani mkubwa kwenye uchaguzi huo.

Alisema kuna njama za kuidhoofisha CHADEMA kabla ya mwaka 2010.

``Wameshajua kwamba huenda janga la ufisadi likawa agenda kubwa sana katika Uchaguzi Mkuu ujao, na hakuna asiyejua kwamba CHADEMA ndio wameibua tatizo hilo na sisi na wabunge wetu ndio tumelishikia bango, sasa kuna njama inafanywa ya kufa na kupona kuhakikisha kwamba tunakosa nguvu,`` alisema.

Mwanasiasa huyo alisema sio siri kwamba tayari kuna watu ndani ya CCM hasa kundi la mafisadi, ambao tayari wameshaanza kupanga mikakati kwa ajili ya uchaguzi huo.

Alisema kwa madai haya hana maana ya kumtuhumu Makamu wake aliyesimamishwa kwamba anashirikiana na mafisadi hao, lakini ukweli kuhusu kila jambo, utafahamika.

``Na moja ya mkakati huo ni kuhakikisha kwamba kabla ya uchaguzi huo nguvu ya CHADEMA inapungua,`` alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo alionya kwamba hakuna mgawanyiko wowote ndani ya CHADEMA kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vinashabikia.

Alisema ruzuku ya chama hicho inatumika kwa mlingano sawa mikoani kwa mujibu wa mahitaji na bajeti ya chama.

Bw. Mbowe, alitoa ufafanuzi huo, kufuatia madai kwamba ruzuku ya CHADEMA inaishia makao makuu na kwamba wale wanaohoji na kutaka isambae zaidi ili kujenga chama chao wanaonekana nuksi.

Mwenyekiti huyo alisema kwa kiasi kikubwa shughuli za makao makuu ya chama hicho, zinaendeshwa kwa kujitolea.

Alisema viongozi wa juu wa CHADEMA, akiwemo yeye, Katibu Mkuu na Naibu wake, wanafanya kazi kwa kujitolea.

``Mimi siku zote sijawahi kupokea mshahara wala posho kutoka CHADEMA, gari ninalotumia ni langu binafsi, dereva namlipa mimi kila kitu najihudumia mwenyewe. Vilevile Katibu Mkuu na hawa akina Zitto hawapokei malipo yoyote kutoka CHADEMA,`` alisema.

Bw. Mbowe, alisema yeye amekuwa akitoa fedha zake binafsi kwa ajili ya kukisaidia chama na wakati mwingine kukikopesha bila riba wala masharti yoyote, pale ambapo kinapungukiwa.

Aliwataka wanachama wa CHADEMA na wale wa kambi ya upinzani na viongozi wake, wasisononeke kutokana na kuchafuka kwa hali ya siasa ndani ya chama hicho, kwa vile hapakuwa na njia nyingine ya kusawazisha mambo.

Alisema hatarajii kwamba hatua ya Kamati Kuu kumsimamisha uongozi Makamu Mwenyekiti, Bw. Chacha Wangwe itazua mtafaruku wowote.

Alisema hatarajii hali hiyo kwa vile Bw. Wangwe, alishirikishwa katika hatua hiyo muhimu.

Bw. Mbowe, alisema hali ya CHADEMA imetulia na kuna mshikamano wa hali ya juu kati ya viongozi wote, vikao vya chama na wanachama.

Alisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo, ili kusawazisha mambo ndani ya chama kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

``Tulikuwa na wasiwasi na baadaye tumethibitisha kwamba kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama lengo lake ni kudhoofisha CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010,`` alisema.

Hata hivyo, Bw. Mbowe, alisema njama zozote za kusambaratisha chama chake hazitawezekana, kwa vile umma wa Watanzania umeshajua vita iliyopo mbele yao ya ufisadi, ambayo kwa kiasi kikubwa imeshikiwa bango na CHADEMA.

Makamu Mwenyekiti aliyesimamishwa, Bw. Chacha Wangwe, amekuwa akidai kwamba mbali na ruzuku, sababu nyingine ya kutoelewana na wenzake ni yeye kuhoji chama chao kutokuwa na sura ya kitaifa kutokana na nafasi nyeti kupeana watu wa mkoa mmoja.

SOURCE: Nipashe
 
mbowe: Wanataka Kuiua Chadema

.......

Hata Hivyo, Bw. Mbowe, Alisema Njama Zozote Za Kusambaratisha chama Chake hazitawezekana, Kwa Vile Umma Wa Watanzania Umeshajua Vita Iliyopo Mbele Yao Ya Ufisadi, Ambayo Kwa Kiasi Kikubwa Imeshikiwa Bango Na Chadema.

Makamu Mwenyekiti Aliyesimamishwa, Bw. Chacha Wangwe, Amekuwa Akidai Kwamba Mbali Na Ruzuku, Sababu Nyingine Ya Kutoelewana Na Wenzake Ni Yeye Kuhoji Chama Chao Kutokuwa Na Sura Ya Kitaifa Kutokana Na Nafasi Nyeti Kupeana Watu Wa Mkoa Mmoja.

Source: Nipashe[/b]



Naam Ni Kweli Hicho Ni Chama Chako Na Si Chama Cha Wanachama Na Ndio Unafanya Utakavyo Asante Kwa Kutwambia Ukweli
 
Mtu wa Pwani,
Hiyo spinning yako haijaenda shule kabisa, Mbowe anaongea hapo kama mwenyekiti wa Chadema, hivyo kusema "chama chake" ni sawa kabisa in that context.
 
Niweke Rekodi Sahihi Hapa ,wilaya Zinapewa Fedha Kulingana Na Vipaumbele Na Ni Mkakati.

Siwezi Kutaja Ila Nitawataka Mmoja Wenu Amuulize Mhe.chacha Wangwe Kuwa Wilaya Ya Tarime Inapewa Laki Nne (400,000) Kila Mwezi Akubali Ama Akatae.

Kwa Hiyo Kila Wilaya Zinapewa Fedha Kulingana Na Vipaumbele Na Pia Mkakati Wa Kukijenga Chama Kwani Chama Hakiwezi Kujengwa Siku Moja Na Kikaweza Kusambaa Nchi Nzima Hivyo Fanyeni Utafiti Kabla Ya Kulaumu.

Kuna Wilaya Zinapewa Laki 4, 3,2 Na 1. Na Hili Linatokana Na Targeting Za Chama ,.

Naomba Kutoa Ufafanuzi Naamini Nitaeleweka.
 
mzee tumekupata!!!!Hayo ndo mambo,tunasubiri kwa hamu japo nasafiri nikifika tu ninafungua
 
Niweke Rekodi Sahihi Hapa ,wilaya Zinapewa Fedha Kulingana Na Vipaumbele Na Ni Mkakati.

Siwezi Kutaja Ila Nitawataka Mmoja Wenu Amuulize Mhe.chacha Wangwe Kuwa Wilaya Ya Tarime Inapewa Laki Nne (400,000) Kila Mwezi Akubali Ama Akatae.

Kwa Hiyo Kila Wilaya Zinapewa Fedha Kulingana Na Vipaumbele Na Pia Mkakati Wa Kukijenga Chama Kwani Chama Hakiwezi Kujengwa Siku Moja Na Kikaweza Kusambaa Nchi Nzima Hivyo Fanyeni Utafiti Kabla Ya Kulaumu.

Kuna Wilaya Zinapewa Laki 4, 3,2 Na 1. Na Hili Linatokana Na Targeting Za Chama ,.

Naomba Kutoa Ufafanuzi Naamini Nitaeleweka.


Hapana hizo wenda zikawa hisia zako kwanini Maana Lisu na Wangwe wakati wanahojiwa naamini hawakuwa sehemu moja.

Na aliyeanza kusema ni laki moja ni Lisu na wangwe naye akasema baadaye hivyohivyo ,wote hawakugusia hizi habari unazoleta hapa. Tupe mchanganuo huo kwa maandishi Maana Lisu amesema habari zote ziko kwenye mtandao .Na nategemeo kabisa kama ni kweli huo mchanganuo utakuwepo.
 
Hapana hizo wenda zikawa hisia zako kwanini Maana Lisu na Wangwe wakati wanahojiwa naamini hawakuwa sehemu moja.

Na aliyeanza kusema ni laki moja ni Lisu na wangwe naye akasema baadaye hivyohivyo ,wote hawakugusia hizi habari unazoleta hapa. Tupe mchanganuo huo kwa maandishi Maana Lisu amesema habari zote ziko kwenye mtandao .Na nategemeo kabisa kama ni kweli huo mchanganuo utakuwepo.

nimekwambia mpigie Wangwe na umuulize kama sio kweli kuwa kila mwezi wilaya yake inapewa laki nne kwa mwezi.

Huyu si ndio utamwamini? mpigie atakupa majibu yeye ndipo uamini.
 
Back
Top Bottom