CHADEMA mkitaka kupata kura 2025 acheni kauli za chuki kwa JPM

kilakitu kipo wazi wananchi wanaona kwa macho mambo gani JPM kafanya nchi nzima wala ahitaji tochi.
Kweli kabisa mkuu
Watanzania waliona jinsi magufuli alivyo poteza watu kisa tu Wana mawazo kinzani na yeye,aliwafunga jela watu wasio na hatia,alichafua uchsguzi 2019 na 2020. Kweli mambo sliyofanya hayahitaji tochi Ili kuyaons
 
Sijawahi acha Wala sitokuja kuacha kumsema Mwendazake humu mitandaoni na mtaani vijiweni popote Huwa namsema Kwa ubaya wake bila kujalisha wengine Wana maoni gani.

Waoga ndio wataogopa kumsema Mwendazake.
Duh! Hutokuja kuacha kumsema!

Kwamba maisha yako yote utakuwa unamsema Rais wa Tano Magufuli?
 
Kweli kabisa mkuu
Watanzania waliona jinsi magufuli alivyo poteza watu kisa tu Wana mawazo kinzani na yeye,aliwafunga jela watu wasio na hatia,alichafua uchsguzi 2019 na 2020. Kweli mambo sliyofanya hayahitaji tochi Ili kuyaona
nimedokezwa JNHPP linajaa maji kwa kasi sana,kwa kufupi miradi aliyoasisi JPM inaenda kwa kasi sana😎
 

Unadhani CDM kumchukua Lowassa kila mfuasi wa CDM aliafikiana na uhuni ule. Kikwete aliiba kura, lakini Magufuli alipora mchakato. Je huo wizi wa kura wa Kikwete uliona ukisifiwa?

Kuungana ni kutokana na msukumo wa jamii, lakini kwangu nilijua sio sahihi kutokana na ubinafsi wa vyama vyote vilivyoungana, na kweli ushirikiano ule haukudumu maana haukuwa wa kisheria, bali utashi wa viongozi zaidi.
 
Mkuu uko sahihi kabisa,mi nadhani probably watu tulipoo humu jf sio watanzania,ukibahatika kutembea kutana na watu mitaani Bado watu wengi wanamkumbuka magu kama mmoja wa viongozi Bora waliotawala nchi hii,kumsema vibaya jpm nadhani haiwajengi cdm wabadilike kabisa.
 
Issue sio kwa sababu ni Lowassa bali ni mtu mwenye mvuto na kutoka ccm, kama CDM ndio inakubalika na wananchi kuna haja gani kufikiria kuchukua watu waliyotoka ccm?

Kikwete kama alikuwa ni mwanademokrasia sio dikteta sasa alikuwa na haja gani nae ya kuiba kura?

Ule muungano ni jitihada za kumshinda ccm kwenye sanduku la kura, na ndio mnajisifu kwa kupata kura nyingi baada ya kuunganisha hiyo nguvu.
 

Tufike wakati kila mtu awe huru kusema lolote analotaka ilimradi liko ndani ya sheria. Kuna faida gani kudanganya ? Yaani mnataka tuendelee na utamaduni wa unafikiri!
 

Kwa taarifa yako pitia post zangu zote kuhusu huo ujio wa Lowassa, toka mwanzo nilisema ni upuuzi kuokoteza mtu toka CCM tena mwenye sifa mbaya. Na nilimlaani Mbowe Sana kwa upuuzi ule. Mwanzo Wafuasi wa CDM hawakunielewa, lakini baada ya Lowassa kurudi CCM kila mmoja alinielewa.

Kikwete alikuwa ana afadhali kidemokrasia kulinganisha na Magufuli. Ila suala la kuiba kura halikukwepeka kwani ndio CCM ilipofikia, kuwa bila wizi wa kura hawatoboi. Magufuli yeye hakuiba kura, bali alinajisi mchakato mzima wa uchaguzi. Hiyo ni tofauti kubwa.

Ule muungano ulikuja kutokana na shinikizo la wafuasi wa upinzani. Kuna mambo hayakwepeki kutokana na nyakati. Mfano mrahisi wa msukumo wa dunia kuhusu mfumo wa vyama vingi. 80% ya maoni hayakutaka mfumo wa vyama vingi, lakini ilibidi huo mfumo ukubaliwe maana mazingira yalikuwa hayo. Kipi huelewi hapo?
 
Wanaomkejeli Magufuli 90% ni CCM!
 
nimedokezwa JNHPP linajaa maji kwa kasi sana,kwa kufupi miradi aliyoasisi JPM inaenda kwa kasi sana[emoji41]
Makaburu weupe kule Africa kusini walifanya mambo makubwa ya kimaendeleo kuliko yaliyofanyaka hapa na Bado walipigwa kwa sababu tu ya udhalimu wao. Wewe na Mimi ni AKINA NANI Hadi tushindwe kumpinga kaburu mweusi? Atapingwa tu hata kama ni mweusi
 

..Jk aliiba.

..Jpm alipora.

..kuna tofauti kati ya mwizi na jambazi.
 
Makaburu weupe kule Africa kusini walifanya mambo makubwa ya kimaendeleo kuliko yaliyofanyaka hapa na Bado walipigwa kwa sababu tu ya udhalimu wao. Wewe na Mimi ni AKINA NANI Hadi tushindwe kumpinga kaburu mweusi? Atapingwa tu hata kama ni mweusi
Atulazimishani kilakitu kipo wazi pumba zipi na mchele ni upi.
 
Na ndio rais anayependwa na wananchi wake,ukibisha nenda kasome andiko la jamii forum Instagram kuhusu mbowe kumsema Vibaya JPM alafu usome moment za WANANCHI utajua nini ninachokimaanisha.
Sukuma Gang ni asilimia ngapi ya watanzania wote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…