CHADEMA mnaendelea kupotosha kuhusu suala la Ngorongoro, ila mtafeli kama mlivyofeli la bandari

DP World inaendelea na kazi na matunda yake yanaonekana,wapiga kelele mko wapi sasa??
Nani kakwambia matunda yanaonekana?.......unajua Stevedoring /Wharfage charges inawekwa kwenye account gani?.....acheni uchawa 🙂 🙂
 
Friends and Our Enemies,

Jana nimemsikiliza Godbless Lema,Kada na Mbunge za zamani wa jimbo la Arusha akiendelea na siasa zake za upotoshaji na kuganga njaa kuhusu suala la wamasai na kinachoendelea ngorongoro.

Lema anasema kwamba,Serikali inakosa mantiki katika kuwaondoa wamasai huku ikiendelea na kutoa vibali vya ujenzi wa hoteli mbali mbali za kitalii ambazo hizo ndizo zitakuwa kinara wa kuharibu ecologia na kuleta pollution kwenye hifadhi na kuathiri wanyama pori.

Well,Ifikie wakati hawa wanasiasa uchwara waache kujitoa ufahamu na kudhihirisha ujinga na upumbavu wao wazi wazi namna hii.

Suala la Ujenzi wa hoteli za kitalii ndani ya mbuga halifanyiki kiholela tuh bila mpangilio maalum,ni suala la kitaalam na siyo mbuga za Tanzania tuh eti ndiyo pekee zinajihusisha na suala la kujenga hoteli na kudesign utalii wa aina hiyo,yeye Lema na CHADEMA wanajua fika kuwa suala hilo linafanyika kote duniani na kila aina ya tahadhari inachukuliwa,na siyo kila mtu tuh atapewa ruhusa ya kujenga kwa kuwa tuh ana mtaji wa kufanya hivyo,kuna study kadhaa zimeshafanyika na kuangalia sustainability ya jambo hilo kwa kuzingatia uhifadhi na maendeleo yake kwa ujumla.

Wamasai ni Jamii ambayo imeendelea kuongezeka na kuzaliana miaka na miaka,na itaendelea kuzaliana hifadhini wao pamoja na mifugo yao.

Ni Jambo ambalo liko wazi tuh kuwa kutokana na kuendelea kwao kuzaliana wao na wanyama obviously population yao itazidi kuongezeka na kupelekea kuathiri maisha na uhai wa hifadhi na wanyama wale kwa maslahi ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Sasa,kuna kosa gani kwa serikali inapochukua hatua za makusudi katika kunusuru hali hiyo??wao CHADEMA na wanaharakati uchwara wanataka Serikali ikae kusubiri hadi lini kunusuru hali hiyo kwa mbuga zetu??

Wanakuja na siasa za kishamba eti ooh wamasai wanaondolewa ili mbuga wauziwe waarabu,ujinga ule ule waliokaja nao kwa kusema Bandari imeuzwa kwa waarabu ili mradi tuh kujenga taharuki na kukwamisha mambo ya msingi kuendelea.

Even kipindi cha Magufuli walikuwa mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji eti kwa kigezo cha kuharibu mazingira ila hivi sasa wao wenyewe wamekaa kimya na kuishiwa maneno.

CHADEMA na wanaharakati uchwara yanapokuja mambo ya msingi ya kitaifa kama mnapinga basi mje na hoja za maana na zinazoeleweka na siyo mnakuwa kama watu ambao hamna akili timamu.

Hoja zenu kuhusu suala hili za ngorongoro zitafeli kama zilivyofeli kwenye sakata la Bandari.
Hii ni nchi yetu sote......kwanini tunaumizana kwa ajili ya uchama?..........Kama wewe ungekuwa Maasai....ungefurahia kinachoendelea kule?
Tuweke ubinadamu mbele hayo mengine hayana nafasi.........sisi wote tutapita hapa duniani hakuna atakaye ishi milele.
Unaleta siasa kwenye maisha ya binadamu mwenzako kwa ajili ya mapenzi yako kwenye chama. Tafakari kwa makini.
 
Hili jambo watu wameingiza siasa na kuchochea chuki dhidi ya serikali pasipo kuzingatia maslahi mapana ya nchi. Kiukweli kwa hili jambo nipo na serikali bega kwa bega. Ni uamuzi mzuri na wa busara
Sahihi kabisa Mkuu,ukitaka ujue ukweli,we waulize hao wanaopinga kuwa wanataka serikali ifanye nini katika kunusuru ile hifadhi na wale wanyama kwa maslahi ya kizazi hiki cha sasa na hivyo vinavyokuja??

Kwa sababu wale maasai ni wanadamu
Hii ni nchi yetu sote......kwanini tunaumizana kwa ajili ya uchama?..........Kama wewe ungekuwa Maasai....ungefurahia kinachoendelea kule?
Tuweke ubinadamu mbele hayo mengine hayana nafasi.........sisi wote tutapita hapa duniani hakuna atakaye ishi milele.
Unaleta siasa kwenye maisha ya binadamu mwenzako kwa ajili ya mapenzi yako kwenye chama. Tafakari kwa makini.
Huelewi unachokisema,na kama huelewi au hujui ni vigumu sana kupata uhalisia wa kinachoendelea kule.
 
Friends and Our Enemies,

Jana nimemsikiliza Godbless Lema,Kada na Mbunge za zamani wa jimbo la Arusha akiendelea na siasa zake za upotoshaji na kuganga njaa kuhusu suala la wamasai na kinachoendelea ngorongoro.

Lema anasema kwamba,Serikali inakosa mantiki katika kuwaondoa wamasai huku ikiendelea na kutoa vibali vya ujenzi wa hoteli mbali mbali za kitalii ambazo hizo ndizo zitakuwa kinara wa kuharibu ecologia na kuleta pollution kwenye hifadhi na kuathiri wanyama pori.

Well,Ifikie wakati hawa wanasiasa uchwara waache kujitoa ufahamu na kudhihirisha ujinga na upumbavu wao wazi wazi namna hii.

Suala la Ujenzi wa hoteli za kitalii ndani ya mbuga halifanyiki kiholela tuh bila mpangilio maalum,ni suala la kitaalam na siyo mbuga za Tanzania tuh eti ndiyo pekee zinajihusisha na suala la kujenga hoteli na kudesign utalii wa aina hiyo,yeye Lema na CHADEMA wanajua fika kuwa suala hilo linafanyika kote duniani na kila aina ya tahadhari inachukuliwa,na siyo kila mtu tuh atapewa ruhusa ya kujenga kwa kuwa tuh ana mtaji wa kufanya hivyo,kuna study kadhaa zimeshafanyika na kuangalia sustainability ya jambo hilo kwa kuzingatia uhifadhi na maendeleo yake kwa ujumla.

Wamasai ni Jamii ambayo imeendelea kuongezeka na kuzaliana miaka na miaka,na itaendelea kuzaliana hifadhini wao pamoja na mifugo yao.

Ni Jambo ambalo liko wazi tuh kuwa kutokana na kuendelea kwao kuzaliana wao na wanyama obviously population yao itazidi kuongezeka na kupelekea kuathiri maisha na uhai wa hifadhi na wanyama wale kwa maslahi ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Sasa,kuna kosa gani kwa serikali inapochukua hatua za makusudi katika kunusuru hali hiyo??wao CHADEMA na wanaharakati uchwara wanataka Serikali ikae kusubiri hadi lini kunusuru hali hiyo kwa mbuga zetu??

Wanakuja na siasa za kishamba eti ooh wamasai wanaondolewa ili mbuga wauziwe waarabu,ujinga ule ule waliokaja nao kwa kusema Bandari imeuzwa kwa waarabu ili mradi tuh kujenga taharuki na kukwamisha mambo ya msingi kuendelea.

Even kipindi cha Magufuli walikuwa mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji eti kwa kigezo cha kuharibu mazingira ila hivi sasa wao wenyewe wamekaa kimya na kuishiwa maneno.

CHADEMA na wanaharakati uchwara yanapokuja mambo ya msingi ya kitaifa kama mnapinga basi mje na hoja za maana na zinazoeleweka na siyo mnakuwa kama watu ambao hamna akili timamu.

Hoja zenu kuhusu suala hili za ngorongoro zitafeli kama zilivyofeli kwenye sakata la Bandari.
Kama suala la ujenzi wa hotels hizo huko hifadhini ni suala la kitaalamu, inashindikana nini kutumia utaalamu huohuo kuwafanya Wamasai walioishi na wanyama ndani ya hifadhi karne na karne wakaendelea kuishi bila kuathiri ikolojia..?

Huoni kwamba wewe ndiye hasa mjinga na mpotoshaji na unashabikia unyanyasaji na utwezaji wa utu wa Wamasai unaifanywa na Rais Samia na watu wake serikalini kwa lengo la kuiuza hifadhi hiyo ya Ngorongoro na ardhi ya Loliondo kwa waarabu wa Oman na Dubai - wajomba zake..?

Please bwana usitufanye sisi ni wajinga na wapumbavu kama nyie kwa maamuzi yenu ya kishenzi na kiharamia namna hii..

Hivi Kuna sababu yoyote justifiable kufuta vijiji 25 vyenye wakazi zaidi ya 100,000+?

Na unaelewa hata logic ya kifuta Kijiji kweli wewe? Maana yake ni kuwa, serikali inaondoa (kufuta) pia huduma zote za kijamii kama maji, shule, hospital (afya) nk ambapo maana yake hao wanahesabiwa ni wanyama pori wasio na thamani yoyote ya ubinadamu. Unaelewa hili? Unaunga mkono hili?

Nakuuliza tena sababu gani justifiable kwa serikali kutaka kufanya mauzi makubwa namna hii ya halaiki (genocide)?

Bora ungenyamaza tu ndugu THE BIG SHOW kuliko kutema utumbo kama huu kumlaumu Lema anayetetea uhai wa binadamu..!
 
Sahihi kabisa Mkuu,ukitaka ujue ukweli,we waulize hao wanaopinga kuwa wanataka serikali ifanye nini katika kunusuru ile hifadhi na wale wanyama kwa maslahi ya kizazi hiki cha sasa na hivyo vinavyokuja??

Kwa sababu wale maasai ni wanadamu

Huelewi unachokisema,na kama huelewi au hujui ni vigumu sana kupata uhalisia wa kinachoendelea kule.
Unauliza serikali ifanye nini kunusuru hifadhi..?

Na nyie wajinga wa akili na ufahamu wenu mdogo huo mnadhani kinachofanyika huko Ngorongoro na Loliondo ni "mpango mzuri wa serikali kunusuru hifadhi na wanyama kwa kizazi cha Sasa na kijacho..??" Hivi kweli wewe THE BIG SHOW na wenzako ndo mnaona hivi kuwa kinachofanyika huko ni kwa ajili ya kunusuru hifadhi na wanyama kwa ajili yetu zote na kizazi kijacho..?? Really?

Aisee nyie akili zenu haziwazi vyema kabisa kwa 100%...

Ninyi hamtumii vyema akili zenu kuchakata mambo na kuelewa....

Ama la, basi nyinyi ni walewale wanyanyasaji na waharibifu wa utu wa binadamu wenzenu kama alivyo Samia Suluhu Hassan..

Kinachofanyika Ngorongoro na Loliondo dhidi wa Wamasai si kulinda hifadhi bali ni mpango mahususi wa Rais Samia Suluhu Hassan (Mzanzibari) kuiuza ardhi hiyo yote kwa Waarabu wajomba zake kutoka Oman na Saudi Arabia na Dubai kwa jina la uwekezaji..

Hata pesa za kulipa familia chache za Wamasai zilizokwisha kuhamia Msomera - Tanga zimetolewa na haohao Waarabu..

Kama unabisha na unasema ni fedha za serikali ya Tanzania, onesha na sema lini Bunge lilipitisha bajeti hiyo na ni shilingi ngapi ziliidhinishwa kwa ajili hiyo..?

Kwa hiyo ni uongo kusema na kudhani kuwa kinachofanyika Ngorongoro na Loliondo ni mkakati wa serikali kuokoa hifadhi hiyo..!

Na umeuliza serikali hii ifanye ni kwa ajili ya kulinda hifadhi hiyo..?

JIBU LAKO NI HILI:
A failed and corrupt government unategemea ifanye nini kizuri na chenye manufaa kwa wote zaidi ya viongozi wake kutumia kila fursa kujipigia pesa za laana kama hivi..???

JIBU zuri ni kuwa, serikali ya Samia Suluhu Hassan na CCM yake imeshindwa kuongoza taifa hili zuri la Tanganyika na watu wake..

Cha kufanya ni aidha iondoke madarakani yenyewe kwa hiari au ifurushwe kwa nguvu Ili kupisha serikali nyingine kuingia na kuwaona Wamasai kama watu na binadamu kama walivyo Watanganyika wengine, serikali inayothamini utu wa mtu
..
 
Wangelikuwa wamelipwa fidia wasingelalamika, na pia lazima pangekuwa na muda (countdown) ya kutosha ya kuwaondoa polepole na kwa staha. Mtu unafurusha kabila nzima lilimekaa pale tangu uumbaji halafu bado wamekuacha hai na unaendelea kuzuia wasipige kura na hata wasipelekewe chakula na huduma za afya. Ingekuwa ni watu wengine wangekuwa wameshamchinja huyo amiri jeshi na kumla nyama siku nyingi. Mjifunze kuheshimu watu nyie ccm.
Mda upo wa kutosha zenzao wengi wameondoka hao wanaobwatuka ni wale wanafadhiliwa na matajiri wa mifugo.

Hakuna wa kumchinja,huo ni uamzi wa Serikali bwashee .

Ngorongoro ni Hifadhi sio eneo la makazi so hameni
 
Hahami mtu na ITAKUWA HIVYO...!!

Ni kweli, iko hivi karne na karne kuwa Ngorongoro ni "Conservation area" ambamo wanyama na binadamu huishi pamoja kwa utaratibu na mpangilio maalumu..

Ngorongoro na Loliondo si kama hifadhi zingine zilivyo kama vile Mikumi, Serengeti, Ruaha nk ambako human settlements and activities are strictly prohibited 🚫 🚫

Leo huko Ngorongoro kipi kimebadilika ghafla kuona binadamu hawa (Wamasai) kugeuka kuwa ni threat dhidi ya hifadhi..?

JIBU NI HILI: Tamaa ya pesa ya viongozi wa serikali hii. Mwaarabu kaiona tamaa hii na Sasa anawalipia tamaa hiyo in exchange na ardhi ya Ngorongoro na Loliondo na kila kilichomo humo isipokuwa wamasai. Nothing more, nothing less...!!

Kwa hiyo ni uamuzi wa serikali yako, Yes.

Lakini ni uamuzi wa hovyo, usiofaa na wenye msukumo wa maslahi binafsi ya viongozi wako hao..

Nakuhakikishia jambo Moja tu kuwa, HILI HALITAFANIKIWA hata kwa kutumia bunduki maana repercussions zake ni lazima ziondoke na watu hawa waovu..!!
 
Iko hivi karne na karne kuwa Ngorongoro ni "Conservation area" ambamo wanyama na binadamu huishi pamoja kwa utaratibu na mpangilio maalumu..

Kipi kumebadilika ghafla kuona binadamu hawa (Wamasai) kugeuka kuwa ni threat dhidi ya hifadhi..?

JIBU NI HILI: Tamaa ya pesa ya viongozi wa serikali hii. Mwaarabu kaiona tamaa hii na Sasa anawalipia tamaa hiyo in exchange na ardhi ya Ngorongoro na Loliondo na kila kilichomo humo isipokuwa wamasai. Nothing more, nothing less...!!

Kwa hiyo ni uamuzi wa serikali yako, Yes.

Lakini ni uamuzi wa hovyo, usiofaa na wenye msukumo wa maslahi binafsi ya viongozi wako hao..

Nakuhakikishia jambo Moja tu kuwa, HILI HALITAFANIKIWA hata kwa kutumia bunduki maana repercussions zake ni lazima ziondoke na watu hawa waovu..!!
Mbona wewe hupendi kuishi na wanyama? Kwamba Masai ni wanyama so wako conserved? 😂😂😂

Ngorongoro ni Hifadhi sio sehemu ya makazi
 
Nani kakuambia sipendi? Unaota au unadhani?

Mimi Niko huku. Haya ndiyo maisha yetu karne na karne...!!

Wanyama wana eneo lao na binadamu vivyo hivyo...

Huu ndio mpango wa Mungu tangu mwanzo binadamu na wanyama kuishi pamoja. Tuko ndani ya mpango wa Mungu. Binadamu gani aweza kutengua..?

Narudia tena kukuambia. HAHAMI MTU HUMO bila kujali serikali yako itafanya nini. Subiri Ili uthibitishe hili..

Kama hao ndugu zako (serikali) hawajui PEOPLE'S POWER basi wataeilewa this time kwamba watu walioiweka serikali madarakani wana nguvu kuliko serikali hiyo..!
 
Nani kakuambia sipendi? Unaota au unadhani?

Mimi Niko huku. Haya ndiyo maisha yenu. Wanyama wana eneo lao. Huu ndio mpango wa Mungu tangu mwanzo binadamu na wanyama kuishi pamoja. Tuko ndani ya mpango wa Mungu..!

Narudia tena kukuambia. HAHAMI MTU HUMO bila kujali serikali yako itafanya nini. Subiri Ili uthibitishe hili..

Kama hao ndugu zako (serikali) hawajui PEOPLE'S POWER basi wataeilewa this time kwamba watu walioiweka serikali madarakani wana nguvu kuliko serikali hiyo..!
Mungu au siyo? Ndio aliwatuma muanze kuharibu Hifadhi Kwa shughuli za kibinadamu?

Ngorongoro sio makazi ya binadamu ni Hifadhi,hameni
 
Mungu au siyo? Ndio aliwatuma muanze kuharibu Hifadhi Kwa shughuli za kibinadamu?
Hao waarabu mnaotaka kutufukuza sisi na kuwapa wao wanakuja kupanda majani na miti kumbe?

Kama ndivyo, kumbe hata sisi Wamasai tunaweza kufanya hivyohivyo ktk ardhi yetu..!

Therefore, please🥺, don't hold such stupid thoughts in your that big head..!!
 
Hao waarabu mnaotaka kutufukuza sisi na kuwapa wao wanakuja kupanda majani na miti kumbe?

Please🥺, don't hold such stupid thoughts in your that big head..!!
Na wewe leta pesa basi Nchi ipate.

Wacheni siasa za kipumbavu,hameni Kwa maslahi ya Nchi , Waarabu ndio wadudu gani?
 
Nimeamini kuwa aliyesema dunia ni duara hakukosea,huyu mwerevu wa leo anayewaita watetea wamasai ni wajinga ndiye yule mjinga aliyekuwa anapinga wachina kupewa gas kwa kusema kuwa gas yetu haitoki hata kwa bomba la bic.
 
Na wewe leta pesa basi Nchi ipate.
Ooh, Sasa unaanza kijifunua na kujiweka wazi sawa na ukweli ulivyo. Ishu ni PESA tu sio kitu kingine. Hakuna cha uharibifu wa mazingira wala nini. Wamehongwa PESA..!!!
Wacheni siasa za kipumbavu
SIASA ZA KIPUMBAVU ni hizo zilizoko huko kwenu. Kutesa na kunyanyasa Wamasai katika ardhi yao aliyowapa Mungu tangu lini ikawa ni uungwana au werevu? Huo ndio upumbavu halisi. STOP 🛑 that immediately...!!
hameni Kwa maslahi ya Nchi
Sio ya nchi. Ya watu binafsi. Yangekuwa ni ya nchi tungekaa chini tukayaweka wazi, tukajadiliana na tukakubaliana peacefully wote kwa kuwa NI MASLAHI YA NCHI. Haya ndugu ChoiceVariable sio. Huu ni uhuni wa watu wachache tu na ndiyo sababu ya resistance hii..

Acha kuihusisha nchi katika tamaa na ujinga wa wachache kwenye hili..!!
Waarabu ndio wadudu gani?
Utajulia wapi maana akili na ufahamu wako ulishakuwa corrupted & polluted na rangi ya kijani..?
 
Sio kujifunua yaani Ngorongoro ni eneo la Kimkakati Kwa biashara ya Utalii ndio maana haitakiwi kuharibuwa Kwa shughuli za binadamu.

So hameni why Tuhatibu Ngorongoro kisa Masai? Kwani Nchi hii imeisha maeneo ya watu kuishi?
 
Wewe sijawahi kukuona hata siku Moja ukakosoa mambo. Wanayofanya serikali hivi serikali haijawahi kukosea yaani wewe jamaa unashangazaga sana mzee hata kaam unapata pesa Kwa hiyo serikali vitu vingine piga kimya hautopata pesa hizo milele uchawa unamwisho
 
Wewe sijawahi kukuona hata siku Moja ukakosoa mambo. Wanayofanya serikali hivi serikali haijawahi kukosea yaani wewe jamaa unashangazaga sana
Pitia upya nyuzi zangu.Mambo ya msingi kama haya siwezi kosoa maana Yana maslahi Kwa Nchi.

Watu wamepisha migodi Kwa maslahi ya Nchi sembuse Masai? Ngorongoro sio Mali ya masai
 
Hamna maslahi yeyote wewe jamaa hujielewi kiufupi haya mambo yanamaslahi ya watu wachache sio Kwa nchi vitu vingine sio lazima uchangie ilimradi na wewe umeonekana umechangia kama unapewa hela huwezi kupewa milele mzee uchawa unamwisho yaani wewe Kila siku kuisifia serikali kama Haina makosa watu wanaiponda serikali ya marekani na za ulaya sembuse hii iliyokua mwisho wa dunia
 
Hamna maslahi yeyote wewe jamaa hujielewi kiufupi haya mambo yanamaslahi ya watu wachache sio Kwa nchi vitu vingine sio lazima uchangie kama unapewa hela huwezi kupewa milele mzee uchawa unamwisho yaani wewe Kila siku kuisifia serikali kama Haina makosa watu wanaiponda serikali ya marekani na za ulaya sembuse hii iliyokua mwisho wa dunia
Sio watu wachache,kwani wawekezaji wakijenga Mahoteli,eneo kubwa la Hifadhi likaongezeka na kuhifadhiwa Nchi hainufaiki? Pesa si inaenda kwenye shughuli za Wananchi au?

Kwani hujaskia Lisu anadai maslahi ya kiuchumi yasiwe mbele ya utu wa Masai?

Na Mimi nasema so long as wanahamishwa na kugidiwa ni jambo zuri maana kuwaacha ni hasara kuliko kuwahamisha na faidia itakayopatikana.
 
Pesa inaenda Kwa maafisa wa juu hamna pesa itayoenda Kwa wananchi hamna raia ataeambulia kitu zaidi ya vumbi hapo unafikili sisi ni wageni wa hii nchi mzee wewe kama umepewa hela kula ila sio Kila kitu uonekane umechangia
 
Back
Top Bottom