Mkuu Mtanzania .Nimekaa muda wote kimya kuutafuta ukweli juu ya Wangwe na Chadema yao hatimaye nimeamua kusema ninalo lijua .Namkatalia Mbowe kusema kwamba Wangwe anauza siri za Chama kwa kusema na traitor Kaburu wa CCM , maana hata mimi sina Chama lakini nina marafiki kote kuanzia CCM hadi Upinzani .Lakini naheshimu maoni yake ambayo mimi nayakosoa .
Wangwe kuwa kwenye payroll ni muda sasa nma soon nitamwaga mboga hapa .Mie sikukurupuki .Kwa tabia za Wangwe za wivu na kutaka asujudiwe na ngumi mkononi na kutoa madai ambayo hawezi kusema anataka kufanya hayawezi kuvumiliwa.Kwa mfano Wangwe amemtukana msanii wa Chama matusi ya nguoni na kuahidi kumuondoa Chadema .Msanii yule ni kijana mdogo sana kwa umri na hata madaraka kwa Wangwe .Kama kweli anataka kurekebisha kwa nini asitumie proper channels ?
Chadema imempa hata nafasi ya kujifunza uongozi lakini yeye kabakia kuwa mtemi na mlalamishi kila kona .Nadhani nakubaliana naye kusema mawazo yake wazi bila ya kufunikwa na Chadema nao wako wazi kusema why kasimamishwa .
Mbowe hana sauti ya mwisho ndani ya Chadema kama mnavyo taka tuamini .Nadhani kuna kuendeleza matakwa ya CCM kwamba Chadema ni Mbowe wakati naja ujua ukweli wote .
Tungoje mkutano mkuu utakuja tutaona lakini watu hawawezi kuogopa kukabiliana na uozo kwenye Chama kama CCM wanavyo fanya .Kukaa kimya wakati wana uozo kutawaondolea wana Chadema uhalali wa kukemea mambo kwa kuwa wao wenyewe hawawezi kukemeana .
Hongereni Chadema .
Lunyungu,
Lete video za Ballali kwanza kabla hata hujatuletea ya Wangwe kwi kwi kwi!!!. Mkuu ukiahidi kitu inabidi utimize vinginevyo tutaanza kukuita msanii kwi kwi kwi!!!
Pia kujifunza uongozi unafikiri ni rahisi sana? Mbona mwenyekitui wenu mwenyewe kazunguka na MBA nchi tatu lakini bado maamuzi mengine ni yale yale ya manguvu tu? Ungetegemea hiyo MBA ingempa busara ya kuchukua maamuzi kwa uangalifu zaidi.
Lunyungu,
Kuwa fair, nani katika CHADEMA ameteswa na CCM zaidi ya Wangwe? Kuanza .
Wangwe hakuteswa kwa ajili ya Chadema, na hiyo so tiketi kwamba akifanya makosa aachwe. kazi mnayofanya hapa kumtetea wangwe na makosa yake, mnapoteza muda kuwafurahisha kina Rostam Aziz, wakidhani hili litafunika mambo yao.
Tuwaache Chadema watekeleze kazi zao, watimuane na kuwekana sawa kadiri ya kanuni zao. Afadhali wao wako kazini wanatenda jambo linaonekana na wanachukua hatua kali kama hizi. Wanaoshindwa kuadhibiana si mnawajua? Hii nayo ni ishara kwamba Chadema kina uongozi unaochukua hatua pale inapobidi, maana wamejitahidi kumrekebisha Wangwe kwa vikao vidogo na vikubwa, hadi hapo walipofika.
Msitake kuvuruga chama. Muwaache wawekane sawa maana wanafahamianan kuliko nyie mnavyowafahamu. Siasa hazifanyiki kwenye mtandao wa JF, wale mnaotaka kufanya siasa, nendeni kazini, kama hamuwezi waache waliothubutu wafanye kazi.
Wangwe hakuteswa kwa ajili ya Chadema, na hiyo so tiketi kwamba akifanya makosa aachwe. kazi mnayofanya hapa kumtetea wangwe na makosa yake, mnapoteza muda kuwafurahisha kina Rostam Aziz, wakidhani hili litafunika mambo yao.
Tuwaache Chadema watekeleze kazi zao, watimuane na kuwekana sawa kadiri ya kanuni zao. Afadhali wao wako kazini wanatenda jambo linaonekana na wanachukua hatua kali kama hizi. Wanaoshindwa kuadhibiana si mnawajua? Hii nayo ni ishara kwamba Chadema kina uongozi unaochukua hatua pale inapobidi, maana wamejitahidi kumrekebisha Wangwe kwa vikao vidogo na vikubwa, hadi hapo walipofika.
Msitake kuvuruga chama. Muwaache wawekane sawa maana wanafahamianan kuliko nyie mnavyowafahamu. Siasa hazifanyiki kwenye mtandao wa JF, wale mnaotaka kufanya siasa, nendeni kazini, kama hamuwezi waache waliothubutu wafanye kazi.
Mkuu Kichwamaji,
Umenena!
kuna watu wanakua mawakala wa shetani bila kujua,sasa watu kama hao ni bora tu hata kutumia muda mwingi kuwakomboa ili tuende sote
[/B]
Naona hili suala la Wangwe si tatizo.Target za CCM na makada wake ziko kuisambaratisha CHADEMA.Hebu ona huu mjadala wa Wangwe ulikoishi.Hebu cheki hapo nilipo-bold.
Sibabaishwi kabisa na maneno kama hayo, mmempaka matope Kabouru, sasa wangwe, mtashindwa kumpaka matope Mtanzania?
Endeleeni na hiyo tabia ya ku question motive na integrity ya watu ambao hata hamuwajui, ni dalili ya kushindwa hoja. No wonder kila mkienda kwa wananchi kuomba kura mnapigwa bao.
CHADEMA ina watu makini wengi tu, mungelikuwa mnawasikiliza wanachosema naamini mungesonga mbele. Lakini hii ya kuwategemea akina kichwamaji, mtachakaa kwenye upinzani kwa muda mrefu sana.
Kwani si ni ukweli mtupu? Toka lini mijadala ya JF ikawa na boarders? Kama Wangwe alipewa nafasi ya kujifunza uongozi bora lakini anachemsha, kuna tofauti gani na Mbowe kusomea MBA ili kujifunza uongozi bora lakini bado anachemsha?
Hoja hujibiwa kwa hoja na mifano hujibiwa kwa mifano, hiyo ndio JF.
Inafurahisha pale inapoonekana kila anayeandika baya kuhusu CHADEMA au Mbowe basi ni kada wa CCM. Ukiandika baya la CCM, wewe ni CHADEMA. Ni mawazo finyu kufikiri kila anayekuja hapa JF ana motives mbaya za kisiasa.
Mkuu Mtanzania,
Naona sasa mkuu una lako jambo,nani kataka kukubabaisha mkuu? It's a pity kwamba unani-quote halafu unani-include katika watu unaowajua wewe wa kupaka watu matope.Mkuu wangu,for this you are wrong unless you come out to prove otherwise
Pili,unatumia neno Endeleeni:sasa hapa ni nani na nani? halafu sijui umahiri wako wa kujenga hoja uko wapi maanke hata runashindwa kutofautisha kati ya kuhoji intergrity ya watu wasiojulikana na kuhusu kutoshinda chaguzi.hivi haya ni mambo yanayofanana kweli?
Tatu,unasema chadema kuna watu Maskini sasa na huko CCM kuliko na watu matajiri kumelifanyia nini taifa?Si ndiko kumekua chanzo cha umaskini wa watanzania?Miaka nenda rudi hatubanduki top ten ya nchi maskini zaidi duniani just because of matajiri walioko CCM? ,naam watu matajiri maanake sijawahi kujua kama CCM ni chama cha matajiri tu,naona hata umeamua kuwa-label watu maskini ni wa CHADEMA kwa hiyo ndiyo wanastahili kuwasikiliza hao maskini! brother,you must be kidding!
Btn: wewe ni mtu unayeheshimika sana hapa jamvini but pls stop personal attacks against others! Umefanya personal attack against mwenyekiti wa CHADEMA,ukaachwa tu.Sasa hapa brother unakurupuka na kuni-quote sehemu ambapo sijakulenga wewe ila ulijishtukia tu
Hivi Mbowe kachemsha wapi?Maanake wewe na personal attacks zako ni mojawapo wa baadhi ya watu wenye mawazo ya kidikteta wanaofikiria Mbowe kama Mwenyekiti ndiye aliyemsimamisha Wangwe uenyekiti.Yaani ninyi watu wa aina hii ndio madikteta kwani mnafikiri mtu yeyote kwa vile ni mwenyekiti anaweza tu kumfukuza mtu kazi au uongozi,yaani kwa maneno mengine mnafikiria siku moja mkiwa wenyeviti basi mnaweza kufanya maamuzi ya kiimla tu kwa kuwa wewe ni mwenyekiti.
Nani kasema kila anayeandika baya kuhusu CHADEMA ni CCM? CHADEMA ni chama cha kidemokrasia na kinathamini constructive criticisms,na hayo si mabaya against CHADEMA. Sasa kwa vile Umesema neno BAYA,basi anayeandika mabaya kuhusu CHADEMA si mtakia mema hicho Chama na possibility kubwa anweza kuwa mpinzani wa Mabadilko ya kweli Nchini,au mpinzani wa uhuru wa kweli!Huyo ni adui mkubwa wa uwakilishi wa mawazo mbadala yatakayoleta fursa ya mapinduzi ya kweli katika taifa letu tukufu.
Pia kuna kila sababu ya kuonekana CCM mhafidhina au CCM mfisadi maanake kuna wana-CCM waadilifu na liberal minded ambao hawakerwi na uwepo wa changamoto kutoka upinzani
Wapi nimeandika CHADEMA kuna watu maskini? Ni ngumu sana kujadiliana na watu wasiosoma kinachoandikwa na badala yake kukimbilia kujibu. Rudi kusoma nilichoandika, vinginevyo ni kupoteza muda hapa.
Aliyeandika wakala wa shetani ni nani kama sio wewe?
Sibabaishwi kabisa na maneno kama hayo, mmempaka matope Kabouru, sasa wangwe, mtashindwa kumpaka matope Mtanzania?
Endeleeni na hiyo tabia ya ku question motive na integrity ya watu ambao hata hamuwajui, ni dalili ya kushindwa hoja. No wonder kila mkienda kwa wananchi kuomba kura mnapigwa bao.
CHADEMA ina watu makini wengi tu, mungelikuwa mnawasikiliza wanachosema naamini mungesonga mbele. Lakini hii ya kuwategemea akina kichwamaji, mtachakaa kwenye upinzani kwa muda mrefu sana.
Ni mimi niliyeandika nikiwalenga wale Mafisadi wanaokerwa na uhai wa CHADEMA kama chama mbadala Tanzania kwa maslahi yao binafsi huku taifa likiangamia,sidhani kama nitakua muumini mzuri wa dini nikiwa-label hao watu kuwa malaika,kwa vyovyote vile hao wanaongozwa na roho mwovu.Jina wanalo-deserve ni mawakala wa Shetani.Sasa sijui wewe umeibukia vipi hapo au kujishtukia tu?
Kuhusu CHADEMA kuwa na watu maskini umesema hapo niko-bold.Wewe ndiye unapoteza muda hapa maanake kumbe hata huelewi unachoandika au tuseme unakimbilia ku-type na kupost bila kusoma.Mkuu mbona hujatulia? yaani kweli mkuuu,wewe unayeheshimika hapa jamvini kwa hoja makini kumbe huwa hujui unaloaandika? Unaonekana wewe ni mtu ambae unashindwa kuwa makini na mambo yako.Jirekebishe brother!
rudi kasome ulichoandika kabla hujakana ulichopost.Kila mwanaJF anaona ulichoandika
Mbowe kachemsha kung'ang'ania kumfukuza Wangwe. Wangwe mwenyewe ameshasema kwamba Mbowe alisema ama za Wangwe ama zake. Kama manager huwezi kuweka board yako kwenye utata wa namna hiyo. Aliiweka kamati kuu kwenye changamoto kubwa la kuchagua upande. Kama aliona hali ni mbaya hiyo basi angeomba uongozi wote ujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya ili wananchi waamue wanamtaka nani na sio kuanza kufukuzana.
Pia Mbowe katoa mahojiano kwenye Tanzania Daima ambayo yalikuwa yanamshambulia Wangwe moja kwa moja, kama huko si kuchemsha ni nini?
Ben,
Hivi wewe unajua kusoma kweli? Kwi kwi kwi!!!
Toka lini neno MAKINI likageuka kuwa MASKINI? Uwe unasoma mkuu, hatushindani nani kaandika haraka. Soma kwanza kabla ya kujibu. Mpaka una highlight neno bado unashindwa kulisoma vizuri? Kweli JF kuna kazi.
Sasa mkuu naona kumbe wewe ndiye ungeharibu kabisa,kwa hiyo solution yako ni kuomba uongozi mzima ujiuzulu? je,ambae angechaguliwa teana akiboronga uongozi mzima pia ujiuzulu then uchaguzi mwingine?
Naomba kusema hiyo ingekua solution ya mtu ambae hajaenda shule kwani ukiangalia Wangwe ana shida na watu wengi katika kambi ya Upinzani.soma katika majira la leo,wangwe amemshambulia hadi kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambae ni mbunge wa CUF pamoja na Slaa,sasa hapa nako ungetaka na upinzania kwapamoja ubadili baraza la mawaziri kivuli pamoja na kiongozi wa upinzani bungeni ujiuzulu?
Mkuu,lazima ujifunze kuelewa solution walioifanya chadema ilikua right.Tatizo ni Wangwe maanke yeye tu ndiye mwenye shida na si CHADEMA pekee na hata CUF,NCCR MAGEUZI pia.Hii solution yako ya kuvunja uongozi ni solution ambayo haitendei haki Muda wa uma,fedha za umma na gharama za kisaikolojia kwa uma! sasa wewe ndiye ungeharibu kabisa!
Kama walichofanya CHADEMA ni right basi mwamuzi ni 2010. Suala la Wangwe ni ugomvi wa mwenyekiti na makamu wake. Mnaweza kubisha lakini ndio ukweli wenyewe. Top wawili wakishindana, dawa ni kurudi kwa wananchi. Tena mna uchaguzi december, si mungesubiri na wananchi ndio waamue?
Kwani wakati mnampa Wangwe kuwa makamu mwenyekiti, mlikuwa hamjui kwamba anaropoka? Hata Tarime wanajua anaropoka na bado wamempa kuwa mbunge wao. Sio kila mtu afuate diplomasia kwenye uongozi.
Ukichanganya waropokaji kama akina wangwe na wafuata diplomasia kwenye chama, ndio unapata chama bora. Kinachotakiwa ni balance nzuri.
Solution ya mtu ambaye hajaenda shule sio? Well, inawezekana, maana shule pia zinatofautiana. Wenzetu wa West ndivyo wanavyofanya na pia vitabu vya uongozi ndio vinavyosemwa, labda vimetungwa na watu ambao hawajaenda shule kwi kwi kwi!!!
Thatcher alipokosana na naibu wake, akaomba maoni ya wanachama, akashindwa ikabidi ajiuzulu na kupoteza kuwa PM, hata Major alipokosana na baadhi ya viongozi wake, akaamua kuomba kura kwa wanachama, bahati akashinda na waliokuwa wanampinga ikabidi wanyamaze kimya. Solution ya wasioenda shule inafanya kazi.
Mbowe angeenda kwenye mkutano mkuu au baraza kuu na kuomba kura na kushinda, hapo Wangwe ingebidi anyamaze tu. Lakini kwasasa anasema mawazo yake yanaungwa mkono na wanachama wengi mikoani, kama yuko sahihi kwanini aache kuyasema mawazo kama hayo?
Tena mna uchaguzi december, si mungesubiri na wananchi ndio waamue?
?
Naona hili la Thatcher unachanganya mambo,kipindi hicho alikua PM na hizi ishus ni za dola na umesoma katiba iliyokua inawaonoza kipindi kile? Na umeona katiba ya CHADEMA imekaa vipi kuhusu hili suala? Kwa mantiki yako Baraza kuu basi litakua halina maana katika ishuz kama hizi?
Mkuu naona unachanganya mambo bure,una-apply mambo kutoka katika mazingira tofauti,kwa muda tofauti na kwa reason tofauti na kutoka katika muongozo tofauti kabisa unaenda moja kwa moja ku-apply mahali pengine.
Hivyo vitabu vya uongozi unavyosema ni vipi maanke sasa naona unajifanye kuwa ni wewe pekee uliyepata opportunity ya kuvisoma hivyo vitabu vya uongozi kutoka western coutries.Hapa JF kuna watu wamevisoma hivyo vitabu ila sema uelewa wa watu ni tofauti na application zake ni relevat in a relevant circumstances