ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
CHADEMA na ACT Wazalendo tunautangazia umma na wanaopinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu kushiriki Maandamano ya Amani kesho Jumatatu ya Tarehe 2/11/20. Madhumuni ya Maandamano ni kudai kurudiwa Uchaguzi Mkuu chini ya Tume Huru ya Uchaguzi.
Maandamano yataanzia sehemu 2, kundi moja litaanzia Buguruni Sheli kuchukua barabara ya Uhuru mpaka Kariakoo, Msimbazi Road mpaka fire, Morogoro road, Bibi Titi mpaka Ofisi za Tume.
Kundi lingine litaanza Ubungo Bus Terminal kuchukua Morogoro road mpaka fire kisha Bibi Titi kuelekea Ofisi ya Tume.
Wajumbe wa Kamati Kuu mnaopenda kushiriki maandamano tafadhali mtachagua kati ya maeneo hayo. Maandamano yanaanza saa mbili kamili asubuhi kuelekea Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu JK Nyerere Conference Center. Viongozi Wakuu wataongoza Maandamano hayo.