CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Nadhani unashindwa kubalance habari yako kwa kuangalia tu upande mmoja. Hv huko Ccm hakuna wanaoondoka? Na kibaya zaidi wanachama wengi wa upande wako ndio hao wanakuwa kama Nyumbu wa Serengeti, miezi hii wanakwenda Masai Mara Kenya, then hurudi Serengeti Tanzania.

Ukiangalia hao wanachama wanaokwenda na kurudi, ni wale wale Kijani.

So ili ulete habari nzuri, basi jaribu kufanya uchambuzi kwa vyama vyote na utaona hilo tatizo ni kwa vyama vyote.

Wahenga walipata kunena "Nyani haoni Kundule".
 
Nyumba ya kina wema sepetu mtaendelea na mpango wa kuivunja? binafsi siwalaumu hawa wanaohangaika kuokoa mali zao. Hapa muhuni ni CCM
 
Nafikiri ni kweli kuwa kuna tatizo na kuondoka kwa hao wavulana na wasichana ndo kuondoka kwa tatizo la Chadema. Chadema inasafishika na come 2020 kitakuwa chama bora zaidi, hata kama kitakuwa na wanachama wachache! Tatizo linaondoka!
Kinasafishika aliekichafua nani.?
 
Wenye nyumba wanakwambia hakuna tatizo, sasa unaposema lipo tatizo pengine labda wewe ndio tatizo.
Anyway nisikupinge, kunaweza kuwa na hoja kwa mfano:-
Kama kuna tatizo sababu yake ni nini?
Wengi tutasema kuwa ni Mwnykt, lakini vipi kuhusu ajenda ndani ya nyumba zipo kama zipo nani wa kuzisimamia na kuhakikisha zinafanziwa kazi?
Je hali hiyo inaweza kuwa inasababishwa na kutokuwepo kwa mmoja ya mwanafamilia machachali?
 
Na wanachama hao wakiondoka lazima waende CCM tu na si kwingineko. We komaa na hali yako huko uliko
 
Wakati wa harakati za ukombozi SA, wakati Nelson Mandela anatumikia kifungo cha maisha (Roben Islands),Chief Matanzima kiukoo alikuwa baba yake mdogo, alikubali uhuru bandia wa jimbo(Bantustan) Transkei, kutoka kwa makaburu. Wasaliti walianza siku nyingi.
 
Sababu ni njaa, wanaohama wana njaa ya pesa. Kuna wanaotishwa wakatishika kupoteza mali zao, wanahamia ccm kulinda maslahi.
Na MTU Wa aina hiyo unakuwa umekwenda mwili sio moyo wake
 
nimekusoma mkuu, hongera. kuna mijitu humu ina akili kipisi inapost ujinga.
 
hili la usaliti halina mashiko tena kwa sasa
 
.....
.....la Umeme?
 
Yaani wachumia tumbo ambao hawajitambui usiku na mchana wanahaha huku na kule kutafuta namna ya kujaza matumbo yao kuondoka kwao Chadema kunahusishwa na matatizo makubwa sana Chadema!!! Kweli akili ni nywele hata MAZWAZWA wana nywele pia.

 
Bado sijaona tatzo, hamna chadema hata mmoja nnaemjua alieondoka chadema
 
Kinasafishika aliekichafua nani.?
Chama kinaweza kuchafuka kwa uzembe uzembe tu na ni sehehe katika mchakato wa kukua. Sasa ikifika mahali ukweli ukadhiri na uchafu kuanza kujitenga na usafi hilo linakuwa ni jambo la kupendeza sana na maswali ya kilichafukaje yanakuwa redundant!
 
Nenda kalitatue, hapo nitakuona wa maana.
 
Kama biashara zako haziendi kisa umehamia Chadema, ubaki ili iweje??!![emoji23] [emoji23] [emoji23]
Cc Kiss Lipstick ( Wema) hazifai kwa matumizi ya binadamu
 
Nadhani ungefanya tathmini kidogo kuanzia 2015 kuona watu waliotoka CDM wakaenda CCM na kutoka CCM wakaenda CDM. Kwa tathmini hiyo ungeweza kuja na asilimia(%) za movements from one party to another and back. Nadhani hiyo ingeweka hali halisi na ingeendana na hoja yako!
 
Chadema atabaki Mbowe na Lissu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…