Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,230
Ben,
Nimegundua husomi hoja vizuri kabla ya kujibu maana hii sijui ni mara ya ngapi nakukamata kwamba unaongelea kitu ambacho mimi sijaongelea.
Ebu highlight mahali popote ambapo mimi nimeongelea western books. Vingine sema umekosea tena kwa mara ya pili. Ni shida sana kubishana kwa hoja na watu ambao huwa hamtulii na kusoma kilichoandikwa kwanza.Nilichoandika ni kama hapa:
"Wenzetu wa West ndivyo wanavyofanya na pia vitabu vya uongozi ndio vinavyosema, labda vimetungwa na watu ambao hawajaenda shule kwi kwi kwi!!!"
Mimi nimeongelea vitabu vya uongozi na wala sio vitabu vya West. Nimeongelea wenzetu wa West na nikatoa na mfano wa Thartcher lakini kwenye vitabu nimeongelea vitabu vya uongozi. Mbona hiyo paragraph iko clear?
Kwenye vitabu hakuna tofauti kati ya vitabu vya West au Afrika, kinacho matter ni ubora wa hicho kitabu. Kwenye demokrasia kuna tofauti kubwa sana kati ya West na Afrika na ndio maana nikatumia wenzetu wa West. Nikiambiwa nichague, nitachagua demokrasia ya West kuliko hiyo ya Afrika ambayo ni ubabe ubabe.
Tatizo la sisi Waafrika ni kuwa negative na kila kitu cha West. Mtu akisifia kitu cha West tayari nongwa. Hayo ndio mawazo ya akina Mugabe na wengine naona mnafuata mkondo huo huo mpaka unajikuta unaandika kitu ambacho hakipo. Hata nilipoamua kutoa mfano wa Thartcher nilijua nini kitakuja na kweli sikukosea. Kuwa UK hainifanyi nijue mambo ya UK kuliko wengine, ni sawa na mimi kuwa hapa hainifanye nisijue mambo ya Tanzania ipasavyo.
Kiburi kile kile kama cha CCM, mtaendelea kupiga kelele wee huku wao wanatumbua pesa za wananchi. Wanasiasa wetu hamna tofauti, ni kuku yule yule ila kapakwa rangi tofauti.
Kama kelele zetu haziwasumbui, si acha kujibu tu? Tuachie sie wapiga kelele tuendelee na kelele zetu. Vinginevyo kushindana na wapiga kelele si inabidi na wewe upige kelele?
Naona weekend imeisha, nimechangia kwa mara ya mwisho hii thread. Inabidi wengine tukawajibike. kinachoendelea sasa ni kubishana ambako hakumsaidii mtu yeyote.
Ben na Kichwamaji, nawatakieni mafanikio mema katika kuijenga CHADEMA!
DAWA ya hawa wapinga maendeleo ya demokrasia ya vymama vingi na makuwadi wa mfumo fisadi ni kwa vijana wapenda maendeleo ya mfumo wa demokrasia makini kujiunga kwa wingi CHADEMA. Nimekuwa nikisita kujiunga na chama chochote lakini sasa naamini kuna umuhimu wa kupitia upya msimamo wangu kwa hili.
Wacha niingie viwanja vya mtambo mkakati kulifanikisha hili. Wale wapiganaji wenzangu wa enzi zile na sasa tuwasiliane kwa majadiliano muhimu.
Saa ya kulinda na kutetea maendeleo ya Demokrasia ni sasa.....
Tanzanianjema
Mtanzania,
Naomba unitake radhi hapa! Hili kwangu ni tusi na umelirudia tena.
Hakuna mtu aliye-negative kwa kila kitu cha West,hayo ni mawazo yako ya kuona suluhisho la matatizo yetu ni kuiga kila kitu cha west,huku ukishindwa ku-apply kuendana na mazingira.Eti,unang'ang'ania kuhusu masuala ya mashirika makubwa kupelekwa ndani ya bodi huku ukishindwa ku-apply theory hiyo ktk huu mgogoro wa CHADEMA ili kuendana na Muongozo wa chama na mazingira ya mgogoro,Si tutauita utaahira huo?
Maanke kwa mtu mwenye akili timamu atakushangaa,halafu kumbe kukurupuka kwako koote kumbe wewe mwenzetu unabishana? and what is the motive behind? Kumbe ndiyo maana hata hoja nilizokukamata nazo hutaki kuzijibu kwa sababu ubishi ndiyo umekuweka hapa? Hii ni dhambi kubwa sana kwa mtu mzima kama wewe kukaa nyuma ya PC na kubishana bila faida yoyote.
Ben,
Nisahihishe jambo moja maana naona umeng'ang'ania huko. Niliandika board kwa makosa, nilikuwa na maana ya shareholders meeting. Wakubwa kwenye kampuni wakikosana kwa mfano mwenyekiti wa board na CEO wanarudi kwenye general meeting ambako ndiko kampuni inaweza kuamua stratergy ipi ifuate.
CEO anaweza kufukuza au kusimamisha kazi watu aliowachagua na sio wale walioteuliwa moja kwa moja kwa niaba ya shareholdes. Hicho ndicho nilichotaka kuandika na sikuwa na maana ya board of directors.
Mnyika kwenye hiyo mikutano yenu mnaandikisha wanachama wapya au mnahutubia tu?
Mnyika kwenye hiyo mikutano yenu mnaandikisha wanachama wapya au mnahutubia tu?
Kitila hizo ndizo habari zinatakiwa kusikika. Mwenzetu "umesikia" kutoka sources zako... sasa mtu mwingine atasikia kutoka wapi. Hazina zikipatikana hazifichwi.
Mtanzania,
Wewe unapenda sana kuji-contradict,unajua pia wakati mwingine ni vigumu kwa shareholders kukutana kwani unakuta wengine ni shareholders waliotapakaa sehemu mbalimbali duniani.
Ben,
Kwa makampuni mengi shareholders wana mkutano kila mwaka. Pia sio lazima wawepo physically na badala yake unatumikwa kabrasha ambalo lina kila kitu pamoja na kura yako.
Ugomvi wa mwenyekiti na CEO hauwezi kuamuliwa na board na hicho ndio nilikuwa nakuambia. Mkutano mkuu ndio unaamua. Of course hata mashirika yanatofautiana kulingana na corporate governance zipi wanafuata. Ukiwa shirika kama BOT hapo board inaamua kila kitu.
Sikusema naenda kazini na naacha kuchangia JF, nilichosema naacha ni huo mabishano ya Wangwe maana hakuna jipya hapo tena. Nimekubali kutokukubaliana.
Sijatoroka kazini, hata nikiwa kazini naweza kuchangia ila ni bora kuchangia pale palipo na faida na sio kwenye ubishi.
Mtanzania,
Pia,wewe ndiye unabisha mpaka mtu unashanga unagain nini?