CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Mawazo mazuri na ushauri murua kabisa ila Pascal siasa za rd ni ngumu. Kikubwa kinachotakiwa kwa opposition ni kugombania tume huru ya uchaguzi yaani waache vitu vyote. Halafu wapambane kupata tume huru hata kama uchaguzi hautafanyika lkn wapaze sauti zao wakiwaelemisha wananchi mpaka kieleweke kwenye tume huru.

Bila tume huru hakuna oppsition na kwa utawala huu. Wengi watapokonywa majimbo yao hata kama watashinda. Lingine Pascal watanzania pia wanapenda maisha ya starehe na rahisi, wanapenda maisha ya juu bila kuifanyia kazi. Uoga wa watanzania pia inachangia sana oppsition kutokuwa na nguvu. Kuna vitu vya msingi ambayo wamenyimwa lkn wako kimya tu. Lazima udai haki yako kwa nguvu hata kwa kupoteza uhai.

Wananchi wangekuwa waelewa mengi yangefanyika hata Magufuli mwenyewe asingeweza kuyazuia. Bila demokrasia ya kweli hakuna maendeleo Paskali. Tunaumia sana ce tunaoona wenzetu wanavyoishi. Inaniuma sana, Pascal ukisafiri au ukiishi nje ya Tanzania ukaishi ktk nchi hizi kubwa zilizoendelea sio rahisi kuishabikia ccm. Mie siwezi kuishabikia ccm kwa sababu kuna mambo mengi ambayo wanafanya bila kujali haki za binadamu.

Na marais wetu na viongozi wetu bado hawajajua thamani ya mtu. Wanaona binadamu wote ni wanyama. Wangejua thamani ya binamu, kwass Tanzania ingekuwa mbali. Hivi mazingira ya vyama vya opposition unavyoiona ipo sawa hebu tizama wanavyoonewa. Wanajitahidi sana, wanao huwezo wa kukaa kimya bungeni lkn wanapigana bila kuogopa.

Ni safari ndefu ndugu yangu. Mwisho watanzania walinyimwa elimu na ccm na viongozi wa serikali na ccm bado wanajua na wataendelea kutaka watanzania wazidi kuwa mambumbumbu, ili waendelee kuwatawala. Ila ipo siku watatoka tu hata Magufuli ipo siku atatoka. Kwanini Magufuli hataki kuwajengea watanzania uongozi thabiti ambayo itawasaidia hata akiondoka madarakani??? Anaogopa nini
 
Hoja zetu kuhusu CHADEMA ni kuukumbusha uongozi kuwa tunatarajia ushindani hai kisiasa na siyo ushindani wa matukio.
 
to be hone
to be honest kuondoka kwa slaa chadema wamedrop hilo liko wazi hata mwenyekiti analijua ila sema tu tatizo watanzania tunajivunia kauli mbiu ya maskini jeuri.
 
 

Ushauri wako rejected, null and void.
strategy ya CHADEMA ni eti kwanza waiuwe CCM from within.
 
Mayala makala zako inabidi mtu usome ukiwa umetulia ni ndefu mnooo.. Mimi heading imenitosha
 

Kung'oana katika vyama si suluhu ya matatizo. Chama kinapaswa kisimame katika misingi yake tu. Lowassa as Lowassa has nothing to do katika kuharibu chama, ni Mtanzania na anayo haki ya kuwa mwanachama kama nilivyo na haki mimi na wewe.
Endapo kama ujio wa Lowassa ungebadili msingi wa chama hapo tungesema hafai ila kwa sasa he is just a member hana impact yoyote katika kuharibu na jambo jema ni kwamba anashiriki katika harakati za kukijenga chama. Anaweza kuwa alikosea akiwa CCM ila hata kanisani wakosaji hutubu! Kilichomsibu kule ni mfumo, hana kosa alotenda yeye personally but mfumo ndo ulimwingiza katika makosa anayotuhumiwa nayo!
 
Tutajie listi ya viongozi wa juu wa chadema na sehemu wanazotoka

-Mwenyekiti Taifa-Freema Mbowe ni Mchaga na Mkristo
-Makamu Menyekiti ni Bara-Prof Safari Mwislam
-Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Mohammed, Mwislam na Mzanzibar
-Katibu Mkuu ni Vicent Mashinji-Msukuma, Mwanza na Mkristo
-Naibu wa Katibu Bara John Mnyika, Mkristo
-Naibu Katibu Visiwani ni Salum Mwalim, Mwislam na Mzanzibar
Kwa mifano hiyo michache pima mwenyewe huo udini na ukanda upo wapi. Mjomba hizo propaganda waliziweka CCM zimepitwa wakati.
 
Siku nyingi sana sijasoma comment zenye akili kama hii yako.
 
to be hone

to be honest kuondoka kwa slaa chadema wamedrop hilo liko wazi hata mwenyekiti analijua ila sema tu tatizo watanzania tunajivunia kauli mbiu ya maskini jeuri.
sijajua bado unafikiria kwa kutumia ubongoo au makalio...
ukisema kuondoka kwa SLAA CDM imeyumba sijui kwa myumbo upi.. sasa kukimbia kwa Le PROFESELIPUMBA wa CUF utasemaje??? angalia vizuri njia unayotumia kufikiria
 
Ahsante kwa hoja chokonozi. nianzie na hilo la ukomo wa uongozi. sidhani kwamba linaweza kutusaidia sana kwa hivi sasa. chama imara ni sharti kiwe na misingi imara, kiwe na "constituency", kuwe na watu hasa waliokereketwa na waliokula yamini kukilinda. hawa ndio wapate wafuasi. ni baada ya chama kujijenga sana kwa muda mrefu, ndio unaweza kuleta hizo taratibu za kutegemea demokrasia. lakini hata hivyo ni lazima kuwe na utaratibu tofauti wa kusimamia wale wanaoingia katika chekeche. katika mazingira ya sasa, ambapo CCM chama dola kinatumia kila mbinu, huwezi kusema tu eti tutegemee demokrasia
 
Lowasa na kundi lake ni mafisadi kulingana na list of shame iliyo tolewa na chadema na sasa wanaona aibu kukemea ufisadi.....
mpaka ifikie idadi YA MAUMIVU YA KUKIMBIWA na MH. NYALANDU nnaimani NYALANDU atakuwa mbali na hamtomfikia. mtambue kuwa kila kichwa mtakachofika bei ndio sawa na gharama ya kumrudisha NYALANDU kama fisiem mtammaind.
 
Mkuu pasco.
Kama ni kushindana kwa hoja, hii unaweza kushindana na atakayekua radhi ushindane naye.

Hatahivyo Mpaka sasa naona CCM haiko tayari kushindana kwa hoja na xhama chochote ikiwemo CDM.

Mfano. Tundu lisu alishindana kwa kujenga hoja makini za kusaidia jamii, matokeo yake sisi tu mashahidi kwa jinsi alivyo nusurika Umauti. Tukashindwa hata kumfanyia maombi ya kitaifa.
Huku wapo wanao hoji uzalendo wa Tundu Lisu kwa Taifa.

So mi nachoona ukiongozwa na dikteta. Kuna kua hakuna the way foward.

Wako wasanii kama akina Roma Mkatoliki.

Mwisho nakubaliana na wewe kua adui wa CDM sio CCM. Kwasababu moja kubwa. Naiona CCM yenyewe ikiwa imeshikwa. CCM imefungiwa minyororo haiwezi kufurukuta. This is one man show.Not a party show.

Sote tulishuhudia swala la kuvamiwa kituo cha Clouds FM lilivyotumika kumng'oa uwaziri Nape.


Mwisho napenda ufahamu kua:-
ushauri wako unaweza kua sehemu ya trial amd era kwa manufaa mapana ya CDM lakini sio suluhisho per Se.
 

Umetumia muda wako mwingi kudadavua siasa ya Chadema; kuna pointi umeongea hazina msingi wowote. wanao hamia CCM, wanafukuzia fursa huko. Huyo Masha ni nani asiye mjua? amekimbilia CCM ili kuficha kucha zake. Ata ukimtazama usoni haaminiki. ndiyo mana ameomba kutumiwa na raisi, kutumiwa maana yake nini? Anataka madaraka.
Huyo Kafulila ndo usiseme, hana mbele wala nyuma; political career yake ni unafki mwanzo mwisho. ni juzi tu hapa alifungua kesi kua CCM kimeiba kura zake, leo hii hao hao waliomuibia kura amerudi kuwakumbatia.

Leo hii unahama chama kwa sababu hukupata madaraka, huko unakoenda utakuta madaraka inakusubiri? Je sisiasa ni kuendana na upepo? Nchi kama India inavyama vya siasa zaidi ya 1000 lakini wanaongoza nchi kwa kuvumiliana, kukosoana na nchi inakwenda mbele. Raisi wa marekani anapingwa kwa sera zake lakini sijawai kusikia wabunge wake wanakiahama chama chake na kukimbilia kwa Democrates. Nini cha kujifunza? wanasiasa wetu bado ni wachanga.

Kumbuka waliokua wakimshangilia Rais wa Zimbabwe hao hao ndiyo waliomuondoa madarakani. Ipo siku utakumbuka haya ninayosema. CCM si salama kama unavyodhani, kule kuna ubabe, kulindana na wizi. wapo kina Yusufu Makamba, kina Muhongo ambao hao ni maaduwi wa Kafulila bado wapo, na wengine wengi. kwa hiyo jawabu si kuhama chama bali kurekebisha makosa na kuendeleza mapambano.

ni nani asiyejua faida ya upinzani nchini? bila upinzani, escrow isingejulikana, bila upinzani neno ufisadi isinge julikana. sasa leo hii kila mtu anataka kua CCM.
Haya wee subiri aongezewe miaka 7 za kutawala ndo utashtuka
 
Mkuu Paschal,

Aliekuwa ameiimarisha Chadema na kuipa nguvu kubwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 alikuwa ni Dr Slaa.

Tunafahamu ni kwanini Dr Slaa aliondoka Chadema na sasa anapumzika kabla ya kurejea CCM (tetesi).

Chadema haina nguvu sana na inachofanya chama hicho kisimame vizuri bungeni ni kujitutumua kwa mwenyekiti wake Freeman Mbowe kwa hoja za matukio badala ya sera.

Kama wote humu tumewasikiliza kwa makini Profesa Kitila Mkumbo na Patrobas Katambi ambao kwa hakika wametoa mwelekeo wa uwezo wa kufikiri wa wapinzani wa Tanzania ambao bado ni mdogo sana.

Simaanishi hawa wawili na wengine wanaohamia CCM kutoka Chadema, au ACT au CUF kwamba wao wana akili sana, la hasha bali wana wezo wa kutathmini yale walokuwa wanayaamini kama kweli ni sera za vyama vyao.

Kama una mwenyekiti wa baraza la vijana katika chama chako na mwenyekiti huyo anaondoka, hilo ni pigo kwa chama kwasababu baraza la vijana ndilo msingi wa ukuaji wa chama chochote kile.

Kama tunakumbuka mwaka 2014 BAVICHA walifanya uchaguzi ambapo Katambi alipambana na vijana wenzie Daniel Naftari na Upendo Peneza ambao wapo Chadema Bavivha kabla ya Katambi.

Sababu za Katambi kushinda uchaguzi ule ilhali alikuwa ni mtu wa nje yaani outsider, kilionyesha uwezo wake wa kujenga hoja na kuzungumza kwa ufasaha anapokuwa jukwaani.

Hivyo ni kweli Chadema inahitaji kujitafakari sana katika uwezo wake wa kupata wanachama wapya na hasa vijana ambao ndiyo msingi wa chama.
 
That's whai yu a mai loyaaaaaa [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…