Never, unataka kusema tanzania hii kuna anayeyaona hayo, never, ni njaa zinawasukuma kuondoka. Mbaya katika Tanzania hii ni Lowasa, Fisadi kuliko wote ni Lowasa (kama kweli tuhuma ni ya kweli). Nakuapia kama hawatapata wilaya na mikoa, watarudi Chadema. Usilete shallow analysis, hawa wanahama baada ya Magufuli kusema atahakikisha anaua upinzani. Njia moja wapo ni kuwanunua (madiwani), sasa anaona wenye njaa kama Kafulila, atawapa vyeo.... etc. Petro, akiwapa vyeo utasemaje? Time will tell. Yule binti tayari ni waziri, na akina kafulila and Co. Ltd wanategemea watafanyiwa hivyo.
Mkuu, "with all due respect" upinzani wa Chadema hauna nguvu sana kwa sasa maana yale yote walokuwa wakiyapigania, serikali chini ya CCM ndiyo inayatekeleza.
Chadema waache kutumia matukio kama sera zao na mikakati ya kutaka kugombea kuingia Ikulu.
Waanze upya kwa kuhakikisha wabunge wanaonekana wanafanya kazi waliyochaguliwa kuifanya.
Waje na sera mbadala na zionekane ni sera zipi ambazo zinakuwa ni zaidi ya zile zinazotekelezwa sasa na CCM na serikali yake.
Usitaje sera kama haki ya kufanya mikutano au kubomolewa nyumba zilizo ndani ya hifadhi ya barabara, hizo siyo sera bali ni hoja ambazo kamwe hazitasikilizwa na wananchi ambao huchambua hoja hizo.
Kama mwananchi anaona barabara inapaswa kupanuliwa kupitia ndani ya hifadhi yake na ni kweli amejenga ndani ya hifadhi basi ni lazima nyumba hiyo ivunjwe na apishe bila kutegemea kulipwa fidia yoyote.
Unapotaja sera Chadema ina sera zipi kuhusu Uchumi, viwanda, teknolojia, miundombinu, ajira, elimu, kilimo na kadhalika.
Unakuja na sera mbadala au "alternatives" unaweka wazi wananchi wanapima ingawa hakuna guarantee ya kuzikiubali kama zile zilizopo zinatekelezwa kwa kasi ya ajabu.
Mkishindwa kwenye uchaguzi mnapika sera zingine na zingine na hata baadae mnapata zile sera ambazo zinauzika kwa wapiga kura na huenda mkashinda uchaguzi.
Leo hii karibu nusu ya wabunge wa upinzani hawaenekani majimboni kwao, na hii ni kasoro kubwa sana kimkakati kwa Chadema ambayo ndiyo inawagharimu.
Pili, Dr Slaa ndiye alikuwa katibu mkuu wenu makini sana na hoja yake kwamba hawezi kula matapishi kwa kumkaribisha Edward Lowasa Chadema ni ya kuizingatia sana.
Vinginevyo ntaendelea kuamini kuwa Edward Lowasa, Fredirick Sumaye na mzee Kingunge Ngombale Mwiru wamehamia Chadema kukidhoofisha zaidi kuliko kukiimarisha.
Wakimaliza kazi hiyo basi mwenyekiti Mbowe atakuwa na wakati mgumu sana.
Naamini hayati Mwalimu Nyerere hakutaka kabisa vyama vya siasa lakini kwa kuwa hakuona faida ya kuendelea kuvikatalia akaamua kuvuruhusu mwaka 1992 na wengi hapa akiwemo Pasco tuliona huo ujio wa hivi vyama.
Lakini alifanya hivo kwa malengo kwamba ni lazima vyama hivi huko mbele visiwe na meno makali na hata vikiota meno makali basi wapo mafundi ya kuyapunguza.
Ndiyo maana Chadema inapaswa kuwa makini na utaratibu wake wa kukaribisha wanachama wapya hasa wale wanaohamia kutoka CCM ambao hakuna ushahidi kama wamerusisha kadi za vyama vyao.
Je, tunajua kama profesa Kitila Mkumbo au, bwana Katambi na wenzao kama walirudisha kadi za CCM walizokuwa nazo kabla hawajahamia Chadema kutoka CCM?
Jibu ni hapana.
Kama kweli Chadema ilitaka kuimarika kikwelikweli basi Freeman Mbiwe alipaswa kumpisha Edward Lowasa awe mwenyekiti wa chama ambapo angalau angeweka usawa katika majukwaa kama mtu "mzito" ingawa bado asingeweza kujisafisha na tuhuma za ufisadi.
Nafikiri utanielewa hapo.