Mkuu Mtanzania .Nimekaa muda wote kimya kuutafuta ukweli juu ya Wangwe na Chadema yao hatimaye nimeamua kusema ninalo lijua .Namkatalia Mbowe kusema kwamba Wangwe anauza siri za Chama kwa kusema na traitor Kaburu wa CCM , maana hata mimi sina Chama lakini nina marafiki kote kuanzia CCM hadi Upinzani .Lakini naheshimu maoni yake ambayo mimi nayakosoa .
Wangwe kuwa kwenye payroll ni muda sasa nma soon nitamwaga mboga hapa .Mie sikukurupuki .Kwa tabia za Wangwe za wivu na kutaka asujudiwe na ngumi mkononi na kutoa madai ambayo hawezi kusema anataka kufanya hayawezi kuvumiliwa.Kwa mfano Wangwe amemtukana msanii wa Chama matusi ya nguoni na kuahidi kumuondoa Chadema .Msanii yule ni kijana mdogo sana kwa umri na hata madaraka kwa Wangwe .Kama kweli anataka kurekebisha kwa nini asitumie proper channels ?
Chadema imempa hata nafasi ya kujifunza uongozi lakini yeye kabakia kuwa mtemi na mlalamishi kila kona .Nadhani nakubaliana naye kusema mawazo yake wazi bila ya kufunikwa na Chadema nao wako wazi kusema why kasimamishwa .
Mbowe hana sauti ya mwisho ndani ya Chadema kama mnavyo taka tuamini .Nadhani kuna kuendeleza matakwa ya CCM kwamba Chadema ni Mbowe wakati naja ujua ukweli wote .
Tungoje mkutano mkuu utakuja tutaona lakini watu hawawezi kuogopa kukabiliana na uozo kwenye Chama kama CCM wanavyo fanya .Kukaa kimya wakati wana uozo kutawaondolea wana Chadema uhalali wa kukemea mambo kwa kuwa wao wenyewe hawawezi kukemeana .
Hongereni Chadema .
Lunyungu,
Lete video za Ballali kwanza kabla hata hujatuletea ya Wangwe kwi kwi kwi!!!. Mkuu ukiahidi kitu inabidi utimize vinginevyo tutaanza kukuita msanii kwi kwi kwi!!!
Pia kujifunza uongozi unafikiri ni rahisi sana? Mbona mwenyekitui wenu mwenyewe kazunguka na MBA nchi tatu lakini bado maamuzi mengine ni yale yale ya manguvu tu? Ungetegemea hiyo MBA ingempa busara ya kuchukua maamuzi kwa uangalifu zaidi.