CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

kwa jinsi tunavyoifaham historia ya wangwe sikubaliani na wewe hata kwa sekunde mbili,,,Mapandikizi ndani ya chadema yapo mengi sana lakini sio wangwe...wangwe amekua diwani siku nyingi sie tuna mfaham kwa muda sana na itikadi na misimamo yake inaeleweka...CHADEMA lazima wakubali kubadilika na sio vizuri kumchukia mtu anaewaambia ukweli...mkiendelea hivyo hatutaona tofauti yenu na CCM ambao huweza hata kumuua mtu anaesema ukweli

Haya na hili nalo
Tarime waunga mkono kusimamishwa kwa Wangwe

2008-07-04 09:21:55
Na Simon Mhina


Uongozi wa CHADEMA wilayani Tarime, umemgeuka mbunge wao, Bw. Chacha Wangwe kuhusiana na kusimamishwa kwake uongozi.

Bw. Wangwe pia ni Makamu Mwenyekiti wa wa chama hicho.

Pamoja na kuunga mkono, uongozi huo umepinga madai yake kwamba rukuzu inayotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa haifikishwi mikoani.

Aidha, uongozi wa chama hicho mkoani Mara, umeelezea kusikitishwa na madai ya Bw. Wangwe na kusema hivi sasa wanamtazama kama mtu asiyekitakia mema chama hicho.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Tarime, Bw. Joseph Anthony alisema inasikitisha kuona kiongozi wa juu wa chama kama Bw. Wangwe anaanzisha hoja ya malumbano yenye nia ya kukiangamiza chama.

Akifafanua alisema inasikitisha kuona Bw. Wangwe akitoa taarifa zisizo sahihi kwenye vyombo vya habari kwamba ruzuku ya chama hicho inaishia makao makuu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Wilaya yake ya Tarime inapokea Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya kukijenga chama.

Kwa msingi hiyo, Bw. Joseph alisema wilaya ya Tarime inaunga mkono kusimamishwa kwa Bw. Wangwe katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Aidha, alimshauri Bw. Wangwe kuacha mipango yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la chama kupinga uamuzi wa kusimamishwa na badala yake asubiri uchaguzi mkuu ujao.

Alisema Bw. Wangwe anatakiwa kujirudi na kujisafisha kwa njia ya kushirikiana na viongozi wenzake, kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari na kukanusha tuhuma dhidi ya viongozi wenzake.

Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafar Kasisiko alisema wao wana wasiwasi mkubwa kwamba Bw. Wangwe anatumiwa kukivuruga chama.

Bw. Kasisiko alisema anachokifanya kiongozi huyo hadi akasimamishwa kina lengo la kuwafanya mafisadi wafurahie.

Mwenyekiti huyo alisema wilaya zake zote zinapata gawiwo la ruzuku tofauti na madai ya Bw. Wangwe.

SOURCE: Nipashe

eeh kama hii ni kweli basi wangwe kwisha habari yake
 
The members, who vowed to vote against the decision during the forthcoming meeting of the council, said the suspension of Mr Wangwe was a result of deep-rooted problems among the party's top brass which should first get cleared instead of "victimising the critics within the leadership".

na Gazeti la The Citizen Ni la ROstam??na hawa wa Kagera wanasema Uongo?

"You know this is costing our party a lot because the defection of Dr Kaborou for instance led our party to lose many councillors to CCM," the concerned activist noted. Dr Kaborou was Kigoma Urban MP for years before crossing over to CCM. The party won a majority of councillors in the town council, holding the Kigoma urban mayorship for two five-year terms.

Hawa mbona wanasema ukweli wa mambo.
"Party members knew nothing about what friends from inside and outside the country had donated to support their party," the Chadema stalwart observed. Kagera is represented by three members in the national governing council, two of whom stay in the region and one resides in Dar es Salaam.

Mpaka kieleweke kawaamshe wenzio waje wakusaidie kujibu haya,Hawa viongozi hawajui hata ni sh. ngapi huwa inatoka Nje?au ndiyo mnatumia nyie watu wa kaskazini
 
Mod. naomba uliunganishe hili na thread ile inayohusu Kusimamishwa kwa Wangwe ili kuwe na mtiriliko Mzuri,Tusishindane kumjadili Wangwe..tumeshaacha Mafisadi wanapumua
 
Mod. naomba uliunganishe hili na thread ile inayohusu Kusimamishwa kwa Wangwe ili kuwe na mtiriliko Mzuri,Tusishindane kumjadili Wangwe..tumeshaacha Mafisadi wanapumua

Nashukuru umeliona hilo japo hili ndio mkakati wenyewe ambao umepangwa kuhakikisha kuwa hatudai ripoti ya EPA hata baada ya muda wa kamati kwisha .

Najibu moja kuhusu Kabourou ni kuwa aliondoka CHADEMA baada ya kushindwa ubunge hivyo madai ya huyu aliyejiita kiongozi ambaye anaogopa kutaja jina lake ni uzushi .
 
Haya na hili nalo
Tarime waunga mkono kusimamishwa kwa Wangwe

2008-07-04 09:21:55
Na Simon Mhina


Uongozi wa CHADEMA wilayani Tarime, umemgeuka mbunge wao, Bw. Chacha Wangwe kuhusiana na kusimamishwa kwake uongozi.

Bw. Wangwe pia ni Makamu Mwenyekiti wa wa chama hicho.

Pamoja na kuunga mkono, uongozi huo umepinga madai yake kwamba rukuzu inayotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa haifikishwi mikoani.

Aidha, uongozi wa chama hicho mkoani Mara, umeelezea kusikitishwa na madai ya Bw. Wangwe na kusema hivi sasa wanamtazama kama mtu asiyekitakia mema chama hicho.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Tarime, Bw. Joseph Anthony alisema inasikitisha kuona kiongozi wa juu wa chama kama Bw. Wangwe anaanzisha hoja ya malumbano yenye nia ya kukiangamiza chama.

Akifafanua alisema inasikitisha kuona Bw. Wangwe akitoa taarifa zisizo sahihi kwenye vyombo vya habari kwamba ruzuku ya chama hicho inaishia makao makuu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Wilaya yake ya Tarime inapokea Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya kukijenga chama.

Kwa msingi hiyo, Bw. Joseph alisema wilaya ya Tarime inaunga mkono kusimamishwa kwa Bw. Wangwe katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Aidha, alimshauri Bw. Wangwe kuacha mipango yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la chama kupinga uamuzi wa kusimamishwa na badala yake asubiri uchaguzi mkuu ujao.

Alisema Bw. Wangwe anatakiwa kujirudi na kujisafisha kwa njia ya kushirikiana na viongozi wenzake, kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari na kukanusha tuhuma dhidi ya viongozi wenzake.

Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafar Kasisiko alisema wao wana wasiwasi mkubwa kwamba Bw. Wangwe anatumiwa kukivuruga chama.

Bw. Kasisiko alisema anachokifanya kiongozi huyo hadi akasimamishwa kina lengo la kuwafanya mafisadi wafurahie.

Mwenyekiti huyo alisema wilaya zake zote zinapata gawiwo la ruzuku tofauti na madai ya Bw. Wangwe.

SOURCE: Nipashe

eeh kama hii ni kweli basi wangwe kwisha habari yake

Ndio hizo siasa za majitaka,,,huyo aliesema ni katibu wa chama wa wilaya na sio Tarime naomba urekebishe msemo wako, hayo ni maoni yake binafsi na sio tamko la wanachama wote wilayani tarime, halafu nenda KLHN kwa mwanakijiji usikilize Wangwe na Lisu wanachosema,,,"kila wilaya inapata 100,000/= kila mwezi" na sio 400,000/= huyo katibu wa wilaya ni msaliti, mnafiki, kuwadi wa mbowe na mfuasi wa siasa za majitaka
 
na Mwandishi Wetu

Mgogoro Wa Uongozi Unaorindima Ndani Ya Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (chadema) Umeingia Katika Sura Mpya Baada Ya Makamu Mwenyekiti Wa Chama Hicho Aliyesimamishwa Hivi Karibuni, Bw. Chacha Wangwe, Kuwapa Siku 14 Viongozi Wa Chama Hicho Kuthibitisha Madai Yao Kwamba Anashirikiana Na Ccm Kukihujumu, Vinginevyo Atawafikisha Mahakamani.

Bw. Wangwe Ambaye Pia Ni Mbunge Wa Tarime Kwa Tiketi Ya Chama Hicho, Aliliambia Gazeti Hili Jana Kuwa Madai Ya Viongozi Hao Yamemchafulia Jina Na Heshima Kiasiasa Aliyoijenga Ndani Ya Chama Hicho Kwa Gharama Kubwa.

Wiki Iliyopita Katika Kikao Chake, Mjini Dodoma, Kamati Kuu Ya Chadema Chini Ya Mwenyekiti Wake, Bw. Freeman Mbowe, Ilimsimamisha Uongozi Bw. Wangwe Kwa Tuhuma Mbalimbali Ikiwamo Kutoa Siri Za Chama Hicho Kwa Viongozi Wa Ccm.

Bw. Wangwe Alituhumiwa Pia Kukashifu Chama Hicho, Viongozi Na Watendaji Wake, Bila Kutofautisha Kashfa Na Ukosoaji Wa Kisiasa Na Kiutendaji, Kwa Kutumia Wanachama Waliochukuliwa Hatua Za Kinidhamu Na Vikao Halali Vya Chama Hicho.

Tuhuma Zingine Ni Pamoja Na Kuwatuhumu Viongozi Wenzake Wa Juu Na Watendaji Wake Kwa Kuwahusisha Na Ukabila Na Kuvujisha Siri Za Vikao Halali Vya Chama Kwa Watu Wenye Lengo La Kukihujumu Chama Hicho.

Akizungumza Katika Ofisi Za Gazeti Hili Dar Es Salaam Jana, Bw. Wangwe Alipinga Madai Hayo Na Kueleza Kuwa Hayana Msingi Na Kwamba Katika Kipindi Chote, Ameipigania Chadema Kwa Nguvu Zake Zote Na Gharama Kubwa, Bila Kuogopa Mazingira Magumu Kwenye Harakati Hizo.

Alisema Akiwa Kiongozi Wa Chama Hicho Wilayani Tarime, Alinyakua Jimbo Hilo Na Halmashauri Ya Wilaya Hiyo Huku 'wapiganaji' Wenzake Wakijeruhiwa Kwa Vipigo, Kupata Vilema Vya Maisha, Kupoteza Ajira Na Hata Maisha.

Kutokana Na Harakati Hizo, Waliwezesha Kupatikana Asilimia 64 Ya Kura Za Jimbo Hilo Ambazo Zilichangia Ushindi Wa Chadema Na Kuiwezesha Kupata Ruzuku Ya Sh. Milioni 66 Kila Mwezi Na Viti Maalumu Sita Bungeni Vya Chama Hicho.

Alisema Jitihada Zake Zilimfanya Mgombea Urais Kwa Tiketi Ya Chadema, Bw. Mbowe Kuibuka Na Kura Nyingi Kumzidi Mgombea Wa Ccm, Rais Jakaya Kikwete Wilayani Humo, Kwenye Uchaguzi Mkuu Uliopita Mwaka 2005.

Akizungumzia Uhusiano Wake Na Dkt. Amani Kabourou Ambaye Alikihama Chama Hicho Na Kwenda Ccm, Alisema Ni Wa Siku Nyingi Hata Kabla Ya Kujiunga Na Ccm Na Uhusiano Huo Haufungamani Kwa Namna Yoyote Ile Na Masuala Ya Kisiasa Kama Inavyodaiwa Na Viongozi Wa Chadema.

"dkt. Kabourou Nashirikiana Naye Siku Nyingi Tangu Aliporudi Kutoka Marekani, Naheshimu Uamuzi Wake Wa Kwenda Ccm Na Huo Ni Uamuzi Wake Mwenyewe, Tangu Aende Ccm Sijakutana Naye Bali Juni 7 Mwaka Huu, Nilikwenda Kwake Kuhani Msiba Wa Mama Yake Mzazi Tukiwa Na Bibi Maulida Anna Komu," Alisema Bw. Wangwe.

Bw. Wangwe Alishangaa Suala Hilo Kuhusishwa Na Hujuma Dhidi Ya Chama Hicho Na Kuzidi Kufafanua Katiba Ya Chadema Haina Kipengele Kinachozuia Mwanachama Kuwa Na Uhusiano Na Wanachama Wa Vyama Vingine, Bali Tofauti Iliyopo Ni Hoja.

Alimshambulia Mwenyekiti Wa Chama Hicho, Bw. Mbowe Kwa Maelezo Kuwa Amekuwa Karibu Zaidi Na Viongozi Wengi Wa Ccm Na Wakati Mwingine Wanakutana Faragha, Lakini Kama Mwanachama Ana Uhuru Wa Kufanya Hivyo Na Hakuna Anayempinga Kwa Hilo.

"dkt. Slaa (wilbroad), Mkewe Ni Kada Wa Ccm Aliyekubuhu Ni Diwani Wa Kuchaguliwa Wanakaa Pamoja, Simu, Nyaraka Zote, Wageni Wote Wanaokuja Mama Anasikiliza, Hawanitendei Haki Mimi Kwa Hili," Alisema Bw. Wangwe.

Alisema Kuengulia Kwake Ni Mkakati Ulioandaliwa Muda Mrefu Kumng'oa Kwenye Nafasi Hiyo, Kutokana Na Dhamira Yake Ya Kutaka Kufanyika Mageuzi Ya Kweli Ndani Ya Chama Hicho.

"nilisema Uongozi Uliopo Tutaupumzisha, Kwani Umeshindwa Kupeleka Chama Mbele," Alisema Mbunge Huyo Machachari Na Kusisitiza Kuwa Ajenda Ya Kumsimamisha Uongozi Haikuwa Kwenye Mkutano Wa Dodoma Ila Kilichokuwapo Ni Kuwasilishwa Ripoti Ya Tume Ya Mzirai, Iliyoundwa Kuchunguza Tuhuma Mbalimbali Ndani Ya Chama Hicho, Lakini Suala Hilo Likaibuliwa.

alibainisha Kuwa Tofauti Iliyojitokeza Kati Yake Na Bw. Mbowe, Ni Suala La Mgawanyo Wa Ruzuku Kati Ya Makao Makuu Kwa Upande Mmoja Na Wilaya Kwa Upande Mwingine, Jambo Alilosema Kwa Muda Mrefu Amekuwa Akipigia Debe Chama Hicho Kujijenga Kuanzia Chini Kwenda Juu, Jambo Linalokinzana Na Msimamo Wa Mwenyekiti Wake.

"ninachopigania Ni Mfumo Wa 'bottom Up' (kuanzia Chini Kwenda Juu) Fedha Zipelekwe Kwenye Vitovu Vya Mapambano Zikajenge Chama Kwenye Maeneo Ambayo Hakipo, Lakini Wenzangu Wanataka Mfumo Wa 'up Bottom' (juu Kwenda Chini).

Alisema Gharama Za Kuendesha Chama Wilayani Ni Ndogo, Kwani Endapo Kila Mwezi Zitapelekwa Sh. 100,000 Zitatosha Kulipa Pango La Ofisi Linaloweza Kugharimu Kati Ya Sh. 25,000 Hadi 30,000 Na Sh. 70,000 Zikabaki Kwa Matumizi Mengine Ya Ofisi. Mbali Na Fedha Hizo, Alishauri Pia Kutolewa Sh. 100,000 Nyingine Kwa Ajili Ya Kulipa Wasimamizi Wa Ofisi Hizo.

"yeye (bw. Mbowe) Anataka Fedha Zitumike Kwa Helikopta, Sisemi Kwamba Helikopta Ni Kitu Kibaya, Lakini Tuangalie Katika Mruko Tulipata Watu Wangapi? Lazima Tuwe Na Majimbo, Wanachama Na Matawi Ya Kutosha, Hata Kama Ccm Itatuzidi Nguvu, Basi Angalau Tupate Majimbo 150, Hata Ruzuku Itapanda.

Alipinga Kile Alichokiita Madeni Hewa Wanayojilipa Viongozi Wakuu Wa Chama Hicho Kwa Madai Ya Kukikopesha Chama Hicho Wakati Wa Uchaguzi Mkuu Uliopita, Ambapo Alisema Bw. Mbowe Alidai Kuikopesha Chadema Sh. Milioni 500, Bw. Philemon Ndesamburo Sh. Milioni 100 Na Bibi Grace Kiwelu Sh. Milioni 100

"nilipochaguliwa Umakamu Niligundua Udhaifu Huu, Mfano Kuhitilafiana Wakati Baraza Kuu Linatoa Ratiba Ya Uchaguzi Wa Ndani Ngazi Zote...baadhi Uchaguzi Hautafanyika Kwa Sababu Hakuna Fedha Zilizotolewa.

"tutapataje Chama Chenye Uhai Kama Hakuna Fredha Za Kuwaewezesha Wanachama Kugombea? Sheria Ya Vyama Inasema Wazi, Kuwa Msajili Wa Vyama Atafuta Chama Kisipochaguana Kwa Kuzingatia Taratibu Zilizopo. Kwa Mwendo Huu Tutazamie Mamluki Bila Uchaguzi," Alisema.

alidai Kuwa Hadi Sasa, Bw. Mbowe Ameshajilipa Sh. 218,330,543.

Kuhusu Ubaguzi Wa Kikabila, Alikariri Taarifa Ya Tume Ya Mzirai Iliyobaini Kuwa Ubaguzi Huo Upo Ikisema Katika Uongozi Wa Juu Wa Chama Hicho, Wakurugenzi, Wenye Watu Wanane, Wanne Ni Kutoka Kaskazini (wachagga).


Alisisitiza Nia Yake Ya Kupinga Kusimamishwa Kwa Kutumia Vikao Vya Juu Vya Chama Hicho Ikiwa Ni Pamoja Na Baraza Kuu, Mkutano Mkuu Na Hata Kulifikisha Suala Hilo Kwa Wanachama Kama Vik

First Lady...pls Tell The President To DO THE People's Job And Not Thre Party's Job!(ccm) Or at least you should advise him to do so!
It Is The Duty For Your Husband To Give Us The Freedom We Want....then The Political Parties Later!
 
Najibu moja kuhusu Kabourou ni kuwa aliondoka CHADEMA baada ya kushindwa ubunge hivyo madai ya huyu aliyejiita kiongozi ambaye anaogopa kutaja jina lake ni uzushi .

Si kweli yeye alisema amechoshwa na viongozi wababaishaji, wababe na wenye kuendekeza ukabila katika chama...ndicho kilichomuondoa chadema kwa mujibu wake otherwise also haya ni majitaka tu...
 
It Is The Duty For Your Husband To Give Us The Freedom We Want....then The Political Parties Later!

Acha jazba wewe....kwa mtazamo wangu umemtukana mtu hapo...sio vizuri chekecha maneno na uonyeshe hekima yako kwa kuficha upu....... wako sio vizuri hapa hoja iliyoko mezani kujadili kuhusu msimamo wa chadema kuhusu Wangwe,,acha Lugha chafu na
 
jmushi1 It Is The Duty For Your Husband To Give Us The Freedom We Want....then The Political Parties Later![/QUOTE said:
Bahati mbaya sijaolewa!ila nikiolewa and as i beliave he will be a future president of TZ!nitamueleza siku akiwa Raisi
 
Nashukuru umeliona hilo japo hili ndio mkakati wenyewe ambao umepangwa kuhakikisha kuwa hatudai ripoti ya EPA hata baada ya muda wa kamati kwisha .

Najibu moja kuhusu Kabourou ni kuwa aliondoka CHADEMA baada ya kushindwa ubunge hivyo madai ya huyu aliyejiita kiongozi ambaye anaogopa kutaja jina lake ni uzushi .

MK,

Kabouru amewahi kushindwa ubunge mara ngapi Kigoma? Mbona safari hizo zote hakuondoka?

Binafsi naona ni very cheap politics kusema aliondoka baada ya kushindwa ubunge. Tatizo hapo ni kushindwa kwenu kushughulikia malalamiko ya wanachama wenu na mnakimbilia kwenye majibu ya haraka haraka.

Pia kama mliona EPA ni muhimu sana, kwanini muanze kufukuzana kipindi ambacho EPA inatakiwa ijadiliwe kwa nguvu zote?

Kama mnaendesha siasa kwa mtindo huo, tegemeeni kuwa upinzani kwa muda mrefu sana.
 
Mtanzania,

Umeuliza swali zuri sana kwa MK kuwa kwa nini waanze kufukuzana kipindi ambacho EPA ilitakiwa ijadiliwe kwa nguvu zote ? Jibu alilitoa mwanzoni aliposema kuwa Wangwe alikuwa na kikao na Rostam Kempinsiki kwa masaa 4. Wangwe hawezi kupangiwa watu wa kukutana naye. Lakini katika mazingira haya kwa nini tusiamini kuwa haya yote yanayotokea ni mkakati wa mafisadi wa EPA kuhakikisha EPA haijadiliwi ? Kama MK anafahamu hadi fedha iliyowekwa kwenye akaunti ya mke wa Wangwe toka kwa mafisadi basi tatizo ni zito kuliko wengi tunavyofikiria. Kama Wangwe alikuwa mmoja wa makamanda tuliowaamini, na bila kutaraji anageuzia mtutu kwa wale aliotakiwa kuwalinda, afanyweje ?
 
naipenda sana CHADEMA lakini sasa naona wameanza kuharibu kiukweli kama swala ni marafiki na maongezi mbona mbowe washkaji au niite marafiki zake wengi ni wana CCM tena wale ambao huwezi kuwanunua hata kwa kiasi gani cha pesa hili halionekani na wanajuaje kama yupo pale kwakukimaliza chama na si kukiimarisha wana CHADEMA kuweni makini na huyo kiongozi wenu wa juu.
 
Acha jazba wewe....kwa mtazamo wangu umemtukana mtu hapo...sio vizuri chekecha maneno na uonyeshe hekima yako kwa kuficha upu....... wako sio vizuri hapa hoja iliyoko mezani kujadili kuhusu msimamo wa chadema kuhusu Wangwe,,acha Lugha chafu na

Umekunwa? Nini kimekuchokonoa?
Mbona kama ni jazba ni wewe nyerererist!Nyererelism failed before it actually started na unyerererist ndio ulioliuza TAIFA LETU!
 
Ndio hizo siasa za majitaka,,,huyo aliesema ni katibu wa chama wa wilaya na sio Tarime naomba urekebishe msemo wako, hayo ni maoni yake binafsi na sio tamko la wanachama wote wilayani tarime, halafu nenda KLHN kwa mwanakijiji usikilize Wangwe na Lisu wanachosema,,,"kila wilaya inapata 100,000/= kila mwezi" na sio 400,000/= huyo katibu wa wilaya ni msaliti, mnafiki, kuwadi wa mbowe na mfuasi wa siasa za majitaka
Nyerererist
Hebu nielewe maneno hayo sijayasema mimi,nimenukuuu habari ya gazeti,na ndio maana nikasema kama haya ni kweli basi jamaa kwisha,ila kwenye post zangu za nyuma kumbuka nimeomba Dr.slaa atupe maelezo ya ripoti ya Mzirai na pia wanaojua mambo ya wangwe waweke hadharani ili tumjudge fairly
 
CCM tukiangalia viongozi wa juu wa chama hicho na erikali kama ni waislamu na wote wanatoka mkoa mmoja au jirani jirani je, huo nao utakuwa ni udini au ukabila?
 
Umekunwa? Nini kimekuchokonoa?
Mbona kama ni jazba ni wewe nyerererist!Nyererelism failed before it actually started na unyerererist ndio ulioliuza TAIFA LETU!

Huo ni mtazamo wako na ukubwa wa upeo wako ndipo unapokomea na siwezi kukulaumu wewe.....na siwezi kubishana na wewe maana we know u mkurupukaji usipoangalia utakua Banned tena ubadili jina na uwe mushij1 kama siku ile,,,,mie nimekwambia tumia lugha nzuri tatizo liko wapi? haya bwana Mushi (Mchaga)
 
Nyerererist
Hebu nielewe maneno hayo sijayasema mimi,nimenukuuu habari ya gazeti,na ndio maana nikasema kama haya ni kweli basi jamaa kwisha,ila kwenye post zangu za nyuma kumbuka nimeomba Dr.slaa atupe maelezo ya ripoti ya Mzirai na pia wanaojua mambo ya wangwe waweke hadharani ili tumjudge fairly

Samahani bwana,,nilichanganya lugha tu but my aim was namwambia huyo katibu wa wilaya,,,heshima yako mkuu
 
CCM tukiangalia viongozi wa juu wa chama hicho na erikali kama ni waislamu na wote wanatoka mkoa mmoja au jirani jirani je, huo nao utakuwa ni udini au ukabila?

Hata madereva, walinzi na viti maalum??? Hata mie nawasupport Chadema but Watatue hilo swala kwa manufaa ya chama
 
Kura zilikuwa ni 24 kwa 7. Mbowe alitowa taarifa akisaidiwa na Lusu na watendaji wakuu wengine. Wangwe ndo anasema wengine wote kwenye kamati wamenyamaza. Nahisi Wangwe nae anyamaze asubiri vikao halali kama kweli anahoja ya msingi ili chama kiwe imara na kama kweli anaitakia mema nchi hii.

Hata wanachama wa ccm wangependa mpaka kwenye mashina wapate pesa ya ruzuku lakini hawapati akitokea hata RA na EL wakisema hilo wataungwa mkono na wengi.
Akitaka afanikiwe atulie afate vikao halali.

Kama kuna matatizo kama hayo watu kutumia pesa binafsi basi wajisahihishe ila kusema kuwa CHADEMA ni NGO ya akina Mbowe, mh hata akina sisemi. AKILI KICHWANI
 
Back
Top Bottom