Inasikitisha sana kuona watu wanapigania vitu wasivyoweza kuvitekeleza wao wenyewe.
Demokrasia ni tamu unapoililia lakini saa nyingine ngumu kui-practice unapokuwa madarakani. Ngoja tuone Chama Cha Demokrasia kinavyoleta Demokrasia ndani yake kabla ya kupewa nchi.
what I See Now Is To Help Chadema Kutambua Kuwa Muelekeo Wanaoufata Si Wenyewe....!
Waombe Sapoti Nje Ya Chama Chao Ktk Chama Wanachodhani Ina Malengo Yanayofanana Nacho....!
Nimesema Hivi Kwani Walio Nje Huona Zaidi Kuliko Wanaocheza....!
tz Kwanza, Ushabiki Baadaye...!
Hakuana cha demokrasia kwa vyama vyetu wote njaa tu na kutaka madaraka kwa malengo yao na si ya wananchi.
Tanzania ili iendelee inahitaji kiongozi Dikteta mwenye Determinations Maana tatizo la Tz kua masikini si tatizo la kifedha wala malighafi.
Maana sasa kila mmoja anatetea anapoguswa na si kutetea wananchi.Mfano hawa polisi Mchezo mchafu wa upekuzi ndio kawaida yao ,yani kule vijijini waliko wananchi akitofautiana na polisi ,polisi anakuja usiku kwako anaficha kadumu kagongo ama bangi anaichomeka kwenye kwenye nyumba yako ya nyasi.Harafu anakuja usubuhi na gobore anajidai kukusachi na anaelekea palepale alipoiweka na kukutia nguvuni ,huu ni mchezo wao wa miaka.Wanasiasa wademokrasia wanatetea mahala ambapo tu maslahi yao yanaguswa.Kazi kweli kweli.
Moderator,
Ningeomba uiache hii thread i-run yenyewe bila kuiunganisha kwa muda, maana kichwa chake cha habari kina uvuto tofauti na ulikoiunganishia. Naona umeiharahisha sana. Thanks.
Wewe kubwa kwani mgeni humu??
Thread yeyote inayogusa chadema inaunganishwa ama kupelekwa kolokoloni mapema sana .
Lakini inayohusu CCM zipo nyingi tu wala haziunganishwi,zinazohusu Mkapa zipo nyingi tu,zinazohusu JK zipo nyingi tu.
Hapo kwa kweli inabidi nihoji Demokrasia ya JF? imekaa vipi? Ama wewe unasema je?
Mkamap,
Kwa kweli hata mimi nimeshangaa kwa spidi iliyotumika kuiunganisha hii thread. Mara tu baada ya kupata wasomaji na wachangiaji wawili ikachomolewa, wakati ina tofauti kubwa sana na ilikotupwa. Ngoja tumsikie Moderator atafanya nini. Yetu macho.
ukitaka kuanzisha thread kuhusu chadema nakushauri iiweke mchana watu wengi wkiona hua wanasita kidogo kuichomeka mahala fulani.japo hua wanavuta pumzi pumzi .Labda hua wanaona iabu watu watalalamika
Ukiianzisha usiku hua haichukui hata dakika mbili maana wanaiwahi ili isipate wachangiaji .
Kama huo ndio ustaarabu, basi wasijifanye wanapigania Demokrasia kama wao wenyewe hawaiwezi.
as usual wakandiaji hamchelewi... kama mnaona JF ni ya kidikteta kwanini msiamie kwingine tu? zimeunganishwa mada nyingi tu hapa na watu hawajalalmika lakini ikiunganishwa inayohusu Chadema ndio watu wanalalamika.
Sidhani kama kuna mtu anaweza kuwabembeleza kwa kila jambo dogo; mada zinaunganishwa na sisi wengine hatulalamiki wala kuuliza. Kama unaona mada inahusiana na mada nyingine nenda uanzishe huko. Lakini tusidhani mlundiko wa mada ile ile kwa kuirudia rudia kunasaidia zaidi kunapoteza mtiririko wa mawazo.
Of course, mida inapopita kuna bada zinazohitaji threads mpya. Tuwaache ma MoD wafanye kazi yao siyo kuikandia JF halafu kuendelea kuwapo hapa. Haya mambo ya kukandia JF kwa vitu vidogo huwa yanakera na kuudhi. Mnaona haiwapendezi, katika uwanja wa demokrasia unaanzisha forum nyingine, na mambo yote ni ushindani tu, ukianzisha na watu wakafuata na kuwa mbadala wa JF ni bora.
Mkamap, basi hamna neno wewe endelea kulia lia, hata kwenye demokrasia kuna taratibu, demokrasia siyo vurugu! Demokrasia siyo kuachia kila kitu, demokrasia siyo kupigiana kelele bila kusikilizana, demokrasia siyo kila mtu kuingia kwenye nyumba ya mtu mwingine ya ibada na kuanza kuhubiri. Demokrasia ina mipaka, inataratibu, na yes, demokrasia ina miongozo yake.
Kama unafikiri demokrasia ni kuachilia kila kitu, wakati wote, na kwa watu wote, inabidi ujifunze tena juu ya demokrasia ni nini.
Ndio maana ni ngumu kupatikana kwa watu wanaovaa ngozi wa kuihubiri yumkini wao ndio wabomoaji wakububwa na kimatendo wanayopingana na dhana nzima.
Ngoja nikuulize swali hivi unafikiri kwanini sehemu za mjini na zawasomi karibu mara zote hu wanaimba CCM kidumu??
kwa sababu kisipodumu, na wao hawatodumu!
Kumbe unakubali kua CCM ni chama cha wasomi Tz na kikifa taifa halitakua na wasomi tena maana hakuna msomi atayedumu.
as usual wakandiaji hamchelewi... kama mnaona JF ni ya kidikteta kwanini msiamie kwingine tu? zimeunganishwa mada nyingi tu hapa na watu hawajalalmika lakini ikiunganishwa inayohusu Chadema ndio watu wanalalamika.
mbona hilo siyo suala la mimi kukubali, wasomi ni wengi CCM ndio maana tumefika hapa tulipofika. Kwa hiyo ndiyo nakubali kuwa wasomi wa CCM ndio wametufikisha hapa.