Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo ni wakati wa kukutana na kutoa tamko la pamoja nini kifanyike

Bado naamini CDM na ACT wanalo jambo kubwa la kufanya ili kutuongoza kwenye hii vita ya utawala wa kidhalimu, tuwape muda haya sio mambo ya kukurupuka tu kama alivyofanya Maalim huko Zanzibar.
 
Mkuu hakuna mbunge wa CHADEMA wala ACT kwa Tanzania bara atakayetangazwa.
CUF watapata wabunge, NCCR mmoja, TADEA ya Shibuda mbunge mmoja. Jumla watano. Lkn ACT na Chadema target yao ni kuviua kabisa.
 
Huyu Mmawia sijui ndio kapotelea wapi. Simsikii kabisaaa.
 
Mawakala walitolewa vituoni
 
Ukandamizwaji wa Haki ,umefikia kiwango Cha doomsday ..ya NI kiwango kikubwa saaana..lakini kwann watu wanakosa utu kabisa!?🙌🙌🙌
 
Wala watu msijipe matumaini. Wapinzani hawatakuwa na tamko lolote la maana.
Kumbukeni kabla ya Lissu kurudi yote yalikuwa yameufyata na kunyikunyata labda Maalim Seif tu ndio alikuwa jasiri kama Lissu.
Yule wanamwita mwamba tuvushe ni bata tu.

Hamna kitu watafanya! Tulionya humu, usiingie kwenye uchaguzi bila tume! Hawakusikia! Mwingine huko Mbeya alisema atashinda tu hata bila tume huru! Leo kiko wapi!
 
Hakuna haja ya wapinzani kufanya press, msiba huu sio wa upinzani, acheni tunyooshwe tu, jambo hili ni la umma wa Tanzania nzima, kama kuna mwanaccm anadhani kutakuwa na upendeleo wa huduma basi asubiri tu, safari hii hakuna wa kuisoma namba, tutaziandika wote, halafu tutazisoma kwa pamoja. JPM for life, CCM mbele kwa mbele! Yajayo yanafurahisha?
 
Ni msiba wa waliowengi hiyo ipo dhahiri. Jambazi ameshafanya yake.
 
Anza we we uwe mfano kwa wenzio. Ule Uhuru wa kuropoka mwisho ulikuwa Oktoba 27, baada ya hapo ni kazi kazi. Jitokeze barabarani ujifanye kama unaandamana uone
 
Sasa mkakamata ushahidi na kuuchoma moto, jamii itawasaidiaje?. Unachoma ushahidi kisha unalalamika?
 
Acha uongo tuliwaambia watz siyo wajinga kama mnavyofikiria. Naona wamewayoosha tayari na huku Kawe Mdee anapumlia mipira!!! hahahahaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…