Wanabodi,
Siku zote Chadema wanaendesha siasa kwa dhana potofu, wanadhani adui yao mkuu anaowafanya kushindwa kwenda Ikulu ni CCM, kiukweli adui mkuu wa Chadema sio CCM, nitawatajia adui mkuu wa Chadema, na mwisho nitawapa ushauri Chadema wafanye nini, waweze kuingia Ikulu 2025 wakati Magufuli atakapomaliza muda wake, tena only if, kama rais Magufuli atamaliza kweli hiyo 2025!, kwa sababu kwa uchaguzi wa 2020, kwa saa hizi tayari ni too little too late, rais Magufuli amefanya makubwa, anakubalika sana na Watanzania, na pia he is just too powerful to be defeated , kiasi kwamba kwa uchaguzi wa 2020 kwa upande wa urais, ni kama hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 kwa mawazo yangu nauhesabu utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, unless Tundu Lissu arejee kugombea urais, na hata akirejea na kugombea, ataongeza tuu hamasa ya uchaguzi na ataleta tuu changamoto kwa Magufuli, lakini Lissu hawezi kushinda urais wa Tanzania, kwasababu has nothing to show. Mshindi wa urais 2020, tayari ameishajulikana ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli wa CCM, hivyo wote watakaompinga rais Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema watake wasitake, ni lazima wabadilike, vinginevyo, 2020 its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya chama kimoja!.
Paskali