CHADEMA, mna haki ya kumuona Lissu kama shujaa wenu, ila si kulazimisha kila mtu amuone ni shujaa

Sioni ajabu kwa kuwa nilitoa nafasi kwa watukanaji
Hongera,kwa ku staarabika mimi siko upande wowote kiitikadi lkn CDM sometimes wanaikosa democracy wanayoihubiri ,they only think all their ideas are positive and strong.
They don't leave space for people to correct them
 
Wewe au ukoo wako mmelifanyia nin hili taifa kumzidi Lissu labda??? Tuanzie hapo!
Mleta thread nimtu mjinga asiye na utafiti... mpaka madikteta ushuzi watake kumuua ujuwe aliyabana kjambio vizuri!
Pambana na kisamvu chako chalii mang'aa si tunakula baga
 
Nilifikiri ni mwanamapinduzi mwenzetu kumbe wapinga maendeleo mnakulana vichwa wenyewe kwa wenyewe.
Hapo naiona pro lissu na pro mbowe chadema zikianza mtifuano.
 
Ukisema hivyo ,unakua unakosea mkuu kwamba ww umelifanyia nini taifa,kila mtu ana nafasi yake katika taifa na analifanyia taifa makubwa kwa nafasi yake,wote hatuwezi kua wanasiasa je unataka na yeye awe mwanasiasa ili alifanyie jambo kubwa taifa?
 
Ukisema hivyo ,unakua unakosea mkuu kwamba ww umelifanyia nini taifa,kila mtu ana nafasi yake katika taifa na analifanyia taifa makubwa kwa nafasi yake,wote hatuwezi kua wanasiasa je unataka na yeye awe mwanasiasa ili alifanyie jambo kubwa taifa?
Hekima hili mkuu! Barikiwa
 
Ndugu
Demokrasia ni kuvumiliana kwa kuwa sote hatuwezi kuwa na mawazo au fikra zinazofanana.....sio dhambi kuwaza tofauti na wengine..........

Sio kila anayetofautiana fikra ni aibu bali ndio ubinadamu.......s

Safi sana mkuu
 
Lisu sio tu shujaa wa chadema ni shujaa wa wakati huu, ni yeye pekee amepigwa risasi nyingi na serikali ili kuzibwa mdomo na bado amebaki hai, ila sasa waliamua na kukataa kughulikia waliohusika wao wameshatangulia mbele ya haki. Sasa hii haitokei hivi hivi kuna namna mwenyezi anataka na wewe uone umuhimu wa kusikia kutoka kwa usiopenda kusikia kutoka kwako.

Yapo mambo Lisu anayaelezea vizuri zaidi kuliko mtu yeyote, zilipita tawala za kina firauni huko ambapo level yao ya udikteta ulipitiliza na leo hawapo tena duniani hapa, sasa sheria na katiba zetu zilitungwa na wakoloni kwa maslahi yao sasa zimepitwa na wakati.
 
Kwa ufupi lissu hana uzalendo wowote ule katika taifa hili ndo maana watoto wake wote wana uraia wa marekani,pili lissu ni mtu mwenye uchu na madaraka yuko tayari kufake issue ili apate madaraka na kingine ni kuwa kibaraka wa wazungu.
 
Una maelezo yanyovutia lakini yenye uhaba wa ukweli;
1.Kusema Lisu alimtukana Baba wa Taifa hili Jambo sijui huwa mnalitoa wapi. Lisu alimkosoa Baba wa Taifa Kwa style aliyotumia kuunda Muungano na akatumia neno ujanja ujanja. Ni Muungano huu àmbao mpaka Leo tunapokaribia miaka 59 ya kuasisiwa kwake bado haijulikani ni Muungano dume au jike. Umejaa kero na nyingine zinazaliwa Kila asubuhi. Tume ya Warioba ilikuja na pendekezo la serikali 3, CCM wakaikataa kwamba itavunja Muungano Kwa kumfanya Rais wa Tanganyika awe na nguvu Sawa na wa Zanzibar na hivyo wa Muungano kubaki anaelea. Hii ndo iliyokuwa hoja ya kina Marehemu Njelu Kasaka na wenzake mwaka '90 iliyozimwa na Mwalimu. Kwa hiyo hoja yako kwamba kilichovunja Bunge la Katiba ni maneno ya Lissu Kwa Baba wa Taifa haina uhalisia na sababu inajulikana Hadi kuzaliwa Kwa UKAWA.
2.Lissu angekwenda Ikulu kumwambia Rais badala ya kuita waandishi wa habari na kwamba si Kila Jambo la nchi linasemwa hadharani.
Kwanza nikupingeze kuwa kukubali kwamba Lissu alikuwa na hoja japokuwa unasema hakuiwasilisha sehemu sahihi. Kwa Taarifa yako na wengine wasioelewa Lissu ni mwanaharakati wa mazingira na mtetezi wa waliodhurumiwa kabla hajawa Mbunge. Nyamongo na Barick wanajua vizuri habari yake. Kumbuka Mzee aliyesafiri toka Tarime kwenda Nairobi hospital kumuona Lissu kilichomsukuma ni nini? Tukirudi kwenye hoja yako Kwa nini asingepeleka ushauri Ikulu, tueleze Ikulu ipi inhempokea Lissu? Nchi zenye DEMOKRASIA iliyopevuka wapinzani huitwa Wenye mawazo mbadala, huku dunia nyeusi wapinzani huwa ni Wakinzani. Spika awatoe nje ya Bunge, wakifuka nje Rais atakula nao sahani moja. Hapo ukategemea Lissu angepokelewa Ikulu na akasikilizwa? Njia pekee iliyokuwa imebaki ni kupiga kelele kunusuru Mali za Watanzania, bahati mbaya aliyepigiwa kelele alikuwa na jibu moja tu, RISASI.
3.Lissu alikuwa na hoja nzuri ya kuzieleza nchi wahisani Kwa utulivu juu ya kilichompata na wangemuelewa na kupiga ban serikali na kwamba hata wewe ulitaka hili litokee.
Sawa kabisa, ulitaka litokee na Kwa Taarifa yako kama ulikuwa hujui lilitokea. Wewe Ulitegemea total ban lakini wenzio Wana akili wakatupiga partial ban tukanyooka. Matendo ya kuchukua hela za watu kwenye akaunti na kesi za uhujumu uchumi Kila mahali hazikuja bure. Ilikuwa last kick of the Horse. Tukaumia kiuchumi tukatafuta marafiki wanafiki lakini hatukupona. Hukumbuki kuna nchi zilitangaza kupunguza kabisa misaada? Au nikutajie?
4.Lissu Hana utulivu katika kuongea na analazimisha aliyokusudia yaaminiwe na watu wote.
Mtu yeyote makini na mwenye hoja zilizoshiba hawezi kupeleka hoja legelege anayoamini eti itapingwa na kukosa mashiko. Hata wewe umeleta hapa hoja yako kuhusu Lissu unataka tukuamini kwamba ulichomwongelea Lissu ndivyo alivyo. Lakini tunaomjua zaidi tunasema hapana. Sasa kama wewe unajiamini kwamba unachosema ndicho sahihi kuhusu Lissu Kwa nini wewe unataka Lissu asijiamini kwamba hoja zake ambazo nyingi anazifanyia utafiti kabla ya kuzisema hadharani ni sahihi?
5.Wanaomwamini Lissu wanalazimisha watu wote waamini kwamba ni Shujaa.
Sidhani. Lini na wapi imetokea hivyo? Hakuna Shujaa wa watu wote. Hajawahi kutokea Shujaa mmoja akaonekana na kukubalika Shujaa wa watu wote. Daudi alimpiga Goliati Kwa jiwe la kombeo lakini hakuhesabika Shujaa wa Wafilisiti Bali wa Waisrael. Mpaka Leo Yesu ni Mwamba na Shujaa wa Wakristo lakini hachukuliwi Kwa uzito huo na Waislamu na Wayahidi. Mtume Mohamed (SAW) ni Mtume wa Mnyazi Mungu kiongozi wa Wengi lakini hatambuliwi hivyo na Wakristo na Wayahudi. Dalai Lama na Agha Khan ni mashujaa katika jurisdiction zào lakini si Kwa watu wote. Kwa maana hiyo wanaomuona Lissu Shujaa Wana haki na hawapaswi kubezwa maana Wana vigezo vyao kama wanaomuona Magufuli Shujaa wakati kuna wanaomuona kuna Mambo mengi kaharibu. Kuwapangia watu Nani au Shujaa wao na Nani awe dhaifu kwao si Sawa.
SABATO NJEMA MTU WA MUNGU.
 
Ujanja ujanja si lugha stahiki kwa mtu yoyote mkubwa wako ama mnayeheshimiana! Hilo ni tusi
 
Umeandika nini hiki? Hata wewe umekielewa ulichoandika ukihusianisha na mada tajwa hapo?
 

Ninakusoma utambulisho wako hapa:

"Niishie kwa kusema' Mh Tundu lissu kinachokosekana kwake ni ile hekima na utulivu, hawapishani tu na mwendazake."

Wewe utakuwa chawa wa Mama; ambalo si kosa.

Umesema:

"Na kwa sababu hiyo! Mh Lisu hakosi kuwepo kwenye lawama za kuwakosesha watanzania katiba yao."

Kwa hiyo una maana ni nani huyo aliyekereka na Lissu kiasi cha kutunyima sisi wengine haki yetu ya kupata katiba mpya?

NIkazie:

"Usicheze mbali na hoja ikiwamo za Lissu. Tunataka katiba mpya sasa."

Angalizo:

"Ushujaa wake ni kwenye hii nia yake ya dhati ya kuidai katiba mpya kama haki yetu."

Labda kama wewe unaidai kuliko sisi au yeye.
 
Yule mzee alikuwa katiri sana na haya ndio matunda ya kuwa na KATIBA mbovu inayo weza kuokoteza mtu yeyote kuwa kiongozi.
Kila nikimbuka machozi ya watu wasio na hatia aliyo watenda nashindwa kumsamehe najikuta tuu napeleka mashitaka Mbele za MUNGU mkuu nikimsihi aangalie machozi na damu za watu Hawa waliotendwa jeuri na bwana yule. Namsihi Mungu anipe moyo wa msamaha ili nami nisihukumiwe kwa kuto msamehe.
 
Kuna nduguyo ulishuhudia akitendwa hivyo mkuu au tu mvumo uliopo na wewe umekukumba!
 
Ukisema hivyo ,unakua unakosea mkuu kwamba ww umelifanyia nini taifa,kila mtu ana nafasi yake katika taifa na analifanyia taifa makubwa kwa nafasi yake,wote hatuwezi kua wanasiasa je unataka na yeye awe mwanasiasa ili alifanyie jambo kubwa taifa?
Soma uelewe broo... wapi nimesema awe mwanasiasa? Wapo wanamziki,wanasoka,wabunifu nk. Walofanyia taifa makubwa!!
Nimemuuliza yeye kafanyia taifa nini mpaka aseme Lisu hajafanya lamaana (kuwa sishujaa) maana navyojua kafanya mengi sana katika kutetea haki kama mwanasheria...leo kisa mrengo wakisiasa unstuoambua hana lolote ??
 
One sided story. Haya, umemaliza kakojoe ulale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…