Tundu Lisu anaanza kuleta habari za mara ooh nilimsaidia Wangwe kutoka jela, mara ooh nilitembea mimi kwa miguu ili kumpigia Wangwe kampeni, yaani anakumbuka wema aliomfanyia Wangwe, lakini haelezei ni kwa namna gani kuwepo kwa wangwe bungeni kunavyoisaidia Chadema kupata ruzuku . ukweli unabaki pale pale, Kumsaidia mtu si maana yake umfanye mtumwa wako, kumsaidia haitakiwi kutegemea kwamba yule mtu asiwe huru kimawazo na kimtazamo.
jambo la pili: busara ya kawaida ni kwamba kuna kuonywa na kukanyana pale mtu anapo
kosea, je ni wapi chadema walimuonya wangwe kutokana na tabia yake ambayo wao wanasema ni mbaya halafu akawa hajajirekebisha mpaka wakaamua kuchukua uamuzi mzito kama huu unaoweza kuyumbisha chama?
Lisu anakiri kwamba yeye hana haki ya kupiga kura, lakini anatueleza yaliyojiri ndani ya kikao, bimaana maana kwamba Wangwe alikuwa anawatukana watu matusi ya nguoni na akasema hawezi kuyarudia katika redi ya mwanakijiji kuonyesha kwamba ana uhakika ya yaliyojiri mle katika kikao kinaga ubaga, sasa swali linakuja kama yeye lisu siyo mjumbe wa hicho kikao alijuaje haya? alikuwepo mle au aliambiwa? na kama alikuwepo, yeye alikuwepo mle kama nani? na kama aliambiwa alichukua juhudi gani kuujua ukweli wa yaliyojiri mle je alisikilza pande zote? au alisikiliza upande wa mwenyekiti tu?, na kwa vipi aje na conclusion ya CHACHA ALIYEMFAHAMU HAPO ZAMANI SIYO CHACHA WA siku hiyo ?
hapa ishu ninayoinona ni kutofutiana kimtizamo baina ya viongozi, halafu badala ya kutafuta suluhu ya kutokuelewana wanadhani solution ni kumu"eliminate" msiyekubaliana naye.