CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Tarime waunga mkono kusimamishwa kwa Wangwe

2008-07-04 09:21:55
Na Simon Mhina

Uongozi wa CHADEMA wilayani Tarime, umemgeuka mbunge wao, Bw. Chacha Wangwe kuhusiana na kusimamishwa kwake uongozi.

Bw. Wangwe pia ni Makamu Mwenyekiti wa wa chama hicho.

Pamoja na kuunga mkono, uongozi huo umepinga madai yake kwamba rukuzu inayotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa haifikishwi mikoani.

Aidha, uongozi wa chama hicho mkoani Mara, umeelezea kusikitishwa na madai ya Bw. Wangwe na kusema hivi sasa wanamtazama kama mtu asiyekitakia mema chama hicho.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Tarime, Bw. Joseph Anthony alisema inasikitisha kuona kiongozi wa juu wa chama kama Bw. Wangwe anaanzisha hoja ya malumbano yenye nia ya kukiangamiza chama.

Akifafanua alisema inasikitisha kuona Bw. Wangwe akitoa taarifa zisizo sahihi kwenye vyombo vya habari kwamba ruzuku ya chama hicho inaishia makao makuu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Wilaya yake ya Tarime inapokea Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya kukijenga chama.

Kwa msingi hiyo, Bw. Joseph alisema wilaya ya Tarime inaunga mkono kusimamishwa kwa Bw. Wangwe katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Aidha, alimshauri Bw. Wangwe kuacha mipango yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la chama kupinga uamuzi wa kusimamishwa na badala yake asubiri uchaguzi mkuu ujao.

Alisema Bw. Wangwe anatakiwa kujirudi na kujisafisha kwa njia ya kushirikiana na viongozi wenzake, kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari na kukanusha tuhuma dhidi ya viongozi wenzake.

Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafar Kasisiko alisema wao wana wasiwasi mkubwa kwamba Bw. Wangwe anatumiwa kukivuruga chama.

Bw. Kasisiko alisema anachokifanya kiongozi huyo hadi akasimamishwa kina lengo la kuwafanya mafisadi wafurahie.

Mwenyekiti huyo alisema wilaya zake zote zinapata gawiwo la ruzuku tofauti na madai ya Bw. Wangwe.

SOURCE: Nipashe
 
Mwanakijiji: Hoja zako kuhusu utetezi wa wagombea wa viti maalumu zina make sense sana kitaaluma lakini, naogopa kusema, hazi-make sense kabisa kisiasa. Pengine hoja zako zinaweza kukubali miongoni mwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA lakini sio rahisi independents na wapinzani wa CHADEMA wakashawishika. To be honest, mimi binafsi nilishakiri siku nyingi kwamba uteuzi wetu wa wabunge wa viti maalumu ni kati ya makosa ya kutisha kisiasa ambayo CHADEMA tumewahi kuyafanya. Itakuchukia miaka mingi sana kuisambaratisha hoja ya wapinzani wetu kwamba kulikuwa na upendeleo wa aina fulani katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Tatizo langu na Mhe Wangwe katika hili ni kwamba kwa nini analitumia hili kosa kujaribu kujijenga kisiasa yeye binafsi bila kujali madhara yake kwa chama? Ninaamini, I am not sure though, hili jambo litakuwa lilishajadiliwa katika vikao vikuu ndani ya CHADEMA ambavyo Chacha ni mjumbe muhimu, na lazima kutakuwa kulishatolewa maelezo na pengine makosa yakakiriwa. Sasa kwa nini yeye analirudiarudia kila mara huku akijua kabisa kwamba utatuzi wake hauwezi kupatikana leo hadi uchaguzi mwingine ufanyike 2010?
 
Kwa juu, ni mpambanaji Wangwe anayetaka kunyoosha mambo ndani ya chama, but deep inside, ni mafisadi wanaopambana na viongozi wa chama ambao wamekuwa mwiba kwa mafisadi. Wangwe anatumiwa tu, sasa mwisho wa mapambano mshindi atakuwa nani, tunafarijika kuwa wananchi wengi sasa hivi wameshashitukia ufisadi huu.
 
hata bado mtasema sana mwaka huu lakini mnalo limewaganda
 
hata bado mtasema sana mwaka huu lakini mnalo limewaganda

kama lile la uislam ndani ya ccm lilivyowaganda wana ccm. Mkuki kwa nguruwe, mlisema ohh CUF chama cha kiislam, ohh viongozi wake wengi ni waislam, ohh CUF chama cha wapemba, ohh UDP chama cha wasukuma, ohh TLP chama cha wachaga, ohh CHADEMA chama cha wachaga.

Sasa imegundulika kuwa CCM ni chama cha waislam. Aibu kweli, mnadaganya watu wa mwanza na shinyanga kuwapigia kura kwa wingi huku mkichagua viongozi wengi toka visiwani? tena wa dini moja?
 
halitunyimi usingizi na tunakunywa maji na kusonga mbele, hasara iko kwenu mnaomwagiana mboga na ugali
 
halitunyimi usingizi na tunakunywa maji na kusonga mbele, hasara iko kwenu mnaomwagiana mboga na ugali

Nilihisi kuwa suala la udini haliwanyimi usingizi maana mmejaa udini hadi kwenye mifupa. Taratibu tu hizi habari za udini ndani ya ccm zitasambazwa kwa wananchi wote Tanzania ili wajue ajenda ya siri ndani ya ccm na jinsi ambavyo viongozi wake udini sio tatizo kwao na hawajali maoni ya wananchi.
 
watanzania wepi ? si wale mliowatukana kuwa wajinga kwa sababu tu wamewakataa malaghai wapinzani

leo hawa mnaowaita wajinga mtaenda kuwaambia nn? ccm inafahamika vyema na wananchi
 
watanzania wepi ? si wale mliowatukana kuwa wajinga kwa sababu tu wamewakataa malaghai wapinzani

leo hawa mnaowaita wajinga mtaenda kuwaambia nn? ccm inafahamika vyema na wananchi

Oh yeah,

na sasa wataijua ccm kama chama cha waislam kama vile ccm mlikuwa mnaiita CUF chama cha waislam. Huu ni mwanzo tu, watanzania wote hadi kule malampaka watajua udini uliojaa ndani ya ccm.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amethibitisha kuwa alikikopesha chama chake sh. milioni 500 kwa ajili ya kampeni na pia amekuwa akikikopesha chama hicho mara kwa mara mahitaji yakijitokeza. Huyu ndio Mbowe anayedaiwa na taifa la Tanzania na ameshindwa kulipa deni hilo kwa taifa kwa madai ya kushindwa kufanya hivyo! kwa hili Mbowe amedhihirisha kuwa kwake yeye chama na maslahi yake binafsi ni muhimu kuliko maslahi ya taifa.

Mbowe hafai kuongoza nchi yetu.
 
..anayekopa na anayejichukulia kwa kughushi,yupi sahihi?

..kuongoza nchi hakuhusiani na kukopa pesa au kujichukulia pesa kwa kughushi.

..nadhani wote tunalifahamu hili, mpaka sasa.
 
..anayekopa na anayejichukulia kwa kughushi,yupi sahihi?

..kuongoza nchi hakuhusiani na kukopa pesa au kujichukulia pesa kwa kughushi.

..nadhani wote tunalifahamu hili, mpaka sasa.

Hapa siko kwenye kucompare and contrast, nimeelezea kuhusu Mbowe ambaye hataki kulilipa taifa.Huyo anayeghushi nyaraka katoka wapi tena?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amethibitisha kuwa alikikopesha chama chake sh. milioni 500 kwa ajili ya kampeni na pia amekuwa akikikopesha chama hicho mara kwa mara mahitaji yakijitokeza. Huyu ndio Mbowe anayedaiwa na taifa la Tanzania na ameshindwa kulipa deni hilo kwa taifa kwa madai ya kushindwa kufanya hivyo! kwa hili Mbowe amedhihirisha kuwa kwake yeye chama na maslahi yake binafsi ni muhimu kuliko maslahi ya taifa.

Mbowe hafai kuongoza nchi yetu.

Nani kakwambia Mbowe ameshindwa kulipa deni lake? Acha kueneza hizo propaganda za CCM.
 
Unajua ukisoma hizi habari zote unafikia conclusion moja tu. Wangwe anatumia kasoro za chama kukisambaratisha.
Pengine huko nyuma alikuwa mwanachama mtiifu na aliyetaka umaarufu. Kaborou alikuwa type ya Wangwe lakini mipesa ya EPA ikamwacha hoi, Wangwe naye naona wajuzi wa CCM wametumia mwanya ulioanza kujitokeza wa tofauti kati yake na ZITTO kumnunua. Tofauti kati yake na Kaburou ni kuwa Kaburou alitakiwa tu na CCM lakini Wangwe anatakiwa pia aisambaratishe CHADEMA. Nadahani pia atakuwa ameahidiwa kubakiziwa jimbo lake atakapoingia CCM baada ya kuisambaratisha Chadema.
Vitendo vya Wangwe ni dalili tosha kuwa yuko njiani kuondoka toka Chadema, tena kwa shari.
 
Kasoro anaozisema Wangwe, zikirekebishwa then Wangwe hatakuwa na hoja wala following kama ilivyo sasa,

Chadema watumie umakini ku-deal na hoja za Wangwe, badala ya kujaribu kupambana na Wangwe as a person, kwa sababu reading between the lines ni clear kuwa Wangwe has nothing to lose, na hii vita isipokuwa ana-gain tu,

So far Chadema, hamjaonyesha umakini kwenye ku-deal na this ishu, na kwakweli binafsi nimesikitishwa sana hasa baada ya kuona vitimbi vingi humu ndani ya forum vya kujaribu ku-deal na hii ishu lakini kwa kweli ni kujishusha hadhi ni afadhali kuwa tumejua mapema,

na binafsi nimeridhishwa sana na maneno mazito sana ya Kitila on this ishu, anaonekana kuwa amekomaaa kisiasa na kitaifa pia na anweza kuwa the best alternative huko mbele ya safari. I wish wale wenzetu wange-invest in him kwa sababu anaonyesha kuwa makini sana.
 
Kwani Wangwe alitoka lini CCM????

Au hajarudisha kadi kama mzee lyatonga????

Demokrasia/mfumo wa vyama vingi bongo ingefaa uitwe "ze comedy"
 
Ndio hizo siasa za majitaka,,,huyo aliesema ni katibu wa chama wa wilaya na sio Tarime naomba urekebishe msemo wako, hayo ni maoni yake binafsi na sio tamko la wanachama wote wilayani tarime, halafu nenda KLHN kwa mwanakijiji usikilize Wangwe na Lisu wanachosema,,,"kila wilaya inapata 100,000/= kila mwezi" na sio 400,000/= huyo katibu wa wilaya ni msaliti, mnafiki, kuwadi wa mbowe na mfuasi wa siasa za majitaka
Nyerereist si kila mtu humu jf ni mwanachama wa chama chochote cha siasa maana kuna wenye vyama na kuna wasio na vyama. Lakini ni vema ujue hata hao wasio na vyama si kwamba hawazifahamu siasa.
Wewe katika thread hii inaonyesha wazi uko upande gani maana unashupalia sana habari ya Wangwe kuonekana hana matatizo. Yawezekana wewe ni Chadema na uko upande wa Wangwe au uko chama cha mijizi na mifisadi na kwa hiyo una lako.
ukweli wenyewe ni kwamba kwa uzoefu wa siasa za vyama, utakuja ona baadaye tu kwamba Wangwe yuko safarini kwenda kuungana na mafisadi na punde utasikia anashabikia chama chao.
Mimi Si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa taarifa zako. Lakini naweza kusoma alama na nikaelewa nini kinaendelea uvunguni.
Demokrasia si kuwa ccm lakini demokrasia ni pale watu walioaminiwa na chama hata kama ni 10 wanapotoa maamuzi mazito ya chama. Kama kweli hoja ya ukabila kwa Wangwe inakuja kwa sababu wengi wamekosa imani naye, na hapo ndipo anazua suala la ukabila, hapa ndiyo wakati wake wa kuisha na hapo namshauri ajitoe na atafute chama kingine anachodhani kitakuwa kikimtendea haki.
Kama ni maswala ya fedha, hata sisi huku ccm tuna shida ile ile maana Ruzuku inakazi nyingi na haiwezekani kumpa kila mtu akatosheka. Wewe unafahamu hata pesa ya serikali toka consolidated fund haitoshi ndiyo sababu bakuli linatembea nje kila siku kuona kama tutasaidiwa. Sasa iwe chama kama Chadema kinachopata tujisenti(sio vijisenti) kisiwe na shida kweli?
Unachoshupalia hapa ni ushabiki wa vyama hilo tu!
 
Back
Top Bottom