CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Nani kawarubuni kwa vitisho unaweza kuthobitisha hoja yako hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi cha kiku wanasiasa walitamba kilamtu akajidai mtaalam was kutukana nk. Sasa zile siasa za janjajanja hamna hivyo mambo yamekuwa magumu sana
 
Nani amutafute mbowe hiv mbowe ndio chadema wewe kilaza nini

Sent using Jamii Forums mobile app
Jifunze kuandika kwa ufasaha kwanza!Amutafute ndio lugha gani?
Nirejee kwenye hoja,hujuma dhidi ya Mbowe tumeziona!Mara mashamba yake yafyekwe,mara biashara zake zitaifishwe,ukigeuka huku kesi kibao mahakamani zisizo na mashiko lakini amesimama imara!Wenye mioyo miepesi kama Sumaye hawawezi kudumu CDM!Kwa jinsi CCM inavyomuandama ndio nazidi kuamini ni mtu sahihi!
 
Sijaona matusi yakikumiminikia huwenda wamekuelewa na kuukubali ushauri wako

Nami niongezee ushauri kidogo kwa hawa ndugu zetu ambao kiuhakika wana kila sababu ya kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani

1. Wawe na mchanganyiko wa viongozi wakuu wa chama kikanda na kidini. Kama mwenyekiti katoka kanda ya kaskazini, katibu atoke kanda ya kusini, mhasibu atoke kanda ya ziwa nk. Lakini pia katibu akiwa mwislam mwekiti awe mkristo. Hii itasaidia kuwaondelea dhana ya kwamba cdm ni ya kanda ya kaskazini na pia ni ya wakristo. Ukweli ni kwamba ukabila na udini bado upo nchini kwetu.

2. Wanachama wa cdm wawe na lugha ya staha. Waache matusi ya hovyo. Kwani kwa tabia yao ya matusi baadhi ya watanzania wanaitafsili kuwa ni chama cha kihuni/wahuni.

3. Wasiwe na siasa za matukio wajikite katika ilani yao. Kuwa na siasa za matukio wanatafasiliwa kuwa hawana iliani bali wanavizia matukio ndiyo inakuwa ilani yao. Mfano ni huu ugonjwa wa coronna wanapiga kelele kuwa wanafunzi wanaosoma nchini China tena jimbo lenye mlipuko wa ugonjwa huo warudishwe nchini. Kisa serikali imesema wasirudi. Hii sijui wanafikilia nini wenzetu hawa.

4. Wawe na kumbukumbu na kusimamia walichokisema. Siyo waseme kitu na serikali ifanye kama walivyosema baadae wageuke kuwa serikali inakosea. Mfano wao miaka yote kabla JPM hajaingia madarakani wamekuwa wakilaumu nchi kutokuwa na usafiri wa ndege zake, Rais kusafiri sana nje ya nchi nk. Serikali au Rais akatekeleza maoni yao hayo. Ingekuwa ni busara kusema kuwa rais ametekeleza ilani au maoni yao. Na siyo kutufanya kana kwamba Watanzania wote hatuna kumbukumbu kwa kuilaumu serikali kwa kutekeleza maombi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafakari viziri usikariri Mbowe ulitaka asarende vipi wakati yeye ndiye Mwenye Chama.
Ruzuku yote anaitumia kwa faida yake sasa ataachia vipi chama?

Anatumia ofisi za umma kama Waziri Mkuu kivuli na heshma kubwa sana Bungeni ataacha vipi chama hicho kinachompa nafasi ya kuwapa hawara wake Ubunge?

Tulidanganywa kuwa Zito ni Msaliti kumbe ni mtu aliyekua na akili kubwa ikawa inashindwa kuelewana na akili ndogo .Leo hii ACT kinaelekea kuwa Chama kikuu cha upinzani 2020. Huku CUF kikifuata na Chadema kushika nafasi ya tatu kwenye upinzani.

Hata Sumaye angepewa Chama asingerudi CCM mana yeye ndiye angekuwa Mkuu wa Chama sasa angekiuza vipi?

Mrema ,Lipumba, Cheyo na Mbowe wametumiwa na CCM kuuza vyama kwa kung'ang"ania uenyekiti hali iliyosababisha vyama hivyo kikimbiwa na kila mtu mwenye ndoto za uongozi na kubakia na bendera fuata upepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila tuna CHAMA CHA UKWELI CCM.ambacho kinanyanyasa upinzani na kuwaonea na kuwaibia kura zao wakiwatumia ccm na NEC
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahamiaji ni sawa na magugu toka lini mmea ukaathirika kuondokewa na magugu jiulize mbona Zanzibar hakuna hamahama ukijua utaelewa
 
Kwahiyo Mbowe anatumiwa na CCM?Yaani unaandika porojo tu!
 
hivii kwa uelewa wako unashindwa kujiuliza why MEKO na timu yake wanahangaika kuchomoa watumishi wa CHADEMA na kuwapa uongozi ndani ya serikali na kuwwacha nyie wafia chama mkiendelea kufukuzia posho ya BUKS 7 na kwanini wasiokkoteze CUF NCCR au kile chama cha ZAMBARAU?
hapo ndo ujue kuwa CHADEMA ni namba nyingine kabisa ni mtambo mzito.
 
Vibaraka wa ccm ndo wanahama
 
Mkuu Mag3, hili la kuamini adui mkubwa wa taifa hili ni CCM, it is a school of thought, na huu ndio mtazamo wa Chadema, mimi naamini otherwise na mawazo yangu niliyatoa kwenye bandiko hili,
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... - JamiiForums

Pia kwenye bandiko hili, nimelisema tena na kuweka a way forward ya kutosha.
Karibu
P
 
Kwa sababu tarehe 28 October, Watanzania tunakwenda kufanya uamuzi, sasa muda huu kabla ya uchaguzi, najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu uchaguzi huu, na baada ya matokeo, nitarejea na kupima kilichotokea na nilichokiona kabla.
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tujitokeze kwa vingi kupiga kura na kuchagua chama, viongozi tunaowataka ambao watatuletea maendeleo ya kweli. Kwa wanaotaka maendeleo ya kweli, watachagua chama na maendeleo ya kweli, lakini kwa wanaotaka porojo tuu, rukhsa kuchagua porojo ni haki yako ya kidrmokrasia kuchagua chama chochote, kiongozi yoyote.
Paskali.
 
Baadhi ya wana jf ni watu wa ajabu sana, eti wanashangazwa na matokeo ya uchaguzi huu na wamekuwa surprised as if they didn't know hiki kingetokea.
Angalia tarehe ya bandiko hili, uone tulisema nini kuhusu uchaguzi huu wa 2020, hivyo kwa matokeo haya, kinachowashangaza watu ni kipi?.
P
 
Kaka umeongea kweli japo ukweli mchungu ila manazi wa CHADEMA , ukikosoa kidogo tu matusi .... Wanashindwa kujihoji wapi wanapwaya na wapi wanakosea kuna vituo huko vijijini wanaambulia kura 1 ,mbunge na raisi ukamanda wao uko wapi? Wajitafakari na kuemdesha siasa za kistarabu sio harakati

sent from HUAWEI
 
Kweli Paskali umeiva. BROTHER Magu anakusoma
 
Naendelea kusisitiza, adui mkubwa wa Chadema sio CCM.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…