CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

sasa mkuu hapa usinilazimishe nifikie mahala nifikirie kwamba wewe ni mmoja wa wasiokitakia CHADEMA mazuri,na si chadema pekee bali wanamgeuzi wote wenye mawazo mbadala nchini.Hivi kweli mkuu unataka mtu avuruge chama kwa muda wooote huo wa miezi sita huku ukimwangalia tu? halafu useme una mapenzi ya kweli na nguvu ya mabadiliko ya kweli katika jamii hii iliyojaa kila aina ya dhuluma,ufisadi,ukandamizaji,wizi wa kutisha katika taasisi nyeti za serikali nk.Are you serious? Au ndivyo vitabu vyote vya western vinavyosema kwi kwi kwi!

Naona sasa umeanza kuwa kama Mugabe, kwasababu nimetumia mfano wa Thatcher, unataka kunilink na West?

Wangwe sasa anaharibu mambo ya CHADEMA kuliko wakati ule mlipokuwa hamjamfukuza. Kama hulioni hilo basi hapo ndio kwenye tatizo.

Ni sawa na CCM walimfukuza Hamad, walifikiri wamemaliza tatizo lakini kumbe ndio wametengeneza tatizo. Yanayowasumbua CCM Pemba ni matokeo ya hizo sera za kufukuzana ambazo wengine tunazipinga.
 
Nyerererist, Zemarcopolo, mtimti na wote mnaochangia hii mada.

Kwa hakika mnajitahidi kujadili ukabila.
Lakini niwahakikishie tu kuwa huo ukabila hamuuji. Na pia ninyi hamjui kuwa mnajadili aina ya ukabila mnaoujadili kwa manufaa ya nani.

Hoja zenu wote mnaonyesha kuzaliwa na kukulia kidogo au sana Tanzania. Lakini hamjawahi kutafuta kujua kwa undani kuhusu historia ya makabila ya Tanzania. Watu wengi wanafikiri kuwa ukabila tunaouona leo ukisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe ndiyo ule wa zamani.

Naomba muelewe huu wa sasa umetiwa hamira na wakoloni. Babu zetu walipopigana kabila moja dhidi ya jingine waliacha mlango mkubwa tu wa kusuluhishana. Walipigana kwa sababu maalum ambayo ukiichunguza utaona kuwa vita isingeepukika. Lakini leo madaraka tu yanatosha kuangamiza jamii nzima. Vita nyingi za kikabila zimepiganwa bila sababu inayojitosheleza.

Hoja ya ukabila, udini na ukanda inatumiwa na CCM kuwamaliza kabisa watanzania. Watanzania hawana sababu yoyote ya kuogopa kuongozwa na watu wa kabila moja. Ingawaje inatafsirika vibaya lakini bado kama kwa kufanya hivyo kuna tija kwa taifa basi sioni sababu hata kidogo ya kuwanyima watu kutumia vipaji vyao kulitumika taifa.

Kwa taarifa yenu CCM wanajua historia vizuri. Wanajua makabila ambayo yamekuwa yakiwapa upinzani toka hata enzi za siasa za chama kimoja. Hicho ni kipaji cha kikanda.
Kuna mikoa kama Musoma ambako huwezi kumtisha mtu kirahisi. Ni mikoa ya kijeshi. Hicho ni kipaji cha kanda yao, Kuna mkoa kama wa Kagera watu wanajipenda sana na ni watafiti na wajanja. Hicho ni kipaji chao cha kimkoa. Kuna mikoa ya soka. Kuna mikoa ya ngoma na sanaa za maonyesho. Kuna mikoa ya chakula, nk.

Wakubwa!! kama hamjapata sababu ya vipaji vyote nilivyotaja hapo juu kutamkwa kuwa ni ukabila na kupigwa vita, basi msiwe na sababu pia ya kukemea mikoa ama makabila yenye vipaji vya kuipinga CCM
Sitoki Kilimanjaro, bali najua huko ndiko ambako TANU na CCM wamekuwa wakikosa kura kwa miaka mingi sasa. Nilijiridhisha na hali hiyo hata kwenye uchaguzi wa mwaka 2005. Katika wagombea 10 wa kiti cha urais walikuwepo wagombea kutoka Kilimanjaro 6. Hawa wana uthubutu mkubwa wa kuiondoa CCM madarakani. Nilipewa habari kuwa CCM pale mjini Moshi inaitwa chama cha upinzani. Maana baada ya kutangazwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa 1992, CCM haijawahi kushinda lile jimbo.

Kwa maana nyingine ni rahisi sana kujua hoja ya ukabila imeasisiwa na nani? na kwa manufaa gani?

Kwa ufafanuzi zaidi. Mch. Christopher Mtikila wa DP alikwishawahi kusema 1993 kwamba zaidi ya 94% ya fedha zilizokuwa kwenye mzunguko nchini Tanzania mwaka huo zilikuwa mikononi mwa watanzania wa asili ya asia. Miaka ile kulitokea mgogoro mkubwa baina ya waasia hao na wazawa. CCM ilikaa kimya. Fikiria watu wasiofikia 5% ya the whole population wanamiliki 94% ya fedha zote na the rest (95% ya population) wanabakia wakigombania 6% ya fedha katika nchi yao walimozaliwa. Kosa la wazawa hawa ni nini?
CCM haikuwahi kutamka lolote hadi leo. Zaidi CCM hiyo hiyo imeendelea kuwakumbatia na kuwafungulia milango ya kujichotea mapesa wanavyotaka wao.

Wakubwa!!!!! Akili kwenu!!! Mnaipenda nchi yenu chunguzeni historia yake kwa undani. CCM ni waongo kila siku!!! Hoja ya ukabila ni silaha yao ya kupunguza makali ya upinzani. Wameshashtukiwa.

Tchao

Du! Yani Kamende kama watu wangekuwa wanasoma maoni ya kila mtu na si ku concentrate kwenye UBISHI WAO...Basi tungekuwa tunasonga mbele!
Hata hivyo kama ulivyosema...Kuna watu hawaijui historia ya Tanzania ama wanajuwa kidogo sana kwa hiyo wao kazi yao ni KU TYPE TUUU!
 
Naona sasa umeanza kuwa kama Mugabe, kwasababu nimetumia mfano wa Thatcher, unataka kunilink na West?

Wangwe sasa anaharibu mambo ya CHADEMA kuliko wakati ule mlipokuwa hamjamfukuza. Kama hulioni hilo basi hapo ndio kwenye tatizo.

Ni sawa na CCM walimfukuza Hamad, walifikiri wamemaliza tatizo lakini kumbe ndio wametengeneza tatizo. Yanayowasumbua CCM Pemba ni matokeo ya hizo sera za kufukuzana ambazo wengine tunazipinga.


Mtanzania
Ur genius
 
Naona sasa umeanza kuwa kama Mugabe, kwasababu nimetumia mfano wa Thatcher, unataka kunilink na West?

.

Mkuu,sasa umeenda mbali! Yaani wewe mkuu mwisho wako wa kufikiria ni mpaka hapo tu? Hilo kwangu ni Tusi.Sasa nilitegemea ungejibu vizuri hoja unaozijua kumbe unajua kutukana sana. Sasa mkuu naomba unitake radhi mara moja! Wewe ni mtu ambae umezoea personal attacks,sasa hata mimi naziweza sana lakini hapa sio mahala pake.

Nimekulink na vitabu ulivyosema vya west baada ya wewe ku-insist twice about western books.Nikakushangaa na jinsi usivyoweza ku-apply hizo theory kulingana na mazingira muafaka.

Ben,
Suala la Thatcher inaelekea hulielewe na sikulaumu badala yake nitakuelemisha. Thatcher alikuwa PM lakini kujiuzulu kwake lilikuwa suala la chama. Hapa UK, PM hachaguliwi, badala yake kiongozi wa chama kinachoshinda ndiye anakuwa PM.

Thatcher alikosana na kiongozi mwenzake kwenye chama, akaomba wanachama waamue. Bahati mbaya kwake wanachama wakashindwa kumuunga mkono, ikabidi aachie uongozi wa chama na hivyo kujiuzulu u-PM.

Siasa ni zile zile mambo yanayofanya kazi sehemu moja yanafanya kazi hata sehemu zingine. Kuna modifications kidogo sana huwa zinatakiwa, kama unaelewa contingency theory utajua nina maana gani. Najua Waafrika wengi wakiambiwa mambo ya West wanaanza kusema mambo ya West hayafanyi kazi Afrika, sio kweli, sisi ndio hatufanyi kazi lakini theory yoyote ya maana inatakiwa ifanye kazi mahali popote baada ya kufanyiwa mabadiliko kidogo.

Hakuna hata sehemu niliposema ni mimi tu niliyesoma vitabu vya uongozi. Wala hutasikia
hata siku moja nikitamba hivyo maana kwangu application ya kile kidogo ulichojifunza matters more kuliko kusoma vitabu 100 ambavyo huwezi kutumia ulichojifunza.

Nilichokuwa nasema na ambacho ndio hata kwenye makampuni makubwa wanatumia, kukiwa na ugomvi kwenye board, dawa sio kufukuzana. Dawa ni kuitisha mkutano wa board na kuamua wao waamue kama strategy unayofuata inafaa au la. Leadership kwenye vyama vya siasa haina tofauti kubwa na kwenye mashirika, of course kuna contingency theory.

Kwanza jielimishe wewe mwenyewe kwanza! wewe kuwa hapo Uk si kweli kwamba unaelewa kila kitu kuhusu Thatcher na chama chake! Maanake unaonekana mambo mengi unarukia tu,umesema makampuni makubwa migogoro huwa wanapeleka kwenye bodi.Sasa mbona unapenda kuhamisha theory wewe? Nakwambia CHADEMA wanafuata utaratibu wa kikatiba,pili hilo suala la migogoro kupelekwa kwenye board kwa makampuni huoni hata CHADEMA wamepeleka kwenye kamati kuu.Lengo la makampuni kupeleka kwenye bodi ni nini hasa? si kuepuka maamuzi ya kidikteta yanayoweza kuchukuliwa na production manager,financial comptroller au Managing Director.kwa hili la managing director tumchukulie kama vile sasa alivyo Mwenekiti wa Chadema na board of directors tuchukulie Baraza au kamati kuu ya Chama

nimeona niseme hivyo ili kukuelewesha maanake unaongea hata hujui unachoandika,unaji-contradict tu.Yaani hiyo theory ya kuendesha makampuni makubwa huoni hata CHADEMA wameitumia?

Unaongea suala la kutimuana,kwani hata katika makampuni makubwa tuseme board of directors hawawezi kufikia hatua ya kumtimua Financial Manager pale inapoona hilo suala ni serious na lina madhara kwa kampuni?

Halafu uache kufanya conclusive assumptions.Maanake unaponihusisha moja kwa moja na CHADEMA sijui haya yote umetoa wapi? Kwa mantiki hiyo hiyo naweza kuandika kuhusu CCM nikaku-refer ninyi
 
hata Mwenyezi Mungu alilichagua taifa la israel ili kwa hilo ulimwengu upate kuokolewa, sasa kama makabila mengine hayataki kujiunga na upinzani tufanyeje? tuta-move na hawa wachache mpaka kileleweke.

fikra pandikizi za uchaga, ukuryaa, ni danganya toto ya ccm ili tusahau ajenda muhimu zilizoko mbele yetu.

kama chadema ni cha wachaga, lakini kinapambana na ufisadi mimi nitakuwa shabiki wake. hata kama siyo mchaga, pale chedema hakuna anyekula kuku, bali ni kazi mtindo mmoja. sasa hivi ni saa tatu usiku, namwona chdema yuko kwenye mtandao wa jf anafa nya kazi. lakini nilitoka mahali dakika 20 zilizopita nilimwacha mzindakaya na wenzake wakitandika ulabu
 
sahihisho-namwona dr slaa na siyo chadema yuko na sisi hapa anakata issue akina nchimbi na wenzake wanakata kinywaji na kuteta kuwa chdema ni chama cha wachaga,

je mmesajiuliza kwa nini gazeti la mtanzania linalomilikiwa na kilaza, fisadi rostam azizi ndili linaloshabikia habari za wangwe na kutabiri mwisho wa chadema?
 
Nimekulink na vitabu ulivyosema vya west baada ya wewe ku-insist twice about western books.Nikakushangaa na jinsi usivyoweza ku-apply hizo theory kulingana na mazingira muafaka.

Ben,

Nimegundua husomi hoja vizuri kabla ya kujibu maana hii sijui ni mara ya ngapi nakukamata kwamba unaongelea kitu ambacho mimi sijaongelea.

Ebu highlight mahali popote ambapo mimi nimeongelea western books. Vingine sema umekosea tena kwa mara ya pili. Ni shida sana kubishana kwa hoja na watu ambao huwa hamtulii na kusoma kilichoandikwa kwanza.

Nilichoandika ni kama hapa:

"Wenzetu wa West ndivyo wanavyofanya na pia vitabu vya uongozi ndio vinavyosema, labda vimetungwa na watu ambao hawajaenda shule kwi kwi kwi!!!"

Mimi nimeongelea vitabu vya uongozi na wala sio vitabu vya West. Nimeongelea wenzetu wa West na nikatoa na mfano wa Thartcher lakini kwenye vitabu nimeongelea vitabu vya uongozi. Mbona hiyo paragraph iko clear?

Kwenye vitabu hakuna tofauti kati ya vitabu vya West au Afrika, kinacho matter ni ubora wa hicho kitabu. Kwenye demokrasia kuna tofauti kubwa sana kati ya West na Afrika na ndio maana nikatumia wenzetu wa West. Nikiambiwa nichague, nitachagua demokrasia ya West kuliko hiyo ya Afrika ambayo ni ubabe ubabe.

Tatizo la sisi Waafrika ni kuwa negative na kila kitu cha West. Mtu akisifia kitu cha West tayari nongwa. Hayo ndio mawazo ya akina Mugabe na wengine naona mnafuata mkondo huo huo mpaka unajikuta unaandika kitu ambacho hakipo. Hata nilipoamua kutoa mfano wa Thartcher nilijua nini kitakuja na kweli sikukosea. Kuwa UK hainifanyi nijue mambo ya UK kuliko wengine, ni sawa na mimi kuwa hapa hainifanye nisijue mambo ya Tanzania ipasavyo.
 
Mbowe kachemsha kung'ang'ania kumfukuza Wangwe. Wangwe mwenyewe ameshasema kwamba Mbowe alisema ama za Wangwe ama zake. Kama manager huwezi kuweka board yako kwenye utata wa namna hiyo. Aliiweka kamati kuu kwenye changamoto kubwa la kuchagua upande. Kama aliona hali ni mbaya hiyo basi angeomba uongozi wote ujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya ili wananchi waamue wanamtaka nani na sio kuanza kufukuzana.

Pia Mbowe katoa mahojiano kwenye Tanzania Daima ambayo yalikuwa yanamshambulia Wangwe moja kwa moja, kama huko si kuchemsha ni nini?

Kwa hiyo wewe Wangwe akisema unaamini, Mbowe akisema unachukia? Kumbuka huyu ana mandate ya kukisemea chama.

Mtaendelea kupia kelele wee! Hili limeshaamuliwa na chama kinasonga mbele. Chadema wameona bora wachukue hatua na watamke wazi kuliko kufichaficha. Kuna ubaya gani? We endelea kulia tu, ulichotaka wafanye sicho walichofanya. Naamini hutajinyonga!
 
Kwani wakati mnampa Wangwe kuwa makamu mwenyekiti, mlikuwa hamjui kwamba anaropoka? Hata Tarime wanajua anaropoka na bado wamempa kuwa mbunge wao. Sio kila mtu afuate diplomasia kwenye uongozi.

Mbowe angeenda kwenye mkutano mkuu au baraza kuu na kuomba kura na kushinda, hapo Wangwe ingebidi anyamaze tu. Lakini kwasasa anasema mawazo yake yanaungwa mkono na wanachama wengi mikoani, kama yuko sahihi kwanini aache kuyasema mawazo kama hayo?

1. Para ya kwanza imejaa hoja za kitoto.
2. Para ya pili iko kwenye kumbukumbu a NCCR-Mageuzi. Chadema wamekataa kurudia makosa hayo.
3. Vile vile, lazima ujue kuwa tatizo lilishagundulika, halikuwa chama wala kundi l watu bali wangwe. Hili ni gugu ambalo dawa yake ni kulin'goa shambani, siyo kutia shamaba zima moto ukachoma magugu na mazao yanayohitajika.

Zipo njia nyingi za kutatua matatizo, siyo lazima wafuate pendekezo lako. Kwa tatizo hili la Wangwe, walichofanya ndicho kilikuwa sahihi kwa wakati huu, badala ya kusbiri sumu isambae hadi Desemba. Na hilo ndilo ulitaka wewe na wengine wanaojifanya mnampenda Wangwe kuliko Chadema, lakini nia yenu inafahamika, na imekomeshwa. Poleni sana!
 
1. Para ya kwanza imejaa hoja za kitoto.
2. Para ya pili iko kwenye kumbukumbu a NCCR-Mageuzi. Chadema wamekataa kurudia makosa hayo.
3. Vile vile, lazima ujue kuwa tatizo lilishagundulika, halikuwa chama wala kundi l watu bali wangwe. Hili ni gugu ambalo dawa yake ni kulin'goa shambani, siyo kutia shamaba zima moto ukachoma magugu na mazao yanayohitajika.

Zipo njia nyingi za kutatua matatizo, siyo lazima wafuate pendekezo lako. Kwa tatizo hili la Wangwe, walichofanya ndicho kilikuwa sahihi kwa wakati huu, badala ya kusbiri sumu isambae hadi Desemba. Na hilo ndilo ulitaka wewe na wengine wanaojifanya mnampenda Wangwe kuliko Chadema, lakini nia yenu inafahamika, na imekomeshwa. Poleni sana!


Hoja ya kitoto siyo? Asante, lete hoja za kikubwa ambazo zitaisaidia CHADEMA ishinde 2010. Naona umechelewa, ungeleta hoja za kikubwa mapema ziwasaidie CHADEMA kushinda Kiteto.

Nia yangu haiwezi kukomeshwa kwasababu sio mwanasiasa na wala shibe yangu haitegemei siasa. I am happy with my profession na ndio inanipa kiburi hata cha kuja kuchat JF.

Ingelikuwa lengo ni kukomoana wala nisingelikuwa hapa JF, kama mna nguvu na uwezo wa kukomesha nia za watu, basi elekezeni huo uwezo wenu mkubwa kwa CCM ambao ndio mnapambana nao. Mchango wangu ni kwa kitu ninachoamini na wala sina nia ya kumkomesha mtu wala kundi la watu.
 
Wangwe ni bora aende kwenye baraza kuu la Chadema na kwa wanachama kueleza uonevu alifanyiwa,

ZITTO KABWE anashirikiana na wabunge wa CCM na anataka kundika kitabu kuhusu maisha ya Amina Chifupa aliyekuwa mbunge wa CCM, kwanini asiandike wasifu wa JUMBE alifariki katika uchaguzi mkuu 2005 kama mgombea mwenza wa Chadema na ameweka historia muhimu zifuatazo, moja ni mgombea pekee wa Chadema kufa ndani ya kampeni za uchaguzi.

pili ni mgombea wa mara ya kwanza ndani ya Chadema kama mgombea mwenza wa Mbowe.

Historia hii nzuri itapotea kama hakuna wa kuandikia, lakini Mwandishi Zitto yuko tayari kutumia resource zake kuandika wasifu wa mtu wa chama pinzani, hivi CCM wanaweza kundika wasifu wa JUMBE wa Chadema?

Wangwe kaondolewa kwa kusemwa kuwa anashirikiana na Kabour na Rostam lakini Zitto alikuwa akivaa koti au akimpa koti lake marehemu Chifupa. kwanini asimwazime koti Muhonga, mdee au Suzan Lyimo wa Chama chake? na kamati kuu ya Chadema haijajadili jambo hili,
Naomba wapenzi wa MBOWE mlete jibu hili.
 
Kwa hiyo wewe Wangwe akisema unaamini, Mbowe akisema unachukia? Kumbuka huyu ana mandate ya kukisemea chama.

Mtaendelea kupia kelele wee! Hili limeshaamuliwa na chama kinasonga mbele. Chadema wameona bora wachukue hatua na watamke wazi kuliko kufichaficha. Kuna ubaya gani? We endelea kulia tu, ulichotaka wafanye sicho walichofanya. Naamini hutajinyonga!

Kiburi kile kile kama cha CCM, mtaendelea kupiga kelele wee huku wao wanatumbua pesa za wananchi. Wanasiasa wetu hamna tofauti, ni kuku yule yule ila kapakwa rangi tofauti.

Kama kelele zetu haziwasumbui, si acha kujibu tu? Tuachie sie wapiga kelele tuendelee na kelele zetu. Vinginevyo kushindana na wapiga kelele si inabidi na wewe upige kelele?

Naona weekend imeisha, nimechangia kwa mara ya mwisho hii thread. Inabidi wengine tukawajibike. kinachoendelea sasa ni kubishana ambako hakumsaidii mtu yeyote.

Ben na Kichwamaji, nawatakieni mafanikio mema katika kuijenga CHADEMA!
 
Walianza mbali mikakati ya kumtoa Wangwe pitieni siri zao.



28th March 2008, 10:37 PM
mtalii
mtalii has no status.
JF Senior Expert Member Join Date: Thu Dec 2006
Posts: 272
Rep Power: 22

Thanks: 58
Thanked 86 Times in 65 Posts
Credits: 9,275

Mwanakijiji Awagombanisha Chadema

--------------------------------------------------------------------------------

Kama kawaida Chama cha Wachagga-Chadema, kimekumbwa na gogoro heavy na mwenyekiti na Makamu wake hawaelewani.

katika hali isiyotarajiwa mtumishi wa Mbowe maarufu kama Mwanakijiji ameporomosha maneno ya kejeri kwa mheshimiwa Wangwe.

habari kamili iko kwenye redio ya Mwanakijiji au redio ya Chadema kwani ccm wanamiliki Redio Uhuru na wenzetu Chadema wamekuja na redio yao.sikiliza vitimbi vya gogoro hilo.
http://mwanakijiji.podomatic.com/ent...22_32_09-07_00
 
mgagagigikoko... miye nina uwezo gani huo? kila mtu anabeba msalaba wake mwenyewe. Jifunze kutaka kila mtu awajibike kwa maneno na matendo yake mwenyewe.
 
Mgagagigikoko...jaribio lako ni dhaifu, kwani hoja ya Wangwe na Chadema watabebeshana wenyewe. Kama tumevisema vitendo vya Lowassa, Kikwete na kiongozi mwingine believe me hakuna mtu ambaye nitamfumbia macho. Kwanini Wangwe awe mti mtakatifu usiokatwa au kusemwa?

SI wa kweli wale wanaoogopa kunyoshea mkono tatizo kwa kuogopa kuonekana wana chuki. Uzuri wa JF na principle yangu ya KLH News ni kuwa "haogopwi mtu, hapendwi mtu, hapendelewi mtu, na yote yanazungumzika". Sorry to disappoint you buddy...!
 
Mkuu Mtanzania

Mbowe hana sauti ya mwisho ndani ya Chadema kama mnavyo taka tuamini .

Lunyungu

Rekebisha usemi wako huu kama kweli wewe siyo CHADEMA kama ulivyojieleza kuwa si mwanachama.

Utayasemaje ya ndani ya CHADEMA ilihali wewe siyo mmoja wao? au huna uhakika na unayosema?

Hivi Mwenyekiti naposema kama Wangwe haondoki basi naondoka mimi na wajumbe wengine wanakaa kimya kuonyesha kukubaliana nae, hiyo siyo kauli ya mwisho ya Mwenyekiti juu ya mustakabali wa Chama? hiyo ni demokrasia ya kweli ya kunyamazisha ukweli wa mambo?

Tafakari kabla hujajibu!!!
 
Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti na jinsi ulivyoitikisa CHADEMA
Theopista Nsanzugwanko
HabariLeo; Tuesday,January 08, 2008 @00:04

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni moja ya vyama vikubwa vya siasa nchini. Kilianzishwa kwa juhudi za waasisi kadhaa wa chama hicho, ambao ni pamoja na Edwin Mtei na Bob Makani.

Mkutano mkuu wake wa kwanza wa chama hicho, ulifanyika katika kituo cha Msimbazi Dar es Salaam kuanzia Desemba 15-17, 1992. Mkutano huu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania na ulichagua viongozi wa kwanza wa chama hicho, majina na vyeo vyao kwenye mabano ni: Edwin Mtei (Mwenyekiti), Ali Suleiman Ahmed (Makamu Mwenyekiti upande wa Zanzibar), Brown Ngwilulupi (Makamu Mwenyekiti Bara), Bob Makani (Katibu Mkuu), Mustafa S. Simba (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar) na Eric Mchatta (Naibu Katibu Mkuu Bara).

Tangu mwaka huo 1992, chama hicho kimeendelea kukua na kufanya uchaguzi wa viongozi wake kila inapobidi. Pia, tangu mwaka huo kimekuwa kikishiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. Matokeo ya kura katika chaguzi hizo yamekuwa ya kuridhisha na hali ya utulivu imekuwa pia inaridhisha.

Hata hivyo, hivi karibuni chama hicho kimetikiswa sana na suala la uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema upande wa Tanzania Bara. Hali hiyo ilijitokeza dhahiri katika vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu vilivyofanyika Dar es Salaam, ambapo baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye alipatikana mshindi, ambaye ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, Chacha Wangwe.

Wakati wa kampeni ya kugombea nafasi hiyo, madai mengi yalitolewa na baadhi ya wanachama wao, kuhusiana na chama hicho hadi ikafika mahali Katibu Mkuu wao, Dk.Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kudaiwa kutaka kujiuzulu nyadhifa zao.

Wanadaiwa walitaka kujiuzulu baada ya kuchukizwa na kitendo cha Chacha Wangwe, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, kukishutumu chama kupitia vipeperushi vilivyosambazwa nchi nzima. Katika vipeperushi hivyo, Wangwe anadaiwa kusema kwamba chama kimegeuzwa kuwa mali ya ukoo na baadhi ya viongozi wa makao makuu.

Vipeperushi hivyo vilisambazwa na wafuasi wa chama hicho, waliokuwa wakimuunga mkono Wangwe katika kinyang'anyiro hicho. Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, zinadai Dk Slaa ambaye ni Mbunge wa Karatu na Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, walifikia uamuzi huo, baada ya hoja kuhusu vipeperushi hivyo kujadiliwa katika kikao hicho.

Hata hivyo, waasisi wa chama hicho, Edwin Mtei na Bob Makani walifanya kazi ya ziada kuwashawishi Dk Slaa na Zitto kubadili uamuzi wao wa kujiuzulu na kuendelea na nyadhifa zao ili kulinda chama kisigawanyike. Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu, kilisema kuwa "Ni kweli Zitto na Slaa walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na vipeperushi vya Wangwe, lakini baada ya mambo kuwekwa sawa na waasisi hao wa chama, walikubali kurejea kwenye nyadhifa zao."

Kutokana na kitendo hicho, Kamati Kuu ilimuonya Wangwe na pia Kamati Kuu ilitishia kufuta uchaguzi huo. Hata hivyo, baadaye Kamati Kuu iliridhia kuwa uchaguzi huo ufanyike. Ilitoa uamuzi huo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupiga kura, ambapo 14 walisema ufanyike na 11 wakasema usifanyike. Ndipo kikao hicho kilifanyika chini ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kuandaa ajenda ambazo zingejadiliwa katika kikao cha Baraza Kuu.

Nalo Baraza Kuu baada ya kujadili ajenda hizo, liliendelea na ajenda ya kumchagua mwanachama atakayejaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti, iliyoachwa wazi na Amani Walid Kabourou, aliyejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana. Lakini, pamoja na kuonywa, Wangwe aliendelea kushikilia msimamo wake ulioko kwenye vipeperushi vyake katika kikao hicho pia. V

ipeperushi hivyo vinawatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kuendesha chama kwa upendeleo, hasa katika mgawo wa ruzuku. Pia, kinawatuhumu viongozi wa Chadema kwa ubaguzi wa misingi ya kidini na Kikanda. Katika vipeperushi hivyo, Wangwe anadai kuwa kutokana na kasoro hizo, atahakikisha analeta mabadiliko ya kweli ndani ya chama ili kukiepusha kuendeshwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO).

"Tunataka kiwe chama cha siasa chenye lengo la kuking'oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010," anasema Wangwe. Anasisitiza kuwa jambo kubwa linalokitia dosari CHADEMA ni ofisi za wilaya na kata kutokuwa na mawasiliano na makao makuu, hasa katika mgawo wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Wangwe anadai mgawo wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu, vimekuwa vikitolewa na uongozi wa Chadema kwa kuangalia upande mmoja wa wanachama wanaotoka Kanda ya Kaskazini hapa nchini. "Chama kimekuwa mali ya koo na familia fulani. Tunataka kiwe cha wanachama," anadai Wangwe, ambaye baadaye alifanikiwa kupata nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti.

Alimshinda Mbunge wa Mpanda Kati kwa tiketi ya Chadema, Said Arfi. Wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Wangwe katika kinyang'anyiro hicho, waliendelea kusambaza vipeperushi hivyo vinavyotuhumu kuwapo na upendeleo katika mgawo wa ruzuku za chama na ubaguzi wa kidini na kikanda katika chama hicho.

Vipeperushi hivyo vilitawanywa makao makuu ya Chadema, mikoani, wilayani na katika eneo ambalo Kamati Kuu ilikutana na vinadai kwamba chama hicho kimekuwa kikipata ruzuku ya Sh milioni 60 kila mwezi, lakini fedha hizo zimekuwa zikiishia makao makuu huku matumizi yake hayawekwi bayana.

"Tunasema inawezekana kila mkoa ukapata Sh milioni 1.5 kila mwezi na makao makuu itabaki na zaidi ya Sh milioni 10 ambazo zinawatosha kwa shughuli za chama," inaeleza sehemu ya kipeperushi hicho.

Kipeperushi kinadai kuwapo kwa "ubinafsi" katika chama, ambao umesababisha karibu wabunge wote wa viti maalumu kuteuliwa kutoka katika mkoa mmoja uliopo eneo la Kaskazini mwa nchi. "Tumchague Chacha ili aweze kubeba majukumu hayo na kuyavalia njuga ili ruzuku igawanywe katika mikoa yote. Chacha pambana kama unavyopambana na CCM katika Jimbo lako la Tarime," kinaeleza kipeperushi hicho.
Kipeperushi hicho kinawataka wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu kutoingia kwenye mtego wa kidini, kwa madai kwamba chama hicho siyo msikiti wala kanisa. "Ni chama cha siasa kinachotaka kuendelezwa na kiongozi jasiri kama Chacha (Wangwe). Hatusemi kwa ushabiki, angalia ukweli hapo makao makuu. Chadema ni chama chetu siyo kampuni ya watu binafsi, tubadilishe hali hii," kilieleza kipeperushi hicho.

Baada ya kutolewa kwa malalamiko hayo yaliyopo katika vipeperushi, Dk.Slaa alikanusha madai yaliyotolewa na kusema kuwa pesa zote za ruzuku, hutumika kutokana na maamuzi ya vikao vya chama.

Pia, alizungumza kuhusu wabunge wa viti maalumu karibu wote kutoka upande mmoja wa Kaskazini, ambapo alisema kutokana na chama hicho kuwa na wabunge wachache, inawabidi kutafuta wenye uwezo katika kutoa hoja za msingi bungeni. "Wabunge huteuliwa kwa kuangalia utendaji wa kazi zao ambazo zinaonekana wakiwa bungeni.

Kule bungeni hatupeleki sura, bali watendakazi ambao ndio jeuri ya chama chetu," anasema. Dk Slaa anasema shutuma zilizotolewa na Wangwe, ambaye alikuwa anagombea umakamu mwenyekiti, ni maneno tu ya kumtaka apate nafasi hiyo.

Wlizungumzia baadhi ya matumizi yaliyoamuliwa katika vikao vya chama, kuwa ni pamoja na kuzunguka nchi nzima kukitambulisha chama kwa Watanzania, ambazo ukiacha usafiri na gharama nyingine zimetumika zaidi ya Sh milioni 200 kutengeneza bendera, kadi na vipeperushi.

Dk. Slaa anasema matumizi kama hayo siyo kwa manufaa ya makao makuu pekee, bali kwa mikoa yote waliyotembelea, ukiacha Mtwara na Lindi, ambayo bado hawajaitembelea kwa lengo la kuwajulisha Watanzania walioko mikoani sera za chama hicho.

"Hakuna chama kingine cha siasa ukiacha chama tawala kilichoweza kuzunguka mikoani na kujitambulisha kwa wananchi kama tulivyofanya sisi kwa shilingi milioni 60 kila mwaka," anasisitiza. Akifungua Baraza Kuu la chama hicho, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alidai suala la kusitishwa kwa mjadala wa Katiba ni ukiritimba. Anasema katiba inapaswa kujadiliwa wakati wowote kwa kuwa ni mali ya wananchi.

Pia, alisema baada ya kutimiza miaka miwili, Rais Jakaya Kikwete inabidi afanyiwe tathmini ya uongozi wake na pia alidai kuwa wananchi wamechoka na kauli za kutia matumaini huku hali ya maisha ikizidi kuwa ngumu. Pia, Mbowe anawataka Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kutoa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwani kampuni iliyopewa kazi ya kuichunguza ilipewa siku 28 tu kukamilisha uchunguzi na kutoa ripoti.

Anadai kuwa siku zimeisha, lakini wananchi bado hawajapewa ripoti hiyo. Baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Baraza Kuu, Mbowe alikanusha kuwa kuna migogoro katika chama chake hicho. Pia, alisema kuwa Chadema itaendelea kutumia helikopta katika awamu nyingine ya ziara zake, baada ya kutafakari gharama za ziara za helikopta.
"Baraza Kuu limetafakari gharama za ziara za helikopta na kuwianisha na ziara nyingine na kuazimia kwa kauli moja kuendelea kutumia usafiri huo katika awamu nyingine ya ziara," anasema.

Mbowe anasema maazimio mengine waliyoyafikia ni pamoja na kuweka hadharani hesabu ya mapato na matumizi, kwani kila mwanachama wa chama hicho ana uhuru wa kufahamu hilo. Alitaka wengine wanaotaka kujua hesabu hizo wafike makao makuu. Pia, Baraza Kuu liliamua kuendeleza ushirikiano wa vyama kwa lengo la kudumisha demokrasia nchini na kuunganisha nguvu katika kutetea maendeleo na hatimaye upinzani uweze kuchukua dola. Baraza hilo lilipitisha azimio la kutangaza ratiba ya uchaguzi wa chama hicho, utakaofanyika kuanzia mwezi Januari hadi Desemba.

Anasema uchaguzi huo utaanzia katika vitongoji, kata, jimbo, wilaya, mikoa na Kanda. Pia, kutakuwa na uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa. Katika uchaguzi wa Makamu wa Mwenyekiti upande wa Tanzania Bara, Baraza Kuu lilimchagua Chacha Wangwe kushika nafasi hiyo, baada ya kupata kura 56 kati ya 94 zilizopigwa. Mpinzani wake Mbunge wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi, alipata kura 38. Akitoa shukrani zake baada ya kutambulishwa rasmi kuwa Makamu, Wangwe anasema atatumia nafasi hiyo kurudisha demokrasia iliyoanza kupotea katika chama hicho. Anasema atafanya hivyo kwa kutumia vikao vya viongozi wa ngazi za juu.
Wangwe anasema kutokana na chama hicho kuwa cha kidemokrasia, mambo yote yaliyotokea ni harakati za kuimarisha demokrasia, hivyo yalikuwa ni sehemu ya midahalo tu; na wala sio migogoro, kama wengi walivyodhania.


Wangwe ahukumiwe kwa yale anayoyadai na wala si vinginevyo.

Katika hali ya kawaida ya wanasiasa wa kiafrika kama Mugabe na wengineo, sidhani kama wako tayari kukubali kupokea maneno kama ya Wangwe kwani siku zote hujiona kuwa wao ni miungu watu.

Sie tuliokuwa nje ya CHADEMA tumekuwa tunapata wasiwasi wa jinsi mambo yanavyokwenda, lakini hayatofautiani na madai halisi yanayotolewa kutoka ndani na kiongozi wa juu kabisa wa chama hicho.

CHADEMA kama mnaona kumuondoa Wangwe ndiyo itakuwa nafuu yenu ya kufanya mambo mnayotaka bila kuulizwa, hapo mnatupa wasiwasi mkubwa wa uaminifu wenu kwa jamii ya watanzania. Ipeni nafasi demokrasia itawale ndani ya Chama chenu na wala siyo kutumia ubinafsi. Hili la Wangwe ni moja mengi mengine huenda yapo lakini yanasubiri wakati yalipuke.

Toeni boriti ndani ya macho yenu kabla hamjamgeukia Wangwe.
 
Pundamilia... tukisema AtCL kuna tatizo, tunaonesha ushahidi japo wa mahali pa kuanzia, tukisema serikali haisimamii vizuri fedha za walipa kodi tuna ripoti ya Mkaguzi Mkuu kuangalia; tukisema sheria fulani ni mbaya tunaonesha sheria hiyo na vipengelle hivyo. Hivyo madai mazitu ambayo mtu anayatoa ni lazima yaendane na ushahidi wa wazi ambao ni kianzio cha uchunguzi.

Mtu akija na kusema nimeibiwa kuku, basi angalau aoneshe aliwahi kuwa na kuku huyo. Habari uliyonukuu toka Januari na madai ambayo yalioneshwa kwenye viperereshi hivyo ni madai tu lakini hayajajengwa katika msingi wowote wa ushahidi.

Hebu tuyaangalie mada haya na angalau ushahidi unaotolewa kuonesha ukweli wake:

baadhi ya viongozi wa Chadema kuendesha chama kwa upendeleo, hasa katika mgawo wa ruzuku.

Basi tuoneshe upendeleo huu kwa mgao wa ruzuku. Ruzuku inatolewa kiasi gani, inapelekwa wapi, na kwanini inapelekwa huko na si kwingine (msingi wa upendeleo?)

Pia, kinawatuhumu viongozi wa Chadema kwa ubaguzi wa misingi ya kidini na Kikanda.

Basi angalau tuoneshwe ushahidi huo wa ubaguzi wa misingi ya kidini na kikanda (baadaye tumesikia ukabila??). Chama kinawanachama wangapi, wamegawanyika vipi n.k Tuoneshwe huo msingi wa "ubaguzi wa kidini na kikanda" ambao si idadi ya watu bali hisia ya upendeleo wa wazi wenye lengo la kunufaisha watu wa dini au kanda fulani.

kukiepusha (chama) kuendeshwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO).

Hili ni dai la kipuuzi (lisiloingia akilini), sasa mdai alitaka chama kiendeshwe kama shirika la kiserikali? the absurdity of the absurdities...

ofisi za wilaya na kata kutokuwa na mawasiliano na makao makuu,

Basi ingetolewa hata mfano kuwa wilaya x au kata y imejaribu kuwasiliana na makao kuhusu jambo hili kwa barua hii au ile na hawakupata majibu. Au kiongozi wa wilaya amejaribu kuwasiliana na viongozi makao makuu na hana namba ya makao makuu n.k n.k Ruzuku??

Wabunge wa viti maalum ni hoja nzuri sana lakini angeonesha basi waliopo wamechaguliwaje, mfumo ulikuwaje, je kama makosa yalitokea yamesahihishwa??? Kwanini kulitokea yaliyotokea n.k
Chama kimekuwa mali ya koo na familia fulani. Tunataka kiwe cha wanachama

Hili ni wazo la hatari ndani yake. Hivi kuna wanachama wangapi wa CCM kutoka familia ya Kikwete? Je kuna wanafamilia wangapi katika CCM kutoka ukoo wa kina Kawawa? Je watu wa familia moja wakiwemo ndani ya chama kunafanya chama hicho kuwa cha koo? Je mtoto wa fulani akijiunga na chama fulani basi asipewe nafasi ya uongozi kwa vile jina lake linatokana na familia fulani. Ukizungumzia ubaguzi basi unaweza kuona unatoka wapi?
 
Back
Top Bottom