CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Hivi kwani CCM mlikosa wanawake mpaka wabunge wenu wengi wa viti maalum ni wachaga kuliko makabila mengine? Ama Kikwete alikosa mawaziri kwenye baraza lake lililopita mpaka akateua wengi wa Kilimanjaro kuliko makabila mengine?

Hivi CHADEMA ilikosa makabila mengine mpaka ikateua wasukuma wengi zaidi katika wakurugenzi na maofisa wake waandamizi katika makao makuu ya chama?

Hivi Mbowe alikosa makabila mengine mpaka akateua wahaya wawili Profesa Baregu na Balozi Ngaiza katika nafasi zake za kuteua wajumbe wa kamati kuu?

Ukabila, ukabila ukukabila. Hata mie Asha leo nikiolewa na Mmakonde mtanivua ungazija wangu kama mlivyomfanyia Maulidah Anna Komu- mlaniwe wanaume nyie.

This is male chauvisism of the highest order. Shame on you Mtanzania

Asha

Who cares if somebody is a chagga or woman? who cares if CCM has more muslims than christians, who cares for what is somebody's made up of before any choice can be made?

This is below our level. Let's get over these dividing lines guys.
 
Kitila Mkumbo,
Mkuu kama ulikuwa akilini wangu, heshima kubwa sana kwako na huu ndio moyo wa kizalendo...

Bi. Asha Abdalla,
Bibie nakuomba samahani kwani binafsi sikubaliani na kile ulichokisema kuhusiana na Wangwe. Hakuna mtu hapa anataka kuzungumzia Wangwe kama Wangwe isipokuwa hoja zake. Kupakana matope bibie haitatufikisha kokote, kesho Wangwe pia atakuja na matusi zaidi ambayo hayajengi sifa ya mtu yeyote wala chama...Yaani sasa hivi ndio mnaharibu kabisaaaa!..

Nirudi kwenye mada husika - Nakuomba uniamini ktk hili kwamba hata kama mliunda kamati ya wanawake kufanya uteuzi huo basi kulifanyika makosa ktk uteuzi.. Kinachozungumziwa hapa ni kupitia maamuzi ambayo yana dosari aidha yalifanywa na viongozi ama kamati...Hakuna haja ya Wangwe azungumze lakini kama unakumbuka hii hoja imekuwepo hapa kijiweni miaka na kila mara mimi binafsi ilinikera kwa sababu ndio picha inayoonekana huko nje. na nje ndiko Chadema wanakotegemea kura za wananchi ambao malezi yao yote toka wakati wa Nyerere hili neno Ukabila ama Udini ni haramu...
Sasa kama wananchi watafikiria hata kwa chembe kuwa ndani ya chama Chadema kuna Ukabila na kumetokana na uchaguzi huo wa wabunge wa viti maalum then, inabidi wewe na wenzako mlioko ktk kamati hiyo mfahamu kwamba maamuzi yenu yalikuwa na makosa ama hayakuangalia athari za maamuzi kama hayo...
Nimefurahi sana uliposema kwamba Chama (Uongozi wa chama) Uliwapa nafasi na jukumu Wanawake kuchagua wabunge hao - swadakta!.. heshima kubwa sana kwa kina mama, lakini mama zangu, dada zangu kubalini hamkuona upende huo ambao ungeweza kuzua hoja kavu kama hii.. na kwa bahati mbaya sasa hivi inapata maji na mmea unakuwa. uchaguzi upo kona tu hapo unajikongoja taratibu kwa madaha!..
Na shukrani nyingine umeweza kuwasafisha viongozi wa juu Chadema ambao ni wanaume kwamba hawakushiriki ktk uteuzi huo, hivyo inaondoa dosari ya madai ya Wangwe kuhusiana na swala hilo..yet, bado picha inaonyesha wazi kwamba uchaguzi wenu (kamati ya wanawake) haukuwa wazi zaidi kutazama nje ya vivuli vyenu mkaweza kuona athari za uteuzi kama huo...
Binafsi nitashukuru sana kama utatueleza ni vigezo gani mlitumia kuwachagua hao wabunge..
 
....
Bi. Asha Abdalla, ...
Binafsi nitashukuru sana kama utatueleza ni vigezo gani mlitumia kuwachagua hao wabunge..

Mkandara..hilo ndilo swali la msingi kabisa kuulizwa na ndilo linalotoa majibu kwenye mada ile ya CCM na hii hapa. Jibu lake ndilo kiini cha tatizo au suluhisho.
 
Hawezi kwa sababu alifanya makusudi kwa malengo mahsusi ya kujaribu kunizushia jambo akiamini kwamba ningekaa kimya. Ambacho hakujua ni kwamba hapa JF ukisema kitu unajibiwa, huwezi kujisemea na watu wakakuacha. Wengine tunaamini kabisa ile falsafa kwamba uongo ukisemwa bila kukanushwa mwishowe huonekana kuwa ni kweli. Sasa nimembana hapa hadi kumpa habari zangu personal kabisa tangu nikiwa sekondari amebaki kubwabwaja maneno mengi.

Kitila Mkumbo amewahi kusema uongo zaidi ya mara mbili hapa hapa JF,kwanza ilikuwa GT anasema kuwa mwanasiasa ni Kitila Mkumbo akabisha sana lakini siku akaja kubadili jina kutoka Mwanasiasa na kuwa Kitila Mkumbo hiyo ilikuwa 2007.
Kitila huyo huyo ilisemwa yuko Ulaya na ni UK, akabisha baadaye akawa yuko kwenye shughuli za watu wa ulaya na mikutano kiasi cha kulumbana na Balozi Mwanaidi Majaar.

Mtu mwingine ambaye ni mwongo ni Fikira Duni kila likija jambo anaweka kinga ya kusema ni Udaku na uzushi,GT aliweka hoja kuwa Membe anamiliki kampuni ya vitambulisho na huo mradi una ufisadi akadaiwa ushahidi na kuambiwa aombe radhi kwa kuwa mwongo.
Ikaja habari ya Membe ya kugombea urais 2010 ikasemwa kuwa ni uzushi na kuna habari ya Tido na Suzane Mungi bwana Fikira Duni akaja juu na kulalama kuwa ni majungu, uzushi na udaku, habari ya vitambulisho Jenerali Ulimwengu alipoipata hapa JF akaifanyia kazi hadi sasa anaendeleza libeneke lakini mwanzo ilisemwa ni uzushi iko www.raiamwema.co.tz kwa zaidi ya matoleo manne yanaeleza habari hiyo.
baada ya FD kuonekana anatumia kinga ya udaku kuficha hoja au kuzima hoja hasa zenye maslahi kwake kwani ni rafiki wa Mwikalo anayeshiriki kutuibia kwenye mradi wa vitambulisho,sasa ameamua kubadili jina lake na kujiita Fair Player.

Fikira Duni na Kitila wamezusha mengi kiasi cha kusema kuwa DR.Warioba hana sifa za kuwa mkuu wa chuo cha Mzumbe, lakini vijana wa Mzumbe hawakusema kuwa tupeni ushahidi ndani ya 24 hours tuliwapa miezi na sasa ni miaka wameshindwa kuthibitisha uongo wao.
kwa maneno yangu ya hapo juu nathibitisha na kuwaomba wana JF hasa GT aje kututhibitisha uongo na ubabaishaji wa Msomi wa Udsm Bwana Kitila Mkumbo, kama aliwahi kulikataa jina lake halisi kipi kitamshinda kukataa kumfuata Mrema alipokuwa huko TLP? au akimuona mtu kashuka kisiasa anaona hafai? ni kweli Mkumbo anatabia hiyo ya uongo na ushahidi uko kwenye maandiko yake hapa hapa jamvini,tumemaliza kesi.

Chacha Wangwe.

Ni mpambanaji mkubwa na anaonewa na Mbowe kwa sababu ni mkweli na muwazi, viti maalum mkoa wa Mara haukupewa kiti hata kimoja wakati mkoa wa Mara hasa TARIME ndio waliopiga kura nyingi kwa upinzani,sielewi Mara haikupewa mbunge mmoja wa viti maalum, wamekwenda kuwapa wachagga watupu,CUF wametoa viti maalum kutokana na kura zinazopatika kwenye mkoa mfano mkoa wa TANGA wamempa mtu kutokana na kura nyingi walizopigiwa,Pemba wamewapa viti maalum kwa kura walizopata,basi wangewapa Sumbawanga kwani Musoma mnawachukia,mchukieni WANGWE kama mlivyomchukia DR.Warioba lakini kazi zao mnaziona. wangwe kapata kura nyingi Tarime kumshinda Slaa, Zitto hadi ALFU.

Nakushukuru kwa kuleta ushahidi wa wazi,kumbe jamaa hakuwa mkweli hapa hapa jamvini? wazungu wanasema' liers should have good memory' labda alipitiwa hakujua mpo wazee wa data na kumbukumbu.
Mie nimetaja mashahidi wangu wa kuthibitisha hilo na shahidi namba moja nimemtoa upande wao Zitto KABWE akasema atamleta imekuwa kimya, nina mashahidi zaidi ya watano, tena siku zote the burden of evidence mounts the defence'side hiyo ndio sheria.
 
Na Mwandishi Wetu

MGOGORO wa uongozi unaorindima ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeingia katika sura mpya baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho aliyesimamishwa hivi karibuni, Bw. Chacha Wangwe, kuwapa siku 14 viongozi wa chama hicho kuthibitisha madai yao kwamba anashirikiana na CCM kukihujumu, vinginevyo atawafikisha mahakamani.

Bw. Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, aliliambia gazeti hili jana kuwa madai ya viongozi hao yamemchafulia jina na heshima kiasiasa aliyoijenga ndani ya chama hicho kwa gharama kubwa.

Wiki iliyopita katika kikao chake, mjini Dodoma, Kamati Kuu ya CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, ilimsimamisha uongozi Bw. Wangwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kutoa siri za chama hicho kwa viongozi wa CCM.

Bw. Wangwe alituhumiwa pia kukashifu chama hicho, viongozi na watendaji wake, bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na kiutendaji, kwa kutumia wanachama waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama hicho.

Tuhuma zingine ni pamoja na kuwatuhumu viongozi wenzake wa juu na watendaji wake kwa kuwahusisha na ukabila na kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wenye lengo la kukihujumu chama hicho.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam jana, Bw. Wangwe alipinga madai hayo na kueleza kuwa hayana msingi na kwamba katika kipindi chote, ameipigania CHADEMA kwa nguvu zake zote na gharama kubwa, bila kuogopa mazingira magumu kwenye harakati hizo.

Alisema akiwa kiongozi wa chama hicho wilayani Tarime, alinyakua jimbo hilo na halmashauri ya wilaya hiyo huku 'wapiganaji' wenzake wakijeruhiwa kwa vipigo, kupata vilema vya maisha, kupoteza ajira na hata maisha.

Kutokana na harakati hizo, waliwezesha kupatikana asilimia 64 ya kura za jimbo hilo ambazo zilichangia ushindi wa CHADEMA na kuiwezesha kupata ruzuku ya sh. milioni 66 kila mwezi na viti maalumu sita bungeni vya chama hicho.

Alisema jitihada zake zilimfanya mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Mbowe kuibuka na kura nyingi kumzidi mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wilayani humo, kwenye uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2005.

Akizungumzia uhusiano wake na Dkt. Amani Kabourou ambaye alikihama chama hicho na kwenda CCM, alisema ni wa siku nyingi hata kabla ya kujiunga na CCM na uhusiano huo haufungamani kwa namna yoyote ile na masuala ya kisiasa kama inavyodaiwa na viongozi wa CHADEMA.

"Dkt. Kabourou nashirikiana naye siku nyingi tangu aliporudi kutoka Marekani, naheshimu uamuzi wake wa kwenda CCM na huo ni uamuzi wake mwenyewe, tangu aende CCM sijakutana naye bali Juni 7 mwaka huu, nilikwenda kwake kuhani msiba wa mama yake mzazi tukiwa na Bibi Maulida Anna Komu," alisema Bw. Wangwe.

Bw. Wangwe alishangaa suala hilo kuhusishwa na hujuma dhidi ya chama hicho na kuzidi kufafanua Katiba ya CHADEMA haina kipengele kinachozuia mwanachama kuwa na uhusiano na wanachama wa vyama vingine, bali tofauti iliyopo ni hoja.

Alimshambulia Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Mbowe kwa maelezo kuwa amekuwa karibu zaidi na viongozi wengi wa CCM na wakati mwingine wanakutana faragha, lakini kama mwanachama ana uhuru wa kufanya hivyo na hakuna anayempinga kwa hilo.

"Dkt. Slaa (Wilbroad), mkewe ni kada wa CCM aliyekubuhu ni Diwani wa kuchaguliwa wanakaa pamoja, simu, nyaraka zote, wageni wote wanaokuja mama anasikiliza, hawanitendei haki mimi kwa hili," alisema Bw. Wangwe.

Alisema kuengulia kwake ni mkakati ulioandaliwa muda mrefu kumng'oa kwenye nafasi hiyo, kutokana na dhamira yake ya kutaka kufanyika mageuzi ya kweli ndani ya chama hicho.

"Nilisema uongozi uliopo tutaupumzisha, kwani umeshindwa kupeleka chama mbele," alisema Mbunge huyo machachari na kusisitiza kuwa ajenda ya kumsimamisha uongozi haikuwa kwenye mkutano wa Dodoma ila kilichokuwapo ni kuwasilishwa Ripoti ya Tume ya Mzirai, iliyoundwa kuchunguza tuhuma mbalimbali ndani ya chama hicho, lakini suala hilo likaibuliwa.

Alibainisha kuwa tofauti iliyojitokeza kati yake na Bw. Mbowe, ni suala la mgawanyo wa ruzuku kati ya makao makuu kwa upande mmoja na wilaya kwa upande mwingine, jambo alilosema kwa muda mrefu amekuwa akipigia debe chama hicho kujijenga kuanzia chini kwenda juu, jambo linalokinzana na msimamo wa mwenyekiti wake.

"Ninachopigania ni mfumo wa 'bottom up' (kuanzia chini kwenda juu) fedha zipelekwe kwenye vitovu vya mapambano zikajenge chama kwenye maeneo ambayo hakipo, lakini wenzangu wanataka mfumo wa 'up bottom' (juu kwenda chini).

Alisema gharama za kuendesha chama wilayani ni ndogo, kwani endapo kila mwezi zitapelekwa sh. 100,000 zitatosha kulipa pango la ofisi linaloweza kugharimu kati ya sh. 25,000 hadi 30,000 na sh. 70,000 zikabaki kwa matumizi mengine ya ofisi. Mbali na fedha hizo, alishauri pia kutolewa sh. 100,000 nyingine kwa ajili ya kulipa wasimamizi wa ofisi hizo.

"Yeye (Bw. Mbowe) anataka fedha zitumike kwa helikopta, sisemi kwamba helikopta ni kitu kibaya, lakini tuangalie katika mruko tulipata watu wangapi? Lazima tuwe na majimbo, wanachama na matawi ya kutosha, hata kama CCM itatuzidi nguvu, basi angalau tupate majimbo 150, hata ruzuku itapanda.

Alipinga kile alichokiita madeni hewa wanayojilipa viongozi wakuu wa chama hicho kwa madai ya kukikopesha chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo alisema Bw. Mbowe alidai kuikopesha CHADEMA sh. milioni 500, Bw. Philemon Ndesamburo sh. milioni 100 na Bibi Grace Kiwelu sh. milioni 100

"Nilipochaguliwa umakamu niligundua udhaifu huu, mfano kuhitilafiana wakati Baraza Kuu linatoa ratiba ya uchaguzi wa ndani ngazi zote...baadhi uchaguzi hautafanyika kwa sababu hakuna fedha zilizotolewa.

"Tutapataje chama chenye uhai kama hakuna fredha za kuwaewezesha wanachama kugombea? Sheria ya vyama inasema wazi, kuwa Msajili wa Vyama atafuta chama kisipochaguana kwa kuzingatia taratibu zilizopo. Kwa mwendo huu tutazamie mamluki bila uchaguzi," alisema.

Alidai kuwa hadi sasa, Bw. Mbowe ameshajilipa sh. 218,330,543.

Kuhusu ubaguzi wa kikabila, alikariri taarifa ya Tume ya Mzirai iliyobaini kuwa ubaguzi huo upo ikisema katika uongozi wa juu wa chama hicho, wakurugenzi, wenye watu wanane, wanne ni kutoka Kaskazini (Wachagga).


Alisisitiza nia yake ya kupinga kusimamishwa kwa kutumia vikao vya juu vya chama hicho ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na hata kulifikisha suala hilo kwa wanachama kama vik
 
Chacha alishika nafasi ya juu sana kwenye CHADEMA, anapokuwa na claims kama hizi ni lazima zifanyiwe uchunguzi wa kina kabla ya kuzidismiss kuwa ni uzushi au ni umamluki.

Mfano swala la kusema kuwa amefanya vikao vya siri na Kabourou ni ridiculous.Kwani katiba ya CHADEMA inawakataza viongozi wake kukutana na wanachama wa vyama vingine?
 
Waliomsimamisha UMAKAMU hawakupata muda wa KUMSIKILIZA? Kura zile 24/7 zilitokana na nini?
 
Chacha alishika nafasi ya juu sana kwenye CHADEMA, anapokuwa na claims kama hizi ni lazima zifanyiwe uchunguzi wa kina kabla ya kuzidismiss kuwa ni uzushi au ni umamluki.

Mfano swala la kusema kuwa amefanya vikao vya siri na Kabourou ni ridiculous.Kwani katiba ya CHADEMA inawakataza viongozi wake kukutana na wanachama wa vyama vingine?

Sio Kabourou tuu aseme na kwa RA alipokutana naye Kilimanjaro Kempinsik room namba 210 kwa masaa manne walienda kufanya nini?

Utajitahidi sana kumtetea na wewe Ballile acha mchezo huo na gazeti lako.
 
kwa mwendo huu ndio chadema mtazidi kujijengea jina la ukabila maana kila mtu anakua anawakimbia hasa anaposhika madaraka ya juu,,,alianza Kabourou na wangwe mtampoteza na ataefuata ni Zito na Mnyika coz watu tunafaham they are not happy though you can try to deny the fact
 
Sio Kabourou tuu aseme na kwa RA alipokutana naye Kilimanjaro Kempinsik room namba 210 kwa masaa manne walienda kufanya nini?

Utajitahidi sana kumtetea na wewe Ballile acha mchezo huo na gazeti lako.

Kumbe hivyo tena hii ni hatari ama kweli.........!kwa hiyo mtu akiwa let say NCCR ni marufuku kuwa na maongezi na mtu wa CCM?
hilo lipo kwenye katiba ya chadema?
 
Kumbe hivyo tena hii ni hatari ama kweli.........!kwa hiyo mtu akiwa let say NCCR ni marufuku kuwa na maongezi na mtu wa CCM?
hilo lipo kwenye katiba ya chadema?

Hapa hata mie ninaona kuna harufu ya "UKABILA" coz sioni kama hiyo ni point kwa chama kinachothamini democracy na kinaendeshwa na watu wapenda siasa za kisasa
 
Chadema ni chama makini, ka alivyowahi kukiri baba wa taifa, ccm watatumia kila njia kukivuruga, wakitumia pesa za epa, richmond nk. ambazo zimetumika kuanzisha au kununua vyombo vya habari, kama new habari corruption na vingine vingi, hata kuwanunua baadhi ya watu ndani ya chadema
 
Kumbe hivyo tena hii ni hatari ama kweli.........!kwa hiyo mtu akiwa let say NCCR ni marufuku kuwa na maongezi na mtu wa CCM?hilo lipo kwenye katiba ya chadema?

Swala siyo kuzuiwa kuwa na maongezi na wengine, jambo la msingi hapa ni maneno yako na matendo yako baada ya kukutana na watu hao!
Leo hii tunaambiwa wapiga kura wake Wangwe wamepinga madai yake kwamba hela ya ruzuku haipelekwi mikoani!,

Tunashuhudia kukurupuka kwake anapodai eti Mbowe ndo huwa anaenda kufanya mikutano ya siri na CCM!

Kwa mtu yeyote mwenye kuweza kufikiria tu, ataona commitment ya Wangwe kwa chama chake ina mashaka, yumkini ni pandikizi la kukidhoofisha chama period!
 
hapo kweli sasa naona Wangwe wamemwonea na madai yake ni ya msingi kabisa.
Chama kinajengwa kuanzia chini kisha kinapamba taratibu laiti wangelijua hili mapema CHADEMA ingekuwa juu sana sasa hivi lakini wao ndo wamebolonga.
Kwa mtindo huu ukabila na up to bottom CHADEMA hamfiki mbali hii ipo wazi mtapoteza mwelekeo na kwenda ICU kabisa...jipangeni upya ondoeni tofauti zenu haraka sana.
 
Hizi siasa za maji taka( sitta 2008) zitaisha lini?Lile jinamizi lililoikumba NCCR Mageuzi ya akina Lyatonga Mrema na Mabere Nyaucho Marando sasa limeingia CHADEMA.
Kama kweli mtu anauza haki ya wananchi kwenye chumba 210 Kempsinki ni lazima awajibishwe,mafisadi sasa hivi wanatapata kweli wanatafuta watu wa kwenda nao uraiani.
 
Wangwe aje hapa na kusema kuwa ni kwanini Tangu issue ya Buzwagi hajawahi kuongelea suala la madini kama ilivyokuwa awali.

Barrick North Mara walikutana naye na kikao kiliendeshwa na Teweli sasa anapaswa kujua kuwa watu walikuwa wanamfuatailia kila kona ya njia zake na hata account ya mkewe ambayo ndio imekuwa ikitumika kuingizia hayo mafungu kutoka kwa mafisadi please lets be realistic na wa kweli .

Hivi Chacha leo ni mtu wa kwenda kujitetea kwenye magazeti ya majira na Mtanzania kweli ....Hamuoni tatizo hapo ?
 
yumkini ni pandikizi la kukidhoofisha chama period!

kwa jinsi tunavyoifaham historia ya wangwe sikubaliani na wewe hata kwa sekunde mbili,,,Mapandikizi ndani ya chadema yapo mengi sana lakini sio wangwe...wangwe amekua diwani siku nyingi sie tuna mfaham kwa muda sana na itikadi na misimamo yake inaeleweka...CHADEMA lazima wakubali kubadilika na sio vizuri kumchukia mtu anaewaambia ukweli...mkiendelea hivyo hatutaona tofauti yenu na CCM ambao huweza hata kumuua mtu anaesema ukweli
 
kwa jinsi tunavyoifaham historia ya wangwe sikubaliani na wewe hata kwa sekunde mbili,,,Mapandikizi ndani ya chadema yapo mengi sana lakini sio wangwe...wangwe amekua diwani siku nyingi sie tuna mfaham kwa muda sana na itikadi na misimamo yake inaeleweka...CHADEMA lazima wakubali kubadilika na sio vizuri kumchukia mtu anaewaambia ukweli...mkiendelea hivyo hatutaona tofauti yenu na CCM ambao huweza hata kumuua mtu anaesema ukweli

Humfahamu hata kidogo ,kwani usingesema kuwa amekuwa diwani wa siku nyingi...hii inaonyesha kuwa hujui.

Pili wewe kama unawajua hao mapandikizi wataje kwa majina yao sio kuishia kusema eti wapo wengi wapi hao?
 
Wangwe aje hapa na kusema kuwa ni kwanini Tangu issue ya Buzwagi hajawahi kuongelea suala la madini kama ilivyokuwa awali.

Barrick North Mara walikutana naye na kikao kiliendeshwa na Teweli sasa anapaswa kujua kuwa watu walikuwa wanamfuatailia kila kona ya njia zake na hata account ya mkewe ambayo ndio imekuwa ikitumika kuingizia hayo mafungu kutoka kwa mafisadi please lets be realistic na wa kweli .

Hivi Chacha leo ni mtu wa kwenda kujitetea kwenye magazeti ya majira na Mtanzania kweli ....Hamuoni tatizo hapo ?
What matters here je yale anayoyasema yana uzito gani?Haijalishi mtanzania majira au Tanzania Daima!
 
Suala la ukabila ni perception ya watu na nashangaa CHADEMA mnatumia muda mwingi
kukanusha lakini hisia sio rahisi kuiondoa kwa kukanusha na kuleta facts zilizo nusu nusu.

Binafsi naona hapo ndio mnakosea. CHADEMA kama chama cha siasa lazima mjitahidi kufanya juhudi kuondoa hiyo perception ya watu walio wengi.

Inawezekana CHADEMA hakuna ukabila lakini hiyo pekee haitoshi maana mnakuwa judged sio mahakamani bali kwenye hisia za watu wa kawaida mitaani. Mtu wa kawaida hawezi kuamini kwamba kuteua wabunge watano kati ya sita wenye uhusiano na mkoa anaotoka Mwenyekiti hakuna ukabila. Hata useme huyu alizaliwa wapi na yule wapi, unaweza kushinda mahakamani lakini sio kwenye opinions za watu wa kawaida mitaani. Hivyo hivyo mtu wa mitaani hawezi kutofautisha mfagiaji makao makuu ya CHADEMA na mkurugenzi wa CHADEMA. Wala ni ngumu kutofautisha aliyeajiriwa na Mwenyekiti kwa pesa zake au yule aliyeajiriwa na chama. Wanachoona ni namba kubwa ya wafanyakazi toka mkoa mmoja.

Nafikiri muhimu kwenye jambo kama hili ni kufanya jitihada za wazi kushughulikia tatizo lililopo hata kama kwa mawazo yenu sio kubwa.

Kama hamtaki kuongoza nchi basi endeleeni kulumbana na matokeo yatajulikana 2010.

Watanzania wana wasiwasi sana na watu toka makabila makubwa, viongozi toka hizo sehemu wanatakiwa kweli waonyeshe hawana hata chembe ndogo za ukabila. Mtu akitoka kabila dogo, hata akijaza watu wa kwao, ni watu wachache sana ambao hata wataanza kuuliza maswali.

Angalia perceptions mbalimbali za Watanzania miaka ya nyuma, Tanesco ya Wachaga, BIMA na NBC ya Wanyakyusa, Jeshi la Wakurya, Mlimani ya Wahaya nk. Kuna watu wengi waliamini hayo hata kama ungechunguza facts ungelikuta ni tofauti.

CHADEMA kama chama cha siasa lazima kifanye juhuzi za kutosha kuonyesha hakina ukabila. Kubishana hapa JF hakusaidii sana na badala yake huenda hata ambao walikuwa hawana uhakika sasa nao wanaanza kujenga opinions zao juu ya hili. Kwa mfano sikujua
wabunge watano kati ya sita wanauhusiano wa karibu anakotoka Mwenyekiti, mpaka niliposikia maelezo ya Lisu.

Hayo ndio mawazo yangu na mnaweza kuyapuuza kama mnaoma hayafai.
 
Back
Top Bottom