CHADEMA msipo badili mbinu ya kisiasa hamuwezi kushika dola


Katiba mpya ndio msingi wa maendeleo. Maana ndio sheria mama. Halafu sio lazima wananchi waandaamane ndio ujue wanataka katiba mpya. Tanzania tuliandika katiba mpya mwaka 1977 na 1984 bila wananchi kuhusika Wala kudai katiba mpya.
 

Kwa akili yako Rais Samiah ni Rais wa Tanzania au wa CCM. Unaongea kana kwamba CHADEMA wasimtambue Samiah Kama Rais wa Tanzania. Kimpa tuzo ilikuwa ishara ya heshima kwa Rais na sio endorsement ya urais. Tatizo CHADEMA imewaweka Kati ndio maana mnaijadili kutwa na kushindwa hata kujadili bajeti za wizara zinazopitishwa bungeni.
 

Leo ndio mmejua CCM na CHADEMA ni wamoja. Mtaongea mengi Sana. Wakati Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi mliongea mambo mengi ya kuonesha CHADEMA ni adui wa serikali, ila leo mmegeuka kuwa CHADEMA na CCM ni kitu kimoja. Sawa nawapa muda mtabadilisha usemi kila siku.
 

Punguza stress utachanganyikiwa. Soma ulichoandika.
 

Hakuna chama halafu mnakijadili kila siku?. CHADEMA itawaumiza kichwa mpaka mchanganyikiwe. Vyama vipo vingi ila nyie unafiki wenu Ni kwa CHADEMA.

Halafu nikusahishe, Kibaki alikuwa tayari upinzani tangu 1992 na chama chake cha DP, waliohama KANU walikuwa Raila, Kalonzo na Saitoti kupitia muungano wa Rainbow Coaliation.
 
Mkuu 'econonist' huwa sipendi kujumuishwa kijumlajumla namna hii unayofanya hapa katika makundi ambayo mimi si mshiriki wake.

Hii inaonyesha ukosefu wa umakini kwa upande wako.

Unaweza kunionyesha mahali popote nilipohusika na hayo uliyonihusisha nayo humu JF, au kwingineko?
 
Kama unashindwa kujua kuwa Rais Samia ndo mwenyekiti wa CCM basi itoshe kusema CHADEMA mwafwa...🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…