CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Ukiangalia TREND YOTE ya jinsi pesa za ufisadi zilivyogawanya...Utangundua kuwa ulikuwa ni mpango maalum kwani pesa zilikuwa nyingi kupindukia!

Waliojimilikisha migodi...Wakaanzisha na EPA na msururu wake ndio kama virusi!

Halafu kila mahali wakaweka wachagga na kuwaingiza humo kwenye ufisadi wao!Wengi tu!Tena pesa zenyewe zilianzia huko kwa wasilamu...Kina Iddi Simba na wamiliki wa BORA APTS,NDOVU SOAP NK!

Pesa hizo wakazi channel kwa watu ambao kisa ni wachaga tu maana hata walikuwa si watu wa ma connection kihivyo!Walizitapakaza kila mahali hadi marekani na kwingineko ulaya!

Sasa mpango wao unakuwa wazi...UDINI NA UKABILA!

Wale waliokuwa wakijuwa kuwa ccm itadaiwa kuwa ni mafisadi na huku ccm yenyewe ikiwa wazi kuwa ni chama cha waislam...Wakazipenyeza pesa za EPA kwa style ya kuchafuana na sasa ni PROPAGANDA TIME!

Tatizo bado narudia...Ni jf!

Trend ya pesa za ufisadi pamoja na kinachohubiriwa na ccm hapa unajuwa kuwa wizi wote ilikuwa ni wa kisiasa uliopangwa kimafia ili hata wale wapinzani wanaoelekea kushinda kwa hoja basi wachafuliwe!

Mfano mwingine ni hata jinsi wamekuwa wakijaribu kumchafua hata MWAKYEMBE!

Pesa walizochukuwa ni nyingi sana!Haziwezi kwisha...Na ni wazi serikali yetu inazitumia tena ili kuwaghilibu wananchi!Sidhani kama ni possible this time.

Ripoti ya EPA iko hapa...Tumeshazisoma na tunajuwa everything na ni nani wanahusika!

Wananchi naomba muelewe hili...Kwamba RIPOTI ZOTE ZIKISHAKUSOMWA...HAPO TUTAKUTA MAFISADI WENGI TU KUANZIA WAKRISTO,WAISLAM,WAHINDI,WACHAGGA,WASUKUMA,
WAMASAI NK!

Wote hao ni MAFISADI NA KAMWE WASILICHAFUE KABILA LOLOTE WALA DINI YOYOTE!

Watanzania DAINI UHURU WENU NA MTAONA MATUNDA YAKE!

TANZANIA NI NCHI TAJIRI INAYOMILIKIWA NA MAFISADI WACHACHE WA DINI TOFAUTI NA MAKABILA TOFAUTI WAKISHIRIKIANA NA MKOLONI WALIYENWUZIA NCHI!

Tunawaomba watanzania muwashurutishe wabunge wenu wadai ripoti za EPA NA MADINI NA ISSUES NYINGINE ZOTE HADI TUERUDISHIWE NCHI YETU!
 
Tarime waunga mkono kusimamishwa kwa Wangwe

2008-07-04 09:21:55
Na Simon Mhina


Uongozi wa CHADEMA wilayani Tarime, umemgeuka mbunge wao, Bw. Chacha Wangwe kuhusiana na kusimamishwa kwake uongozi.

Bw. Wangwe pia ni Makamu Mwenyekiti wa wa chama hicho.

Pamoja na kuunga mkono, uongozi huo umepinga madai yake kwamba rukuzu inayotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa haifikishwi mikoani.

Aidha, uongozi wa chama hicho mkoani Mara, umeelezea kusikitishwa na madai ya Bw. Wangwe na kusema hivi sasa wanamtazama kama mtu asiyekitakia mema chama hicho.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Tarime, Bw. Joseph Anthony alisema inasikitisha kuona kiongozi wa juu wa chama kama Bw. Wangwe anaanzisha hoja ya malumbano yenye nia ya kukiangamiza chama.

Akifafanua alisema inasikitisha kuona Bw. Wangwe akitoa taarifa zisizo sahihi kwenye vyombo vya habari kwamba ruzuku ya chama hicho inaishia makao makuu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Wilaya yake ya Tarime inapokea Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya kukijenga chama.

Kwa msingi hiyo, Bw. Joseph alisema wilaya ya Tarime inaunga mkono kusimamishwa kwa Bw. Wangwe katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Aidha, alimshauri Bw. Wangwe kuacha mipango yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la chama kupinga uamuzi wa kusimamishwa na badala yake asubiri uchaguzi mkuu ujao.

Alisema Bw. Wangwe anatakiwa kujirudi na kujisafisha kwa njia ya kushirikiana na viongozi wenzake, kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari na kukanusha tuhuma dhidi ya viongozi wenzake.

Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafar Kasisiko alisema wao wana wasiwasi mkubwa kwamba Bw. Wangwe anatumiwa kukivuruga chama.

Bw. Kasisiko alisema anachokifanya kiongozi huyo hadi akasimamishwa kina lengo la kuwafanya mafisadi wafurahie.

Mwenyekiti huyo alisema wilaya zake zote zinapata gawiwo la ruzuku tofauti na madai ya Bw. Wangwe.

SOURCE: Nipashe

Kwanini hawataki aende baraza kuu la Chadema? kila taasisi inaposhindwa kutoa haki kwa ngazi fulani inampa nafasi mtu kwenda mbele zaidi hadi mwisho ili kuona haki imetendeka. ni haki yake aende anakotaka, kumsema au kumtisha asilipeleka mbele suala lake ni kunyima haki ya msingi ya binadamu kusilizwa kilio chake, hata mahakama zina ngazi nyingi hadi mahakama ya rufaa.
 
mgagagigikoko, soma tena haijasemwa "wamemtaka" asiende Baraza Kuu... mbona inakuwa kazi...?
 
mgagagigikoko, soma tena haijasemwa "wamemtaka" asiende Baraza Kuu... mbona inakuwa kazi...?

Wanasema bora asiende huko, wao wamenyima haki na hao hao wanamshauri asiende mbele ya safari akasafishe jina lake au akapate haki yake ili uamuzi utenguliwe,Mtikila kila mara anakwenda mahakamani na anapata haki yake.
 
Wanasema bora asiende huko, wao wamenyima haki na hao hao wanamshauri asiende mbele ya safari akasafishe jina lake au akapate haki yake ili uamuzi utenguliwe,Mtikila kila mara anakwenda mahakamani na anapata haki yake.

unasoma mengi kuliko kilichoandikwa. Ukisoma kilichoandikwa hutapata hayo yote unless that is what you want to read.
 
ningependa siku moja nikutane na huyu mushi maana ananishangaza sana kwa wepesi na haraka yake ya kuandika
 
ningependa siku moja nikutane na huyu mushi maana ananishangaza sana kwa wepesi na haraka yake ya kuandika

Ningependa siku moja mafisadi wakutane na sheria...Kwani wananishangaza na wepesi na haraka zao za kuiba mali za Taifa na kuturudisha UTUMWANI!
WE WANT FREEDOM NOW!
 
Siku zote chama kinakosa msimamo mara tu kinapofikiriwa kuwa kinamilikiwa na mtu fulani au watu wanapofikiria kuwa chama ni cha mtu fulani. Kazi sas ni kwa Chadema kuwa convince wananchi waone kuwa chama ni cha wananchi na sio cha Mbowe au Wangwe.
 
Kasoro anaozisema Wangwe, zikirekebishwa then Wangwe hatakuwa na hoja wala following kama ilivyo sasa,

Chadema watumie umakini ku-deal na hoja za Wangwe, badala ya kujaribu kupambana na Wangwe as a person, kwa sababu reading between the lines ni clear kuwa Wangwe has nothing to lose, na hii vita isipokuwa ana-gain tu,

So far Chadema, hamjaonyesha umakini kwenye ku-deal na this ishu, na kwakweli binafsi nimesikitishwa sana hasa baada ya kuona vitimbi vingi humu ndani ya forum vya kujaribu ku-deal na hii ishu lakini kwa kweli ni kujishusha hadhi ni afadhali kuwa tumejua mapema,

na binafsi nimeridhishwa sana na maneno mazito sana ya Kitila on this ishu, anaonekana kuwa amekomaaa kisiasa na kitaifa pia na anweza kuwa the best alternative huko mbele ya safari. I wish wale wenzetu wange-invest in him kwa sababu anaonyesha kuwa makini sana.

Kosa kubwa sana kwa CHADEMA, na ni kweli inabidi wasahihishe hilo kosa. You can not afford to loose this man. Kwa mawazo yangu faida anazoipa Chadema huyu Wangwe zinazidi kabisa zile weakness zake; na wangepima kwenye mzani wao ni hatua gani zingepefaa kuondoa hizo weakness zake. Political parties especially those which are emerging should avoid such prolems and try to diffuse problems internally. Aliyoyasema Wangwe kuhusu jimbo la Tarime zile statistics pamoja na how to build the part from bottom to the top are very reasonable. Sometimes you have to love your enemy in order to solve some of the problems in the face of the public. In a long term I don't see if Chadema will trimph without solving this issue especially to moderates like us. Chadema leave the politics of gossip and grow up!
 
Kha! kumbe zemarcopolo ni Balile?

Kama huyu ndiye Balile niliyekua namuona mtu makini,sasa nikiangalia alivyokua anaandika hapa nabaki Hoi kabisa!


Mkuu FMES,

CHADEMA wasipokua makini hiii ishu itawayumbisha sana.Sasa hivi mwaka mmoja na nusu umebaki kuingia kwenye uchaguzi,sasa doa kama hili likiingia kwenye vichwa vya wananchi itakua balaa.

Hata hivyo,watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa finally aliyemsimamisha Wangwe si Mbowe bali ni kamati.Watu wanaofikiria kuwa Mbowe ndiye aliyemsimamisha Wangwe basi ndiyo wenye mawazo ya kidikteta zaidi kwa kuamini hata wao wangekua wenyeviti wa CHADEMA au taasisi nyingine wangeeweza kumsimamisha mtu kazi bila kufuata Demokrasia.Sasa unakuta watu wametingwa na mawazo ya kidikteta zaidi ndiyo maana perception yao imefikia huko kwa urahisi
 
Kama huyu ndiye Balile niliyekua namuona mtu makini,sasa nikiangalia alivyokua anaandika hapa nabaki Hoi kabisa!


Mkuu FMES,

CHADEMA wasipokua makini hiii ishu itawayumbisha sana.Sasa hivi mwaka mmoja na nusu umebaki kuingia kwenye uchaguzi,sasa doa kama hili likiingia kwenye vichwa vya wananchi itakua balaa.

Hata hivyo,watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa finally aliyemsimamisha Wangwe si Mbowe bali ni kamati.Watu wanaofikiria kuwa Mbowe ndiye aliyemsimamisha Wangwe basi ndiyo wenye mawazo ya kidikteta zaidi kwa kuamini hata wao wangekua wenyeviti wa CHADEMA au taasisi nyingine wangeeweza kumsimamisha mtu kazi bila kufuata Demokrasia.Sasa unakuta watu wametingwa na mawazo ya kidikteta zaidi ndiyo maana perception yao imefikia huko kwa urahisi

Mkubwa mambo mengine sio lazima pale Mbowe asimame aseme nimekufukuza CHACHA.
Mbowe alisimama ktk kikao hicho akasema Ama mimi nijiuzueu yani yeye Mbowe ama yeye Chacha ajiuzuru Na akaongeza hawezi fanya kazi na Chacha,Hizi statement za kiditeta na alisema hivyo akijua kwa njia yoyote lazima wangwe atoswe ,jamaa si ndio anatoa dau.

Milion 500 alikikopesha chama Masikini harafu bajeti yake ikaiingizwa kukodi Helkopita na kupaa nayo huyohuyo aliyewakopesha.Biashara zingine bwana.
 
Tunapozungumzia mambo ya ukabila kwenye vyama au mahali pengine popote pale tunathibitisha aliyowahi kusema Mwalimu Nyerere katika kutahadharisha kwamba ukabila bado upo nchini. Alisema kwamba tukikunwa kidogo tu, chini ya ngozi zetu ukabila utaonekana bado upo. Ninachokiona kwenye shutuma zinazotolewa kuhusu upendeleo wa Mbowe kwa walioteuliwa ubunge wa viti maalum ni kwamba yawezekana hao walioteuliwa ndio walikuwa wakikidhi vigezo vya kuwawezesha kuchaguliwa kuwa wawakilishi wa CHADEMA Bungeni.

Historia ya kuanzishwa Chama cha NCCR-Mageuzi ni mfano mmoja. Katika uchaguzi ule wa mwaka 1995, Mzee Lyatonga alipata wafuasi na mashabiki wengi wa kabila la Kichagga kwa sababu yeye ni mchagga. Ni dhahiri wapo wana CCM ambao ni wachagga waliompigia kura Mrema hawakumpigia kura Mkapa aliyekuwa mgombea wa CCM! Kwa hiyo, inawezekana pia wapo waliojiunga na CHADEMA kwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ni Freeman Mbowe - Mchagga. Matokeo yake ndio hayo malalamiko ya akina Wangwe.

Bado ni muhimu sana kurejea kwenye MISINGI waliyotuwekea waasisi wa Taifa hili na kuifanyika kazi ipasavyo ili tuondokane na mambo ya ukabila ambayo kwa kweli yameshapitwa na wakati.
 
CHADEMA mtimueni Wangwe - NCCR

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumtimua uanachama mara moja, Mbunge wake, Chacha Wangwe, kwa madai kuwa ni pandikizi anayetumika kukidhoofisha chama pamoja na kambi mzima ya mageuzi nchini.

Akizungumza na ‘Tanzania Daima' jijini jana, Kaimu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini, alisema chama hicho kimesikitishwa na kufadhahishwa sana na utovu wa nidhamu, unaoonyeshwa na Wangwe, ambaye kabla ya kuvuliwa wadhifa wake, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA,. inayoongozwa na Freeman Mbowe.

Seleasini ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, alikitahadharisha chama hicho kutompuuzia Chacha. Badala yake wamshughulikie haraka, kwani mbunge huyo kabla ya kujiunga na CHADEMA, alikuwa Diwani na Mwenyekiti wa Mkoa wa NCCR-Mageuzi, Mkoa wa Mara.

Mambo anayoyafanya sasa ndani ya CHADEMA, ndiyo aliyoyafanya NCCR-Mageuzi na kukiathiri kwa kiasi kikubwa chama hicho hadi leo.

"NCCR tunamfahamu Wangwe, ni mtu mkorofi, mgomvi, kwani alishawahi kutaka kumpiga mhasibu wetu, ni mtu asiyetosheka, mlalamishi na anayolalamikia leo CHADEMA, ndiyo aliyoyalalamikia akiwa NCCR- Mageuzi. Ombi letu kwa CHADEMA ni kwamba wasifanye mzaha na jambo hili, mtimueni Chacha," alisisitiza Selasini.

Selasini alisema kitendo cha Chacha hata baada ya maamuzi ya chama kuendelea kupingana na uamuzi huo, huku akiwakashifu viongozi wake kupitia vyombo vya habari, ni mwendelezo wa vitendo vya utovu wa nidhamu anavyovionyesha mbunge huyo.

"Mtu umesimamishwa na kikao halali cha chama, unapata wapi ujasiri wa kuwapa siku 14, eti wakuombe radhi na kusafisha jina lako. Huu ni mwendelezo wa vitendo vya utovu wa nidhamu. CHADEMA wanapaswa kutoliacha hivi hivi na ikibidi afukuzwe uanachama maana ni afadhali kumpoteza Wangwe kuliko kuangamiza mageuzi iliyokwishajijengea heshima nchini," alisema Seleasini.

Wangwe amesimamishwa wadhifa wake na Kikao cha Kamati Kuu kwa madai ya kukigawa chama na kutoelewana na viongozi na watendaji wengine wa chama hicho.
 
Mwenyekiti wa Taifa NCCR ni Mbatia mtu wa Kilimanjaro, mgombea urais kwa tiketi ya NCCR alikuwa kutoka Kilimanjaro bwana Mvungi, nadhani ni mkakati ule ule wa Kanda ya kaskazini,
maandishi haya yameandikwa na gazeti linalomilikiwa na Mbowe-Tanzania Daima.
 
Mwenyekiti wa Taifa NCCR ni Mbatia mtu wa Kilimanjaro, mgombea urais kwa tiketi ya NCCR alikuwa kutoka Kilimanjaro bwana Mvungi, nadhani ni mkakati ule ule wa Kanda ya kaskazini,
maandishi haya yameandikwa na gazeti linalomilikiwa na Mbowe-Tanzania Daima.

Lakini aliyeongea siye Mbatia au Selasini alitumwa aje kuongea kwa niaba ya Mbatia na gazeti la TD lilimwambia nini anachostahili kuongea? Je, huoni huyu jamaa ana history ya kuleta kasheshe na matokeo yake aliwahi pia kufukuzwa huko NCCR? Bora sasa aende CCM akapige watu ngumi huko.

Ama kweli nyani haoni kundule!! CCM kuendelea kuwakumbatia mafisadi akina Mkapa, Mramba, Rostam, Azizi, Lowassa, Karamagi, Chenge kwa kukwapua mabilioni ya peza ambazo zinakaribia shilingi bilioni 500 ndani ya CCM wengi wamekunyamazia ukiondoa wachache wanaopiga kelele, lakini hili la Wangwe kufukuzwa CHADEMA wamelivalia njuga na kutaka kulikuza kuliko inavyostahili!!!! Kwa CCM hili la kufukuzwa Wangwe kwa wao CCM hili lina maslahi makubwa kwa nchi kuliko lile la mafisadi ambao bado wamekumbatiwa kwenye chama hicho.
 
JASILI HAACHI ASILI,tatizo la wangwe ni kabila analotoka!...............MWINJUMA MUUMINI aliwahi kukiri kuwa tatizo linalomsumbua ni uzalamu wake,hivyo na WANGWE nae ubabe anaounesha ni kuuendekeza ukulya wake
 
Hayo ni maoni ya bwana 30 (selasini) au ya chama cha NCCR? ikumbukwe hata NCCR ilishutumiwa hivihivi na mnaona ilipo sasa NCCR...Ni wakati wa CHADEMA kuyashughullikia maneno haya ambayo yamekua yakiongelewa na watu wengi "SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU"......sasa hivi NCCR imebaki na Mbatia+Mvungi hata huyo selasini wengine ndio leo tunamsikia...ni lazima baadhi ya vyama vya upinzani vibadilike ili tuweze kupiga hatua la sivyo mtapaa na helkopta for nothing
 
JASILI HAACHI ASILI,tatizo la wangwe ni kabila analotoka!...............MWINJUMA MUUMINI aliwahi kukiri kuwa tatizo linalomsumbua ni uzalamu wake,hivyo na WANGWE nae ubabe anaounesha ni kuuendekeza ukulya wake

Nakubali asili ya Wangwe ni ubabe wa kikulya,,,haya kama we ni muungwana naomba utuambie kinachowasumbua waliomfukuza (Wachaga)...kisha utukumbushe na Kabourou alisema nini baada ya kujiengua chadema,,,,lazima mkubali sauti ya watu ni sauiti ya mungu,,,angekua wangwe ndie wa kwanza kuwatuhum ukabila ningekuunga mkono but for that you are wrong dawg
 
Back
Top Bottom