CHADEMA mnachukua ruzuku ya nini wakati Wabunge 19 mmewafukuza?

Sasa Mkuu, CHADEMA tayari wamewatimua hawa covid-19, siyo wanachama wao. Kwa mujibu wa Katiba yetu, hao siyo wabunge tena. Kwaiyo. Mambo ya covid-19 usiwaulize CHADEMA!

Kwa mujibu wa taratibu za ruzuku, chama kinakokotolewa ruzuku kutokana na sifa mbalimbali ikiwemo idadi ya kura za urais na idadi ya wabunge, na sifa zingine. Tena hii ya idadi ya kura za urais ndiyo inabeba asilimia kubwa zaidi. CHADEMA ilipewa kura za urais asilimia 13. Nasema walizopewa, kwa kuwa kura zao kihalali zilikuwa nyingi zaidi.

CHADEMA tayari wametekeleza wanayohitajika kufanya kwa mujibu wa taratibu. Si jukumu la CHADEMA kuanza kujiuliza fedha wanayopata kutokana na covid-19 ni ngapi, kati ya sifa ambazo wanazo tayari.

Ni kama tu unawekewa mshahara mkubwa kuliko stahili zako. Wala huhitaji kuhangaika. Wenyewe watafanya makato na kurekebisha inavyotakiwa. Acheni kupotosha mambo
 
Kwahali ilivyo sasa hela ya ruzuku inaingizwa kwa nguvu kwenye akaunti ya chadema .nashauri wafuatilie kujuwa hiyo hela wamepewa kwa sababu zipi.
 
Hakuna walichochukua kaka, anyway baada ya kumsapoti dictator sasa umehamia huku.

Bi kizee hajambo? Kaadimika sana jukwaani
 
Acha uongo....then UMEFUNGA...AISEE,MUNGU ANA KAZI....
 
Una uhakika wameenda kwa msajili kuichikua hiyo cheki au msajili kawapelekea???? Tulete uthibitisho ya kusaini hayo makabidhiano. Sidhani kama wamechukua hiyo cheki.
Ruzuku wanaangalia idadi chama kilichoshinda kura za urais Kama umezid asilimia 5 unapewa acha uongo
 
Shughuli za saccos ni kukusanya pesa za wanachama wao!
 
1. Spika Job Ndugai amewalazimishia CHADEMA wabunge 19 wa VM...

2. Sasa Msajili naye anawalazimishia CHADEMA wachukue fedha inayoitwa "ruzuku"...

3. Na nyie wapiga matarumbeta mmezidaka taarifa hizo na sasa mnazifanyia propaganda...

4. THE FACT IS THIS: Pesa zinaweza kuwa zinaingia. Lakini utatumiaje pesa ambazo siyo zako hata kama zimeingia kwenye Bank Account yako..?
 
Kwanza tuambie mini maana ya ruziku
 
Hivi CHADEMA wakitumia pesa hiyo ya kulazimishwa itakuwa ni ishara ya kukubali uhalifu wa Ndugai?

Hili ni swali mkuu, siyo maoni!
 
Hata ningekuwa Mimi ningechukua,cdm hawajaomba ruzuku,serikali imeona umhim wa kuwa na wapinzani ndoo maana inawalazimisha kuwa nao akina halima mdee

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Wakuulizwa ni serikali ya CCM. Kwa nini inatumia kodi za wananchi wanyonge kulipa chama kisicho na wabunge? Kwa nini isipeleke pesa hiyo kujenga zahanati au kununua madawa?

Umewasikia huko bungeni lakini wanavyojichanganya? Wanafundishana kufuta kauli....yaani hii nchi(soma CCM!) haiishi vituko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…