CHADEMA mkitaka kupata kura 2025 acheni kauli za chuki kwa JPM

CHADEMA mkitaka kupata kura 2025 acheni kauli za chuki kwa JPM

Nimekuwa nikifuatilia posti nyingi hapa jamii forums zinazomuhusu aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, pia hata mitaani na kwenye vyanzo vingi vya habari ikitokea magufuli ametajwa na kiongozi yeyote kwa lengo la kumfedhehesha basi 90% ya watoa maoni watakuwa upande wa JPM.

Sasa rahi yangu kwa CHADEMA ni kwamba wanapaswa waelewe kwamba wananchi wa kawaida wao shida yao haikuwa demokrasia ila ni unafuu wa maisha, hivyo unaposimama jukwaani kumponda Magufuli na kumsifia Samia ukidhani unawafuraisha ni kujichimbia kaburi.

Nimefuatilia hotuba ya Mbowe ni wazi watu hawana imani nae tena si mtetezi wa wananchi tena na mbaya zaidi alipomsema vibaya JPM na kumsifia Samia wengi waliguna na kuonyesha wazi kuwa kalamba asali ya ikulu.

Tulishakubaliana mikutano ya siasa sio takwa la Rais lipo kikatiba inakuwaje tena mwenyekiti wa chama anamsifia Rais kuwa anamshukuru kwa kuruhusu, haki inadaiwa na haiombwi sasa wamekuwaje tena.

Nawasisitiza Magufuli mkimtumia vizuri kwenye sera zenu ndiye anaweza kuwapeleka Ikulu kwa sababu yeye alikuwa kipenzi cha wananchi.
Usiwapangie ,kwa jinsi alivyoendesha nchi kidikteta lazima waTZ waambiwe "UKWERI" wa madhara yake.
 
Lakini akubalika na wewe jifanye ili ukubalike au hao viongozi wako washairi

..ni kwasababu mifumo yetu ya upashanaji habari bado ni dhaifu.

..wananchi wangekuwa na taarifa za unyama na ukatili wake wangemkataa.

..historia itamtambua kama kiongozi aliyekuwa na damu ktk mikono yake.
 
Hizo habar ulizipat wap kam hyo mifumo dhaifu
 
Kweli kabisa mkuu
Watanzania waliona jinsi magufuli alivyo poteza watu kisa tu Wana mawazo kinzani na yeye,aliwafunga jela watu wasio na hatia,alichafua uchsguzi 2019 na 2020. Kweli mambo sliyofanya hayahitaji tochi Ili kuyaons

Kama wananchi wote wanajua na waliona mbona hamuachi wao wenyewe waamue kila wakati mnawakumbusha!!!
 
Lakini ulimpa kura yako?

Sikumpa Lowassa kwa kumuamini, bali nilitoa kura kwa nafasi ya urais kwa mgombea wa upinzani ili kuifanya CDM kuwa na kura nyingi. Lakini ningesikitika sana kama kura yangu ndio ingeamua Lowassa kubwa rais.
 
..jpm alimzidi Jk kwa kupiga na kuumiza wapinzani, hilo halina ubishi.

..na baada ya kuumiza wapinzani jpm akasambaza watu wake wa propaganda kuzidi kuwachafua wahanga walioumizwa.

..kwa mfano sikuwahi kumsikia mzee kinana km Ccm wakati wa Jk akimchafua dr.ulimboka.

..wakati wa jpm km dr.bashiru na mwenezi polepole, waziri wa mambo ya ndani, msemaji wa serikali, igp, walikuwa mstari wa mbele kupayuka matusi dhidi ya majeruhi wa utawala wa jpm.
Hao chadema washapigwa hadi bomu huko Arusha, huko Zanzibar cuf waliuliwa kama kuku hadi wakakimbilia huku. Unataka kutuaminisha upinzani umeanza kupata mateso kipindi cha Magufuli tu?
 
Fanyeni tafiti vizuri hasa kwa tabaka la chini ambalo ndio wapiga kura , Magufuli kwao atabaki shujaa na wengi wanaamini aliuawa

Hivyo ni ngumu kwa mwanasiasa yeyote kukubalika kama atamkashifu Magufuli

Someni upepo
 
Sikumpa Lowassa kwa kumuamini, bali nilitoa kura kwa nafasi ya urais kwa mgombea wa upinzani ili kuifanya CDM kuwa na kura nyingi. Lakini ningesikitika sana kama kura yangu ndio ingeamua Lowassa kubwa rais.
Wewe si lolote kwa chadema mkuu hauna athari yeyote, jaribu kutenganisha chadema na mitazamo yako binafsi wewe kama wewe. Nakwambia hivyo kwa sababu kuna wakati mtu anapozungumzia jambo kuhusu Chadema kwamba imefanya hiki na kile ajabu unakuja wewe kusema mie sikutaka hivyo sijui sikuunga mkono, sasa inahusiana vp kwani wewe ni nani kwa Chadema?
 
Hivi kuna ubaya gani kumpa mtu sifa zake?
Acheni apate 'sifa' alizoacha duniani! pambaf ninyi!
Kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema na makatili watapigwa laana milele!
 
Nimekuwa nikifuatilia posti nyingi hapa jamii forums zinazomuhusu aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, pia hata mitaani na kwenye vyanzo vingi vya habari ikitokea magufuli ametajwa na kiongozi yeyote kwa lengo la kumfedhehesha basi 90% ya watoa maoni watakuwa upande wa JPM.

Sasa rahi yangu kwa CHADEMA ni kwamba wanapaswa waelewe kwamba wananchi wa kawaida wao shida yao haikuwa demokrasia ila ni unafuu wa maisha, hivyo unaposimama jukwaani kumponda Magufuli na kumsifia Samia ukidhani unawafuraisha ni kujichimbia kaburi.

Nimefuatilia hotuba ya Mbowe ni wazi watu hawana imani nae tena si mtetezi wa wananchi tena na mbaya zaidi alipomsema vibaya JPM na kumsifia Samia wengi waliguna na kuonyesha wazi kuwa kalamba asali ya ikulu.

Tulishakubaliana mikutano ya siasa sio takwa la Rais lipo kikatiba inakuwaje tena mwenyekiti wa chama anamsifia Rais kuwa anamshukuru kwa kuruhusu, haki inadaiwa na haiombwi sasa wamekuwaje tena.

Nawasisitiza Magufuli mkimtumia vizuri kwenye sera zenu ndiye anaweza kuwapeleka Ikulu kwa sababu yeye alikuwa kipenzi cha wananchi.
Waambie Kabisa
 
Fanyeni tafiti vizuri hasa kwa tabaka la chini ambalo ndio wapiga kura , Magufuli kwao atabaki shujaa na wengi wanaamini aliuawa

Hivyo ni ngumu kwa mwanasiasa yeyote kukubalika kama atamkashifu Magufuli

Someni upepo
Nyundo kwa nyundo!
jembe kwa jembe!
msumari kwa msumari!
Jiwe kwa jiwe!
Ubaya kwa ubaya!
 
Alisababisha madhila makubwa kwa binadamu wengi na bado vidonda ndani ya mioyo yao havijapona, acha watu wateme nyongo kwani ni namna mojawapo ya kuviponya hivyo vidonda.
Wewe fanya yako na endelea kuamini unachokiamini.
Madhila Makubwa kwa mafisadi na wezi ila sio kwa wananchi wa hali ya chini ambao ndio kundi kubwa
 
Sijawahi acha Wala sitokuja kuacha kumsema Mwendazake humu mitandaoni na mtaani vijiweni popote Huwa namsema Kwa ubaya wake bila kujalisha wengine Wana maoni gani.

Waoga ndio wataogopa kumsema Mwendazake.
We si cheti feki lazma umseme tu ila haibadilishi maana kuwa alikunyoosha kenge wewe
 
Na magufuli hakua kipenzi cha wananchi bure tu. Aliyabeba matakwa yao moyoni.
Nyie mnaompima magufuli kwa kupotea ben saanane, kupotea yule mwandishi jasusi aliyekua anaenda kule rufiji kupeleleza jinsi polisi wanawafyeka wale magaidi, kupigwa risasi tundu lissu mtu aliyemtukana jpm eti ndio rais wa ovyo haijawahi kutokea, mkidhani ndio mambo yatawafanya watanzania kumchukia magufuli hakika mnapoteza muda na mumepotea dira.
Maguguli alikua anaongoza vita vya kiuchumi kulikomboa taifa kutoka unyonyaji wa mabeberu na vikaragosi wake nchini. Hili wananchi walielewa sana. Nyie vikaragosi wa mabeberu mnajua kazi aliyofanya magufuli kuwazibia rizki kwa kuwaibia na kuwanyonya raia. Hamlitaji hili la uchumi ila mnaleta mambo ya kipuuzi tu hayana maana kwa maslahi ya umma. Eti magufuli alikua dikteta, ooh ben saa nane kapotea. Ujinga mtupu.
Wafuasi wa umagufuli wanajipanga kupata mrithi atakayeendeleza ndoto na maono ya magufuli. Wasipompata ccm watamtafuta kwingine.
Wapuuzi wanakimbiliaga kwenye uzushi wa ben sanane ikiwa hata mwenye ushahidi na hilo hayupo. Mi nawaonaga ni wacenge tu, Magufuli alikuwa mtu na nusu.
 
..ni kwasababu mifumo yetu ya upashanaji habari bado ni dhaifu.

..wananchi wangekuwa na taarifa za unyama na ukatili wake wangemkataa.

..historia itamtambua kama kiongozi aliyekuwa na damu ktk mikono yake.
Wewe mmoja unamkata wenzio million 50 wanamkubali sasa ujioni kama ni tahira.
 
Hivi kuna ubaya gani kumpa mtu sifa zake?
Acheni apate 'sifa' alizoacha duniani! pambaf ninyi!
Kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema na makatili watapigwa laana milele!
Wema huwa hawafi, marais wastaafu wakristo wote wamekufa na kubaki waislamu. Kwa maslahi ya taifa kwa kuepuka madikteta na kuwepo demokrasia tuchague marais waislamu tu si unaona Mzee Mwinyi,Kikwete na Samia ni watu safi.
 
Back
Top Bottom