Tarime waunga mkono kusimamishwa kwa Wangwe
2008-07-04 09:21:55
Na Simon Mhina
Uongozi wa CHADEMA wilayani Tarime, umemgeuka mbunge wao, Bw. Chacha Wangwe kuhusiana na kusimamishwa kwake uongozi.
Bw. Wangwe pia ni Makamu Mwenyekiti wa wa chama hicho.
Pamoja na kuunga mkono, uongozi huo umepinga madai yake kwamba rukuzu inayotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa haifikishwi mikoani.
Aidha, uongozi wa chama hicho mkoani Mara, umeelezea kusikitishwa na madai ya Bw. Wangwe na kusema hivi sasa wanamtazama kama mtu asiyekitakia mema chama hicho.
Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Tarime, Bw. Joseph Anthony alisema inasikitisha kuona kiongozi wa juu wa chama kama Bw. Wangwe anaanzisha hoja ya malumbano yenye nia ya kukiangamiza chama.
Akifafanua alisema inasikitisha kuona Bw. Wangwe akitoa taarifa zisizo sahihi kwenye vyombo vya habari kwamba ruzuku ya chama hicho inaishia makao makuu.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Wilaya yake ya Tarime inapokea Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya kukijenga chama.
Kwa msingi hiyo, Bw. Joseph alisema wilaya ya Tarime inaunga mkono kusimamishwa kwa Bw. Wangwe katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.
Aidha, alimshauri Bw. Wangwe kuacha mipango yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la chama kupinga uamuzi wa kusimamishwa na badala yake asubiri uchaguzi mkuu ujao.
Alisema Bw. Wangwe anatakiwa kujirudi na kujisafisha kwa njia ya kushirikiana na viongozi wenzake, kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari na kukanusha tuhuma dhidi ya viongozi wenzake.
Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafar Kasisiko alisema wao wana wasiwasi mkubwa kwamba Bw. Wangwe anatumiwa kukivuruga chama.
Bw. Kasisiko alisema anachokifanya kiongozi huyo hadi akasimamishwa kina lengo la kuwafanya mafisadi wafurahie.
Mwenyekiti huyo alisema wilaya zake zote zinapata gawiwo la ruzuku tofauti na madai ya Bw. Wangwe.
SOURCE: Nipashe
mgagagigikoko, soma tena haijasemwa "wamemtaka" asiende Baraza Kuu... mbona inakuwa kazi...?
Wanasema bora asiende huko, wao wamenyima haki na hao hao wanamshauri asiende mbele ya safari akasafishe jina lake au akapate haki yake ili uamuzi utenguliwe,Mtikila kila mara anakwenda mahakamani na anapata haki yake.
ningependa siku moja nikutane na huyu mushi maana ananishangaza sana kwa wepesi na haraka yake ya kuandika
Kasoro anaozisema Wangwe, zikirekebishwa then Wangwe hatakuwa na hoja wala following kama ilivyo sasa,
Chadema watumie umakini ku-deal na hoja za Wangwe, badala ya kujaribu kupambana na Wangwe as a person, kwa sababu reading between the lines ni clear kuwa Wangwe has nothing to lose, na hii vita isipokuwa ana-gain tu,
So far Chadema, hamjaonyesha umakini kwenye ku-deal na this ishu, na kwakweli binafsi nimesikitishwa sana hasa baada ya kuona vitimbi vingi humu ndani ya forum vya kujaribu ku-deal na hii ishu lakini kwa kweli ni kujishusha hadhi ni afadhali kuwa tumejua mapema,
na binafsi nimeridhishwa sana na maneno mazito sana ya Kitila on this ishu, anaonekana kuwa amekomaaa kisiasa na kitaifa pia na anweza kuwa the best alternative huko mbele ya safari. I wish wale wenzetu wange-invest in him kwa sababu anaonyesha kuwa makini sana.
Kha! kumbe zemarcopolo ni Balile?
Kama huyu ndiye Balile niliyekua namuona mtu makini,sasa nikiangalia alivyokua anaandika hapa nabaki Hoi kabisa!
Mkuu FMES,
CHADEMA wasipokua makini hiii ishu itawayumbisha sana.Sasa hivi mwaka mmoja na nusu umebaki kuingia kwenye uchaguzi,sasa doa kama hili likiingia kwenye vichwa vya wananchi itakua balaa.
Hata hivyo,watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa finally aliyemsimamisha Wangwe si Mbowe bali ni kamati.Watu wanaofikiria kuwa Mbowe ndiye aliyemsimamisha Wangwe basi ndiyo wenye mawazo ya kidikteta zaidi kwa kuamini hata wao wangekua wenyeviti wa CHADEMA au taasisi nyingine wangeeweza kumsimamisha mtu kazi bila kufuata Demokrasia.Sasa unakuta watu wametingwa na mawazo ya kidikteta zaidi ndiyo maana perception yao imefikia huko kwa urahisi
Mwenyekiti wa Taifa NCCR ni Mbatia mtu wa Kilimanjaro, mgombea urais kwa tiketi ya NCCR alikuwa kutoka Kilimanjaro bwana Mvungi, nadhani ni mkakati ule ule wa Kanda ya kaskazini,
maandishi haya yameandikwa na gazeti linalomilikiwa na Mbowe-Tanzania Daima.
vijana achaneni na hizi one-man parties.jiungeni na vyama vya umma.
JASILI HAACHI ASILI,tatizo la wangwe ni kabila analotoka!...............MWINJUMA MUUMINI aliwahi kukiri kuwa tatizo linalomsumbua ni uzalamu wake,hivyo na WANGWE nae ubabe anaounesha ni kuuendekeza ukulya wake