CHADEMA msipo badili mbinu ya kisiasa hamuwezi kushika dola

CHADEMA msipo badili mbinu ya kisiasa hamuwezi kushika dola

Katika andiko lako, hoja yenye msingi, na ambayo ndiyo lengo kuu la viongozi wa upinzani ni katiba mpya itakayo waweka madarakani na siyo maendeleo ya nchi, kama ulivyodokeza kuwa katiba mpya is fine lakini mnaidai huku government ikiwa ime relax, no pressure from the citizens. Wananchi wanahitaji maendeleo na si Katiba mpya.

Ili nia hiyo (maendeleo) iwe kweli kunahitajika mifumo shirikishi ya maendeleo na mamlaka za kuwajibisha watendaji wasiotimiza wajibu wao na wale wanaotumia madaraka vibaya kwa manufaa binafsi.

Katiba mpya ndio msingi wa maendeleo. Maana ndio sheria mama. Halafu sio lazima wananchi waandaamane ndio ujue wanataka katiba mpya. Tanzania tuliandika katiba mpya mwaka 1977 na 1984 bila wananchi kuhusika Wala kudai katiba mpya.
 
Acha kuwadanganya CHADEMA kuwa nje ni nyeupe 2025. Au ulimaanisha uchaguzi mkuu wa Twitter? Hakuna namna ambayo CHADEMA wanaweza kuleta ushindani kwenye uchaguzi mkuu 2025 dhidi ya Mama Samia. Kwanza hata wao wanakushangaa kwasababu tayari wameshampatia tuzo mgombea wetu mtarajiwa kwa tiketi ya CCM. Ile tuzo peke yake ni ishara kwamba CHADEMA wamempitisha Mama Samia kwenye urais 2025.

Kuhusu katiba mpya ni kwamba wananchi hawawezi kusapoti CHADEMA kwasababu kuna ya vitu wanavyovitaka CHADEMA kwenye katiba mpya ni tofauti kabisa na wananchi tunayoyataka. CHADEMA wao wanachotaka ni serikali tatu ili kuongeza nafasi za ulaji wakati sisi wananchi tunataka hata serikali moja kama ingewezekana ili kupunguza gharama na pia kuimarisha zaidi umoja.

Ninawashauri CHADEMA wapuuze huu ushauri wako na kujikita zaidi kwenye kumsapoti Mama Samia.

Kwa akili yako Rais Samiah ni Rais wa Tanzania au wa CCM. Unaongea kana kwamba CHADEMA wasimtambue Samiah Kama Rais wa Tanzania. Kimpa tuzo ilikuwa ishara ya heshima kwa Rais na sio endorsement ya urais. Tatizo CHADEMA imewaweka Kati ndio maana mnaijadili kutwa na kushindwa hata kujadili bajeti za wizara zinazopitishwa bungeni.
 
Nimekusoma hadi hapo katikati, mkuu 'Mhuli ya Matenga'; kuna mambo umeyaandika ninakubaliana nayo na mengine,... aha, ndiyo hivyo tena, hatuwezi kukubaliana kwa kila kitu.

Jambo ambalo limenipa msukumo niku'quote' ni kwa kutowaelewa vizuri hao CHADEMA unaowananga hapa. Na ili nieleweke vyema nitaje moja kwa moja CHADEMA anayoisimamia Mbowe.

Hii CHADEMA ya Mbowe, ni hiyo hiyo CCM anayoiongoza Samia, na ni CCM ile ile aliyokuwa akiisimamia Kikwete.

Sasa wewe unapokuja hapa na kuhimiza CHADEMA na viongozi wake waliopo upande wa Mbowe wafanye tofauti na anayofanya Samia, ina maana kwamba uelewa wako wa CHADEMA unao upungufu fulani.
Kwa hiyo, kwa hili usiitegemee CHADEMA, ambayo kiongozi wake ni Mbowe iwe mbali na CCM anayoiongoza Samia. Hili kamwe halitatokea.

Kinachosubiriwa tu sasa ni jinsi watakavyounganisha hivi vyama viwili ili wote wawe kwenye ulaji mhula unaofuata endapo kama waTanzania unaowasema hapa hawatakuwa makini.

Umewekeza sana upande wa waTanzania kuendelea kuenzi ya Magufuli, lakini usisahau kwamba mbinu zitatumika kukiondoa kizingiti hicho, hasa hapo itakapobainika kwamba hakuna mbadala wa kuaminika dhidi ya CCM (hata hiyo CCM pungufu chini ya Samia).
Ondoa matuaini yako juu ya CHADEMA ambayo itaendelea kuwa chini ya uongozi wa Mbowe. CHADEMA hiyo haitakuwa na tofauti yoyote na CCM anayoiongoza Samia, baada ya kuzima masalia yote ya Magufuli.

Leo ndio mmejua CCM na CHADEMA ni wamoja. Mtaongea mengi Sana. Wakati Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi mliongea mambo mengi ya kuonesha CHADEMA ni adui wa serikali, ila leo mmegeuka kuwa CHADEMA na CCM ni kitu kimoja. Sawa nawapa muda mtabadilisha usemi kila siku.
 
Wamefikishwa Mahakamani na magerezani mafisadi na masaliti na magaidi ya Nchi hii.....

Wametolewa Magerezani mafisadi na masaliti na magaidi ya Nchi hii....


Matusi ni yale yale......Mnasomeka, ila ninawaonea huruma sana walio kwenye madaraka na kuwasoma. Ni kweli hakuna atakayekuja kumkomboa Mtanzania mbele ya wanafiki na wazodoaji.

R.I.P Comrade J.P.Magufuli

Laana ipo Ulaya na Kwingi eko.....
".... uso wa nchi nyingi za Kikristo unaleta hali ya kutisha ya ujinga, unafiki na uchoyo." William Carey fundi viatu wa Uingereza ambaye ninaweza kusema ndie alikuwa muasisi wa Faharasa ya Uchumi wa Dunia au World Economic Index

Punguza stress utachanganyikiwa. Soma ulichoandika.
 
Hamna chama mule,wale wah*ni wameshaaidiwa kupewa vijimbo kadhaa uchaguzi ujao basi.
Lowasa alijaribu kutikisa Mbuyu ila alikosa support;Ile CCM inatakiwa igawanyike wengine waende upinzani kama walivyofanya akina Hayati Kibaki kuiacha KANU na kuungana na upinzani,apo ndipo tutakuwa na mageuzi ya kweli ya kisiasa na siasa za ushindani wa hoja siyo viroja vya akina Mbowe.

Hakuna chama halafu mnakijadili kila siku?. CHADEMA itawaumiza kichwa mpaka mchanganyikiwe. Vyama vipo vingi ila nyie unafiki wenu Ni kwa CHADEMA.

Halafu nikusahishe, Kibaki alikuwa tayari upinzani tangu 1992 na chama chake cha DP, waliohama KANU walikuwa Raila, Kalonzo na Saitoti kupitia muungano wa Rainbow Coaliation.
 
Leo ndio mmejua CCM na CHADEMA ni wamoja. Mtaongea mengi Sana. Wakati Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi mliongea mambo mengi ya kuonesha CHADEMA ni adui wa serikali, ila leo mmegeuka kuwa CHADEMA na CCM ni kitu kimoja. Sawa nawapa muda mtabadilisha usemi kila siku.
Mkuu 'econonist' huwa sipendi kujumuishwa kijumlajumla namna hii unayofanya hapa katika makundi ambayo mimi si mshiriki wake.

Hii inaonyesha ukosefu wa umakini kwa upande wako.

Unaweza kunionyesha mahali popote nilipohusika na hayo uliyonihusisha nayo humu JF, au kwingineko?
 
Kwa akili yako Rais Samiah ni Rais wa Tanzania au wa CCM. Unaongea kana kwamba CHADEMA wasimtambue Samiah Kama Rais wa Tanzania. Kimpa tuzo ilikuwa ishara ya heshima kwa Rais na sio endorsement ya urais. Tatizo CHADEMA imewaweka Kati ndio maana mnaijadili kutwa na kushindwa hata kujadili bajeti za wizara zinazopitishwa bungeni.
Kama unashindwa kujua kuwa Rais Samia ndo mwenyekiti wa CCM basi itoshe kusema CHADEMA mwafwa...🤔
 
Back
Top Bottom