CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Wangwe ni YESU WA KABILA GANI?
WAKURYA?
NA CHENGE NI YESU WA WASUKUMA?
WEWE UNATAKA KULICHAGULIA KILA KABILA YESU WAKE?
NYIE MNATAKA KUANZISHA VITA BONGO?
Tutarudi huko na mnajuwa ni upande gani tupo?

Jmushi mbavu sina hapa nilipo!
Jamani nilitoa mfano tu kwa kumtumia YESU!lakini Wangwe siyo YESU.Kwa kifupi YESU siyo chenge wala wangwe! Chadema wafikirie uamuzi wao wa kumfukuza makamu wao,pia wayafanyie kazi madai yake!
 
Ila Hollo kama wewe ni CHENGE...The hauna UKABILA?

Chenge: Nimezushiwa

na Jane Kajoki, Bariadi



MBUNGE wa Bariadi Magharibi aliyejiuzulu uwaziri hivi karibuni kwa kashfa ya kukutwa na fedha zinazohusishwa na ufisadi, Andrew Chenge amewataka wananchi wa jimbo lake kuendelea kumwamini kwa kuwa yeye ni mtu safi na asiye na hatia yoyote kwani tuhuma dhidi yake ni za kuzushwa.
Mbali ya hilo, Chenge alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu zaidi ya wiki mbili zilizopita si kwa sababu ya kukiri makosa, bali ili kutoa fursa kwa taasisi zinazochunguza kashfa yake kufanya kazi yake kwa uwazi.
Chenge ambaye jana alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Bariadi Mjini, Ramadi, Nyakabimbi na Kapiwi, alisema wakazi wa Dar es Salaam ndio ambao wamekuwa wakimuona kuwa mtu asiyefaa kutokana na kubebeshwa tuhuma zisizo za ukweli, ikiwa ni pamoja na kuzushiwa kifo.
“Dar es Salaam wanasema sifai labda kwa sababu ya sura yangu...Pamoja na watu wa Dar es Salaam kupiga kelele kuwa sifai, naamini sina hatia yoyote, na ndiyo maana nilijiuzulu. Ninyi wakazi wa jimboni kwangu ndio mnajua kama sifai au nafaa.
“Haya mambo yaliyotokea ni ajali ya kisiasa. Ni mambo ya kupikwa na watu, lakini kwa tuhuma hizi wacha tuwape nafasi waendelee na uchunguzi. Sitakiwi kuzungumzia hilo kwa sasa, nimekuja nyumbani kuhimiza shughuli za maendeleo katika jimbo letu katika nyanja zote za barabara, elimu, afya na maji,” alisema Chenge ambaye alivuta umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimshangilia kila alipokuwa akihutubia.
Alisema pamoja na kujiuzulu uwaziri, aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake na akasema anaamini ifikapo mwaka 2010 atakuwa ametekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010.
“Walio na ndoto za ubunge tukutane kwenye hoja za utekelezaji wa ilani mwaka 2010. Mmeona tulivyojenga shule za sekondari, barabara, mabwawa, visima, vituo vya afya vyote hivyo ni katika jimbo letu. Pamoja na habari ya kuzushiwa kifo, nawaomba mtulie, tushirikiane kwa kutembea kifua mbele kufanya kazi na kujiletea maendeleo,” alisema Chenge ambaye anatembelea jimbo lake kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu.
Akiwa katika Kijiji cha Dutwa alisema alitaja vijisenti si kwa nia ya kukejeli bali akiwa na mtazamo wa Kisukuma ambao wao wanapoongelea ng’ombe 100 kwa mfano wanasema ‘vijing’ombe’.
Hii ni mara ya pili kwa Chenge kuzungumzia kauli yake ya vijisenti ambayo kwa kiwango kikubwa ndiyo inayoonekana kuwa iliyokuza tuhuma alizokuwa akihusishwa nazo.
Kwa mara ya kwanza, Chenge alizungumzia kauli yake hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya mahojiano kwa njia ya simu na gazeti hili, ambapo aliwaomba radhi Watanzania ambao walikwazika au kuumizwa na kauli yake hiyo ya vijisenti.
Alisema halikuwa lengo lake kuwakera wananchi kwa kauli hiyo iliyozua mjadala kiasi cha baadhi ya makundi ya watu wa kada tofauti kutoa maoni yao wakimtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe.
“Mimi siyo Mzaramo. Hiki ni Kiswahili. Sisi wengine kule Usukumani kusema vijimambo, au vijisenti, vijitoto hivi ni kawaida kwa desturi zetu...ndiyo maana napenda kusema wazi kwamba iwapo kuna Watanzania niliwaumiza kwa kauli ile niliyoitoa kwa nia njema kabisa na wala si kwa lengo la kuwakejeli, naomba radhi kwa hilo,” alisema Chenge wakati huo.
Tuhuma dhidi ya Chenge ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza likikariri taarifa kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini humo (SFO).
Gazeti hilo liliandika kuwa, uchunguzi wa SFO uligundua akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.
Gazeti hilo liliandika kwamba, SFO ilikuwa ikitarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zilikuwa na uhusiano na zile zinazoaminika kuwa zilitolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 70, mwaka 2002.
The Guardian katika habari yake hiyo liliripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo,” alisema Chenge.
Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Mbali ya hilo, gazeti hilo lilimkariri mwanasheria wa Chenge anayeishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani, J Lewis Madorsky, akikanusha kwa niaba ya mteja wake huyo, kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha zake na tuhuma zozote.
“Wakati tukitambua kuwa masuala hayo yalitokea muda mrefu uliopita, tunaweza tu tukathibitisha kuwa, tuhuma zozote za ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji wa maadili, kutenda isivyo sawa na mambo mengine ya hivyo dhidi ya mteja wetu ni mambo ambayo kimsingi tunayakanusha kwa nguvu kubwa,” alisema mwanasheria huyo wa Chenge. Hata hivyo, gazeti hilo liliandika uchunguzi huo dhidi ya Chenge unamfanya yeye kuwa tu shahidi muhimu, kwani wanaielenga zaidi BAE ambayo inadaiwa ilimlipa wakala mmoja wa Tanzania mamilioni ya fedha ili kujenga ushawishi wa rada iliyokuwa ikiiuza kununuliwa. Wakala huyo ambaye amekuwa akitajwa kwa muda mrefu, na ambaye sasa anaaminika kukimbia nchini na kutafutwa na polisi wa kimataifa ni, Shailesh Vithlani.
 
Jamani MKK kweli mtatushinda kwa kura kama ndo hata pesa za kuanzisha matawi wilayani mnabana?Sasa hizo kura mtazipata wapi za kuishnda CCM?

Angalau chadema hawaibi pesa BoT kugharimia chaguzi. That makes me sleep better at night.
 
Watu wa Mara ni shupavu na hawaburuzwi ndio maana tukawapa jeshi watuongoze kwani tunahitaji wenye msimamo na uwezo wa kuamua mambo.
watu wa mkoa kama Singida kwa Kitila hawana uwezo kuwa na maamuzi mazito au ya maana tunaweza kuwaita (wajumbe Ndiyo).

Kwahiyo kama wanaongoza jeshi wapewe na VYAMA?
Nimesema kuna nia ya MAKUSUDI KABISA YA KUVURUGA JITIHADA NA VITA YA UFISADI!
TUTAPAMBANA!
 
Kuhani,
Hili sio swala la ass kisser ni mila na Tamaduni ambazo zina malengo ya kukamilisha kitu kimoja...
Nimetumia harusi kama mfano hai ambao binafsi siwezi kusema ni hulka mbaya kwa upande wowote ule isipokuwa ni ktk Kuifahamisha jamii hii Utamaduni na mila za sehemu fulani. Leo hii Chadema wana deal na Tanzania nzima ni vizuri wakifahamu kinachowezekana Kilimanjaro sii lazima kiwezekane Mara..Kusema hivyo sio Ukabila hata kidogo!
Na kutokana na mjumuiko wa makabila mengi nchini ni lazima tuziheshimu sifa za waliochaguliwa hata kama hawakubaliki ktk mawazo ya baadhi yetu....hoja za mtu ni muhimu zijibiwe kwa hoja hata kama zinaashiria Ukabila kwa mtazamo wenu.
Hivyo mfano wa harusi haisemi kabisa kuwa Wachagga ni ass kisser isipokuwa ni Mila yao kuhakikisha harusi inafana... Wengine hata Michango ya harusi kuwafuata baadhi ya watu wenye uwezo badala ya nia kama vile leo hii ktk chaguzi za Marekani. Obama kawweza kuwaonyesha Wamarekani kwamba sii lazima kupata michango mikubwa kwa kutumia Lobbiest na kafanikiwa lakini haina maana wale wanaotumia ni ass kisser!..

Nachojaribu kuwakilisha kwenu ni kuonyesha kwamba Wangwe kachaguliwa na watu wenye kila aina ya uwezo wa Kieleimu, kifedha na isije kuwa wapo watu wanaofikiria kwamba elimu ndio CV kubwa ya mwenyekiti au makamu mwenyekiti.. Sii watu wote wanatazama hivyo.. Kachaguliwa na wanachama hivyo ni muhimu kuwepo na utaratibu mzuri zaidi ya huo uliotumika... Laa sivyo itakuwa kazi kubwa kuwafahamisha wananchi wanaokitazama chama hiki kama chama cha Maskini na Matajiri, wasomi na wale wasiokuwa na elimu..Nafasi za Uongozi ndani ya chama unatokana na uwezo wa mtu huyo kuendesha mabo ya chama yanayokubalika ama kuwavutia wananchi zaidi..malengo ya chama ni muhimu zaidi kutazamwa ktk darubini huru ya kifikra!
 
Watu wa Mara ni shupavu na hawaburuzwi ndio maana tukawapa jeshi watuongoze kwani tunahitaji wenye msimamo na uwezo wa kuamua mambo.
watu wa mkoa kama Singida kwa Kitila hawana uwezo kuwa na maamuzi mazito au ya maana tunaweza kuwaita (wajumbe Ndiyo).

Acha kashfa kwa watu wa Mara, watu wa Mara wanafanya kazi nyingi tu duniani na sio jeshi peke yake. WEwe unatia kinyaa sasa.
 
Jmushi mbavu sina hapa nilipo!
Jamani nilitoa mfano tu kwa kumtumia YESU!lakini Wangwe siyo YESU.Kwa kifupi YESU siyo chenge wala wangwe! Chadema wafikirie uamuzi wao wa kumfukuza makamu wao,pia wayafanyie kazi madai yake!

Umeamua kumtumia YESU hapa baada ya kugundua kuwa ccm ni chama cha kiislam na sasa unajifanya kutaja jina la YESU. Huna hata heshima kwa jina la YESU wewe?
 
Jmushi hapa tunazungumzia Chadema kumsimamishaWANGWE!Mambo ya chenge yanaingiaje tena jamani?
 
Kuhani,
Hili sio swala la ass kisser ni mila na Tamaduni ambazo zina malengo ya kukamilisha kitu kimoja...
Nimetumia harusi kama mfano hai ambao binafsi siwezi kusema ni hulka mbaya kwa upande wowote ule isipokuwa ni ktk Kuifahamisha jamii hii Utamaduni na mila za sehemu fulani. Leo hii Chadema wana deal na Tanzania nzima ni vizuri wakifahamu kinachowezekana Kilimanjaro sii lazima kiwezekane Mara..Kusema hivyo sio Ukabila hata kidogo!
Na kutokana na mjumuiko wa makabila mengi nchini ni lazima tuziheshimu sifa za waliochaguliwa hata kama hawakubaliki ktk mawazo ya baadhi yetu....hoja za mtu ni muhimu zijibiwe kwa hoja hata kama zinaashiria Ukabila kwa mtazamo wenu.
Hivyo mfano wa harusi haisemi kabisa kuwa Wachagga ni ass kisser isipokuwa ni Mila yao kuhakikisha harusi inafana... Wengine hata Michango ya harusi kuwafuata baadhi ya watu wenye uwezo badala ya nia kama vile leo hii ktk chaguzi za Marekani. Obama kawweza kuwaonyesha Wamarekani kwamba sii lazima kupata michango mikubwa kwa kutumia Lobbiest na kafanikiwa lakini haina maana wale wanaotumia ni ass kisser!..

Nachojaribu kuwakilisha kwenu ni kuonyesha kwamba Wangwe kachaguliwa na watu wenye kila aina ya uwezo wa Kieleimu, kifedha na isije kuwa wapo watu wanaofikiria kwamba elimu ndio CV kubwa ya mwenyekiti au makamu mwenyekiti.. Sii watu wote wanatazama hivyo.. Kachaguliwa na wanachama hivyo ni muhimu kuwepo na utaratibu mzuri zaidi ya huo uliotumika... Laa sivyo itakuwa kazi kubwa kuwafahamisha wananchi wanaokitazama chama hiki kama chama cha Maskini na Matajiri, wasomi na wale wasiokuwa na elimu..Nafasi za Uongozi ndani ya chama unatokana na uwezo wa mtu huyo kuendesha mabo ya chama yanayokubalika ama kuwavutia wananchi zaidi..

Mkandara wewe unaelekea unajuwa sana HISTORIA YA KILIMANJARO...Ebu nipe hint bana!
Maana sasa naona unaelekea kuleee kwenye STERIOTYPE!
Kwamba hata hapa USA...Kuna wale wakiona mweusi...Basi wanajuwa ni mbaya!
Si weusi wote wabaya!
Na ndiyo vita hapa USA!
Niliwaahidi kila kitu kuanzia kule kwenye thread ya OBAMA...Na karibia kila kitu kinatokea!
INANIKUMBUSHIA ULE WIMBO WA NAS NAOUZIMIA KWA SANA..."IF I RULE THE WORLD"
Acheni UKABILA!
Na kama hujui HISTORIA YA KILIMANJARO...BASI HATA YA POPOTE PALE ITAKUWA NI MISCONSTRUED!
 
Umeamua kumtumia YESU hapa baada ya kugundua kuwa ccm ni chama cha kiislam na sasa unajifanya kutaja jina la YESU. Huna hata heshima kwa jina la YESU wewe?
Wewe wasema!
 
...Ukweli nimeuweka na nimesema muulizeni Zitto shahidi kwa hili la Kitila kubadili vyama ..

Ukweli na uthibitisho uko wapi hapa, kama sio unsubstantiated scuttlebutt na marudio rudio ya kusingizia bila uthibitisho?

...wako wengi waliokuwa NCCR mmoja wapo Kitila Mkumbo nae anawasumbua?

... at any time hukuwa mfuasi wa Mrema alipokuwa NCCR na ukahama nae kwenda TLP?

Nina ushahidi mkubwa sana wa jambo hili na unajua unasema uongo,kwani kuna kosa gani wewe kuwa NCCR? KITILA wewe ni public figure maisha yako huwezi kuyaficha hasa hapa JF kila siku watu wanaumbuka.


Umeamua kusema uongo kama ulivyosema kuwa Mbowe sio aliowachagua kina Ngaiza kwenye nafasi walizopo.

Kitila Mkumbo aliomba uenyikiti wa vijana mkoa wa Dar-es-salaam akakosa kuchaguliwa ndio akaenda NCCR,TLP na sasa Chadema.

Alikuwa mwanachama mwanadamizi NCCR hadi mwaka 2000 akahamia TLP.nasema kwa hili ataumbuka sana bora anyamaze.Mheshimiwa Mwanakijiji vyama vina rekodi za wanachama wao.inapotokea Mtu anaficha sehemu ya CV yake lazima tumuogope kwani si mkweli.
kwa hili Mwanakijiji ukicheki na Lyatonga Mrema atakupa,najua kutofautisha kuwa kocha wa timu ya Taifa ni mbrazil hamfanyi awe mtanzania ,Kuku kuzaliwa kwenye ziziz la ng'ombe hamfanyi kuwa ng'ombe. Mbowe alihudhuria sherehe za rais JK kuapishwa sio CCM.
Kitila Tumekuwa nae Daruso alikuwa rais wetu tunamjua vizuri sana.

Ni wewe uliyenihusia kuwa JF ina sheria zake, nimekupa hadi mwaka aliokwenda TLP unataka nini zaidi, nimekwambia alikuwa rais wetu Daruso mtu anapokuwa rais wako lazima umjue na umfutilie baada ya kumaliza chuo,jamaa ali SACRIFICE sana Udsm kwa hili tunampa tano zake.
Tatizo lake anapenda kuwa wenye vyama vinapokuwa juu akiona ovyo anahama.
Naomba niishie hapa labda akija bwana Kitila akitaka maelekezo zaidi nitarudi kumpa kumbukumbu.


...Kitila hakuomba 2005 uenyekiti ilikuwa nyuma baada ya kuukosa uenyekiti wa mkoa wa Dar-es-salaam, akaenda NCCR na TLP, wewe ni mwandishi wa habari za utafiti ukipewa dondoo basi unachimba deep, kukusaidia wapi uanzie muulize Zitto Kabwe.

Jk ni mwenyekiti wa CCM sote tunamiini hivyo kama Ilivyo kwa Mbowe na Mbatia ni wenyeviti wa Taifa lakini sidhani kama wewe au mimi tunajua kadi namba zao kuthibitisha hilo.
John Komba ni mwanaccm au John Mnyika lakini mimi na wewe hatujui namba zao ila kuna ushahidi mwingi wa kimazingira kuthibitisha hoja hii.
vyama vyote vina regista ya wanachama wake ukienda huko utapata hadi kadi namba ya Kitila Mkumbo, alikuwa rais wetu wa UDSM kwa kauli hii ujue kuwa alikuwa mtu maarufu na anachofanya tulikifuatilia kwa makini.

...

naomba nishie hapa
sitamjadaili zaidi RAIS wetu wa Daruso lakini kuyakimbia haya ndio baadae mtakuja kusema kuwa 'alikuwa mzigo' au alikuwa mvuta bangi au alikuwa ...... wa kisiasa.

Sio wote wanaelewa darasani, nimetoa darasa na wenye kuelewa wamelewa ni mwaka 2000 ndio alikwenda TLP,muulize Zitto Kabwe labda utamuelewa.

Samahani sana mie siishi kwa kuGuess kama wewe, ushahidi gani unaotaka kuhusu Kitila, nimekupa kila kitu kama umeshindwa kujua ni uzito wa akili yako sio kosa langu,

Mwk.
Umeshinda ...Kitila, nataka kukwambia kitu kimoja mchujo wa ccm....
....yeah yeah yeah...mchujo wa CCM... yaddi yiddi yadda

ume makini siku nyingine, kabla ya kusingizia vitu. Tena kama alivyo pendekeza Mwnkjj, mwombe msamaha Kitila Mkumbo.
 
Halafu ccm wana haki gani ya kuingilia mjadala huu na wakati hata bado hatujajua what was THE BUTIAMA DECLERATION?
Ama wanafikiri wakikataa kusema basi HISTORIA HAITAANDIKWA?
 
Ukweli na uthibitisho uko wapi hapa, kama sio unsubstantiiated scuttlebutt na marudio rudio ya kusingizia bila uthibitisho?
























yeah yeah yeah...yaddi yiddi yadda

ume makini siku nyingine, kabla ya kusingizia vitu. Tena kama alivyo pendekeza Mwnkjj, mwombe msamaha Kitila Mkumbo.

Kuhani,

bado nasubiria sana kumwona akifanya hivi.

Asante kwa kumkumbusha.
 
Halafu ccm wana haki gani ya kuingilia mjadala huu na wakati hata bado hatujajua what was THE BUTIAMA DECLERATION?
Ama wanafikiri wakikataa kusema basi HISTORIA HAITAANDIKWA?

Wao wanataka watu wasijadili mambo yao ya kifisadi na badala yake wajadili ugomvi ambao haupo. Usishangae wakileta mambo ya ajabu ajabu kama ukabila chadema nk kwa vile hawana hoja.
 
Kwa vile umeshindwa na umekubali kuwa umeshindwa kuthibitisha madai hayo ya Kitila kuwa mwanachama wa NCCR na TLP aidha kwa kukosa ushahidi au kwa kutotaka kuendelea na mjadala huo naamini itakuwa ni uungwana ili angalau kurudisha credibility yako (kama hilo linawezekana) kwa kuondoa madai hayo na kumuomba radhi Kitila kwani kama watu wangeyaamini ingekuwa ni kumchafulia jina.

Tunaposema kitu juu ya mtu fulani aidha tujifunze "kuqualify" au kuweka in search a way that it is not definitive but rather speculative.

Hawezi kwa sababu alifanya makusudi kwa malengo mahsusi ya kujaribu kunizushia jambo akiamini kwamba ningekaa kimya. Ambacho hakujua ni kwamba hapa JF ukisema kitu unajibiwa, huwezi kujisemea na watu wakakuacha. Wengine tunaamini kabisa ile falsafa kwamba uongo ukisemwa bila kukanushwa mwishowe huonekana kuwa ni kweli. Sasa nimembana hapa hadi kumpa habari zangu personal kabisa tangu nikiwa sekondari amebaki kubwabwaja maneno mengi.

Sasa amehamia kwa Zitto kwamba ndiye anayenijua na ndiye atakayethibitisha kuwa mimi nilikuwa mwanachama wa NCCR na TLP. Ok, Zitto ni mwanachama, msomaji na mchangaiji mzuri wa JF ngoja tusubiri hiyo turufu yake ya mwisho atakapojibu Zitto tuone nani mwongo.
 
Kuhani,
Mkuu lugha inakupiga chenga?...
Soma tena maelezo yangu unambie wapi kunakohusiana na Obama na rangi yake!.. Hata kama Obama angekuwa mweupe bado ningetumia mfano huo huo...Ni wewe uliyetafsiri rangi ya Obama ktk utendaji kazi wake, tofauti na kutazama watu anaowawakilisha..Mbinu za Obama zinatazama watu anaowawakilisha sio rangi yake yeye, hivyo tunapomzungumzia Obama ni ktk kuangalia Malengo yake kwa wananchi sio rangi yake yeye.
Sijasema Wangwe ni Mkurya wala hoja yangu haihusiani na kabila ya Wangwe isipokuwa wanachama wa Chadema na wasiokuwa wanachama jinsi wanavyolitazama sakata hili. Hawa ni watu w toka sehemu tofauti, vyama tofauti na kadhalika..
Mfano hoja ya Pundit inayouliza kwa nini wabunge wa chama hiki walioteuliwa wanatoka mkoa wa Kilimanjaro!.. laweza kuwa swala duni kwa mtazamo wa baadhi yetu lakini ukweli ni kwamba hili ni swali zito sana kwa baadhi ya wananchi wengi..na linahitaji majibu ya kurudhisha na ni muhimu kwa wahusika kutazama majibu kwa darubini huru ya kifikra laa sivyo majibu yatakuwa na mgongano mkubwa zaidi.
 
Hawezi kwa sababu alifanya makusudi kwa malengo mahsusi ya kujaribu kunizushia jambo akiamini kwamba ningekaa kimya. Ambacho hakujua ni kwamba hapa JF ukisema kitu unajibiwa, huwezi kujisemea na watu wakakuacha. Wengine tunaamini kabisa ile falsafa kwamba uongo ukisemwa bila kukanushwa mwishowe huonekana kuwa ni kweli. Sasa nimembana hapa hadi kumpa habari zangu personal kabisa tangu nikiwa sekondari amebaki kubwabwaja maneno mengi.

Sasa amehamia kwa Zitto kwamba ndiye anayenijua na ndiye atakayethibitisha kuwa mimi nilikuwa mwanachama wa NCCR na TLP. Ok, Zitto ni mwanachama, msomaji na mchangaiji mzuri wa JF ngoja tusubiri hiyo turufu yake ya mwisho atakapojibu Zitto tuone nani mwongo.

Hapana sizushi ninasema kwa ushahidi, nimemtaja Zitto kwa vile ni mtu wa upande wa huko, kila ninalosema hawataki kuelewa.Zitto anakuja muda gani?
 
Wakuu Wa Chadema Kama Ni Kweli Mna Nia Nzuri...then Wapatanisheni Mbowe Na Wangwe Mara Moja!
Ugomvi Wao Ni Mdogo Sana...hivyo Hakuna Haja Ya Kupoteza Muda.
Na Kama Ugomvi Wao Ni Wa Tofauti Na Yale Tuliyosikia Kwenye Klh News...basi Mtueleze Pia.
 
Back
Top Bottom