CHADEMA mnaweza kuchukua nchi 2025 ila kama mtafanyia kazi mambo yafuatayo

CDM kina nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi iwapo tu itafanyia kazi mambo yafuatayo.

1. Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.
2. Katibu mkuu awe Heche.
3. Mgombea Urais atoke CCM (Tulizeni kichwa hapa).
4. Kwenye Majukwaa sera zenu ziwe against awamu ya sita na sio awamu zilizopita.
5. Muwape Vijana wengi kugombea udiwa na ubunge (Vija ni chini ya miaka 40).

Kwa leo ni hayo tu.
Ninakubaliana nawe jambo moja tu, la CHADEMA kuwa na nafasi nzuri sana kuliko wakati mwingine wowote wa kuchukua madaraka ya nchi kama watajipanga vizuri kuifanya kazi ya kufanikisha hilo.

Hayo mengine uliyoorodhesha hapo chini hayana uhusiano wowote na mafanikio ya kazi hiyo.
 
Sijui kama Chadema wa jf watakuelewa labda wa nje ya hapa jukwaani. Kuna wakati nahisi humu jukwaani kuna watu wanajulikiana kuwa ni chadema damu lakini kiuhalisua sio chadema sababu haiwezekani kila ushauri unaotelwa kwa ajili yakuimarisha chama chao wao wanaupinga.

Huwa najiridhisha kuwa huwa ni chadema baada ya kuona top leaders wao nao wakiact kama wanavyoact wa humu jukwaani, ikiwemo kuendeleza visasi na chuki ambazo zitawaletea athari kwenye uchaguzi.

Ukweli ni kuwa ilikuwa ni rahisi kwa mwanasiasa yeyote kusimama jukwaani na kuwaambia watu JPM ni mbaya kipindi akiwa madarakani na baadhi ya watu wakakuelewa. Ila sio kwa sasa wakati ambapo watu wengi hata wale waliomuona mbaya enzi zile wanamkumbuka kwa kasi sana, sidhani kama chadema wao watakikubali hili.

Nahisi yatakuwa yale yale ya mzee Lowasa aliyekuwa mbaya alipokuwa ccm alipoenda chadema akawa malaika.
 
Yaani mwanaccm kindaki ndaki tena chawa wa magufuli aliyekuwa na chuki dhidi ya Chadema ndio awe mshauri wa jinsi Chadema inapaswa kushinda?

Sipo kushoto wala kulia. Ila wewe ndo umepotea. Watu wote ni watanzania. Hivi Unajua wezi wengi wa maofisini na wasiolipa Kodi ni wanachama wa Vyama vyote na yapo humu yanaandika mauzi kupinga na kujifanya wazalendo?

Tuachane hayo, angalia content na Sio nani kasema. Unaweza okota jambo. Kwenye Siasa ukaribu na adui yako ndo silaha ya maangamizi.
 
Content inakuwa nullfied na sifa za mwandishi
 
Ukweli ni kuwa ilikuwa ni rahisi kwa mwanasiasa yeyote kusimama jukwaani na kuwaambia watu JPM ni mbaya kipindi akiwa madarakani na baadhi ya watu wakakuelewa. Ila sio kwa sasa wakati ambapo watu wengi hata wale waliomuona mbaya enzi zile wanamkumbuka kwa kasi sana, sidhani kama chadema wao watakikubali hili.
Acha uongo. Unajilisha matumaini hewa.
 
CHADEMA kina nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi iwapo tu itafanyia kazi mambo yafuatayo.

1. Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.
2. Katibu mkuu awe Heche.
3. Mgombea Urais atoke CCM (Tulizeni kichwa hapa).
4. Kwenye Majukwaa sera zenu ziwe against awamu ya sita na sio awamu zilizopita.
5. Muwape Vijana wengi kugombea udiwani na ubunge (Vijana ni chini ya miaka 40).

Kwa leo ni hayo tu.
Labda akigombea Joseph magufuli
 
Chadema waungane na zito zuberi kabwe waungane na hashimu rungwe na yule ITUTU waingie uwanjani kwa nia moja...asubuhi mapema sana wanamaliza mahesabu. ajenda za kuwamaliza ccm zipo nyingi sana kwasasa na zinazidi kuongezeka. CCM wanajikaanga wenyewe kwenye mafuta yao 😀 😀 😀 .

Hawana plan yoyote pale, zaidi wamekazania haki sawa wanawake sijui nini, na kurudisha makapa ambayo tulielezwa kwamba hayafai na tukapewa sababu natukazielewa sababu zile na aliyekuwa Rais, sasa leo tunarudishiwa makapi yale pasipo sababu za kuyasafisha kwa ukamilifu...yanarudishwa kwa spidi yatutawale. CHADEMA MCHUKUENI NA Dr WILBROAD SLAA muyajenge mapema sana muanze mikakati. Wananchi wamechoka sana na wameshakata tamaa tayari msifanye kosa.

Mkumbuke CCM 2015 iliokolewa na Magufuli (yeye binafsi), kwasasa hamna dalili ya kunasibu lile gurudumu ifikapo 2025😎😎
Zitto ni msaliti waachane naye
 
Ninakubaliana nawe jambo moja tu, la CHADEMA kuwa na nafasi nzuri sana kuliko wakati mwingine wowote wa kuchukua madaraka ya nchi kama watajipanga vizuri kuifanya kazi ya kufanikisha hilo.

Hayo mengine uliyoorodhesha hapo chini hayana uhusiano wowote na mafanikio ya kazi hiyo.
Bila kufuata hayo mambo hawataweza kuchukua nchi.

Kwa Nini nasema wachukue mgombea toka CCM?

Huko kuna watu wanao ungwa mkono na system na bado ni wasafi sio kama alivyokuwa Lowasa.

System ikiwaunga mkono hata CCM wenyewe watasanda.

Bila hivyo wasahau kuchukua nchi. Maana system ni ngumu kururhusu mtu wasie mjua kuingia Ikulu.

Ya 2020 yanaweza yakajirudia.
 
CHADEMA kina nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi iwapo tu itafanyia kazi mambo yafuatayo.

1. Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.
2. Katibu mkuu awe Heche.
3. Mgombea Urais atoke CCM (Tulizeni kichwa hapa).
4. Kwenye Majukwaa sera zenu ziwe against awamu ya sita na sio awamu zilizopita.
5. Muwape Vijana wengi kugombea udiwani na ubunge (Vijana ni chini ya miaka 40).

Kwa leo ni hayo tu.
Mkuu sidhani yale maridhiano na mama Ni kuwa wapewe nchi nadhani Ni kurudishiwa Mali zao pamoja na walio jela kutoka + kesi mchongo kufutwa na kupewa fidia, mikutano na vingine virudi Kama zamani, Majimbo yao watapewa na madiwani wao watarudi + wenyeviti nadhani uraisi atawaachia 2030 alafu yeye kukimbilia zenji
 
Hakuna kesi ya mchongo.. zote ni kesi kamili sema kwa vile ni wanasiasa kesi zao humalizana wenyewe.

Mi nimewapa mwanga tu wa namna watachukua nchi. Ila wasipotaka basi wafanye kinyume Cha hapo .
 
Bila kufuata hayo mambo hawataweza kuchukua nchi.

Kwa Nini nasema wachukue mgombea toka CCM?

Huko kuna watu wanao ungwa mkono na system na bado ni wasafi sio kama alivyokuwa Lowasa.

System ikiwaunga mkono hata CCM wenyewe watasanda.

Bila hivyo wasahau kuchukua nchi. Maana system ni ngumu kururhusu mtu wasie mjua kuingia Ikulu.

Ya 2020 yanaweza yakajirudia.
Mkuu, 'JF Member'.

Unazungumzia 'system', isyo na uwezo wa kumjua mtu anayefaa bila hata kujali yupo CCM au la. Hiyo ni 'system' ya aina gani hiyo!
Huoni kwamba hapo tu, katika dhana yako hii moja tayari kasoro kubwa inajitokeza katika yote unayofikiri CHADEMA wanayahitaji?

Hiyo ni 'system' ya namna gani isiyoona ubovu wa uongozi tulionao sasa hivi ndani ya nchi hii; halafu tuitegemee 'system' hiyo hiyo kuibuka na watu fulani walioko CCM, wasioweza kuwepo mahali kwingine kokote?

Hiyo 'system' ilikuwa wapi hadi CCM ikafikia kwenye ubovu wa namna hii!
 
CHADEMA kina nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi iwapo tu itafanyia kazi mambo yafuatayo.

1. Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.
2. Katibu mkuu awe Heche.
3. Mgombea Urais atoke CCM (Tulizeni kichwa hapa).
4. Kwenye Majukwaa sera zenu ziwe against awamu ya sita na sio awamu zilizopita.
5. Muwape Vijana wengi kugombea udiwani na ubunge (Vijana ni chini ya miaka 40).

Kwa leo ni hayo tu.
Kwamba Mgombea urais wamsubiri kutoka CCM? Yale yaleeeeee!!!!😂😂
 
CHADEMA kina nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi iwapo tu itafanyia kazi mambo yafuatayo.

1. Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.
2. Katibu mkuu awe Heche.
3. Mgombea Urais atoke CCM (Tulizeni kichwa hapa).
4. Kwenye Majukwaa sera zenu ziwe against awamu ya sita na sio awamu zilizopita.
5. Muwape Vijana wengi kugombea udiwani na ubunge (Vijana ni chini ya miaka 40).

Kwa leo ni hayo tu.
No.6.Wamkubali JEMBE Magu majukwwaani Kwa KAZI nzuri alofanya.
 
Mgombea urais Mnyika akisimama na Mlawi, itafana sana.😃😃😃😃
 
Chadema haitaki kuchukua nchi. Iichukue kuipeleka wapi? Chadema inataka kuchukua madaraka na mamlaka ya kidola
 
kwa jinisi ninavyojua mimi , hata wasipofanya kampeni chadema wanapita . Aidha umuhimu upo katika wizi wa kura na figisu za kupiga kura . Siku ukiona haya mambo hamna chadema ipo ikulu . sababu kubwa ni kwamba CCM wamejitanabaisha kuwa wapinzani wakitoka nchi hii itakuwa na maendeleo .

juzi mama yangu mfurukutwa mzuri wa ccm anasema hakika wapinzani walikuwa wanatusaidia sana angalau kujua vitu fulani . leo kila kitu hakieleweki na hatujui ni nini kinaendelea .

watanzania wameelewa na hata uchaguzi uliopita walishinda . figisu figisu ilikuwa ni kubwa . yaani mama tayari kisha angukia pua .
 
Back
Top Bottom