Hayo ni maoni ya bwana 30 (selasini) au ya chama cha NCCR? ikumbukwe hata NCCR ilishutumiwa hivihivi na mnaona ilipo sasa NCCR...Ni wakati wa CHADEMA kuyashughullikia maneno haya ambayo yamekua yakiongelewa na watu wengi "SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU"......sasa hivi NCCR imebaki na Mbatia+Mvungi hata huyo selasini wengine ndio leo tunamsikia...ni lazima baadhi ya vyama vya upinzani vibadilike ili tuweze kupiga hatua la sivyo mtapaa na helkopta for nothing
Son, vyama vya umma ndiyo vipi hivyo?
akili kichwani.
Je, una maoni gani kuhusiana na udini wa mafisadi na ukabila wa ufisadi ndani ya Chama Cha Mafisadi? Je, nako kuna sauti ya Mungu inayowaambia wana CCM waendelee kuukumbatia udini na ukabila wa kifisadi?
Nakubali asili ya Wangwe ni ubabe wa kikulya,,,haya kama we ni muungwana naomba utuambie kinachowasumbua waliomfukuza (Wachaga)...kisha utukumbushe na Kabourou alisema nini baada ya kujiengua chadema,,,,lazima mkubali sauti ya watu ni sauiti ya mungu,,,angekua wangwe ndie wa kwanza kuwatuhum ukabila ningekuunga mkono but for that you are wrong dawg
CCM ndiyo chama cha umma? 😕😕😕😕
Kama unazungumzia umma wa mafisadi akina Mkapa, Chenge, Karamagi, Lowassa, Msabaha, RA na wengine basi hujakosea lakini kama unazungumzia umma wa Watanzania basi kwa taarifa yako umma wa Watanzania umepoteza imani na chama cha mapinduzi ambacho sasa kimegeuka na kuwa ni chama cha mafisadi. Ndiyo maana wanaparurana makucha hadharani wenyewe kwa wenyewe.
Acha jazba mkubwa,,,hata kama utanishambulia ntaendelea kukheshim kwa michango yako hapa JF....Pia naomba unielewe mie siko chama chochote hususani CCM...ila niko upande wa chama chochote chenye mwelekeo wa kuleta mabadiliko hususani katika siasa na maendeleo...CHADEMA ni mbadala mzuri endapo wataendelea na kuendesha siasa safi ya kidemocrsia..Kwa mtu mwenye uelewa mdogo hueda akajua mie ni ANT-CHADEMA..lah hasha, mie ninataka warekebishe kasoro zilizopo kwenye chama ambazo zinaleta sura mbayakwa jamii...ni hayo tu
watanzania mmezoea kulalamikia pembeni,mkiambiwa msimame mbele ya umma na kuongea mnanywea,mkiambiwa mjitokeze mkagombee nafasi katika vyama hamjitokezi,wenzenu wakijitokeza mnadai ukabila!...kipindi cha mwinyi mlisema anawapendelea waislam,alipoingia mkapa mkasema amejaza wakristo kwenye uongozi wake,mtabakia kalaghabao!!
kaka,kama kujiabisha basi wanaaibika ccm kwa kukumbatia mambo ya ajabu(ufisadi)
Acha jazba mkubwa,,,hata kama utanishambulia ntaendelea kukheshim kwa michango yako hapa JF....Pia naomba unielewe mie siko chama chochote hususani CCM...ila niko upande wa chama chochote chenye mwelekeo wa kuleta mabadiliko hususani katika siasa na maendeleo...CHADEMA ni mbadala mzuri endapo wataendelea na kuendesha siasa safi ya kidemocrsia..Kwa mtu mwenye uelewa mdogo hueda akajua mie ni ANT-CHADEMA..lah hasha, mie ninataka warekebishe kasoro zilizopo kwenye chama ambazo zinaleta sura mbayakwa jamii...ni hayo tu
Sentensi gani hapo juu ambayo nimekushambulia? Tangu lini kuuliza maswali ikawa na kushambulia? Hebu soma tena uone kama nimekushambulia. Kama bado utaamini nimekushambulia basi iweke hiyo sentensi ambayo nimekushambulia hadharani.
Mimi sina chama wala sina mpango wa kujiunga na chama chochote, labda mpaka pale wapinzani watakapoamua kusikiliza maoni ya Watanzania wengi wanaotaka vyama hivyo viungane ili kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kiing'oe CCM madarakani.
Pamoja na kuwa sina chama sitasista kujadili kuhusu unafiki wowote unaonyeshwa na CCM kutaka kulikuza swala la Wangwe kama vile lina maslahi makubwa kwa Tanzania kuliko maswala la EPA, Richmond, Kiwira, Mikataba mibovu ya madini ambayo wahusika wake wote bado wamekumbatiwa ndani ya chama hicho pamoja na kuwa wamefanya ufisadi wa hali ya juu kwa kukwapua zaidi ya shilingi bilioni 500 na mpaka leo leo hakuna dalili kama sheria itafuata mkondo wake ili mafisadi hao wachukuliwe hatua na hatimaye kufilisiwa.
Ndugu yangu lazima uelewe siasa ya dunia ya leo inataka nini na umma unaelewa nini kuhusu kinachoendelea katika siasa,,swala sio kulalamika hapa,swala ni je hoja za wangwe ni reasonable na je? zinaukweli wowote ndani yake?.Kwa sasa uelewa katika jamii umeongezeka watu wanapima mambo na sio kufuata upepo eti kwa vile flani kasema!!!!! Mambo ya rushwa hayajaanza juzi, yameanza siku nyingi hata hapa kwetu tanzania, lakini tofauti ni kwamba watu kwa sasa wana uelewa wa hali ya juu sana katika maswala ya siasa na baada ya miaka michache ijayo ndio itakua balaa zaidi maana watu hawatadanganywa hata kwa sekunde 2
Nashukulu sasa umeanza kuelewa bwana mdogo,,,ni kweli CCM wanakumbatia ufisadi,,na ili kuuondoa ufisadi tunahitaji chama mbadala chenye mwelekeo mzuri na chenye sura ya kitaifa (CHADEMA safi)....lazima wakubali kurekebisha makosa yaliyopo waache propaganda za kizamani la sivyo hata huo umaarufu walonao sasa utakua kazi bure
kwa kiongozi kama yeye aliyekuwa katika nafasi ya juu katika chama si vizuri kukurupuka na kuropoka ropoka bila kuwasiliana kwanza na chama,!
siku watu wote duniani wakija kuwa na mawazo na akili sawa basi ndio itakuwa mwisho wa dunia hii!mi siwezi kuihukumu CHADEMA kwa uhuni wa WANGWE,kumbuka mtu huyo alifanya nini NCCR,ni sawa kuihukumu CUF kwa maneno ya TAMBWE utakuwa unakosea sana
Nini maana ya democrasia?? Mie nilidhani CHADEMA chama cha democrasia?!!! kwamba mtu ana uhuru wa kutoa na kuongea maoni yake ati?!?!?...aise hizo siasa zilishapitwa na wakati hata ccm wameacha kuzifuata,
Juzi tumeshuhudia wana CCM wakiropoka kwa nguvu kwa maslahi ya wananchi na kwa maslahi ya chama chao kina Mwakyembe, Anna etc,
sasa leo wangwe akitaka kutoa maoni yake utoka kichwani kwake ni lazima awasiliane na chama au sio?? Kumbe bado tuna safari ndefu sana katika siasa kwa mwendo huu maana nilikua sijui hilo kama CHADEMA bado wanaliendekeza
,ni sawa kuihukumu CUF kwa maneno ya TAMBWE utakuwa unakosea sana
fahamu kuwa NENO LA RAIS NI NENO LA SERIKALI,hivyo na NENO LA KIONGOZI MKUBWA KAMA YEYE NI NENO LA CHAMA,unafikiri rais huwa anakurupuka kuropoka bila kupata japo ushauri katika mambo yanayoihusu nchi kwa sababu yeye ndio mwenye POWER?
Siasa za kizamaaaani eti maneno ya rais ni maneno ya chama?!?!?!?.... Kwa maana hiyo mbowe anapotuhumiwa ufisadi ni kwamba chadema nao ni mafisadi??
soma vizuri kitu nilichoandika,uzamani gani unaosema wewe?we unadhani rais au kiongozi yoyote wajuu ni watu wa kuropokaropoka tu,nenda ukajifunze utambue kuwa MATAMSHI yatolewayo na wakuu wa serikari na chama yana uzito gani katika jamii sio kubisha tu