The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,006
- 3,281
Sijakuelewa. Halafu zingatia kuwa Chacha hajafukuzwa, AMESIMAMISHWA. Na si kwa hoja zake, ila kwa VIOJA vyake vya kukikuka kanuni, maadili na itifaki.
Hoja zake za ruzuku, ukabila nk mbona tayari zilishafanyiwa kazi na chama tayari kabla hata ya yeye kuwa makamu?
Asha
Unahitaji kupata mahojiano ya Wangwe na TBC Radio..., halafu ukitafuta kwa muda kidogo utaona kuna mada nyingi zaidi humu zilizoupande wa Wangwe. So it is not 2:1 kama unavyojaribu kusuggest..
Kuhusu hoja za Fikra Mbadala nilijaribu kuzichambua hapa moja baada ya nyingine na baadhi ya maswali uliyoyauliza yana majibu yake hapa:
Once again... wangeanza kwa kututafsiria wanaposema "Ukabila" wanamaanisha nini kwa sababu kaw muda wote ambao nimekuwa nikisoma jambo hili wanazungumzia kana kwamba tunakubaliana maana ya ukabila ni nini. Naamini kwa kuwasoma vizuri kwao ukabila si hisia za kabila moja kujitukuza dhidi ya mengine, au kujiona bora na wanastahili zaidi kuliko makabila mengine bali kwao ukabila is simply idadi. It has nothing to do with vitendo vya kabila fulani dhidi ya makabila mengine. :
Huyo aliyeigawa katika makundi hayo ndiye mwenye lengo la kuonesha kugawanyika? Kwanini isiwe CHADEMA - KATIBA na CHADEMA - MALALAMISHI; Kwanini isiwe CHADEMA - UMOJA na CHADEMA - UTENGANO? n.K NI wazi jibu ni kuwa watu na watu ndio wanajitengenezea agenda.
Malalamiko ya wanachama wa Chadema au mwanachama mmoja. Hadi hivi sasa sijasikia mwanachama mwingine wa Chadema aliyetoa tuhuma au madai hayo ukiondoa mtu mmoja. Basi hao wengine wajitokeze na wenyewe angalau wampe nguvu huyo mwanachama mmoja. Hao "wanachama" wako wapi?
Well, it went back to the two! Hakuna makundi as far as one can see; kuna mtu anayejidhania kundi na kuna chama ambacho kina uongozi ambao uko msimamo mmoja. Halafu Wangwe hakuwa Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Kukaimu tu.
Hili ni wazo zuri, lakini unapotakiwa kujibu tuhuma basi utoe ushahidi wa tuhuma hizo kusema namtuhumu fulani hivi halafu uoneshe msingi wa tuhuma hizo ni kejeli. Tunaposema kwa mfano kuna matumizi mabaya ya fedha katika serikali hatusemi hewan, tunachukua ripoti ya Mkaguzi Mkuu na kuiweka hadharani na kusema ripoti hii inasema hivi, namba ni hizi, na authority ya hiyo namba ni hizi. Tuhuma za Wangwe zina msingi huo?
hebu tuziangalie tuhuma hizo na kama zina "msingi"
Vyama vya kisiasa vinatakiwa kutoa ripoti ya matumizi ya fedha za ruzuku kwa Msajili wa vyama vya siasa nchini. Chadema ni mojawapo ya vyama hivyo vya siasa. Katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2007 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ilionesha kuwa kuna zaidi ya Shilingi Bilioni 13 ambazo vyama vya kisiasa havikutokea maelezo jinsi gani walizitumia. Bilioni hizi 13 zinahusisha fedha siyo za Chadema tu bali CCM, CUF, TLP n.k
Kwa hiyo, Chacha ana hoja hapa na yeye angeweza kutumia ripoti ya mkaguzi mkuu kama msingi wake wa kuhoji matumizi ya ruzuku inayoenda kwenye chama chake.
Chacha amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chake na ameushika umakamu. Inaonekana yeye ameona vitu ambavyo watu wengi hawajahi kuviona. Kama yeye ana msingi wa madai basi aseme na kujenga hoja kuwa Chama kilipokea kiasi fulani cha ruzuku, vitabuni imeoneshwa hivi, na matumizi yake yameoneshwa vile na haiingii akilini.
Kama kweli alikuwa ananita ya kutatuta ukweli suala la ruzuku haliendi mbali, angeenda kwa Msajili wa vyama vya siasa, angefungua kesi, n.k ili kuweza kupata taarifa hizo. Akienda kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa na kuuliza kuhusu Chadema kama kinatoa ripoti ya matumizi ya ruzuku kama inavyotakiwa na kama angeweza kuona ripoti hiyo. Hiyo ndiyo njia rahisi ya kuonesha jinsi ruzuku inavyotumika. Yawezekana Wangwe hajui ilipo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa na majukumu yake?
Mwanzoni ilikuwa ni "Mbowe" sasa wameamua kuongeza na "Dr. Slaa" na muda si mrefu watamuongeza na "Zitto" na wakiona haviendi wataongeza "Kamati Kuu nzima" n.k Swali ambalo Wangwe angelijibu kwanza kabla ya kuendelea na kauli yake ni lini, wapi, na kwa amri gani ambayo Dr. Slaa na Mbowe walifanya "kitendo" cha kuzuia ruzuku isifike mikoani. Hapa kwa kumsaidia anaweza akatoa barua, email, mazungumzo, kikao, au ushahidi wowote kuwa kuna agizo au uamuzi kama huo uliochukuliwa na watu hao wawili bila kumhusisha yeye kama Kaimu Makamu Mwenyekiti.
Sasa hili la kufungua matawi ya chama halihusiani na fedha moja kwa moja, kwani matawi mangapi ya vyama vingine yanayofunguliwa na fedha toka makao makuu? Ni hoja ya kilaghai kutaka kufanya watu waamini kuwa bila fedha toka Makao Makuu matawi hayafunguliwi. Kosa kubwa la Chadema hadi hivi ni kuwa wameshindwa kuwatia moyo mashabiki wao mikoani na wilani kujianzishia matawi yao wao wenyewe. Matawi yanayoanzishwa kwa misingi ya kupewa fedha mikoani yatakufa fedha hizo zikikoma!
Nadharia hii ya Wangwe siyo tu haina msingi lakini is impractical. Matawi yanaanzishwa na mashabiki, na kwa kadiri yanavyoongezeka hadi pale yanapofikia ngazi fulani ndivyo pesa ya kuendeshea inapoanza kutolewa. Hata CCM na mabilioni yake ya fedha haitoi ruzuku kwenye matawi yake, vinginevyo wangefilisika!
Zaidi ya yote hili wazo kuwa matazi yanaanzishwa kutoka juu halina msingi, matawi ya vyama huanza kuanzia kweny shina ambako wananchi wenyewe wanaamua kuanzisha tawi la chama chao. kwa wale wanakumbuka watakumbuka jinsi gani vyama vya NCCR na CCM vilivyokuwa vinashindana kufungua matawi na hata kule Zanzibar mashindano ya CUF na CCM. NI mara ngapi fedha toka makao makuu zimetumika kufungua matawi vijijini au mitaani? Kwanini Chadema itakiwe kutumia fedha kidogo ya ruzuku kufungua matawi vijijini?
Hoja ya Wangwe ingekuwa ya msingi kama angesema uongozi wa makao makuu haujahamisha wanachama kufungua matawi sehemu mbalimbali nchini na hivyo kukosa wanachama wengi zaidi na mapato yanayotokana na mauzo ya kadi na michango ya wanachama. That is a more valid argument than saying Makao Makuu haijatuma fedha za kuanzisha matawi! this is ab absurdo
Hii nayo ni hoja dhaifu. Kama Kamati Kuu au ile ya uchaguzi (whatever final authority is ) waliacha Mbowe atumie helikopta kufanya kampeni hilo ni kosa lao wao wenyewe. Wangwe mwenyewe ni sehemu ya Kamati hiyo. Njia pekee ya kumbebesha lawama Mbowe ni kuonesha kuwa viongozi wengine wote walikataa na walipiga kura ya kukataa lakini Mbowe AKAWALAZIMISHA aidha kwa ahadi au vitisho. Na kama waliogopa kumsimamia (akiwemo Wangwe) basi Mbowe ana ubavu mkubwa sana na hao wengine hawana ubavu wa kumpinga. Hilo linasema zaidi kuhusu wao kuliko yeye.
Hata hivyo, kama maamuzi yalichukuliwa kwa pamoja na uamuzi wa kutumia helikopta ulipitishwa kwa pamoja basi hapa ndio collective responsibility inapokuja. Hivyo Mbowe, Wangwe, Zitto, Slaa na wengine waliopitisha uamuzi huo wanawajibika moja kwa moja kwa kuwaacha "wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama." Ina maana kile anachomtuhumu Mbowe, na yeye anahusika.
kama wote walihusika na mchakato wa kuruhusu hiyo chopa, the answer is simple uongozi mzima wa Chadema akiwemo Chacha Wangwe.
There it is! "Mbowe ni Mchagga wa Kilimanjaro"! Sitaki kujua wachagga wengine wanatoka wapi. Hili la Wabunge wote "kutoka mkoa wa Kilimanjaro" limeshajibiwa mara nyingi sana kiasi kwamba hata sitojaribu kuelezea. Tukumbuke tu kuwa kwa Wangwe madai ya ukabila kwake ni idadi. Period. Kuna Ukabila pale penye idadi ya watu wengi wa kabila moja mahali fulani. Ukifiria sana msimamo huu utashangaa ni sehemu ngapi tanzania kuna ukabila!
Mbowe ndiye aliyefanya maamuzi haya? Au ndiye mwenye kubebeshwa lawama hizo. Kwanini asiseme chombo au watu waliotoa uamuzi huu ili tuweze kuona msingi wake. Maana huyu Mbowe inawezekana ana nguvu kubwa sana kiasi watu kama kina Mbowe wanashindwa kumhoji humo humo ndani.
Hili ni suala la ajira, lakini well bado tatizo ni "Wachagga wa Kilimanjaro" na kama mtu haoni sumu ya ukabila na chuki dhidi ya Wachagga wa "kilimanjaro" sijui iwekwe vipi ili ionekane.
lakini kama nilivyosema hapo juu kuwa kwa Wangwe Ukabilla ni idadi anaonesha namba. Basi si wangetoa na majina ya hao wakurugenzi ili tuweze kuamua kuona ukweli (validit) wa hoja yake? Hao wakurugenzi ni kina nani na je ni kweli ni Wachagga, na kweli wanatoka "Kilimanjaro"?
Once again tatizo siyo ajira ya watanzania bali walioajiriwa ni "wachagga" wa kutoka Kilimanjaro. Hata hivyo hili ni rahisi kwani tunayo majina ya madereva wa makao makuu.
1.Juma waziri- kutoka nachingwea.
2.Pella Ngunagwa-huyu sijui katoka wapi ila ni kusini.
3.Waziri Simba -Mkwere bagamoyo.
4.Baraka Daud -Tanga.
5.Olvary Karia -mchagga.kibosho
6.Kalikisha -Kigoma.
Sasa njia pekee ya dai hili kuwa na nguvu ni kwa Wangwe kutoa majina yake ya madereva wa makao makuu na kuonesha kuwa ni "Wachagga wa Kilimanjaro". Haitoshi tu kusema bali angalau aoneshe chembe ya ushahidi wa madai kama haya kuwa "Madereva wote".
Hili ni swali zuri lakini lina ufundi. Je kuna wanachama ambao waliamua kukikopesha fedha chama fedha ambazo wanatarajia kulipwa? Kama wapo wanachama hao na ni kweli waliingia makubaliano na chama, wakatia sahihi na masharti yapo na wakatoa fedha hizo, swali kwanini wasilipwe? Jambo pekee ambalo Wangwe anaweza kulionesha ni kusema kuwa hakuna makubaliano yoyote ya kukikopesha chama na hivyo malipo wanayojilipa hayana msingi wa kisheria.
In that case kinachofanyika ni wizi na Wangwe ana haki ya kwenda mahakamani siyo kulalamika. Kwa mpambanaji kama yeye anajua wapi pa kukimbilia.
Kuhusu wanachama wengine, swali ni hilo hilo je na wao waliingia mkataba wa kukikopesha chama na hadi sasa hawalipwi? Ni kina nani hao na waliingia mkataba huo lini na kwa makubaliano gani?
kwa mara nyingine tena, anampa nguvu kubwa sana Mbowe. Wanachama wa Chadema Dar wako wapi kutoa malalamiko haya? Kama kuna mtu anataka kuanzisha tawi dar kwanini wasianzishe? Je ni kweli Mbowe ndiye aliyevunja tawi hilo? Hapa tunahitaji habari zaidi maana mtu mwenye nguvu ya kuvunja tawi zima na viongozi wenzie kama kina Wangwe wakawa wanamuangalia basi wamempa nguvu za kidikteta; aidha wanahitaji kubadili Katiba au kumuondoa madarakani!
Hapa inabidi atuoneshe angalau hiyo Katiba inasema nini kuhusu Wakurugenzi wa Chama. Kwa kuisoma kwangu kwa haraka inasema kuwa Kamati Kuu itakuwa ina jukumu la kuwateua "Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu"
Sasa kama kweli Mbowe ndiye aliyewateua wakurungezi hao (note a fine difference from what the constitution says and what Wangwe alleges) basi tatizo bado liko kwenye uongozi mzima wa Chadema kwa kumuacha Mbowe avunje Katiba na badala ya kumshtaki au kujenga hoja ya kuondolewa madarakani kwa kuvunja Katiba mtu anaamua kulalamika pembeni. Kumbuka hapo juu tayari ameshadai kuwa wakurunzi wanne ni "Wachagga wa Kilimanjaro".
Nimeangalia kwenye Katiba iliyoko kwenye tovuti yao na sijaona kipengele hicho ambacho kinasema Katibu Mkuu anatakiwa kuwajibikwa kwa Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti. Kipengele hicho kinasema hivi:
yawezekana Katiba iliongezwa kipengele kidogo cha (iii). Mwenye nacho naomba akiweke na kusema kinasemaje.
very vague.. taja majina au nafasi yoyote au viongozi ambao hawakufika kwa sababu walifichwa habari hizo. Kwa mujibu wa kanuni za Chadema, sasa basi angalau taja hizo kanuni ziko wapi. Kwa mujibu wa hiyo Katiba mahali pekee ambapo suala la siku 21 lipo ni hapa:
Hadi leo sijasikia matawi yaliyojitokeza kumuunga mkono Wangwe, maana hata tawi la kwake Tarime wameanza kumgeuka. Natoa wito kwa matawi yanayomuunga Wangwe kujitokeza na kumuunga mkono hadharani. Lakini hili swali la "kutenda haki na kusimamia ukweli" tungewauliza wachagga ambao wanajikuta wanatakiwa kufanya kazi na Wangwe kama wanajisikia kutendewa haki na kufanyiwa mambo kwa ukweli. Sitoshangaa kama Wangwe anaweza kumkataa dereva Mchagga akipatiwa!
Katika
hili ni wazi kuwa ni suala binafsi sana kati ya Wangwe na Mbowe at least kwa upande wa Wangwe. Ushauri wangu ni kuwa nyinyi watu wawili tu muitane Ngurdoto yenu na mkae mzungumze, no TV no radio, no newspaper na mkimaliza mje na msimamo wenu, mambo ya kukubaliana mkubaliane ya kupingana mpingane, lakini inaonekana kuna mambo mawili yanayowahusu ninyi watu wawili. It is more personal than professional.
WoW shujaa amesimama na kujitangaza kuwa kazi anaifanya peke yake! Well, wakati mwingine mtoto anaweza kuingia chumbani na akaanza kupigana na jinamizi la chini ya uvungu, jinamizi ambalo ni yeye pekee analiona!
Kama Wangwe ana ripoti hiyo, basi aitoe, kama Mziray (yeye siyo mtu wa Kilimanjaro?) na yeye aitoe ili kijulikane kilichomo.
1. Ushahidi wa Rostam Aziz na Kaborou kuhusika: si lazima hapa utolewe hapa Jambo Forum, Kubwa Jinga umezidi kuwa kuwadi wa watu hawa! Michango yako humu inakuanika ulivyo. Dr Slaa na wenzako, msianike ushahidi wowote hapa. Huyu jamaa anataka kujua mikakati yenu awapekelekee Rostam na Balille. Ushahidi endeleeni kuutoa kwenye vikao vyenu vya chama. Na kama wao wanataka kuuona si waende mahakamani kwa kuchafulia majina yao ushahidi utatolewa huko? Rostam, Kaborou na Chacha- nendeni mahakamani kwa kusingiziwa!
2. Ripoti ya Mziray imeshawekwa wazi kwenye gazeti la Fisadi Rostam la Rai vipande kwa vipande toka wiki iliyopita. Na imechapwa kwa ukamilifu wake kwenye gazeti dada la mafisadi la Majira. Wewe hujaisoma? Kama bado wasiliana na rafiki yako Bwana Balille akupe nakala? Dr Slaa hawezi kuitoa hapa ripoti ambayo imekataliwa na kamati ya Chama as no document, atakuwa ameihalalisha kuwa ni nyaraka ya chama. Weka wewe
3. Mbowe hawezi kufanya mahojiano na MMJJ kujibu tuhuma zisizokuwepo. Tundu Lissu ameshaeleza bayana kwanini Wangwe amesimamishwa. Kama una tuhuma mpya zaidi ya zile ambazo Dr Slaa, Tundu Lissu, Zitto nk wameshazitolea ufafanuzi hapa ziweke. Kama huna, nyamaza!
5. Mziray amechukuliwa hatua kwa ripoti yake kukataliwa na wajumbe wamemkaripia. Tatizo la Chacha ni tofauti na la Mziray, yeye amepotosha taarifa ndani ya vikao vya chama. Chacha amepeleka siri za chama kwa kaborou na rostam, amekosa uwajibikaji wa pamoja, amekiuka maamuzi ya chama, amechochea makundi, ameleta matusi na ugomvi vikaoni, amepingana na maamuzi halali ya chama nk na hivyo Kamati Kuu ya Chama kukosa imani naye kama makamu mwenyekiti. Haya ni Makosa tofauti kabisa na adhabu ni tofauti kabisa! Sasa kumchukulia hatua mkosaji sio kuanzisha mgogoro, kuendelea kulea makosa ni kuweka msingi wa migogoro mibaya zaidi kwa taasisi. CCM imezoea kulindana ndio maana CHADEMA kuchukua hatua imeonekana ni mgogoro.
Kwa maelezo ya Wangwe ni kuwa, Dr.Slaa ni mmoja kati ya wanaolipwa pesa walizotumia kwenye kampeni zao za uchaguzi, kitu anachopinga Wangwe. Je hii inaweza kuwa ndio sababu? Who knows.
Kubwajinga huo ni uongo Dr.Slaa hakidai chama na wala hajawhi kulipwa hata senti tano kama deni analokidai chama .
Ni kweli Wangwe yupo peke yake, maana kwa sababu zisizoeleweka, akina Dr.Slaa, Zitto n.k., wote wako upande wa Mbowe hata pale outsiders wanapoona ualakini kama Wangwe alivyoelezea.
Wangwe ana point nzuri nyingi kwenye maelezo yake na ni vema zikafanyiwa kazi kuliko nyote mkajirundika nyuma ya Mbowe mkifikiria anayosema Wangwe yatapita tu kirahisiKwani wewe ni mtabiri ama mganga kuwa hayatapita ya Wangwe?
Kubwajinga umetumwa ila huna facts,wewe fanya utafiti kama uko upande wa Wangwe na sio kuja hapa bila kuwa na hoja za msingi.
Nataka kuamini kuwa wewe umetumwa tangu sakata hili ila huna hoja jibu hoja sio kutaka kusema huku huna facts.
By the way Wangwe leo yupo bungeni na ameamua kwenda kuwatetea wananchi wake huko.
Wewe unala kwako ama ni fulani wewe?
Huo ushahidi wa majina ni mzuri, ingawa hatufahamu ni waajiriwa tokea lini, kwa hiyo tungependa kusikia upande wa Wangwe maana naamini kuwa hakuwa kichaa alipotoa hizo shutuma.
Unataka majibu gani kama majina uliyopewa ni ya uongo si ulete majina ya madereva kama hukubaliani nayo.
Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
Kubwa Jinga kwa taarifa yako hakuna makundi ndani ya CHADEMA kwani wanachama na viongozi wa CHADEMA wanaijua katiba yao ila wewe hujui hata katiba yao ndio maana .
Tangu sakata hili umeanzisha post mpya zaidfi ya kumi juu ya jambo hili huku ukijifanya kuwa huna upande huu ni unafiki .
Watu hapa wanajua kusoma maandishi na kuyatafakari.
Huu ni ukuwadi .
Wewe kubwa JINGA ndio usikitike na 'mgogoro' wa CHADEMA! Wewe kubwa JINGA ambaye toka uingie hapa JF wakati wote kazi yako ni kuiponda CHADEMA, wewe au mwingine.
Naipenda staili yako ya kubomoa, ya kung'ata kama hung'ati. Kujifanya unajali kumbe hujali. Huu mkakati wa kinafiki, ni staili hiyo hiyo inatumiwa na mwenzako KUHANI mkuu! Waumini wa hoja alizoleta FIKRA MBADALA, kumbe LOL!.
Asha
NYOANENI NA WENGINE WAJITIE MAJI........! " raskazone hiyooo...!
what I See Now Is To Help Chadema Kutambua Kuwa Muelekeo Wanaoufata Si Wenyewe....!inasikitisha Sana Kuona Watu Wanapigania Vitu Wasivyoweza Kuvitekeleza Wao Wenyewe.
Demokrasia Ni Tamu Unapoililia Lakini Saa Nyingine Ngumu Kui-practice Unapokuwa Madarakani. Ngoja Tuone Chama Cha Demokrasia Kinavyoleta Demokrasia Ndani Yake Kabla Ya Kupewa Nchi.