CHADEMA mnaweza kuchukua nchi 2025 ila kama mtafanyia kazi mambo yafuatayo

Ninakubaliana nawe jambo moja tu, la CHADEMA kuwa na nafasi nzuri sana kuliko wakati mwingine wowote wa kuchukua madaraka ya nchi kama watajipanga vizuri kuifanya kazi ya kufanikisha hilo.

Hayo mengine uliyoorodhesha hapo chini hayana uhusiano wowote na mafanikio ya kazi hiyo.
 
Sijui kama Chadema wa jf watakuelewa labda wa nje ya hapa jukwaani. Kuna wakati nahisi humu jukwaani kuna watu wanajulikiana kuwa ni chadema damu lakini kiuhalisua sio chadema sababu haiwezekani kila ushauri unaotelwa kwa ajili yakuimarisha chama chao wao wanaupinga.

Huwa najiridhisha kuwa huwa ni chadema baada ya kuona top leaders wao nao wakiact kama wanavyoact wa humu jukwaani, ikiwemo kuendeleza visasi na chuki ambazo zitawaletea athari kwenye uchaguzi.

Ukweli ni kuwa ilikuwa ni rahisi kwa mwanasiasa yeyote kusimama jukwaani na kuwaambia watu JPM ni mbaya kipindi akiwa madarakani na baadhi ya watu wakakuelewa. Ila sio kwa sasa wakati ambapo watu wengi hata wale waliomuona mbaya enzi zile wanamkumbuka kwa kasi sana, sidhani kama chadema wao watakikubali hili.

Nahisi yatakuwa yale yale ya mzee Lowasa aliyekuwa mbaya alipokuwa ccm alipoenda chadema akawa malaika.
 
Yaani mwanaccm kindaki ndaki tena chawa wa magufuli aliyekuwa na chuki dhidi ya Chadema ndio awe mshauri wa jinsi Chadema inapaswa kushinda?

Sipo kushoto wala kulia. Ila wewe ndo umepotea. Watu wote ni watanzania. Hivi Unajua wezi wengi wa maofisini na wasiolipa Kodi ni wanachama wa Vyama vyote na yapo humu yanaandika mauzi kupinga na kujifanya wazalendo?

Tuachane hayo, angalia content na Sio nani kasema. Unaweza okota jambo. Kwenye Siasa ukaribu na adui yako ndo silaha ya maangamizi.
 
Content inakuwa nullfied na sifa za mwandishi
 
Acha uongo. Unajilisha matumaini hewa.
 
Labda akigombea Joseph magufuli
 
Zitto ni msaliti waachane naye
 
Bila kufuata hayo mambo hawataweza kuchukua nchi.


Kwa Nini nasema wachukue mgombea toka CCM?

Huko kuna watu wanao ungwa mkono na system na bado ni wasafi sio kama alivyokuwa Lowasa.

System ikiwaunga mkono hata CCM wenyewe watasanda.

Bila hivyo wasahau kuchukua nchi. Maana system ni ngumu kururhusu mtu wasie mjua kuingia Ikulu.

Ya 2020 yanaweza yakajirudia.
 
Mkuu sidhani yale maridhiano na mama Ni kuwa wapewe nchi nadhani Ni kurudishiwa Mali zao pamoja na walio jela kutoka + kesi mchongo kufutwa na kupewa fidia, mikutano na vingine virudi Kama zamani, Majimbo yao watapewa na madiwani wao watarudi + wenyeviti nadhani uraisi atawaachia 2030 alafu yeye kukimbilia zenji
 
Hakuna kesi ya mchongo.. zote ni kesi kamili sema kwa vile ni wanasiasa kesi zao humalizana wenyewe.

Mi nimewapa mwanga tu wa namna watachukua nchi. Ila wasipotaka basi wafanye kinyume Cha hapo .
 
Mkuu, 'JF Member'.

Unazungumzia 'system', isyo na uwezo wa kumjua mtu anayefaa bila hata kujali yupo CCM au la. Hiyo ni 'system' ya aina gani hiyo!
Huoni kwamba hapo tu, katika dhana yako hii moja tayari kasoro kubwa inajitokeza katika yote unayofikiri CHADEMA wanayahitaji?

Hiyo ni 'system' ya namna gani isiyoona ubovu wa uongozi tulionao sasa hivi ndani ya nchi hii; halafu tuitegemee 'system' hiyo hiyo kuibuka na watu fulani walioko CCM, wasioweza kuwepo mahali kwingine kokote?

Hiyo 'system' ilikuwa wapi hadi CCM ikafikia kwenye ubovu wa namna hii!
 
Kwamba Mgombea urais wamsubiri kutoka CCM? Yale yaleeeeee!!!!πŸ˜‚πŸ˜‚
 
No.6.Wamkubali JEMBE Magu majukwwaani Kwa KAZI nzuri alofanya.
 
Mgombea urais Mnyika akisimama na Mlawi, itafana sana.πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Chadema haitaki kuchukua nchi. Iichukue kuipeleka wapi? Chadema inataka kuchukua madaraka na mamlaka ya kidola
 
kwa jinisi ninavyojua mimi , hata wasipofanya kampeni chadema wanapita . Aidha umuhimu upo katika wizi wa kura na figisu za kupiga kura . Siku ukiona haya mambo hamna chadema ipo ikulu . sababu kubwa ni kwamba CCM wamejitanabaisha kuwa wapinzani wakitoka nchi hii itakuwa na maendeleo .

juzi mama yangu mfurukutwa mzuri wa ccm anasema hakika wapinzani walikuwa wanatusaidia sana angalau kujua vitu fulani . leo kila kitu hakieleweki na hatujui ni nini kinaendelea .

watanzania wameelewa na hata uchaguzi uliopita walishinda . figisu figisu ilikuwa ni kubwa . yaani mama tayari kisha angukia pua .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…