CHADEMA mtatoka na ajenda gani baada ya kurudi kwa mikutano ya hadhara ya siasa

CHADEMA mtatoka na ajenda gani baada ya kurudi kwa mikutano ya hadhara ya siasa

Bila kumuunganisha marehemu na chadema mjisikii rahaa ccm.
 
Hahahaaa!! Mtu kakufa Kakufa tu. Aina mashiko kabisa.
 
CHADEMA mna wakati mgumu Sana kunadi será zenú.

Mnamsema vibaya Magufuli huku wananchi tukimwona ndiyo alikuwa mkombozi wetu.

Hata CCM wameruhusu mikiutano wajue mtaongea nini. Tena huko Mwanza msije mkansema vibaya Magufuli.

Nasubiri Kwa hamu nione agenda zenú, ila kumbukeni bila kuwa mlengo wa Magufuli mtapata tabu Sana

CHADEMA sio chama kilichofilisika kisiasa. Magufuli aliitesa CHADEMA na watu wake. Magufuli hamna namna yeyite anaweza kusemwa na CHADEMA kwamba alikuwa ni baba wa demokrasia
 
Wewe una akili gani? Unashindwa kuandika hata neno hawana. Awana ndio mdudu gani?
Haaaaa kumbe ni hawana tatizo mimi natumia kiswaili wewe unatumia kiswahili tatizo ni gani [emoji1787]
 
20 January 2023
KATIBA MPYA KUBEBA MKUTANO WA CHADEMA VIONGOZI WAWASILI MWANZA!

Viongozi wa mabaraza ya wazee, wanawake na vijana wa CHADEMA pamoja na wabunge wa bunge la wananchi ambao walikuwa wagombea ubunge kuputia CHADEMA katika uchaguzi mkuu uliovurugwa 2020 katika majimbo yote Tanzania wameanza kuwasili jijini Mwanza kuungana na viongozi wa kitaifa, kanda na mikoa.
 
Kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara ya siasa ni fursa nyingine inayofungua milango ya kisiasa kujenga na kumarisha demokrasia ya Tanzania wapinzani wanapaswa kuchanga karata zao vizuri katika agenda watakazotoka nazo.

Japo mlikuwa wahanga wakubwa wa utawala wake mnatakiwa kuachana na kumzungumzia au kulitaja jina la Magufuli kabisa katika majukwaa ya hadhara ya kisiasa. Magufuli haipaswi kuwa mojawapo ya ajenda kwa sababu hayagusi maisha ya raia tena kwa namna yoyote kwa sasa, hata hivyo mnaweza kuwazungumzia watu wake aina ya kina Mnyeti, Gelasius Byakanwa, Makonda, Sabaya, Muro n.k

Ajenda kuu za upinzani zinatakiwa kuwa

1. Hali ya maisha kiuchumi
2. Upatikanaji wa huduma za kijamii
3. Miondombinu
4. Hali ya kidemokrasia
5. Tume huru ya uchaguzi
6. Katiba mpya
7. Mikopo ya nchi
8. Mazingira ya kufanya biashara
9. Matumizi ya serikali
10. Uvunaji na uhifadhi wa maliasili zetu.
Usiwafundishe maadui zako cha kusema.Mnapenda siasa za uhasama nyie msio wazalendo.
 
Watu wanaweza kuudhuria siyo kwa kuikubali chadema ...ukweli chadema ni kama matapishi kwa watz walio wengi ...chadema kimekuwa chama cha wapuuzi ...walamba makalio ya mabeberu
Hapa tayari umeshapanic 😂😂😂
 
Mimi nadhani kama JPM ataguswa, basi aguswe positively na siyo negatively, hapo CDM watapata wafuasi wengi sana.

Ukweli ni kwamba, JPM anaishi mioyoni mwa Watanzania wengi sana. Lakini pia ikumbukwe kuwa si kila unayemchukia wewe anachukiwa pia na watu wengine, hapana.

Kuna watu waliumbwa kwa namna ya pekee sana Duniani. Hata afanye mabaya mengi namna gani, atapendwa tu na watu.
Huyo ndiye JPM.
 
Kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara ya siasa ni fursa nyingine inayofungua milango ya kisiasa kujenga na kumarisha demokrasia ya Tanzania wapinzani wanapaswa kuchanga karata zao vizuri katika agenda watakazotoka nazo.

Japo mlikuwa wahanga wakubwa wa utawala wake mnatakiwa kuachana na kumzungumzia au kulitaja jina la Magufuli kabisa katika majukwaa ya hadhara ya kisiasa. Magufuli haipaswi kuwa mojawapo ya ajenda kwa sababu hayagusi maisha ya raia tena kwa namna yoyote kwa sasa, hata hivyo mnaweza kuwazungumzia watu wake aina ya kina Mnyeti, Gelasius Byakanwa, Makonda, Sabaya, Muro n.k

Ajenda kuu za upinzani zinatakiwa kuwa

1. Hali ya maisha kiuchumi
2. Upatikanaji wa huduma za kijamii
3. Miondombinu
4. Hali ya kidemokrasia
5. Tume huru ya uchaguzi
6. Katiba mpya
7. Mikopo ya nchi
8. Mazingira ya kufanya biashara
9. Matumizi ya serikali
10. Uvunaji na uhifadhi wa maliasili zetu.
Jiwe lazima atajwe, kuna uchafu wake mwingi sana ambao ulisababisha madhara mengi ila obviously hatakuwa main agenda.
 
Mimi kama mjasiliamali wa kuprinti tisheti nimeanza kupokea order za kuprint tisheti zenye picha ya hayati Magufuli zitazovaliwa siku ya mkutano mkubwa wa Chadema pale jijini Mwanza.

Mtu mmoja aliyenipa order aliuliza.

Tisheti za JPM zinauzwa wapi, ndio za kuvaa nyakati hizi za mikutano sasa, bila kujali upo mkutano gani, no matter what kuna ujumbe utapenya, tena wenye nguvu, usiobezeka..

Njooni Mwanza tuwalie hela zenu na mtueleze kwa nini mlishangilia kifo cha Magufuli, na mtueleze pia kwa nini watoto wa Mbowe ,Lisu na Lema ni raia wa Marekani.

Niko hapa naprint za kutosha
Uko vizuri, baada ya Jiwe kuzuia umma wa Watanzania wasivae T-shirts za 'Get well soon Lissu' na akafa huku Lissu yuko hai basi endelea kwani Sukuma gang wapo wa kutosha watanunua.
 
Hapa tayari umeshapanic [emoji23][emoji23][emoji23]
Watu wanaweza kuudhuria ila ukaishia kuzomewa tu ...kumbuka magufuli alipo pokea kijiti kwa muhuni mzee wa msoga alivyo pata tabu mikoa ya mbeya watu walikuwa wanakwenda ila wanazomea na hata zito kabwe kakutana na kashi kashi za hivyo walikuwa wanakenda kwa wingi ila wanapiga kelele yuda yuda
 
Haya tuma salamu kwa mataga 50 popote walipo.
 
Lazima wamzungumzie Magufuli japo kwa mafumbo kwa sababu wanaamini nchi hii ilikuwa shwari ila Magufuli ndio kavuruga kila kitu, hadi hao ccm wenyewe kama akina Nape na Mzee makamba bado wanamzungumzia Magufuli sasa Chadema wanaachaje kumzungumzia Magufuli?

Kama tunaamini Magufuli ndio chanzo cha matatizo ya nchii hii basi huwezi kukwepa kumtaja.
 
Back
Top Bottom