CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Huu ni wakati wa democrasia,,achana na siasa za kijamaa,,hata kama kiongozi akiropoka jamii ndio itayo reason,,Clinton alitembea na secretary wake na watu wakawa na ushahidi lakin jamii ili reason ikaona nini cha kufanya na sio chama ndio kiseme na kuchuja kila kitu....naona unaniaasa nikajifunze,,teh teh teh teh teh teh,,,nimeshajifunza sana kuhusu matamshi ya kiongozi katika siasa za kisasa...so we ndio kajifunze siasa za kisasa (wash your brain..this is new era,,,ukweli na uwazi)

nadhani wewe unachanganya siasa na mambo binafsi ya kiongozi,unakubaliana na la clinton kisha unalazimisha la ufisadi wa mbowe..we mtu wa wapi nadhani unatoka KIGOMA!
 
hapa hua hatutukanani,,,anyway ngoja niangalie status yako kwanza
 
sijakutukana,binadamu tumeumbwa tofauti,hata maisha tunayoishi pia na nchi tunazokaa zinaweza kuwa tofauti,hivyo hata kwenye kufikiri na kuchanganua pia speed zinatofautiana!
 
we mtu wa wapi nadhani unatoka KIGOMA!

unafikiri maneno uliyoyatumia ni ya busara hapo,,,hapa hua tunashindanisha hoja tu ndugu yangu,,hakunakutumia maneno yasiyoendana na upeo wako sio vizuri after all hujui mie ni rika gani,,,tumia maneno mazuri bwana mdogo
 
...heshma yako mkuu,tuendelee kumkoma nyani gilani
 
Mwenyekiti wa Taifa NCCR ni Mbatia mtu wa Kilimanjaro, mgombea urais kwa tiketi ya NCCR alikuwa kutoka Kilimanjaro bwana Mvungi, nadhani ni mkakati ule ule wa Kanda ya kaskazini,
maandishi haya yameandikwa na gazeti linalomilikiwa na Mbowe-Tanzania Daima.

Mgagagigikoko, nadhani hukwenda shule kabisa au ulikwenda kukusanya vyeti lakini hukuelimika kabisa. Katika karne hii, unatazama makabila ya watu si hoja zao? Kipimo chako cha ubora na ubaya wa mtu ni kabila lake? Fisadi mkubwa!
 
Mzee nasisitiza usikurupuke mimi na wewe tuna historia katika kujenga hoja,,, hakuna mtu hapa JF anawasupport hao uliowataja hapo juu (mafisadi)..na ili kuwaondoa kabisa katika jamii,,ni lazima tujenge chama mbadala chenye mwelekeo mzuri na chenye kuheshim democrasia...chadema kwangu ni mbadala but kwa hitilafu kama hizi ni lazima wazizime kwa gharama yoyote ili kukijenga chama...nasisitiza sina ugomvi wa hila na chadema

Nimeuliza swali maana umesema nimekushambulia nikaomba ufafanuzi wapi nilipokushambulia? Sasa unaniambia nimekurupuka! Ni lipi hilo ambalo linaonyesha nimekurupuka? Unajua ubaya wa maandishi ni lazima uweze kuthibitisha kile unachokisema hasa unapomtuhumu mtu kwamba, 'amekushambulia au amekurupuka'.

Muungwana narudia tena ombi langu kwako naomba uweke sentesi niliyokushambulia na kukurupuka hadharani kama nimefanya hivyo sitosita kukuomba samahani maana muungwana ni vitendo.
 
Nashukulu sasa umeanza kuelewa bwana mdogo,,,ni kweli CCM wanakumbatia ufisadi,,na ili kuuondoa ufisadi tunahitaji chama mbadala chenye mwelekeo mzuri na chenye sura ya kitaifa (CHADEMA safi)....lazima wakubali kurekebisha makosa yaliyopo waache propaganda za kizamani la sivyo hata huo umaarufu walonao sasa utakua kazi bure

Huu nao bado ni ugonjwa mbaya wa akili. Utaifa hauonekani katika makabila ya watu bali katika dhima inayowakusanyisha, masuala wanyojadili na mipango wanayoweka. Hata wakati wa TANU walikuwapo wananchi wenye akili hizi hizi, maana asilimia 8o ya waanzilishi walikuwa watu wa Pwani na Waislamu. Kina Nyerere alijiunga kama wageni, tena wabara, na wakristo wachache sana. Bahati ya Nyerere alikuwa amesoma, ana akili anajua dunia na anajua kujenga hoja, wale wazee wakaonahuyu ndiye anaweza kujibizana na mkoloni, wakamwamini na kumkabidhi uongozi wa chama.

Kama wangeendeleza ugonjwa huu, chama kisingekuwa kabisa, na CCM ya leo mnayoshabikia isingekuwa na sura ya kitaifa. Ukweli ni kwamba jambo lolote lazima lianzie mahali fulani. TANU/CCM ilianzia Pwani, CUF kimeanzia Visiwani, UDP imeanzia usukumani, Chadema uchaggani na kadhalika. Lakini malengo ya vyama vyte hivyo ni ya kitaifa. Kama yangekuwa ya kikabila wala visingesajiliwa. Tujifunze kutazama mbali ya pua zetu, tusijiingize kwenye propaganda za watu bila kujua. Hata kama tunafanya makusudi, tujue kwamba katika karne hii watadanganywa wachache sasa....

Kila mtu anajua Chadema ni chama cha kitaifa kama vingine, na kwamba Chacha Wangwe ni tatizo. Angalia hata behaviour yake bungeni. Haelewani na kambi ya upinzani,, lakini anaelewana na Kabourou! Yeye ndiye nani? Hivi mnamjua au mnasubiri majira na Mtanzania yawaandikie? Wamefanya vema kumshughulikia mapema, vinginevyo yangewapata makubwa.
 
umemaliza kila kitu,sina cha kuongeza!
 
nadhani wewe unachanganya siasa na mambo binafsi ya kiongozi,unakubaliana na la clinton kisha unalazimisha la ufisadi wa mbowe..we mtu wa wapi nadhani unatoka KIGOMA!

JASILI HAACHI ASILI,tatizo la wangwe ni kabila analotoka!...............MWINJUMA MUUMINI aliwahi kukiri kuwa tatizo linalomsumbua ni uzalamu wake,hivyo na WANGWE nae ubabe anaounesha ni kuuendekeza ukulya wake

Mkuu,

Matamshi yako hapo juu siyo ya kiungwana. Ni ya kashfa za jumla jumla.

Na hayana busara. Unajuaje kwamba hakuna watu wa Kigoma na Wakurya wanaokusoma hapa ambao kesho na keshokutwa ungependa kujadiliana nao katika mambo mengine mbali mbali? Na hapa umesha wamaliza? We huna washikaji wa kutoka Kigoma au Mara?

Huo ni ukambunga mjomba. Watu wote tunajichanganya hapa, na mjanja hawezi kumkandya mwingine kwa sababu ya kabila au Mkoa anaotoka.

Sio zenyewe hizo mwanangu.
 
Huu nao bado ni ugonjwa mbaya wa akili. Utaifa hauonekani katika makabila ya watu bali katika dhima inayowakusanyisha, masuala wanyojadili na mipango wanayoweka. Hata wakati wa TANU walikuwapo wananchi wenye akili hizi hizi, maana asilimia 8o ya waanzilishi walikuwa watu wa Pwani na Waislamu. Kina Nyerere alijiunga kama wageni, tena wabara, na wakristo wachache sana. Bahati ya Nyerere alikuwa amesoma, ana akili anajua dunia na anajua kujenga hoja, wale wazee wakaonahuyu ndiye anaweza kujibizana na mkoloni, wakamwamini na kumkabidhi uongozi wa chama.

Kama wangeendeleza ugonjwa huu, chama kisingekuwa kabisa, na CCM ya leo mnayoshabikia isingekuwa na sura ya kitaifa. Ukweli ni kwamba jambo lolote lazima lianzie mahali fulani. TANU/CCM ilianzia Pwani, CUF kimeanzia Visiwani, UDP imeanzia usukumani, Chadema uchaggani na kadhalika. Lakini malengo ya vyama vyte hivyo ni ya kitaifa. Kama yangekuwa ya kikabila wala visingesajiliwa. Tujifunze kutazama mbali ya pua zetu, tusijiingize kwenye propaganda za watu bila kujua. Hata kama tunafanya makusudi, tujue kwamba katika karne hii watadanganywa wachache sasa....

Kila mtu anajua Chadema ni chama cha kitaifa kama vingine, na kwamba Chacha Wangwe ni tatizo. Angalia hata behaviour yake bungeni. Haelewani na kambi ya upinzani,, lakini anaelewana na Kabourou! Yeye ndiye nani? Hivi mnamjua au mnasubiri majira na Mtanzania yawaandikie? Wamefanya vema kumshughulikia mapema, vinginevyo yangewapata makubwa.

Kama sikosei mwanzirishi wa CUF alikua Mapalala mnyamwezi wa Zenga ,bado siamini kama CUF ilianzia visiwani.
 
Mgagagigikoko, nadhani hukwenda shule kabisa au ulikwenda kukusanya vyeti lakini hukuelimika kabisa. Katika karne hii, unatazama makabila ya watu si hoja zao? Kipimo chako cha ubora na ubaya wa mtu ni kabila lake? Fisadi mkubwa!
Tusifunike mgongo mwanaharamu apite ukabila upo!Bwana eeh kabila fulani lina sifa zake ambazo zinatumika kuliidentify!hata kama ni general lakini kuna ukweli ndani yake ni kweli wakurya ni wakorofi,wahaya wanatabia zao,wasukuma nao wana karacter yao
 
Mimi kwa kweli Sielewi kwanini tuko hivyo-

Nani aliwaambia ukiwa Upinzani lazima Rafiki zako wawe wapinzani na CCM ni adui ,Huo ni mtazamo legevu

Wengi wapinzani yaniwanataka eti kujenga uadui hata wa kijamii eti kwa vile ni CCM ,kumbukeni hawa watu wenda wamesoma pamoja,ni ndugu na jamaa kwa namna moja ama nyingine ama ni wabia ktk biashara zao ama maisha yao ya kawaida.

Kumutuhumu mtu eti kwa vile anaongea na rafiki zake ni kabouru ama Azizi ni pia ni ulegevu ,hiyo inamaana ukiwa CHADEMA lazima uchaguliwe rafiki na chadema.

Hii ishu Mbona hamumukomalii DR SLAA anayelala na Mkewe chumba kimoja kila siku.mkewe ambaye ni diwani wa CCM.Japo hii si ISUE

Ktk CHADEMA mie nayemwona mwanademokrasia wa kweli ni DR SLAA sio dikteta na mwanademokrasia wa kweli toka ndani kwa kuruhusu mkewe kuchukua chama apendacho na akipendacho na si kulazimishana kama ambavyo wanataka kumlazimisha Wangwe lazima rafiki zake wawe CHADEMA.
 
Mkuu,

Matamshi yako hapo juu siyo ya kiungwana. Ni ya kashfa za jumla jumla.

Na hayana busara. Unajuaje kwamba hakuna watu wa Kigoma na Wakurya wanaokusoma hapa ambao kesho na keshokutwa ungependa kujadiliana nao katika mambo mengine mbali mbali? Na hapa umesha wamaliza? We huna washikaji wa kutoka Kigoma au Mara?

Huo ni ukambunga mjomba. Watu wote tunajichanganya hapa, na mjanja hawezi kumkandya mwingine kwa sababu ya kabila au Mkoa anaotoka.

Sio zenyewe hizo mwanangu.

ukambunga unaufanya wewe unaeona tabu kumwambia mtu ukweli,sio siri kuwa wakulya wanaeleweka SIFA ya UKOROFI na watu wa KIGOMA(WAHA)wana SIFA ya UBISHI,sasa mimi NIMEKASHFU au NIMEWAPA SIFA YAO?
 
Shorten the story kwa kutuambia tabia za wachaga...maana inaonekana una uelewa mkubwa wa tabia za makabila...la sivyo nasisitiza na ninarudia kukuambia kwamba sio vizuri kujadili makabila hapa ila kwa vile umeonyesha kuikubali chadema basi naomba ukubali hoja iliyoko mezani kwamba ni kweli chadema inaonekana kua na sura ya ukanda (ukabila)..kama we ni shabiki mzuri na ulie iva wa chadema utakubali kwa kutoa maoni chanya yenye kuisaidia chadema...la sivyo utatufanya tuelewe wewe ni mchaga ulie kasilika kuambiwa ukweli wa mambo yanayoendelea ndani ya chadema
 
Mimi binafsi sioni CHADEMA kama chama watanufaika kwa kumsimamisha Mh. Chacha Wangwe kwenye uongozi, isipokuwa matakwa na utashi binafsi wa kiongozi wa juu wa chama hicho.

Kama itakumbukwa pale Msimbazi (naweza kurekebishwa) Mh. Wangwe tayari alikuwa amepigwa zengwe la kuondolewa asigombee na nafasi hiyo alitakiwa apewe mbunge wa Mpanda Mh. Arfi.

Kutokutakiwa Mh. Wangwe katika safu ya juu ya uongozi inatokana na mwelekeo wa kweli anautaka kuujenga ndani ya CHADEMA kwa kujenga nguvu kwenye ngazi za chini ambapo watakuwa karibu na wanachama.

Kama ilivyo katika siasa utekelezaji wa mpango huo ni wazi na ukweli usiofichika utakuwa umempandisha juu sana Mh. Wangwe katika medani za kisiasa na ndio maana wanasiasa wa karibu kama Mwenyekiti anahofia kufunikwa (japokuwa ni uoga usiokuwa na maana)

Ni vyema CHADEMA ikasikiliza mawazo ya Mh. Wangwe na kuyafanyia kazi kwa manufaa ya walio wengi kulikoni hali ilivyo hivi sasa. Mh. Wangwe si mwendawazimu ana hoja ya msingi na isijaribiwe kuzimwa kwa kutumia siasa rahisi.

Ni vyema CHADEMA ikajiangalia na kuona kuwa je yenyewe ina demokrasia ya kutosha ndani yake?

Je, ni kwanini kuna malalamiko ya siyokwisha juu ya ukabila na upendeleo wa kanda?

Je, Wangwe alikuwa ni mwenzenu tu wakati wa kutafuta kura za Rais kule Tarime?
 
Tatizo la Wangwe si ubabe pekee nadhani pia umimi na roho mbaya .Nadhani uelewa wake na shule yake ni ndogo.Wangwe kufikia kutumia maneno kama ya JK kwamba anataka kuwakomboa na kukomaza Chama bila ya kusema tafanyaje ni ujinga wa hali ya juu .Chadema mkabeni koo huyu jamaa maana yeye na Cheyo wako kwenye payroll ya CCM.It is time aende huko aache watu wapigane na ufisadi .

Wangwe kutoa matusi ya nguoni na kutangaza ngumi na kuwatuhumu wenzake ndani ya Chadema ni aibu kubwa na haiwezi kuvumiliwa hii tabia .Nin hatari kwa Chama .

Nawapongeza Chadema wameamua kuuva huu mgogoro mapema na kuupatia majibu bila kuleta mambo ya kufanyia chumbani kama CCM.Chadema hongereni na kuyakabili matatizo makubwa kama haya ni sehemu ya kukomaa kwa Chama makini .

Wangwe hufai hata kuwa diwani .Chadema Tarime watakumwaga ndipo utajua na nakataa kwamba kumekuwa na mkakati wa Uchaga .

Leo mtu asema historia ya wagombea wa NCCR ni wachaga .Swali kama je sisi watu wa kawaida tuko kimya na tunataka kuwanyooshea vidole wengine na wachaga wanajitolea na kujitoa hata kugombea uongozi na wewe uko pembeni unangoja kusema ni Uchaga na Ukabila tukufanyeje ?

Jitokezeni mshiriki na si kuleta majungu JF.
 
Lunyungu umenena!

Labda niwaulize watu swali moja,mtu yeyote asiye mchaga ndani ya CHADEMA hastahili kufukuzwa au kusimamishwa kazi au uaanachama endapo amefanya kosa? Katika hali na mazingira yanayowekwa sasa hamuoni pia mtakua mnapalilia kansa fulani ndani ya CHADEMA kutokana na jinsi hili suala la Wangwe linavyojadiliwa? Sasa kwa mfano Dr.Slaa si mchaga,je hamuoni leo hii Dr Slaa anaweza kufanya kosa ambalo analijua kabisa ni kosa lakini kwa vile anajua kwamba atatetewa na watu kwa kuonekana anaonewa kwa kutumia kigezo cha ukabila basi na afanye anavyotaka kwa maslahi yake binafsi? Huu ni mfano tu maanake shujaa Slaa ni mtu makini na mzalendo wa kweli kwa taifa letu.

Hapo mimi nataka wale ambao wanamtetea Wangwe kwa nia njema au kwa vyovyote wajue pia haya mazingara yanaandalia watu fulani katika hii jamii,ili kuua upinzani au kupunguza nguvu za vyama mbadala katika mapambano ya haki
 
Tatizo la Wangwe si ubabe pekee nadhani pia umimi na roho mbaya .Nadhani uelewa wake na shule yake ni ndogo.Wangwe kufikia kutumia maneno kama ya JK kwamba anataka kuwakomboa na kukomaza Chama bila ya kusema tafanyaje ni ujinga wa hali ya juu .Chadema mkabeni koo huyu jamaa maana yeye na Cheyo wako kwenye payroll ya CCM.It is time aende huko aache watu wapigane na ufisadi .

Wangwe kutoa matusi ya nguoni na kutangaza ngumi na kuwatuhumu wenzake ndani ya Chadema ni aibu kubwa na haiwezi kuvumiliwa hii tabia .Nin hatari kwa Chama .

Nawapongeza Chadema wameamua kuuva huu mgogoro mapema na kuupatia majibu bila kuleta mambo ya kufanyia chumbani kama CCM.Chadema hongereni na kuyakabili matatizo makubwa kama haya ni sehemu ya kukomaa kwa Chama makini .

Wangwe hufai hata kuwa diwani .Chadema Tarime watakumwaga ndipo utajua na nakataa kwamba kumekuwa na mkakati wa Uchaga .

Leo mtu asema historia ya wagombea wa NCCR ni wachaga .Swali kama je sisi watu wa kawaida tuko kimya na tunataka kuwanyooshea vidole wengine na wachaga wanajitolea na kujitoa hata kugombea uongozi na wewe uko pembeni unangoja kusema ni Uchaga na Ukabila tukufanyeje ?

Jitokezeni mshiriki na si kuleta majungu JF.

Lunyungu,

Kuwa fair, nani katika CHADEMA ameteswa na CCM zaidi ya Wangwe? Kuanza kumwambia yuko kwenye payroll ya CCM bila ushahidi wowote sio tu unamdhalilisha Wangwe lakini unaweza jikuta unajidhalilisha hata mwenyewe.

Watu wote hawawezi kufanana, mfano hapo hapa UK, kulikuwa na naibu PM Prescott wakati wa Blair, ingelikuwa TZ si ajabu angeshatimuliwa kwasababu alikuwa hayuko kama akina Blair. Lakini Blair kila siku alikuwa anasema Prescott is Prescott, akiwa na maana kuna mambo Prescott anaweza akafanya na ikawa OK wakati angefanya kiongozi mwingine ingeleta balaa. Bado Prescott alitoa mchango mkubwa sana kwenye chama chao cha Labour.

Mnamtukana Wangwe kwasababu kasema yale ambayo hamtaki kuambiwa. Angelikuwa anaimba sifa kwa mwenyekiti wake, hapo angeambiwa ni kiongozi bora. Kama hafai kuwa mbunge na diwani, ilikuwaje yeye akashinda viti vyote viwili wakati wanaofaa CHADEMA wakachemsha kwenye nafasi walizogombea?

Shughulikieni matatizo ambayo yanasemwa tokea uchaguzi wa 2005. Mkishughulikia hayo, wangwe atakosa cha kusema. Vinginevyo mtakiua chama, maana kila anayetaka kuhama CHADEMA atatumia maneno hayo hayo na baada ya muda itaonekana kama watu wengi wanaongelea kitu hicho hicho kumbe kuhama kwa wengine kulikuwa na sababu tofauti kabisa.

Hii personal vendetta dhidi ya Wangwe haisaidii sana, shughulikieni hoja zake.

Mkiiga ya NCCR, baada ya miaka kumi chama kinaweza kujikuta na wabunge wachache kuliko ilivyo sasa. NCCR ni wasalati wa wapenda mabadiliko, yaani kati ya mwaka 1995 na 2000, walitusaliti sana wananchi kwa kugombana gombana na kusahau kwamba wananchi tulikuwa tunawategemea kutuletea mabadiliko.
 
Mkuu Mtanzania .Nimekaa muda wote kimya kuutafuta ukweli juu ya Wangwe na Chadema yao hatimaye nimeamua kusema ninalo lijua .Namkatalia Mbowe kusema kwamba Wangwe anauza siri za Chama kwa kusema na traitor Kaburu wa CCM , maana hata mimi sina Chama lakini nina marafiki kote kuanzia CCM hadi Upinzani .Lakini naheshimu maoni yake ambayo mimi nayakosoa .

Wangwe kuwa kwenye payroll ni muda sasa nma soon nitamwaga mboga hapa .Mie sikukurupuki .Kwa tabia za Wangwe za wivu na kutaka asujudiwe na ngumi mkononi na kutoa madai ambayo hawezi kusema anataka kufanya hayawezi kuvumiliwa.Kwa mfano Wangwe amemtukana msanii wa Chama matusi ya nguoni na kuahidi kumuondoa Chadema .Msanii yule ni kijana mdogo sana kwa umri na hata madaraka kwa Wangwe .Kama kweli anataka kurekebisha kwa nini asitumie proper channels ?

Chadema imempa hata nafasi ya kujifunza uongozi lakini yeye kabakia kuwa mtemi na mlalamishi kila kona .Nadhani nakubaliana naye kusema mawazo yake wazi bila ya kufunikwa na Chadema nao wako wazi kusema why kasimamishwa .

Mbowe hana sauti ya mwisho ndani ya Chadema kama mnavyo taka tuamini .Nadhani kuna kuendeleza matakwa ya CCM kwamba Chadema ni Mbowe wakati naja ujua ukweli wote .

Tungoje mkutano mkuu utakuja tutaona lakini watu hawawezi kuogopa kukabiliana na uozo kwenye Chama kama CCM wanavyo fanya .Kukaa kimya wakati wana uozo kutawaondolea wana Chadema uhalali wa kukemea mambo kwa kuwa wao wenyewe hawawezi kukemeana .

Hongereni Chadema .
 
Back
Top Bottom