Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,230
Ben,
Nimegundua husomi hoja vizuri kabla ya kujibu maana hii sijui ni mara ya ngapi nakukamata kwamba unaongelea kitu ambacho mimi sijaongelea.
Ebu highlight mahali popote ambapo mimi nimeongelea western books. Vingine sema umekosea tena kwa mara ya pili. Ni shida sana kubishana kwa hoja na watu ambao huwa hamtulii na kusoma kilichoandikwa kwanza.Nilichoandika ni kama hapa:
"Wenzetu wa West ndivyo wanavyofanya na pia vitabu vya uongozi ndio vinavyosema, labda vimetungwa na watu ambao hawajaenda shule kwi kwi kwi!!!"
Mimi nimeongelea vitabu vya uongozi na wala sio vitabu vya West. Nimeongelea wenzetu wa West na nikatoa na mfano wa Thartcher lakini kwenye vitabu nimeongelea vitabu vya uongozi. Mbona hiyo paragraph iko clear?
Kwenye vitabu hakuna tofauti kati ya vitabu vya West au Afrika, kinacho matter ni ubora wa hicho kitabu. Kwenye demokrasia kuna tofauti kubwa sana kati ya West na Afrika na ndio maana nikatumia wenzetu wa West. Nikiambiwa nichague, nitachagua demokrasia ya West kuliko hiyo ya Afrika ambayo ni ubabe ubabe.
Tatizo la sisi Waafrika ni kuwa negative na kila kitu cha West. Mtu akisifia kitu cha West tayari nongwa. Hayo ndio mawazo ya akina Mugabe na wengine naona mnafuata mkondo huo huo mpaka unajikuta unaandika kitu ambacho hakipo. Hata nilipoamua kutoa mfano wa Thartcher nilijua nini kitakuja na kweli sikukosea. Kuwa UK hainifanyi nijue mambo ya UK kuliko wengine, ni sawa na mimi kuwa hapa hainifanye nisijue mambo ya Tanzania ipasavyo.
Mtanzania,
Naomba unitake radhi hapa! Hili kwangu ni tusi na umelirudia tena.
Hakuna mtu aliye-negative kwa kila kitu cha West,hayo ni mawazo yako ya kuona suluhisho la matatizo yetu ni kuiga kila kitu cha west,huku ukishindwa ku-apply kuendana na mazingira.Eti,unang'ang'ania kuhusu masuala ya mashirika makubwa kupelekwa ndani ya bodi huku ukishindwa ku-apply theory hiyo ktk huu mgogoro wa CHADEMA ili kuendana na Muongozo wa chama na mazingira ya mgogoro,Si tutauita utaahira huo?
Maanke kwa mtu mwenye akili timamu atakushangaa,halafu kumbe kukurupuka kwako koote kumbe wewe mwenzetu unabishana? and what is the motive behind? Kumbe ndiyo maana hata hoja nilizokukamata nazo hutaki kuzijibu kwa sababu ubishi ndiyo umekuweka hapa? Hii ni dhambi kubwa sana kwa mtu mzima kama wewe kukaa nyuma ya PC na kubishana bila faida yoyote.