CHADEMA mnatuchanganya. Tunataka Katiba inayosimamia haki na sio Katiba Mpya. Kamwe Katiba hiyo haiwezi kutengenezwa na Wanasiasa

Kati ya vitu CCM walivyoweza ni kufanya brainwashing kwa watu.

Taifa likiwa na watu wasiotambua haki zao vizuri na waoga ni rahisi sana kufanya spinning.

Watoto wamekuzwa kuaminishwa mzungu ni adui

Watoto wanaaminishwa mchango wa kuanzia TAA,TANU mpaka CCM ndio ulichangia nchi kupata uhuru huku wakiaminishwa hakuna chama bora zaidi ya CCM.

Je, kipindi kile watu wote walikua TANU?

Kwa jibu jepesi ni kuwa watu walitaka uhuru hata wale wasokua na vyama ila ubabe wa kuungishwa TANU ndio ulionekana kama ndio chama cha kikombozi ila mzungu angeweza kutoka bila hata kuwa TANU.

Historia hii hii ndio imefanyiwa janja janja za Washirika wa CCM mtu kama Okello hatambuliki kwa usahihi.
 
Ubarikiwe ndugu mtoa mada kwa kuanzisha mjadala wenye afya kwenye taifa letu kwa wakati muafaka. Najua huu mjadala utachafuliwa na wanachama wenye mahaba na vyama vyao kwa matusi dhidi ya watu watakaotoa mawazo yatakayokinzana na utashi wao huku wakijinasibu kuwa wapiganiaji wa demokrasia na uhuru wa kutoa maoni.
 
Tungekuwa na katiba sahihi inayodhibiti maamuzi mabovu ya Rais, kuna uwezekano mkubwa kuwa JPM angekuwa hai leo hii. Asingepuuza Covid-19 kama alivyofanya na yeye binafsi angechukua tahadhari zote kuhakikisha hivyo virusi havimsogelei.

Mapambio ya sifa za unafiki kama haya ndiyo yamemtowesha kabla ya wakati wake. Kama alivyoshindwa yeye, hakuna anayeweza kuangamiza upinzani nchini na duniani. Msijidanganye.
 

Katiba ndio msingi wa sheria zote. Katiba hii inampa absolute powers Rais wa JMT. Ushahidi wa hatari yake tumeushuhudia kupitia matendo ya JPM alivyotupilia mbali sheria mbalimbali na kukiuka mifumo iliyowekwa kisheria ili kukidhi matakwa yake binafsi.

Huwezi kupigania haki zilizopo kikatiba kabla hujarekebisha vifungu kinzani kama vile vinavyowezesha madaraka ya Rais kuchezea haki hizo kwa kadiri “anavyojisikia”. Rais kudai kuwa baadhi ya maamuzi muhimu kwa taifa yatategemea “ameamkaje siku hiyo” si kitu cha kusherehekewa. Katiba inayomuwezesha Rais wakati wowote anapojisikia kupiga marufuku shughuli na mikutano ya kisiasa ambayo ipo kikatiba na kisheria!

Tunazidi kushuhudia Rais wa sasa Mama SSH akisahihisha makosa mengi ya JPM yaliyoathiri watu binafsi na uchumi wa Taifa kwa ujumla yaliyotendwa kutokana na mikingamo ya katiba.

Katiba yetu imejaa controversies na contradictions kibao kiasi kwamba Rais anaweza kufanya chochote; kukubali chochote au kukataa chochote kinacholetwa kwake na watu au taasisi husika bila kuwajibika kisheria.

Hivyo ni fallacy (dhana potofu) kuwaambia wapinzani “wapiganie haki za kikatiba” kwanza kabla hawajadai marekebisho ya Katiba hiyo.
 

Mkuu cdm watadai katiba mpya, ww na hao wenzako daini katiba ya haki maana hakuna anayewazuia.
 
Kama hayo makundi mengine hayawezi hata kutetea maslahi yao ndio wataweza kuandika hiyo katiba? Ukiachia wanasiasa hasa wa upinzani, hao unaowasema wataandika katiba ya haki, ni lini uliwahi kuwasikia wakiogelea katiba hata isiyo ya haki?
 
Unataka wachukue copy ya bible labda
 
Kama hayo makundi mengine hayawezi hata kutetea maslahi yao ndio wataweza kuandika hiyo katiba? Ukiachia wanasiasa hasa wa upinzani, hao unaowasema wataandika katiba ya haki, ni lini uliwahi kuwasikia wakiogelea katiba hata isiyo ya haki?
Hoja yangu wao wapiganie Uhuru wa kufanya siasa kwanza. Kupitia Uhuru huo watoe elimu ya Katiba kwenye jamii Tena wakiwa watulivu Kama motivation speaker. Waweke mazingira ya kupatikana Katiba ya haki. Nachosema hapa Katiba ikitungwa na wanasiasa itakuwa mbovu Sana na CCM watapanga wanachotaka kwani kwenye siasa wao ndio Wana nguvu ya maamuzi.
 

Hiyo katiba mpya ambayo mtaandika nyie ya haki isiyo na wanasiasa mmefikia wapi hadi sasa? Au mtaanza lini mchakato wake? Au umekuja kupambaza watu kwa faida ya ccm Boss?
 
Katiba
Katiba mpya ianzie kwenye vyama vya siasa
 
Hayo ya Tume huru, katiba mpya na bunge live wanayasemea wapi ???

Muda huu watumie kupigania haki zilizopo kikatiba Ila zimezimwa. Kama kuwepo wabunge waliovuliwa uanachama, kuzuiwa mikutano ya kisiasa na Uhuru wa habari. Watumie fursa hiyo kuweka ELIMU ya Katiba ili mchakato ukianza upya uwe na Afya
 
Nimesema kwenye kulejea mchakato slogan iwe Katiba inayolinda haki. Na tukiulejea Katiba mpya Sasa itatawaliwa na siasa na CCM wataiunda yote na Wale mnaowaita Covid 19 kwani ndio wapo bungeni na watageuka kuwa bunge la Katiba.
 
Katiba NI kitu kikubwa Sana. Sio Cha kwenda nacho haraka wakati tupo kwenye hasira na makovu kibao. Kwenye uadui mkubwa wa kisiasa na siasa za visasi. Mchakato huo ukianza Sasa hautaleta Katiba Bali wachumia tumbo na watafuta fursa. Lazma tuwe na mazingira ya Maridhiano. Kusiwe na uadui mkubwa Kati ya wapinzani na utawala.
Sasa ukianza mchakato chadema watataka tubadili kila kitu huku CCM wengi wakitaka Katiba itakayowalinda wasitoke madarakani milele.

Tutawaleta akina makonda, Polepole na Kabudi wapya.
 
Nimesema kwenye kulejea mchakato slogan iwe Katiba inayolinda haki. Na tukiulejea Katiba mpya Sasa itatawaliwa na siasa na CCM wataiunda yote na Wale mnaowaita Covid 19 kwani ndio wapo bungeni na watageuka kuwa bunge la Katiba.

Tuko pamoja mkuu.

La msingi tukubaliane katiba ni kipaumbele.

Kusukuma mbele busara hii kueleweka nani anafanya?

Schedules and modalities those are details to follow.

Kupatikana busara ndipo ngoma ilipo sasa. Au Chadema awe sawa na ban-yan mbaya kiatu chake dawa?

Au siyo mkuu?
 
Naunga mkono hoja,wanasiasa wa chama chochote wakae mbali kabisaaa maana ni vigeugeu kabisaaaa.
Leo LOWASA FISADI,KESHO WANATAKA USHAHIDI.
LEO SETH NA ESCROW MAFISADI,KESHO WAACHIWE.
LEO NYALANDU ANABEBA TWIGA,KESHO NI MGOMBEA WETU NA MJUMBE KAMATI KUU
 
Katiba

Katiba mpya ianzie kwenye vyama vya siasa
Katiba nzuri sio NI kwa manufaa ya wananchi na sio wanasiasa. Na maswala ya kisiasa ndio ganayofanya swala la Katiba kuonekana kuwa ipo kwa manufaa ya kisiasa tu. Ndio maana tunakosa maridhiano
 
Katiba Ni waraka wa kisiasa, pia katiba Ni waraka wa kisheria.Unawezaje kuwaweka wanasiasa pembeni..
 
JPM alikua anawapeleka kwenye total extinction...kingebaki kama chama kilichosajiliwa tu basi kama kilivyo JAHAZI ASILIA ... Chadema ni Chama cha wahuni na ni kama kikundi cha kigaidi wao ni waumini wa vurugu , matusi , hawana hoja zinazoeleweka wanazidiwa hadi na ACT WAZALENDO ...
 
NI kweli kabisa, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…